18/11/2022
NGUVU YA SADAKA INAYOTOLEWA KWA MAELEKEZO YA MUNGU
Bwana Yesu Kristo Asifiwe sana.
Leo imempendeza Mungu tena tujifunze kwa habari ya sadaka ama matoleo yanayolewa kwa maelekezo ya Mungu.
Utaratibu wa kupokea ni kutoa kwanza, yaani wewe uwe wa kwanza kutoa. Unapotoa kwa mwanadamu mwenzako ama Mungu, unatengeneza nafasi ya wewe kupokea.
Luka 6:38
38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
Kumbuka hakuna mwanadamu ambaye aliwahi kutoa sadaka kubwa akamzidi Mungu, Mungu ndo Mwanzilishi wa kutoa na ndio Mtoaji Mkubwa( Jehovah-Jireh). Mungu alitoa kipi? Alimtoa Mwana wake wa Pekee kwa Upendo kabisa( Yohana 3:16). So, tambua unapotoa unaonyesha upendo kwa Mungu kwani Mungu ni Pendo.
Sasa yamkini kuna jambo ama mambo kadha wa kadha unatamani ama umekuwa ukimwomba Mungu akumilikishe( akurithishe), na hujajua kwa nini mpaka leo bado hujayapokea/hujayamiliki/hujayarithi na kuwa yako.
Mwanzo 15::
7 Kisha akamwambia, Mimi ni Bwana, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uirithi.
8 Akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitairithi
9 Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu, na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wa miaka mitatu, na hua, na mwana njiwa.
10 Akampatia hao wote, akawapasua vipande viwili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuwapasua.
11 Hata tai walipotua juu ya mizoga Abramu akawafukuza
Mungu alimtaka Ibrahim atoe SADAKA YA AGANO ili kuirithi hiyo nchi aliyoambiwa. Kuna mambo Mungu hawezi kuyafanya kwako ikiwa hujaugusa moyo wake. Sulemani alipogusa Moyo wa Mungu, Mungu alimwendea usiku katika ndoto na akamwambia aombe chochote atakacho na atampa. Ili Ibrahim airithi nchi, alitakiwa kutoa sadaka.
Sasa, utajuaje kuwa Mungu anataka utoe sadaka juu ya jambo fulani ndipo upokee muujiza wako ama utajuaje Mungu anataka utoe SADAKA YA AGANO? Njia rahisi na nyepesi Mungu anayoitumiaga ni MSUKUMO WA MOYO TOKA NDANI. Biblia inasema AMANI ya Mungu iamue mioyoni mwenu. K**a ni Mungu anakusemesha juu ya jambo tokea moyoni, utajihisi kuwa na amani.
Wako watu wengi Mungu aliwasemesha kwa habari ya kusapoti ujenzi wa huduma/makanisa na hawakufanya hivyo; wako watu wengi Mungu aliwasemesha kwa habari ya kusimama na kuombea watumishi wa Mungu na hawataki kufanya hivyo; na kadhalika na kadhalika. So, kwa kutokufanya hivyo, wamejikuta mipango yao, maisha yao, malengo yao hayatimii wala kufanikiwa. Kwa nini? Kwa sababu walikataa KUTII SAUTI YA MUNGU.
Sasa kuna wengine huwa wanasikia sauti ya Mungu na kuelewa kile ambacho Mungu anawataka wafanye, ila shetani anainuka, anawak**ata moyo na hatimaye wanashindwa kutimiza kile Mungu alichowasemesha. Tunaona katika mstari wa 11, tai wanatoa kwenye hiyo sadaka Abram aliyomwandalia Mungu kabla ya kupokelewa/kukubaliwa na Mungu na hivyo, Ibrahim anawafukuza hawo tai na anabaki kuilinda sadaka yake mpaka Mungu aipokee. Je, unajua kuwa nguvu ya giza huwa zinaibuka na kutaka kuzuia usimtolee Mungu wako SADAKA aliyokusemesha ili usije ukapokea baraka zako, muujiza wako, urithi wako?? Je, huwa unang'ang'ana kuhakikisha kuwa nguvu za giza hazikuzuii kumtolea Mungu wako na unatoa sadaka kamili aliyokuagiza Mungu??
Kila baraka ya Mungu ina kanuni yake. So, tujifunze kuwa watii na kusikiliza sauti ya Mungu ili tupate kufanikiwa kiroho na kimwili pia.
Mungu anapenda tuwe wasikivu na watii. Mungu anayo mengi ya kututendea ila kuwa wakati sisi wenyewe tunam-limit( tunamwekea mpaka) japo Yeye anatamani kufanya zaidi na kwa ukubwa.
Mungu awabariki na kuwalinda In Jesus Mighty Name
By Elisha!!