Ideca J. Ehembwe

Ideca J. Ehembwe Preaching and Teaching the word
Mentorship and Coaching

Siku hizi kila kijana anayechipuka utasikia ni mtume au ni nabii na ukimuuliza sababu alizotumia kujiita mtume ama nabii...
09/05/2026

Siku hizi kila kijana anayechipuka utasikia ni mtume au ni nabii na ukimuuliza sababu alizotumia kujiita mtume ama nabii utasikia ni vile anaweza kuona mambo ya rohoni au utasikia ni vile alivyo na neema ya kuombea watu na wakafunguliwa.

Hii inachekesha sana na kufurahisha sana kwasababu watu wanatamani majina (Titles) ambayo hawajui gharama yake. Acha nikusaidie kitu leo;
1. Kuwa na uwezo wa kiroho wa kuona au kuombea watu haikufanyi kuwa Mtume au nabii kwasababu hizo ni mambo kila mkristo anaweza kufanya k**a ishara ya Imani na roho Mtakatifu ndani yake (Marko 16:17).

2. Kuwa na jina (Title) sio shida lakini kabla ya kuamua kuanza kujiita au kuitwa mtume, nabii, mchungaji, mwinjilisti, mwalimu au Askofu jiulize maswali haya mawili
a. Je, ninaweza kukinywea kikombe cha jina ninalofurahia kuitwa au ninalojiita, nipo tayari kulipa gharama ya jina hili na kwa kiwango gani nishalipia gharama hii (Mathayo 20:20-23)
b. Je, huo ndio wakati sahihi wa wewe kuitwa kwa jina Hilo au umeamua kujipa na kufurahia kuitwa kwa jina Hilo kisa unafikiri linakupa heshima (Mathayo 16:20)

Yesu akiwa mfano halisi kwetu hebu tazama kidogo hapa k**a anavyofafanua ndugu yangu Tr Mgina Jr.

Mwamba (Yesu) alikubali mchakato: mara kadhaa alikuwa akiwakemea watu walio taka ku harakaisha huu mchakato au kumpitisha njia ya mkato.

1. Mathayo 16:20 – Baada ya Petro kumkiri Yesu kuwa Kristo, Yesu aliwaonya wanafunzi wake kwa nguvu wasimwambie mtu yeyote.

2. Marko 1:23-25 – Katika sinagogi, pepo mchafu alimwita "Mtakatifu wa Mungu" na Yesu akamkemea akisema "Nyamaza!"

3. Luka 4:35 – Alimkemea pepo akisema "Nyamaza na umtoke!"
Sio kwamba title ni kitu kibaya, ofcoz we should have title but kwa wakati sahihi, ulio ukusudia Bwana.
_____________

Ushauri wangu;
Usikurupukie vyeo na majina makubwa katika huduma, kuwa Mnyenyekevu kwa Mungu, subiri wakati na zaidi jiandae kwanza kwa vita za jina unaloliendea.

Address

P. O Box 157
Kigoma
47103

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ideca J. Ehembwe posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Ideca J. Ehembwe:

Shortcuts

Share