Kijana wa Nuru

Kijana wa Nuru This page is purposely to convey the true gospel of Christ the Truth and life. The light of the world

  WATU WAZURI MNAO PENDA SANA KUTUMIA MTANDAO WA FACEBOOK KWANI MTANDAONI WA FACEBOOK HAUNA SHINDA YEYOTE ILA SHINDA INA...
07/04/2024



WATU WAZURI MNAO PENDA SANA KUTUMIA MTANDAO WA FACEBOOK KWANI MTANDAONI WA FACEBOOK HAUNA SHINDA YEYOTE ILA SHINDA INA KUJA KWA WATU WA CHACHE AMBAO WANA TUMIA MTANDO HUU KUWA CHAFUA WENGINE HASA WATUMISHI MUNGU NA WATU WANAO MPEBNDA MUNGU NA WATU WENGNE

SASA KUNA JAMBO HILI LA KUHUSIANA NA FEDHA ZA. .HII INATUMIKA K**A NJIA YA KUCHUKULIA YA MTU.

KWANI WAO WATA KUTUMI LINK UKISHA IBONYEZA HIYO LINK TAYA ACCOUNT YAKO INA CHUKULIWA,

HAFU WANACHO KIFANYA HAWATOI PICHA ILIYOPO KWENYE PROFILE YA ACCOUNT YAKO WENYEWE WANA AZA KUITUMIA HIVYO HIVYO IKIWA NA PICHA YAKO POST ZAO PICHA NA VIDEO CHAFU KUPITIA ACCOUNT YAKO WALIYO ICHUKUA

KUWA MAKINI WATU WENGI SANA SAIVI ACCOUNT ZAO ZIMESHA CHUKULIWA NA HAWA WATU

Hello May.🥳BINTI K**A MAMA...hata mama alikuwa binti!Kwa Neema ya Mungu tutakuwa na uzinduzi wa kitabu chetu kizuri cha ...
22/03/2024

Hello May.🥳

BINTI K**A MAMA...hata mama alikuwa binti!

Kwa Neema ya Mungu tutakuwa na uzinduzi wa kitabu chetu kizuri cha BINTI K**A MAMA.
Tarehe 12.5.2024, save.
Kanisa la wanavyuo, ABC GLOBAL UBUNGO MSEWE kwa mchungaji Jordan Yusuph.
Saa 9 kamili alasiri hadi 12 kamili jioni.

Mkaribishe binti mmoja, mkaribishe mama mmoja, na wewe kaka, baba karibu sana.

Kwa wale wanaotaka kuweka oda ya kitabu ,mnaweza kutumia namba hii 0747335012.

Unakaribishwa ku-support:
NMB 4041001129
Tigo pesa 0716379719.

Shalom In Christ
Sis Furahayao
Serving Christ, Saving Souls.
21st March 2024.

 Habari ya Muda huu ndugu zangu wana FB huu mtandao umekwisha ingiliwa na mashetani na mambo ya ajabu sana yasio yakawai...
09/03/2024



Habari ya Muda huu ndugu zangu wana FB huu mtandao umekwisha ingiliwa na mashetani na mambo ya ajabu sana yasio yakawaida .

Kuna post zinaendelea kusambaa huku mtandaoni inaonekana mtu unaye mjua amepost na ku tag watu kadhaa lakini kumbe huyo mtu ata yeye hajui k**a kuna post ipo kwenye account yake mbaya zaidi ni post za video za ngono jambo ambalo linasikitisha sana kuona mtu unayemuheshimu anapost uchafu mbele ya public.

Post yoyote mtayoiona ya video za ngono mkae mkitambua kua huyo ambaye amepost ka hakiwa na watu wasiojulikana na hata yeye mwenyewe hajui k**a amepost kwasababu kwake haionekani.

Yawezekana tukapoteza marafiki wengi na kuvunja heshima tulizo nazo bila sisi kujua tuweni makini sana huu ndio mtandao pekee ambao upo free kuliko mitandao yoyote ya kijamii .

Atakaye ona Account yangu imepost ujinga wowote naomba anipe taarifa atakua amenisaidia sana pia tuwape taarifa ndugu zetu ambao hawaingii Fb lakini wanaonekana wamepost.

CHUKUA TAHADHARI ⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️

Happy 7th  Anniversary to my Spiritual Parents....
07/01/2024

Happy 7th Anniversary to my Spiritual Parents....

DARE TO BE DANIEL-Mwl. Samwel Mkumbo -Bishop. KABIGUMILAFree Usafiri kwa Wanafunzi wa VyuoTarehe 1 December,POSTA JIJINI...
18/11/2023

DARE TO BE DANIEL
-Mwl. Samwel Mkumbo
-Bishop. KABIGUMILA

Free Usafiri kwa Wanafunzi wa Vyuo
Tarehe 1 December,
POSTA JIJINI DAR ES SALAAM.

MAKUNDI MAWILI YA WATU DUNIANI2. Walioumbwa kutumika chini ya watu, chini ya maono ya wengine (Part 02)Sehemu ya kwanza ...
16/11/2023

MAKUNDI MAWILI YA WATU DUNIANI

2. Walioumbwa kutumika chini ya watu, chini ya maono ya wengine (Part 02)

Sehemu ya kwanza nilikuonesha kutumika chini ya, au chini ya maono ya mwingine si kizuizi cha wewe kuonekana, kutambulika, kazi yako kuonekana na kuwa mkuu!

Sasa tuendelee...

HAWA WALIOUMBWA KUTUMIKA CHINI YA;

• Sio wazuri wa kuanza vitu vyao wenyewe au kuanzisha vitu

• Ni watu ambao ni watulivu mno, watu wa mipango, wasiokurupuka k**a wale walioumbwa kuanza vitu, na kwa sababu ya utulivu huu na kutokurupuka, hawawezi kuchukua hatua za hatari (taking risk), na hivyo si rahisi kwao kuanza vitu

• Ni watu ambao ili wachukue hatua, lazima kwanza wajiridhishe uhakika na usalama tofauti na wale ambao wameumbwa kuanzisha vitu, huwa wanaanza na wanachoweza na walipo, mengine watajua hukohuko mbele

• Ni wasimamizi wazuri, wakikuta kitu kipo tayari, kwa uangalizi na usimamizi wao, lazima kikue, kiwe bora kuliko mwanzo
Mfano: Yusufu (Mwanzo 39:1-5)

• Uwezo wao hupata maana wakikuta tayari kitu kipo na wao waje kukiboresha, kukirekebisha, kukipa sura au mwonekano mzuri zaidi

• Watu hawa wana neema ya ubora, mpangilio kuliko waanzilishi, wasipoutumia huu uwezo kujenga, wanaishia kuwa wakosoaji, wapinzani wa wabeba maono

CHANGAMOTO ZAO

•Kwa kuwa ni watulivu, watu wa ubora, watu wa mipangilio, watu huanza kuwasifia kwamba wao ni bora kuliko waanzilishi, baba zao wa kiroho, waasisi walio juu yao, WASIPOKUWA NA HEKIMA KUJUA HICHO NDICHO WALICHOKUJA KULETA KWENYE TAASISI, WATAJUKUTA WANATAKA KUPINDUA TAASISI AU KUTAKA KUANZA VYA KWAO BADALA YA KUTUMIA UWEZO WAO HUO KUBORESHA KILE KILICHOPO WANACHOTUMIKA CHINI YAKE!

• Watu hawa hukutana na sifa za watu na kuwaonesha WANAWAZIDI AU NI BORA KIUTENDAJI, KIVIPAWA KULIKO WALIOJENGA TAASISI AMBAO NDIO SABABU YAO KUONESHA UWEZO NA WALICHOBEBA!

• Watu hawa hurogwa na sifa wanazopewa na kuamua wakaanze vyao, WAKIKUTANA NA MASHETANI YANAYOPAMBANA NA WAANZILISHI, NA VITA WAKUTANA NAZO WAANZILISHI, HUPOTEANA NA KILE TULICHOKUWA TUKIKIONA KWAO HUYEYUKA!

NINI WAFANYE WATU HAWA;

• Furahia kutumika chini ya, fanya kazi chini ya, k**a yako, bila kujali unalipwa mema, unatambuliwa, unaheshimiwa au la! Dunia haiwezi kukaa kimya kwa mtu anayejitoa, wa ubora na upekee, lazima utaonekana tu!

• Epuka jaribu la kutaka kuanza kitu chako, hautaweza hekaheka, ligi na mapambano ambayo wameumbwa kuanza vitu, baki kwenye kuboresha na kuvipa maana vilivyozalishwa na waanzilishi!

• Sikia furaha kuwa sababu ya maongezeko, utaratibu, mipangilio kwenye taasisi kwa sababu ya hekima zako, usitake kufanya zaidi ya hayo, utakwama!

• Mkubali na kumheshimu mwanzilishi, maana NDIYE ALIYETENGENEZA TAASISI, HUDUMA, KAMPUNI, MFUMO AU JUKWAA AMBALO WEWE UNATUMIKA NALO NA KUONESHA UWEZO WAKO, AMBAPO ASINGEFANYA HIVYO HUENDA TUSINGEKIONA ULICHOBEBA...

• Uwe mrekebishaji mtiifu, mboreshaji chini ya mamlaka, afanyaye mambo bora na mazuri lakini kwa ruhusa ya mwanzilishi na baraka zake, HAPO UTAUSHANGAZA ULIMWENGU NA HAUTAKWEPA UKUU!

Askofu Dickson Cornel Kabigumila
ABC GLOBAL DUNIANI
16.11.2023

KUNA MAKUNDI MAWILI YA WATU DUNIANI1. Waliotumwa kuanzisha vitu (Wabeba maono/ waanzilishi)Waanzilishi wa mataifa, makan...
16/11/2023

KUNA MAKUNDI MAWILI YA WATU DUNIANI

1. Waliotumwa kuanzisha vitu (Wabeba maono/ waanzilishi)
Waanzilishi wa mataifa, makanisa, huduma, vyama vya siasa, makampuni, sanaa fulani, tasnia fulani, mfumo fulani nk.

HAWA

•Wana neema ya kufyeka mapori na kuchonga barabara ili wengine wapite kwa urahisi

• Wana neema ya kuzaa vitu japo si wote wana uwezo kwenye kuvikuza na kuviendeleza, ndio maana Mungu ameumba walioumbwa kutumika chini ya, ili wawasaidie kutimiza maono makubwa waliyonayo

•Wana uwezo mkubwa wa kuthubutu, kuchukua hatua na kuzaa vitu mahali ambapo mtu aliyeumbwa kutumika chini ya, hawezi kuthubutu kuchukua hatua

•Wana uwezo mkubwa wa kujihatarisha, kufanya maamuzi ya hatari bila kujali nini kitatokea! Si wazuri wa kupanga, ni wepesi kufuata wanachoona au kusikia moyoni bila kujali lolote

ILI WAWE NA UFANISI

i) Wanahitaji kulipa gharama ya kusoma na kutafuta maarifa mengi karibu ya kila kitu kuhusu maono na eneo wanalotaka kuwa bora, ili hekima na ufahamu huo uwasaidie kwenye kujilipua kwao na ujasiri ambako tayari wanako kwa kuzaliwa nako

ii) Wanahitaji kujizungushia watu wenye matokeo kuliko wao, wanaojifunza kwao na kujikosoa kwa kuwasikiliza au kuwaangalia wanavyofanya (learning through observation).

iii) Wanahitaji watu wa mipango, mikakati na utaratibu chini yao, watakaoyatafsiri maono yao na kuyapa muundo na sura inayoeleweka ili yatendeke kwa urahisi

iv) Wanahitaji watu wengi kwenye kila eneo la maisha, walioumbwa kutumika chini ya, ambao kwa kushirikiana nao, mambo makubwa yatazaliwa

TUWAANGALIE KUNDI LA PILI

2. WALIOUMBWA KUTUMIKA CHINI YA MAONO AU CHINI YA WENGINE...

Askofu Dickson Cornel Kabigumila
ABC GLOBAL DUNIANI
15.11.2023

 .   .
15/11/2023

.

.

Address

Kahama

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kijana wa Nuru posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share