23/10/2024
*ALINIFUATA ATUBU,JAMBO AMBALO AMEKAA NALO NA LINAMHUKUMU SANA*
Aliingia kwenye mahusiano na mume wa mtu mwenye mke na watoto watatu.
Na huyo dada hakuwa tayari kuendelea kuwa mchepuko ila aliiwinda sana nafsi ya kuwa mke halali wa ndoa bila kujali afya ya ndoa ya mwanamke mwenziwe.
Na alizidi kumsumbua jamaa ili amhalalishe,jamaa shida ikawa kwamba ana ndoa tena halali kabisa na watoto..kwa hiyo ilikuwa ni ngumu otherwise waendelee kuwa na mahusiano ya siri. Mahusiano yakaendelea na walipendana mno! Kuna wakati ulifika hadi mwanaume akaanza kutamani wangeishi k**a mume na mke lakini atamwachaje wa ndani?
Mwanamke alikuwa ni mwenye akili nyingi sana. Alichofanya ni kuforce ndoa..ilibidi amshawishi amwache afanye mchezo ambao utatoa uhalali wa yeye kuachana na mke wake. Jamaa akatoa idhini.....
Dada akampanga mtu na kumlipa pesa iwapo k**a angefanikisha jambo lao...iko hivi;
Akamtuma ajenge ukaribu na mwanamke wa huyo brother awe anaenda ofisini kwake k**a kumuungisha vitu kwenye biashara yake.
(Huyo mwanamke alikuwa na duka na anauza vitu online)
Huyo jamaa akaipata namba ya huyo mwanamke akaanza kuagiza vitu,analetewa,siku zingine anafuata mwenyewe,wakawa wanachati,kwa kifupi wakazoeana,huku mwanamke asijue huyo mtu katumwa kuharibu ndoa yake....siku zingine akinunua kitu cha elfu 30 anaongeza 30 nyengine...wakati mwingine anamtumia hadi Elfu 50 k**a hela ya soda. K2a kifupi wakazoeana.
Basi kuna siku akamtongoza na kumwambia anampenda....haikuwa rahisi kwa mwanamke lakini kuna siku alinasa,akiangalia wameshazoeana na jamaa anamjali sana. Akamkubalia wakapanga waonane lodge fulani hapa hapa Dar es Salaam.
Siku waliyopanga kukutana,yule jamaa akamwambia aliyemtuma kwamba tayari kakubaliwa na wanaonana mahali fulani...akamtumia screenshorts zote
Na yule dada akaziforward kwa mwanamme wake.
Wakajipanga Mumewe aende akafanye fumanizi hiyo lodge,huku wakimpanga yule jamaa kule chumbani asibane mlango na wakiwa watupu ndio awaruhisu. Na kweli mume akapewa ishara aingie....huyo mchepuko akiwa ni k**a mwandishi akichukua matukio yote.
Jamaa akafanikiwa kumfuma mkewe akiwa wazi japo hawakuanza kitendo chochote...cha kwanza ni kuchukua nguo zote za mkewe na kushika mkononi na kumpiga picha...kisha akampigapiga mkewe na kumwambia nipe kwa hiari yako pete niliyokuvisha na kwamba amevunja agano la ndoa. Na akamwambia arudi nyumbani moja kwa moja akamtisha aondoke aende kwao nyumbani na kila kitu chake,halafu aandike talaka ama sivyo atazirusha picha zote mtandaoni na kuwaonyesha wazazi wake.
Mama akaandika talaka kwa hofu huku akimwomba mumewe misamaha akakataliwa na akaondoka jumla na kurudi kwao. Duka akaliacha nyumba akaiacha akaondoka na mtoto mdogo...wengine walikuwa shule za boarding.
Baada ya huo mchezo jamaa akaoa haraka wakaanza kuishi kwenye nyumba ile ile,mapenzi motomoto, wakakaa k**a miaka miwili na kitu fulani...mume akaanza kuungua ugonjwa usiojulikana,akawa anadhoofu tu...hangaika wee,tibu hiki na kile wapi.
Akaja kuporomoka kiuchumi kiasi cha kuuza nyumba na mali nyingi sana...akaendelea kudhoofu na akafa mwaka huu mwezi wa pili. Nasikitika kuwa hakupata neema ya kutubu.
Mwanamke aliachwa nyumba ya kupanga madeni yakawa mengi,na aliachwa na mtoto mmoja,akaanza kuugua pia. Nilikutana nae akiwa hospitali amekatwa ziwa la kulia kwasababu ya kansa. Yupo kwenye matibabu kichwani hana unyewele hata mmoja ndipo akakumbuka juu ya uovu walipmfanyia yule mama. Nikatafutwa nimwombee na kumkutanisha na yule mama na hajui kwa kumpata....Maana hana mawasiliano nae wala kufahamu aliko ni wapi.
Nikiwa namwombea niliambiwa kitu kigumu sana na cha kukatisha tamaa,nikaambiwa usiombe....mimi sikuacha kuonba rehema za Mungu juu yake nikimkumbusha rehema zake kwa mtumishi wake Daudi na wazawa wake.
Msidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtu ndicho atakachovuna. Apandaye katika tamaa za kidunia, atavuna humo uharibifu;Wagalatia 6:7-8
Mimi nadhani inawezekana ukajenga mahusiano na mtu bila kumharibia mwingine...Hawa waitwao wakristu hawa,ni wabaya sana wanapotaka kufosi mahusiano yasiyokuwa yao...wanawake wa kiislamu akifuatwa na mume wa mtu akamtaka amwoe,yeye ndio anamshauri huyo mume akaongee kwanza na mke wake ikiwa ataridhia ili kutunza amani.
Ila hawa wa kwetu wapo tayari hata kuomba mke afe ili yeye ajimilikishe.
Inawezekana ukajenga familia yako bora bila kutoa machozi wengine...Mungu anaitwa mhukumu wa haki,mambo yanayofanywa na wanadamu mipango yao yote ya sirini anafuatilia ili ahukumu kwa haki.
By Kuhani Atson Mwansepe