The Truth Sets Free church - Kibaha

The Truth Sets Free church - Kibaha Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from The Truth Sets Free church - Kibaha, Religious organisation, Kibaha.

Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali weny...
20/04/2025

Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.

Tukiwa tunaendelea katika kujenga nyumba ya Bwana tawi la Kibaha- Pwani kanisa la The Truth Sets Free Church, Tunazidi k...
11/03/2025

Tukiwa tunaendelea katika kujenga nyumba ya Bwana tawi la Kibaha- Pwani kanisa la The Truth Sets Free Church, Tunazidi kumtukuza Mungu ambaye anatuwezesha na kutufanikisha katika hili

Kutoka 35:20-21
[20]Basi mkutano wote wa wana wa Israeli wakaondoka hapo mbele ya Musa.

[21]Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa BWANA, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu.

19/01/2025

Wewe ni Mungu wa wote wenye mwili hakuna jambo usiloliweza

Yeremia 29:11Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi t...
01/01/2025

Yeremia 29:11
Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

30/09/2024

Unahitaji neema na kibali kutoka kwa Mungu
Pastor Rehema Maro

DALILI ZA MTU ALIYE NA LAANANa mch. Rehema Maro Laana ni hali au nguvu fulani inayomsukuma mtu na kumpelekea kushindwa k...
09/07/2024

DALILI ZA MTU ALIYE NA LAANA
Na mch. Rehema Maro

Laana ni hali au nguvu fulani inayomsukuma mtu na kumpelekea kushindwa katika mambo au maeneo mbalimbali licha ya kuweka juhudi au jitihada nyingi.

Kutegemeana na aina ya laana iliyopo kwenye ukoo unaotokea
Kwa mfano laana ya magongwa, laana ya umaskini, laana ya kukataliwa, laana za uzinzi, upagani, ushirikina, n. K

Watu wengi hawajui chanzo cha hayo matatizo

Maombolezo 5:7
[7]Baba zetu walitenda dhambi hata hawako;
Na sisi tumeyachukua maovu yao.

DALILI ZA MTU MWENYE LAANA
1. Kotofanikiwa kwenye kila kitu na kila uendako Kumb 28;1-14,16

2.Kila upatacho huisha na kupotea bila kutosheleza. Na akiba ya vitu haikai
Hagai 1;6

3.Uzao wako haufanikiwi yaani mifugo, mashamba, watoto wako na kila kitu
Kumb 28;18

4. Kutojiamini kwenye kila unachofanya Mithali 28:1

5. Magonjwa yasiyoisha kwa mtu Kumb 28;22

6. Kila alichokitegemea kiwe msaada kwake hakimsaidii. Laana huondoa tumaini la maisha na unachokitegemea
Kumb 28;23, 28;51

7.Kuwa mtu wa kushindwa na kuonewa, unapigwa na adui zako Kumb 28;25

8.kukataliwa hata baada ya kufa Kumb 28;26

9.Kukosa mwelekeo wa maisha siku zote Kumb 28;28-29

10. Kila upatapo kitu unanyang'anywa Kumb 28:31-33

11. Kuwa mtumwa kwa kila umuonaye mbele yako Kumb 28;36,48

12.Kudharaulika na watu wote Kumb 28:27

13.Kutopiga hatua yoyote kimaisha. Hali hii inamfuata mtu bila hata yeye kujua Kumb 28; 43-44

14. Familia kupungukiwa na mema
15. Mateso yanayo jirudiarudia Kumb28;67
16. Tabia fulani fulani zisizofaa mfano ulevi, uzinzi,ukahaba,nk
17.Kupoteza uwezo fulani ambao ulikuwa nao Kumb 28;37
18.Vifo vya mapema ndani ya familia au ukoo
19.Vifo vya ghafla visivyoeleweka vizuri kumb 28:67
20.Magonjwa ya akili na kuchanganyikiwa
21.Vifo vya kujinyonga au kunywa sumu
22. Kutokuolewa au kuoa
23.kutokusona au kukosa elimu
24.kupata au kunusurika ajali za mara kwa mara
25.Umaskini mkubwa (kutokuwa na chochote)
26.Kesi za mara kwa mara, kusingiziwa na hali ya madeni yasiyoisha Kumb 28;44
27. Hali ya watu kupotea na kutokujulikana waliko kwenye ukoo
28. Mimba kuharibika mara kwa mara
29.Kufa kwa watoto baada ya kuzaliwa
30. Mtu kutoona kutoka kwenye mkwamo wa maisha anaopitia
31. Akienda kwa wataalamu wa afya wanamwambia hawaoni chochote, wakati huo yeye anapata shida.

09/07/2024

Praise session

26/06/2024
27/05/2024

Kuwa mwangalifu sana na mawazo unayowaza, maana unapowaza sana mambo yasiyo na manufaa kwenye maisha yako hayo ndio huwa matendo yako. Jifunze kudhibiti vitu unavyowaza, usiruhusu mawazo mabaya kwenye ajili yako.

Kuwa mwangalifu na vitu unavyotazama, maana kila kitu unachotazama kina roho nyuma yake. Wengine wanapokea roho za uzinzi kutoka kwenye mitandao kwa kutazama picha za ngono.

Ukihitaji kufika mbali katika maono yako usitazame kila kitu na usiruhusu mawazo hasi au mawazo yasiyoendana na neno la Mungu .
Pastor Rehema Maro

Address

Kibaha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Truth Sets Free church - Kibaha posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share