Watson Shija

Watson Shija Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Watson Shija, Kibamba.

11/04/2026

Luka 16:19-31

19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.

20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,

21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.

22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.

23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.

24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.

25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.

26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.

27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,

28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.

29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.

30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini k**a akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.

31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.

📌 Just as we take time to reflect on what our future life will be like, so also take time to reflect on where you will go if you haven't reached it yet.

09/04/2026

Zaburi 146:3-8
3 Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.

4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.

5 Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, Na tumaini lake ni kwa Bwana, Mungu wake,

6 Aliyezifanya mbingu na nchi, Bahari na vitu vyote vilivyomo. Huishika kweli milele,

7 Huwafanyia hukumu walioonewa, Huwapa wenye njaa chakula; Bwana hufungua waliofungwa;

8 Bwana huwafumbua macho waliopofuka; Bwana huwainua walioinama; Bwana huwapenda wenye haki.

Zaburi 118:8-9
8 Ni heri kumkimbilia Bwana Kuliko kuwatumainia wanadamu.

9 Ni heri kumkimbilia Bwana. Kuliko kuwatumainia wakuu.

USIMWAMINI MWANADAMU ASILIMIA 💯 MAAN UPENDO WA MWANADAMU UNA KIKOMO CHAKE BALI UPENDO WA MUNGU HAUNA KIKOMO HAPA DUNIANI NA HATA UKIFIKA MBINGUNI.

JIFUNZE KUMTEGEMEA MUNGU KWENYE NJIA ZAKO, UTAONA MANUFAA YAKE.

It is not a sin to be born poor, but it is a sin to die poor.
27/02/2026

It is not a sin to be born poor, but it is a sin to die poor.

Address

Kibamba
255

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Watson Shija posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share