06/11/2024
*SOMO: K**A YEYE ALIVYO ~ 6/11/2024*
📖📖*1 Yohane 4:17 BHND*
*…………..kwani maisha yetu hapa duniani ni k**a yale ya Kristo*
TAFAKARI 👇
Inaweza Kukustaajabisha Unaposikia Maisha Yetu Ni Sawa Na Maisha Ya Bwana Yesu Alipokuwa Dunia. Unaweza Jiuliza Ni Kwa Namna Gani Hili Linawezekana Au Linatendeka? Lakini Hii Isikupe Mashaka, Huo Ndio Uhalisia, Aina Ya Maisha Aliokuwa Nayo Bwana Yesu, Yenye Sifa Ya Utawala Mkamilifu Na Uzoefu Wa Ushindi Dhidi Ya Kila Hali, Ndio Aina Ya Maisha Tuliopewa Na Tunayopaswa Kuishi K**a Watoto Wa Mungu; Bwana Yesu Alitamka Maneno Haya Wakati Wa Sala Yake Kwa Mungu Kwaajili Ya Watu Wote, Alisema; {*Yohana 17:22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja k**a sisi tulivyo umoja*} Tunayo Aina Moja Na Maisha Na Kristo, Asili Kamili Sawa Nae Ipo Ndani Yetu, Maisha Yetu Yanasifa Ya Ushindi, Ukuu, Ubora, Mafanikio, Utoshelevu, K**a Yeye Kristo Yesu, Alivyo!
MAOMBI 🙏
Asante Baba Kwaajili Ya Maisha Ya Bwana Yesu Kristo, Asante Kwa Kunipatia Asili Moja Nae. Naishi Katika Ubora Na Uweza Mkuu Sana Sawa Nae. Nikipokea Matokeo Yenye Uzoefu Sawa Kristo, Ambayo Ni Matokeo Ya Ushindi Na Ustawi Siku Zote, Katika Jina La Bwana Yesu, Amen!
Please Follow
Twitter :
Insta : &
Whatsapp : https://chat.whatsapp.com/Fd5pMyi0P9J7WvDnQ3hXCZ
Facebook : Word For All Nations Int’l Ministry
MINISTER HERY INOCENT
0620141375