Efatha YOUTH Champions

Efatha YOUTH Champions Hii ni page maalumu ya vijana washindi katika Kristo Yesu ndani ya kanisa la Efatha dunia nzima.

UMEWAHI KUSIKIA KWAMBA MITUME NA MANABII WAMERUNDIKANA MJINI?INADAIWA WAMERUNDIKANA KWENYE MAJIJI K**A DAR ES SALAAM, MB...
02/04/2024

UMEWAHI KUSIKIA KWAMBA MITUME NA MANABII WAMERUNDIKANA MJINI?

INADAIWA WAMERUNDIKANA KWENYE MAJIJI K**A DAR ES SALAAM, MBEYA, ARUSHA, DODOMA, MWANZA NK

DAR ES SALAAM PEKEE INA WATU ZAIDI YA MILIONI SITA

ILI DAR ES SALAAM WALAU IFIKIWE

INAHITAJI MAKANISA YENYE WATU 1000 WALAU 6000

K**A YATAKUWEPO YA WATU 2000 BASI YANAHITAJIKA WALAU 3000

YAKIWEPO YENYE WATU 5000 YANAHITAJIKA MAKANISA 1200 ILI DAR ES SALAAM IFIKIWE

YAKIWEPO YENYE WATU 10,000 YANAHITAJIKA MAKANISA 600

UNAWEZA KUELEWA MIJI HAIJAFIKIWA KABISA NA WATU WENGI MNO HAWAKO MAKANISANI...

KWA MIJIJI MAKANISA MAKUBWA NI YA WATU 500, 1000, 2000 NA BAADHI YAMEFIKIA 5000,
MAKANISA YA WATU 10,000 YANAHESABIKA MNO...

KAZI KWENYE MIJI NA MAJIJI NI KUBWA MNO BADO...

MIJINI KUNA MATUKIO YA INJILI MENGI NA MATUKIO YA MAKANISA MENGI, LAKINI HAKUNA MAKANISA YA KUTOSHELEZA MIJI...

KAZI NI KUBWA MIJINI,
TUIVUNE MIJI IJE KWA YESU,
WAKATI TUNAPOKOSOA WALIOPO MJINI TUJITAHIDI TUZIJUE NA TAKWIMU ZA MIJI ZILIVYOKAA,

Askofu Dickson Kabigumila
ABC GLOBAL DUNIANI
25.03.2024

UKIRIEeh! Bwana Yesu nataka nguvu itakayo nitengenezea nafasi, nguvu itakayo nifungulia njia, itakayonifanya nifanye jam...
02/04/2024

UKIRI
Eeh! Bwana Yesu nataka nguvu itakayo nitengenezea nafasi, nguvu itakayo nifungulia njia, itakayonifanya nifanye jambo ambalo litafanya maisha yangu yawe bora, Bwana Yesu nataka nguvu ili niweze kuwa na ushuhuda wa matendo yako makuu katika maisha yangu.

TANGAZO:
Kuanzia leo ukapokee nguvu yakukutengenezea nafasi katika maisha yako,

© Efatha Precious Centre Kibaha

2024 ni mwaka wetu wa kumiliki.Ni neno zito kusema namiliki kwa maana umiliki ni hali ya kuwa au kushikilia kitu huku uk...
01/04/2024

2024 ni mwaka wetu wa kumiliki.

Ni neno zito kusema namiliki kwa maana umiliki ni hali ya kuwa au kushikilia kitu huku ukiwa na hati miliki / risiti yenye kuonesha aina ya umiliki ulio nao.

ZABURI 24:1
Ni lazima kwanza tutambue mmiliki wa kwanza wa kila tunachokihitaji au tunachokiona ni Mungu Baba Mwenyewe.
Yaani kwa wewe mwana wa Mungu ili uweze kumiliki ni lazima uwe na uhusiano au patano na Mungu Baba na hapa ukubali:
* Uwe k**a Yeye alivyo (Utakatifu) - Walawi 19:20
Na ili uweze kuwa k**a Yeye ni lazima umpokee Mwanae wa pekee Yesu Kristi nawe uzaliwe mara ya pili YOHANA 1:12, Mtu wa Mungu hauwezi kuwa k**a Mungu ikiwa haupo tayari kuingia katika mlango unaokuruhusu kufanana na Yeye na ni kupitia Yesu Kristo unapata hiyo nafasi ya wewe kuwa k**a Mungu maana alivyo Baba ndivyo alivyo mwana.

Hebu kiri maneno haya siku hii ya leo.....
"Eeh Baba Mungu, Mimi mwanao / binti yako nipo mbele zako, najua sistahili kuingia kwako ila kwa Neema ya Mwanao Yesu Kristo naomba unipokee Baba kwani ninajua mimi ni mkosefu na nisiyestahili kusogea mbele zako ila Baba naomba unirehemu maana dhambi zimenichosha na uovu umenichelewesha nami leo nachukua hatua ya kuja kwako nikiomba Neema yako iliyo kuu na ya ajabu inikubali nawe Baba kupitia Mwanao Yesu Kristo unisamehe dhambi zangu na kufuta maovu yangu na hatia zangu zisikumbukwe mbele zako, jina langu na maisha yangu viandikwe kwa upya katika kitabu cha uzima na mauti isionekane tena kwangu. AMEN"

Baada ya ombi hili naomba uandae siku 3 za kufunga na kuomba ukiitaka Nguvu ya Mungu kwa uweza wa Roho Mtakatifu ikuwezeshe kudumu katika pendo la Mungu Baba.

K**a unaanza maombi haya naomba utujulishe inbox au hapo kwenye comment.

They do this just to watch their favorite sport but when I do the same for Jesus they called me brainwashed.They buy jer...
04/03/2024

They do this just to watch their favorite sport but when I do the same for Jesus they called me brainwashed.

They buy jersey, stickers, key holders of their favorite team but when I buy my church t-shirt, sticker they said I'm being brainwashed.

They buy ticket to watch their favorite team every week forgetting the poor but when I give my offering and tithe to the church,then boom!!! They remember that the poor exist.

They shout,cry,kneel and do all manner of crazy stuffs when they meet their favorite super stars but when I honor my pastor, they say I'm being mentally slaved.

They proclaimed their love for their favorite team and Superstars but when I proclaimed my love for my church and Jesus they called me brainwashed.

They sponsor their favorite team and Superstars but when I sponsor the gospel they vexed and they say my pastor is extorting me to enrich himself.

Dear church, the world will never love you because you're not of it own.

Credit: Emmanuel Omachile Akogun

The time has come for children of God to stand tall and fasting before God our Father.Are you ready .
30/04/2022

The time has come for children of God to stand tall and fasting before God our Father.

Are you ready .

MSINGI WA KUABUDU:Msingi wa ibada yako lazima uanze na kutengwa, Mungu akamwambia Musa “Nenda kwa Farao umwambie awaachi...
03/12/2021

MSINGI WA KUABUDU:

Msingi wa ibada yako lazima uanze na kutengwa, Mungu akamwambia Musa “Nenda kwa Farao umwambie awaachie watu wangu ili waje waniabudu”, Ibada ni lazima iwe mahali ambapo mtesi wako hawezi kuwepo.

Isaya 35:8 “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo. ”

Hii inamaana gani? Hiyo njia ni safari ambayo mtu anaiendea ili kuabudu.
• Ukifika mahali pa kuabudu hautazuiliwa na chochote wala hakuna wa kukusumbua.

• Mwabuduo hajipiganii bali kuna anayempigania.

• Mwabuduo akiwa mahali analeta pumziko.

Yeyote anayekwenda kuabudu hawezi kupotea wala hawezi kuacha kumwabudu Mungu kwa sababu ya kitu, ambaye si mwabudu anapokwenda kanisani na akasikia watu wanamsema harudi tena kanisani, waabuduo hata uwasengenye na kuwasema kiasi gani kamwe hawarudi nyuma.

Mtu yeyote akishafika ibadani anakuwa na raha ya ajabu, tamani kuwa mahali pa ibada.

Isaya 35:9-10 “Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo. Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.”

Waabuduo ndio watu pekee walio na furaha juu ya vichwa vyao na sio moyoni mwao.
Upumbavu upo kwenye akili, akili ikiwa na uerevu, ufahamu, maarifa na hekima hicho ndicho kinaitwa kicheko, kwa maana mwenye hekima hauwezi kumdanganya chochote kwa sababu ana ufahamu. Waabuduo wana ukamilifu katika akili zao kwa sababu hiyo wanaijua jana yao, leo na hata kesho yao hivyo hawawezi kupotea.

MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA - KANISA LA EFATHA.

Pendo la Mungu litawalapo hufungulia Maongezeko na kuzidishwa.Karibu kwenye whatsapp group lenye lengo la kuinua viwango...
17/08/2021

Pendo la Mungu litawalapo hufungulia Maongezeko na kuzidishwa.

Karibu kwenye whatsapp group lenye lengo la kuinua viwango vya kiroho, kukumbushana ahadi za Mungu na kushauriana.

Neema ya Mungu izidi kuwa nawe.

WhatsApp Group Invite

06/08/2021
31/05/2021


Bwana Yesu asifiwe wateule.

Mara nyingi huwa tunakuwa na shauku ya kuona matokeo chanya baada ya kutoka kwenye mifungo mbalimbali ambayo watu wa Mungu huwa tunafunga.

Leo naomba nikukumbushe jambo la muhimu linalotokea pale tu unapomaliza mfungo wako wa maombi na inahitaji nguvu ya kiroho kushughulikia hayo utakayoyaona.

1. Kujaribiwa
Mara baada ya wewe kutoka kwenye mfungo utakutana na mjaribu mlangoni akikusudia kukuangusha ili upoteze uelekeo wa kile umepokea kutoka kwenye mfungo huo.

LUKA 4:1-2
Hapa kuna jambo au mambo ya kuzingatia kuwa yaani anamaanisha kuwa mara baada ya siku za kufunga kwake Bwana Yesu kutimia ndipo mjaribu alijitokeza.
Kumbe katikati ya kufunga kwako, katikati ya wewe kujimimina mbele za Mungu adui huwa hana nafasi bali hutamani sana na husubiria sana siku utakayotoka kwenye huo mfungo au kwenye hicho chanzo chako cha kiroho ndipo aje kukujaribu yaani adui husubiria hadi pale wewe utakapojinasua kutoka kwenye chanzo chako cha nguvu ndipo hapo hapo huibuka na kukushawishi uzisaliti ahadi zote ulizopokea toka kwenye huo mfungo wako.

Atakujaribu vipi?
A. Kwa kukushawishiwi
Atatumia yale usiyokuwa nayo ili akupate na kukuangusha yaani hutumia mahitaji yako ili kukuangusha hivyo yakupasa kushiba Neno ili uweze kumshinda.

Aina za ushawishi:
- ushawishi wa kifedha na fursa
- ushawishi wa kihisia na mahusiano
- ushawishi wa vitu vya kutamanika na hali ya kimaisha n.k

Kumaliza kwako mfungo kuwe ni mwanzo mpya wa kuyashinda mazingira na changamoto zilizokuwa zinakusumbua.

MWANZO 4:7
ISAYA 60:1

Na Mtumishi wa Mungu Mchungaji Joyce Itebuka

You're all welcome.....
01/05/2021

You're all welcome.....

meaning of Fasting.
01/05/2021

meaning of Fasting.

Hatua za Mfungo.1. Kuweka nia ya kufunga (dhamira thabiti ya kufunga na nia ya kujidhiri)2. Kuweka malengo ndani ya mfun...
01/05/2021

Hatua za Mfungo.
1. Kuweka nia ya kufunga (dhamira thabiti ya kufunga na nia ya kujidhiri)

2. Kuweka malengo ndani ya mfungo.
(Malengo ya kiroho, kiuchumi, kimahusiano n.k)

3. Utakaso na toba
Weka ratiba ya kujitakasa walau siku 3 au 5 au 7 ila itapendeza ukitumia siku 7 kwani unakuwa ndani ya ukamilifu.

4. Shukurani
Tumia siku 3 hadi 7 kumshukuru Mungu kwa yote aliyokutendea maishani mwako haswa kwa mwaka uliopita.
Namba 3 na 7 ni namba zenye nguvu ya kiroho.

5. Sadaka
Hakikisha unakuwa na sadaka ya kusogeza mbele za Mungu kila wiki au kila unaposogeza maombi yako mbele za Bwana.

*KUMBUKA*
Unapoingia kwenye kuomba ombi lolote hakikisha unaomba kwa kumaanisha na hadi uone umeutua mzigo uliokuwa nao (omba kwa mzigo).

Nakupenda na nakutakia mafanikio katika mfungo huu.

Address

Kibaha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha YOUTH Champions posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share