Efatha Church Karatu

Efatha Church Karatu Kanisa la ukombozi na uponyaji kwa Damu ya Yesu

28/02/2022

NAIBARIKI JUMATATU YANGU.

Maana BWANA ameiruhusu niyaone Matunda yake.

31/12/2021

HAPPY NEW YEAR 2022 - THE YEAR OF JUBILEE

NAIBARIKI ALHAMISI YANGU.Mwanangu, FURAHA ya Moyo, AMANI ya Moyo, KICHEKO cha Moyo, UZIMA wa Moyo, BARAKA za Moyo zinapa...
02/12/2021

NAIBARIKI ALHAMISI YANGU.

Mwanangu, FURAHA ya Moyo, AMANI ya Moyo, KICHEKO cha Moyo, UZIMA wa Moyo, BARAKA za Moyo zinapatikana katika KRISTO YESU.

Acha MASHANGILIO na FURAHA vikawe na Wewe katika KRISTO YESU Aliye BWANA na MWOKOZI wa Maisha yako.

Alhamisi yako IMEBARIKIWA NA BWANA.

NAIBARIKI ALHAMISI YANGU.Wanangu, UTII wako, KUJITOA Kwako, UAMINIFU wako utakufanya uwe wa Thamani na kukupelekea kuwa ...
04/11/2021

NAIBARIKI ALHAMISI YANGU.

Wanangu, UTII wako, KUJITOA Kwako, UAMINIFU wako utakufanya uwe wa Thamani na kukupelekea kuwa MTU MKUU.

NAIBARIKI JUMATANO YANGU.Wanangu 'Elewa WITO WAKO MKUU Ulioitiwa, Wewe UMECHAGULIWA, Wewe ni wa KUMILIKI na KUTAWALA, We...
03/11/2021

NAIBARIKI JUMATANO YANGU.

Wanangu 'Elewa WITO WAKO MKUU Ulioitiwa, Wewe UMECHAGULIWA, Wewe ni wa KUMILIKI na KUTAWALA, Wewe ni MWANA wa MUNGU, Wewe ni MTAKATIFU unayempendeza MUNGU 'BABA' hapa Duniani, hivyo popote ulipo, Afrika, Ulaya, Amerika, Asia,.......... popote ISHI kwa KUJIELEWA WEWE NI NANI.

Jumatano yako IMEBARIKIWA.

MUNGU ANAITAMBUA FAMILIA NA ANAPENDA UMOJA.Tunasoma katika KUTOKA 24: 1 kuwa, "BWANA alimwambia Musa, akwee na Haruni, N...
29/10/2021

MUNGU ANAITAMBUA FAMILIA NA ANAPENDA UMOJA.

Tunasoma katika KUTOKA 24: 1 kuwa, "BWANA alimwambia Musa, akwee na Haruni, Nadabu na Abihu na watu sabini wa wazee wa Israeli".

Mungu anatambua familia na anapenda Umoja. Alipomtuma Musa kwa Farao alimpa Haruni ndugu yake awe mkalimani wake kwa kuwa alikuwa na kigugumizi hawezi kuongea vizuri. Wakati wa kutoa amri kumi Mungu alimwambia Musa akwee mlimani na baadhi ya hawa ndugu zake hadi hatua fulani. Alifanya hivyo kwa sababu alitaka pasiwepo na mtu asiyekuwa sehemu ya kile wanachokwenda kufanya akasababisha uharibifu.

Umoja wa familia ni jambo la msingi sana unapotaka kumshinda kwa wepesi adui anayesumbua ndani ya familia. Hivyo basi, unapaswa kufahamu mnyororo wa kizazi chenu ukianzia na ndugu wa kuzaliwa na kisha familia yote. Umoja unapokosekana ndani ya familia inakuwa vigumu kupata ushindi kwa wepesi kwa kuwa ni wanafamilia wenyewe watakaoanzisha vikwazo vitakavyoleta uharibifu.

Kwa mfano; Unapooa au kuolewa unapaswa kuwa makini sana kuhakikisha mahari inapotolewa kila anayestahili anapata sehemu yake. Mtu akinyimwa anaweza kutamka maneno yatakayosababisha uharibifu kwenye hiyo ndoa.

MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA - KANISA LA EFATHA.

NAIBARIKI IJUMAA YANGU.Maisha ya TOBA ni Maisha ya USHINDI, ni Maisha ya KUSONGA MBELE, ni Maisha ya kukupeleka katika U...
29/10/2021

NAIBARIKI IJUMAA YANGU.

Maisha ya TOBA ni Maisha ya USHINDI, ni Maisha ya KUSONGA MBELE, ni Maisha ya kukupeleka katika UWEPO wa MUNGU BABA yetu, ni Maisha ya AMANI, ni Maisha ya FURAHA, ni Maisha ya UTAKATIFU.

NAIBARIKI ALHAMISI YANGU.Kupitia maneno ya Kinywa changu, sitampa ibilisi nafasi hata kidogo Siku ya leo. Najitamkia BAR...
28/10/2021

NAIBARIKI ALHAMISI YANGU.

Kupitia maneno ya Kinywa changu, sitampa ibilisi nafasi hata kidogo Siku ya leo. Najitamkia BARAKA, AMANI na USHINDI katika Siku yangu, Amen.

NAIBARIKI JUMANNE YANGU.Mwanangu, ukiwa ndani ya PENDO la MUNGU unapata Ufahamu wa Wewe ni nani na wapi umetoka lakini u...
15/06/2021

NAIBARIKI JUMANNE YANGU.

Mwanangu, ukiwa ndani ya PENDO la MUNGU unapata Ufahamu wa Wewe ni nani na wapi umetoka lakini usipokuwa ndani ya PENDO LAKE kamwe hauwezi kujua hayo.

Mwanangu JUMAMOSI YAKO IMEBARIKIWA NA BWANA.Nguvu ya MUNGU ni ya Pekee, Hakika, Kweli na Msaada.Nguvu ya MUNGU isikutoke...
05/06/2021

Mwanangu JUMAMOSI YAKO IMEBARIKIWA NA BWANA.

Nguvu ya MUNGU ni ya Pekee, Hakika, Kweli na Msaada.

Nguvu ya MUNGU isikutoke katika Maisha yako.

Mwanangu ALHAMISI YAKO IMEBARIKIWA NA BWANA.Mbele za Uso wa BWANA kuna Furaha tele na katika Mkono wake wa KUUME mna Mem...
03/06/2021

Mwanangu ALHAMISI YAKO IMEBARIKIWA NA BWANA.

Mbele za Uso wa BWANA kuna Furaha tele na katika Mkono wake wa KUUME mna Mema ya Milele.

Uwepo wa BWANA usitoke Mbele zako.

Mwanangu JUMATANO YAKO IMEBARIKIWA NA BWANA.Uliumbwa ili Vitu vikutumikie na sio Wewe kuvitumikia.
02/06/2021

Mwanangu JUMATANO YAKO IMEBARIKIWA NA BWANA.

Uliumbwa ili Vitu vikutumikie na sio Wewe kuvitumikia.

Address

Karatu

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church Karatu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Efatha Church Karatu:

Share