Efatha Church Kahama

Efatha Church Kahama we bring the world to JESUS WE BRING THE WORLD TO JESUS

07/09/2026
IBADA YA JUMAPILI TAREHE 06/09/2026SOMO: ENENDA KWA HEKIMA NA UTAMBUE SAFARI YAKO.Usiishi kwa mwili wakati umeitwa kuish...
06/09/2026

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 06/09/2026

SOMO: ENENDA KWA HEKIMA NA UTAMBUE SAFARI YAKO.

Usiishi kwa mwili wakati umeitwa kuishi kwa Roho. Usitumie karama bila hekima. Usifikiri umefika; endelea kukua. Hekima itakusaidia kuenenda sawasawa, maarifa yatakusaidia kutekeleza unachofundishwa, na ukomavu utakusaidia kumaliza safari yako vizuri.

Waefeso 5:15 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si k**a watu wasio na hekima bali k**a watu wenye hekima.”

Mtu aliyeokoka anapaswa kukua na kukomaa kiroho. Wengi wanachelewa kukua kwa sababu hawajatambua majukumu yao katika Kristo. Ili kutambua mambo ya rohoni, lazima uwe mtu wa rohoni.

Hekima hukusaidia kuenenda kwa usahihi, kujibu ipasavyo na kushughulikia mambo ya mwilini bila kuanguka. Maarifa hukupa uwezo wa kuelewa maelekezo na kuyafanyia kazi.

Wafilipi 3:12 "Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu."

Paulo alitambua kwamba bado alikuwa katika safari. Vivyo hivyo, usifikiri umefika kwa sababu umeokoka au umetumika kwa muda mrefu. Endelea kukua, kujifunza na kuchuchumilia mpaka mwisho.

Karama ni zawadi Mungu anaweka ndani ya mtu, lakini ikitumika bila hekima inaweza kuvuruga utaratibu na kuleta madhara. Si kila kitu unachoweza kufanya ndicho unachopaswa kufanya kila wakati. Karama inahitaji tabia, hekima na utii.

Mtu anayezira kila mara anahitaji kusaidiwa kukua katika tabia. Hata katika ndoa, mwanaume au mwanamke anayezira kila anapoonywa au kuambiwa wajibu wake anahitaji kujengwa. Ukomavu ni uwezo wa kusikia, kujifunza, kurekebika na kuendelea.

©Mchungaji Simon

MATOLEOMalaki 3:10  “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu; mkanijaribu kwa njia hiyo, asem...
06/09/2026

MATOLEO

Malaki 3:10 “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu; mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue k**a sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.”

Mathayo 18:20 “Kwa maana walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”
06/09/2026

Mathayo 18:20 “Kwa maana walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”

06/09/2026

MAOMBI KATIKA IBADA YA JUMAPILI 06/09/2026

Waefeso 5:25 “Enyi waume, wapendeni wake zenu, k**a Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake.”Kuwa mume...
06/09/2026

Waefeso 5:25 “Enyi waume, wapendeni wake zenu, k**a Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake.”

Kuwa mume si kuwa mtawala wa nyumba kwa mabavu, bali ni kuwa kiongozi mwenye upendo, anayewajibika, anayelinda na kujitoa kwa ajili ya familia yake. Mume anapaswa ampende mke wake. Upendo wa mume unatakiwa uwe k**a wa Kristo kwa Kanisa—upendo wa kujitoa.

Mume hapaswi kumpenda mke wake kwa maneno pekee, bali kwa: Kumjali, Kumheshimu, Kumsikiliza, Kumsaidia, Kumthamini, Kusimama naye wakati wa shida, Upendo wa kweli unaonekana katika matendo.

SOMO: WAZALIWA WA MWEZI WA TISA.Waefeso 5:14-17 “Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atak...
02/09/2026

SOMO: WAZALIWA WA MWEZI WA TISA.

Waefeso 5:14-17 “Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza. Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si k**a watu wasio na hekima bali k**a watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.”

Watu waliozaliwa mwezi wa Tisa ni Fungu la Kumi kwa maana hakuna watu wenye maumivu k**a wao. Watu hawa ni wahesabu makosa kuliko wengine, matokeo yake wanajikuta wanahangaikia mambo ya ulimwengu huu ambayo hawawezi kuyatatua kuliko kushughulikia yale ambayo ni ya faida kwao. Amua kutoka huko.

Pamoja na machungu yao watu hawa wanampenda Mungu sana. Wanakasirika haraka sana lakini wakimuona mtu ambaye amewaudhi anapitia matatizo wanasamehe yale waliyotendewa na kuanza kumsaidia kwa sababu wana kiu ya Mbinguni.

K**a wewe ni mzaliwa wa Mwezi wa Tisa usiumie mtu anapokuumiza, msamehe bure.

Faraja yao ipo katika; Yeremia 29:11 “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”

Ili ufikie hayo mawazo ya Mungu ambayo ni Mema, lazima jifunze kwa Bidii; Ayubu 22:21 “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.”

Mwana wa Mungu hakikisha unafanya na kusema kile Neno linasema maana ndivyo utakavyostawi na kukomesha maumivu unayopitia.

NAIBARIKI JUMATANO YANGU. Mimi ni Hodari, katika BWANA Mimi ninazo Nguvu na katika yeye Mimi ni namiliki na kutawala na ...
02/09/2026

NAIBARIKI JUMATANO YANGU.

Mimi ni Hodari, katika BWANA Mimi ninazo Nguvu na katika yeye Mimi ni namiliki na kutawala na hakuna cha kunishinda.

YESU ni Mzuri.

Septemba ni mwezi wa neema, kibali na ushindi. Nitaingia katika mambo mapya ambayo Bwana ameniandalia. Kila mlango uliof...
01/09/2026

Septemba ni mwezi wa neema, kibali na ushindi. Nitaingia katika mambo mapya ambayo Bwana ameniandalia. Kila mlango uliofungwa utafunguliwa kwa wakati wake, na kila kilichochelewa kitaanza kusonga. Sitatawaliwa na hofu, kwa maana Bwana yuko pamoja nami.

Isaya 43:19 “Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! hamtalijua?”

UKIRI WA SIKU. NAIBARIKI JUMATATU YANGU. Mimi nakula NENO, Mimi natafakari NENO, Mimi natamka NENO; Mimi ni Hodari, Mimi...
31/08/2026

UKIRI WA SIKU.

NAIBARIKI JUMATATU YANGU.

Mimi nakula NENO, Mimi natafakari NENO, Mimi natamka NENO; Mimi ni Hodari, Mimi ni Mshindi, Mimi ni Kichwa.

Asante YESU, WEWE ni Mzuri BWANA.

Address

Kahama
717903744

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church Kahama posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Efatha Church Kahama:

Shortcuts

Share