08/09/2024
IBADA YA LEO JUMAPILI TAREHE 08/09/2024
SOMO: JIFUNZE KUTHAMINI KILE AMBACHO MUNGU AMEKUPA
Utakapothamini kile ambacho MUNGU amekupa ndipo utakapopata matokeo/matunda mazuri.
Uaminifu wa mtu kwa MUNGU unapimwa katika kile MUNGU amempa, MUNGU anaangalia
unafanya nini katika kile alichokupa na unakitendeaje kazi.
Ukiwa mwaminifu utaona faida ya kutunza na kuthamini kile ulichopewa
Waebrania 2:3
[3]sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na
Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;
©️ John Ignas Sanga Mchungaji Efatha Church Kasulu