Kanisa la utimilifu

Kanisa la utimilifu JIFUNZE BIBLIA KWA NJIA YA VIDEO:0713724066

24/01/2022

Mwanangu sikia hekima ya baba yako ukaishi.✍️

Mwanangu.Hunipendi kwakuwa umesimuliwa mabaya yangu kiufundi kupitia kwa mama yako, ila unampenda mama yako kwakuwa niliamua kuyaficha mabaya yake.. njoo uniombe radhi.

Mwanangu. usijisifu kwamba wewe ni mti wenye matunda ndio maana unapigwa mawe... kunamiti mingine ina nyoka..Huenda wewe ni mfalme/Malkia mwenye mkia.... jichunguze.. Kisha chukua hatua... yakuukata.

Mwanangu. ukiwa na marafiki 9 Malaya ama majambazi, tegemea wewe kuwa wa kumi, kwani ndege wafananao huruka pamoja.

Mwanangu ikiwa kimvulichako chenyewe kinakusaliti giza likiingia...vivyo hivyo usiiwaamini hao wanaosema tupo nyuma yako unaweza kugeuga ukiwa umefilisika usiwaone... mweshimu Mkeo/Mumeo na wazazi... hawa hatamgombane kilasiku hawapo tayari kukuona unanyanyaswa ama kuteseka.

Mwanangu. JIFUNZE kuwa mnyenyekevu kwa mumeo/Mkeo na kwa Muumba wako. kwani ndicho kiwango cha juu cha matumizi ya akili.. kamwe usijikombe kwa mtu, asije kukununua kwa fedha ukafadhaika utakapo mzidi.

Mwanangu.Wakikufungia mlango pitia hata dirishani...hakikisha unatimiza malengo yako hatak**a itakulazimu kubaki pekeyako,ilimradi umuasi MUNGU

Mwanangu.mla! mla! leo.mlajana kala nini....sio sabuni useme itaisha...hata kijiko cha hoteli huoshwa..k**a upawa ukapika ukapakuliwa...JIFUNZE kupuuza yaumizayo moyo...nakuyadharau.kwa kuitazama kesho iliyo mpya.

Mwanangu.kamwe usikubali kuufanya mwili wako kuwa choo cha stand...kila mtu aingie..kwa sababu ya kulipiza kisasi. juu ya mumeo/Mkeo.

Mwanangu.kuanza upya sio ujinga...hatak**a umeshafika mbali kiasi gani...k**a umegundua ukifanyacho sio sahihi...Rudi omba radhi kwa wanadamu na Muumba wako...kuliko kuendelea upotee kabisa.

Mwanangu.usiutizame umri wako ukadhani huwezi kushindana nao...wewe pambana ukifanikiwa watakuja kuyabusu mashavu yako hata k**a yatakuwa yamedondoka.

Mwanangu.kamwe usihukumu mtu wa kwenu hususani Mumeo/Mkeo..kwa maneno ya kuambiwa, wengine hawapendi kuona hapo mlipo fikia...nawengine huamini kuwa karibu na wewe kupitia habari hizo aweze kunufaika na wewe pasipo wewe kujua.
Ningekuwa mjukuu wa Nabii Selemani wa kitabu cha MITHALI .ningekuandikia zaidi..ila Mimi ni mjukuu wa Mkulima naomba niishie hapa.(imerekebishwa kutoka maali)
Wewe nyundo sio kila kosa ni msumari.

Mtendakazi.Manase Rhite.0713-724066✍️

KANISA LA UTIMILIFU
20/05/2020

KANISA LA UTIMILIFU

Address

Keko Chini
0703

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kanisa la utimilifu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Kanisa la utimilifu:

Share