26/02/2026
OLDUPAI (OLDUVAI) GORGE NDO PALIKUA SODOMA NA GOMORA?
Ushahidi wa kuwa Olduvai Gorge au Oldupai ndo Sodoma na Gomora iliyoteketezwa na moto enzi hizo. na nyayo za miguu ya Laitoli ni ushahidi wa Lutu na Familia yake walipokua wakiondoka baada ya miamba kuyeyushwa na Moto.
kwanini ndiyo Sodoma na Gomora?
tuanze na Maandiko
✍🏾BIBLIA INASEMAJE ?
BIBLIA INASEMA NI MJI ULIOKUWA BONDENI NA OLDUVAI NI BONDENI
Mwanzo 19:28 SUV
📖naye akatazama upande wa Sodoma na Gomora na nchi yote ya hilo Bonde, akaona, na tazama, moshi wa nchi ukapanda, k**a moshi wa tanuru.
*******************************
✍🏾Biblia inasema ni Mji unaofanana na Mji uliopo Misri unaoitwa Soari na ukicheki kweli Bonde la Olduvai ndo Bonde pekee lililopo Duniani linalofanana na Soari
Soari kuna Mitende na pia ugunduzi wa mabaki unaonesha pia Olduvai pana mabaki ya Mitende.
✍🏾IMEANDIKWA
Mwa 13:10 SUV
📖Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla BWANA hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa k**a bustani ya BWANA, k**a nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari.
*******************************
👉🏽unaambiwa Kabla ya Sodoma na Gomora kuharibiwa palikua k**a Bustani ya Bwana na palikua na maji , mabaki ya mitende ni ushahidi kuwa palikua na maji maana mitende huota penye maji tu. na Ngorongoro na wanyama ni sehemu iliyobaki pekee Duniani ambapo ndo panafanana na Bustani ya Bwana k**a inavyoelezewa kwenye maandiko Matakatifu kuwa kwenye Bustani ya Bwana wanyama wanaishi na Binadamu.
✍🏾🏛IMEANDIKWA Sodoma na Gomora ulikua ni Mji
Mwanzo 19:4 SUV
📖Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote.
🤯Ugunduzi wa Kisayansi na wa mambo ya kale unasema Olduvai ilikua ni Mji mkubwa sana na mabaki yapo yanathinitisha hilo hadi leo tena mengine yaliunguzwa na ule Moto
✍🏾Imeandikwa
Mwa 19:24 SUV
📖Ndipo BWANA akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa BWANA.
*******************************
🤯Ugunduzi Wa Kisayansi unasemaje ?
Kuhusu 🔥MOTO?
🦶🏼ukienda Oldupai Gorge utakuta kuwa kweli kuna miamba ina moshi na iliunguzwa kwa moto .Wanasayansi na wataalam wa mambo ya kale wanasema paliungua kiasili (Naturally) na k**a ni naturally inamaanisha hakuna mtu aliyeuwasha Moto huo yani Mungu ndo alipaunguza. Fikiria vizuri hapo.
✍🏾Biblia inasema Mke wa Lutu aligeuka Jiwe la Chumvi na ugunduzi unaonesha kuwa Olduvai pana asili ya Chumvi hadi leo.
💀Kingine kikubwa ni Fuvu la mtu wa kale lililogunduliwa hapo Limeungua hii inaonesha wazi kuwa Ni miongoni mwa watu waliounguzwa na Moto wakati ule.
MBALI NA HILO TUNAJUA SODOMA NA GOMORA VIPO KARIBU NA KAANANI NA KAANAN WAPO WANA ISRAEL NA SIFA YA WANAISRAEL NI KUTAHIRIWA
wakazi wanaozunguka Olduvai (Kaanan) ambao ni wamasai /Watanzania Tumetahiriwa k**a Vile Mwenyezi Mungu alivyoagiza
✍🏾Imeandikwa
AGANO LA WANAISRAEL KUTAHIRIWA.
Mpaka sasa Watanzania na waafrika wengine Waisrael tunatahiriwa na ni moja ya ushahidi wa wana Israel .
Mababu zetu wamekua wakitahiriwa tokea enzi za Ibrahim kwa maana babu yetu Ibrahim aliweka agano hilo na Mwenyezi Mungu.
✍🏾Imeandikwa
Mwa 17:10-11 SUV
📖Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi.
TUPO NCHI AMBAYO WANYAMA WANAISHI NA BINADAMU JE? BIBLIA INASEMAJE KUHUSU WANYAMA KUUSHI NA WATU? NA NINI KINATOKEA SASA?
✍🏾IMEANDIKWA
Isaya 11:1-10 SUV
📖Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda. Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA; na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya. Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia. Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani k**a ng’ombe. Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira. Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua BWANA, k**a vile maji yanavyoifunika bahari. Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu.
*********************************
🤔Je unafikiri huyo chipukizi K*toka Nyumba ya Yese ni Yesu ?
HITIMISHO
🙌🏽Sijawahi Kufika Olduvai Gorge ila haya ni mambo ambayo kuna Sauti ipo ndani yangu hunionesha na kunisemesha . Nitaendelea kuwaandikia kwa kadri nitakavyojaaliwa.
ILI USIPITWE,
follow
Mrkilimanjaro Nyumbayamungu
Amani ya Mwenyezi Mungu ikae nanyi Nyote
by Mwal: Imanueli Minja