26/02/2026
S E R V I C E D E C O M U N I C A T I O N/26èCMLC.
MAELEKEZO KUHUSU KUTEKELEZA MFUMO MPYA WA 52 ENVELOPPES.
------------------------
Baada ya kutuma barua yetu ya tarehe 12 Februari 2026 iliyokuwa na shabaa ya kutekeleza azimio ya Halmashauri ya Baraza Kuu 2025 kuhusu mfumo mpya wa sadaka ya 52 enveloppes, tumepokea maulizo na maoni mengi kutoka kwenye Maparokia ambazo zinahunda Mabaraza yetu ya mwaka.
Kulingana na hayo yote, tunawatolea maelekezo yafuatayo kwa kuboresha mfumo huo mpya wa Shirika letu :
1. Mfumo wa 52 enveloppes umekomboa moja kwa moja mfumo wa Hiari ambao ulikuwa ukitumika miaka iliyopita;
2. Sadaka ya 52 enveloppes itakuwa inatolewa na kila mwanamemba wa Parokia anayebatizwa na asiyebatizwa bado. Naye anajiamulia kwa uhuru kiwango (engagement) atakachotoa kila siku ya Mungu kulingana na pato au uweza wake. Mkristo akizuilika siku ya Mungu moja au zaidi bila kuja kanisani, anawajibika kutimiza engagement yake aliyopatana na Mungu wake kwa kutoa. Yaani asikose kutoa hata siku ya Mungu moja;
3. Sadaka ya 52 enveloppes itatolewa kipesa. Mwanamemba akikosa pesa, ana uhuru wa kutoa mifugo, mazao ya shamba, au kitu Cho chote alicho nacho. K**ati ya 52 enveloppes ya Parokia itakadirisha beyi ya kitu kilichotolewa na kuamua kwamba kiwango chake kinafunika matoleo ya siku ya Mungu ngapi ;
4. Ikiwa mwanamemba ana ahidi kutoa kila siku ya Mungu au kila mwezi kitu fulani, matoleo yake yatakubaliwa vile ilivyo pasipo kugawanywa kwa kufunika siku za Mungu zingine au miezi mingine;
5. Kila Parokia itaunda K**ati (Comité) ya watu wasio chini ya 3 na wasiozidi 7, wanaume na wanawake, wakiwemo watu wawili wa K**ati ya Fedha ya Parokia. Kazi ya K**ati hiyo ni :
▫️ Kuhamasisha (sensibiliser) wanamemba ,
▫️ Kutengeneza orodha ya wanamemba ambao wanatoa sadaka hiyo kila siku ya Mungu ,
▫️ Kuhesabu pesa zilizotolewa ndani ya enveloppes na kuandika ndani ya buku lao kiwango kilichotolewa siku ile, wakishirikiana na K**ati ya Fedha ya Parokia,
▫️ Kutoa mashauri kwa wapastori kuhusu kuboresha zaidi mfumo huu,
▫️ Kupanga mishahara (barème salarial) ya wachungaji wakisaidiana na K**ati ya Fedha ya Parokia ,
▫️ Kila mwisho wa mwezi kutayarisha na kusahini PV ya pesa jinsi zilivyoingia, jinsi zilivyogawanywa na kutoa ripoti kwa wapastori.
6. Sadaka ya 52 enveloppes sio pesa za kufanya nazo garama nyingine za kibinafsi au za kanisa, bali ni pesa za kulipa mishahara ya wachungaji wetu ili wafikie kufanya kazi zao vizuri k**a walivyoitwa na Mungu na jinsi wanavyoelekezwa na KITABU CHA MAONGOZI cha Shirika letu;
7. Wachungaji wa Parokia wasingejiruhusu kuamuru lo lote kuhusu mfuko huo kwa K**ati ya 52 enveloppes kinyume na utaratibu wa mfumo wenyewe;
8. Kwenye Ofisi ya Shirika kuna K**ati(Comité) ya 52 enveloppes yenye kufuatilia kindani K**ati za Maparokia ili kuhakikisha kwamba K**ati hizo zinafanya kazi zao vizuri na zinatekeleza vema mfumo huu. Lakini pia ina kazi ya kujua shida au changamoto wanazokumbana nazo na kutoa mwelekeo;
9. Pakiwepo swali juu ya utekelezaji bora wa mfumo huu, ni vema K**ati ya Parokia na wote wahusikao wawasiliane na K**ati ya Ofisi ya Shirika kwa ajili ya kupata maelezo zaidi;
10. Kwa ajili ya kulinda utaratibu mwema, ni K**ati ya Ofisi ya Shirika pekee ndiyo ina jukumu ya kuwasiliana na Askofu kwa maswali yo yote kuhusu mfumo huu;
11. Sadaka ya 52 enveloppes sio pesa za kutuma kwa Jimbo au Baraza la mwaka, apana. Ifikapo kila mwisho wa mwezi K**ati ya kila Parokia ihusikayo na 52 enveloppes itajumuhisha pesa zote ambazo zilizotolewa kwa mwezi mzima na kuzigawa sehemu 4 sawa sawa;
12. Sehemu moja ya nne ( 1/4) itatumwa moja kwa moja kwa Ofisi ya Shirika kupitia namba za wachunga hazina wa Shirika zifuatazo 0975238710 na 0975035524 pasipo kupitia Jimbo wala Baraza. Na sehemu tatu ya nne (3/4) itabaki kwa Parokia kwa ajili ya kulipa mishahara ya wachungaji pasipo kutuma asilimia kwa Jimbo wala Baraza ;
13. Mara tu wanapotuma sehemu ya Shirika (1/4), Parokia itafanya capture d'écran ya pesa walizotuma kwa K**ati ya Shirika ili ifuatilie. Pamoja na hayo Parokia itaripotia kwa Jimbo pesa zilizotumwa kwa Shirika ;
14. Ripoti ya 52 enveloppes itasomwa na K**ati za Fedha ya vikao vya Parokia, Jimbo na Mabaraza ya mwaka;
15. Sadaka ya 52 enveloppes haiji kwa kuvunja sadaka ya KAWAIDA, CHAKUMI wala SHUKRANI. Sadaka hizo zinabaki vile vile na zinagawanywa kwa asilimia zile zile munazotuma kwa Baraza na Jimbo. Kinachoombwa ni kufanya matumizi bora ya sadaka hizo ili kupunguza uwingi wa michango kanisani ;
16. Wachungaji walio kwa ngazi ya Parokia na ambao hawakutumwa na Baraza la mwaka, watatunzwa kwa njia ya mapato mengine ya kawaida ya Parokia;
17. Wa délégués Laïcs wa Mabaraza ya mwaka, na Wakuu viongozi wa LAÏCAT Shirika wahusike sana kwa kufanya uhamasishaji (sensibilisation) na ufuatiliaji(suivi) wa kazi za K**ati za 52 enveloppes kwenye Maparokia yetu na kutoa Ripoti kwa K**ati ya enveloppes ya Shirika.
Imefanyika pa Bukavu, tarehe, 25 Februari 2026.
Katibu Mtendaji wa ECC/26è CMLC
Joseph AFUMBA SAMBO ALIMASI.
Imetangazwa na:
©️ Communicateur wa Ofisi ya Shirika
Clément ABABELE✍🏽