Umoja Wa Vijana Kkkt Kinondoni

Umoja Wa Vijana Kkkt Kinondoni Ukurasa maalum kwa ajili ya Mawasiliano ya Umoja wa Vijana Kkkt Kinondoni.

25/08/2026

25/08/2026 - JUMANNE.

Tutumie ndimi zetu kwa Utukufu wa Mungu.
Waamuzi 11:29-33 & Waamuzi 11:34-40.

Tunakumbushwa kuendelea kujiliwa na roho wa Bwana na kutenda yatupasayo kutenda huku tukikumbuka kuziondoa nadhiri tulizoziweka katika maisha yetu yote ya kila siku ya hapa duniani.

Eng. Richard R. Mwambije

25/08/2026
24/08/2026

24/08/2026 - JUMATATU.

Tutumie ndimi zetu kwa Utukufu wa Mungu.
Hesabu 14:1-10 & Yakobo 3:1-4.

Tunakumbushwa kuendelea kutokuogopa maana Bwana yupo pamoja nasi huku tukiacha kunung'unika, kumwasi Bwana na kusema sana ili tusijikwae katika kunena katika maisha yetu yote ya kila siku ya hapa duniani.

Eng. Richard R. Mwambije

22/08/2026

22/08/2026 - JUMAMOSI.

Mungu Huwainua wanyenyekevu.
Luka 18:9-14 & Waebrania 11:24-26.

Tunakumbushwa kuendelea kuikumbuka siku ya Bwana na kuitakasa ili tuwe watu wa Mungu na kuwa na imani nae pasipo kusahau kutokudharau wengine katika maisha yetu yote ya kila siku ya hapa duniani.

Eng. Richard R. Mwambije

21/08/2026

21/08/2026 - IJUMAA.

Mungu Huwainua wanyenyekevu.
Mathayo 15:21-28 & Waebrania 13:17.

Tunakumbushwa kuendelea kumfuata Yesu Kristo huku tukimsujudia na kuwa na imani nae pamoja na kuwatii na kuwanyenyekea viongozi wetu katika maisha yetu yote ya kila siku ya hapa duniani.

Eng. Richard R. Mwambije

20/08/2026

20/08/2026 - ALHAMISI.

Mungu Huwainua wanyenyekevu.
2 Wakorintho 11:7-15 & Matendo ya Mitume 14:14-18.

Tunakumbushwa kuendelea kuhubiri injili ya Mungu yaani kuhubiri habari njema ya kuacha mambo ya ubatili na kugeuka kumwelekea Mungu ili kupata nguvu ya kutokufanya dhambi katika maisha yetu yote ya kila siku ya hapa duniani.

Eng. Richard R. Mwambije

Address

Kinondoni

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Umoja Wa Vijana Kkkt Kinondoni posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Umoja Wa Vijana Kkkt Kinondoni:

Shortcuts

Share