Askari Wa Yesu

Askari Wa Yesu kujifunza namna ya kumjua Yesu na kumtegemea

07/02/2020

TUNAMUHITAJI YESU WAKATI HUU
Ukikaa ukafikiri jinsi ambavyo dunia ilivyo kwa Sasa ya kupasa kutubu na kuiamini injili na kumkiri Yesu kwa kinywa chako kuwa Bwana na mwokozi ili upate iliyo kweli ndani yako maana yeye ndio lango la mbinguni hakuna mlango mwingine was kuingilia zaidi ya YESU ©Yohana 10:7, 9 Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo.9 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.
©Mambo mengi Sana yanatokea kwasasa mathayo 24: 6 -8 Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado 7 Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali. 8 Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.
©Utungu maana yake karibia kitu kinazaliwa K**a mama mjamzito anapotaka kujifungua lazima uchungu uanze huu ndio uchungu wenyewe siku yoyote ile Yesu atarudi kulichukua kanisa
© Tumeisha sikia juu ya tetesi za Vita Kati ya marekani na Iran Tena haya ni mataifa makubwa Sasa tishio limekuja la Corona vyombo vya habari vinasema takribani mataifa kumi tayari yameambukizwa virus vya Corona vilivyoanzia China wenzetu wapo kwenye kipindi kigumu mno mpk imefika hatua hawaruhusiwi kutoka nje na ugonjwa unasambaa kwa Kasi mno mpk Sasa takwimu zinasema watu 600 tayari wamepoteza maisha na watu laki moja tayari wameambukizwa hiyo ya mwezi mmoja tu. Na Uingereza na marekani tayari umefk ugonjwa,tuwe macho tusisinzie .
©mathayo 24: 29 Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; dunia kwa sasa ipo katika dhiki kubwa ikitafuta suluhisho la kuendelea kuishi
©Manabii wa uongo palipo na manabii wa uongo Basi na manabii wa ukweli wapo lakini tuwe macho Sana na kupenda miujiza. mathayo 24:11 Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.
Bali tumtafute Yesu anayetenda miujiza ©Yohana 16: 2-3 Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. 3 Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. Tujitahidi ndugu zangu kumtafuta Yesu was kweli na Mungu was kweli yeye mwenyewe anasema tumtafute madamu anapatikana ukishindwa kuishi katika kipindi Cha neema hiki je kipindi Cha kujiokoa mwenyewe utawezaje kilichojaa mateso makali
©Ufunuo 9:5 -6 Wakapewa amri kwamba wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao yalikuwa k**a kuumwa na nge, aumapo mwanadamu.
6 Na siku zile wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe. Nao watatamani kufa, nayo mauti itawakimbia. Chukua hatua wokovu ni sasa.
Sala ya kumpokea bwana Yesu awe Bwana na mwokozi kwako Sema kwa imani ukimwamini utapokea wokovu
©Bwana Yesu ninatubu dhambi zangu zote nilizotenda kwa maneno, mawazo na vitendo ninazokumbuka na nisizo kumbuka naomba unisamehe futa jina langu kwenye kitabu Cha hukumu andika jina langu kwenye kitabu Cha uzima uwe kwangu Bwana na mwokozi wangu dhambi isinishinde kwa jina la Yesu. Imani ni kuwa na uhakika na Mambo yatarajiwayo imani yako iwe kwa Yesu.

✓✓7 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.
Ufunuo wa Yohana 2:7✓✓✓✓✓✓

God is my everything
21/01/2020

God is my everything

18/01/2020

KUBALI KUWA NA MUNGU KATIKA FAHAMU ZAKO
Ufahamu ni kitendo Cha kuelewa Jambo au kulifanunua ndani ya akili.
Kufanikiwa kwa mtu kunategemea jinsi ufahamu wake ulivyopokea maarifa mapya ambayo yatageuza akili yake ifanye kazi katika mazingira anayoishi.
Na k**a walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
Warumi 1:28
^^Hasara ya kutokuwa na Mungu Katika fahamu zako ni kubwa mno, duniani Kuna roho mbili zinazozunguka roho ya Mungu na roho ya shetani K**a umekataa kuwa na Mungu Katika fahamu zako jua wazi shetani atakuwa kwenye fahamu zako na atakushauri yakwake uyafanye ndio tunasikia kwenye vyombo vya habari mtu ameua mke wake watu wengine wanafanya mambo ambayo hata baadae mwenyewe akikumbuka haamini K**a ni yeye aliyefanya.
^^ Apataye hekima hujipenda nafsi yake; Ashikaye ufahamu atapata mema.
Mithali 19:8
Ufahamu wako ukiwa na Mungu utapata mema utapokea mashauri ambayo yatakujenga, yatakuondoa kwenye njia potofu
^^ Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao; Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao.
Mithali 16:22 Mungu anapokuwa nawe katika ufahamu wako unapata uzima kwenye akili yako hautapata hasara Kila Jambo utalolifanya litakuwa linaongozwa na Bwana katika kitabu Cha kutoka Musa anamwambia Mungu uso wako usipokwenda nasi usituchukue mahali hapa alijua Kila kitu anamtegemea Mungu asipokuwa naye ni hasara kwake
Uso wa Mungu uende nawe Kila hatua ya maisha yako na upokee kufadhiliwa na Bwana
^^Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa; Bali kinywa cha wapumbavu hula upumbavu.
Mithali 15:14 Omba Mungu akupe ufahamu ndani ya Moyo wako ili uweze kutafuta maarifa yanayompendeza Mungu, yapo maarifa mengi Sana duniani mengine ni chukizo mbele za Mungu hivyo ukitaka kukaa vizuri na Mungu utafute maarifa yake.
^^ Ufahamu mwema huleta upendeleo; Bali njia ya haini huparuza.
Mithali 13:15
^^Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.
Mithali 11:12 ufahamu unaojazwa na Mungu utakupa uvumilivu utakusaidia kuepuka malumbano yasioofaa.
Mwenye dharau hutafuta hekima, asiipate; Bali maarifa huwa mepesi kwa mwenye ufahamu.
Mithali 14:6
√√5 Bwana ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unaishika kura yangu.
Kamba zangu zimeniangukia mahali pema, Naam, nimepata urithi mzuri.Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri, Naam, mtima wangu umenifundisha usiku. Nimemweka Bwana mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.
Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nao utukufu wangu unashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.
Zaburi 16:5-9
∆Mungu akumbuke Kila hatua uliyokuwa nayo, iliyombele yako akupelekee msaada wake toka patakatifu pake jina la Mungu was Yakobo likuinue kwa jina la Yesu kristo.

12/01/2020
09/01/2020

Date: Jan 9, 2020
Subject: SIRI KUBWA YA MAOMBI ILIYOKO MWEZI WA KWANZA

Mwezi wa Kwanza wa mwaka Bwana anawatoa Israel katika nchi ya misri majira ambayo yeye aliyakusudia kuwatoa kutoka12:2 Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu.
^^Omba Mungu Mwezi huu uwe wa kutoka kwako kwenye Kila utumwa uishi maisha mapya sio ya utumwa tena, uishi ukiwa mwenye fikra mpya K**a mwaka ulivyompya
^^Mungu anagiza watoe sadaka ya mwanakondoo wakiwa katika nchi ya utumwa huko misri watakapochinja hiyo damu wapake katika miimo ya miwili ya milango yao kutoka 12: 13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri.
^^Omba kwa damu ya Yesu na kunyunyuzia kwenye mipango yako mwanakondoo wetu amekwisha kutolewa ambaye ni Yesu kristo chukua damu ya YESU kwa imani nyunyuzia kwenye mipango yako ili mharibu atakapokuwa amepita kuharibu asiweze kwa maana damu ya Yesu inanguvu ya ulinzi, kuponya na kuhuisha vilivyokufa kuwa na uhai Tena katika maisha yetu
^^Mungu alihukumu miungu ya familia inayong'ang'ania maisha yako usije ukafanikiwa kiroho na kimwili. Kutoka12:12 Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana.
^^Mungu aliwakomboa kutoka katika miungu waliyokuwa wanaiabudu kupitia ile damu iliyokuwa katika miimo ya nyumba zao kutoka
^^Adui zako watakuhimiza utoke katika kifungo walichokuwa wamekufunga kwa kuwa Bwana atatetanao kutoka 12: 29 Hata ikawa, usiku wa manane Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama 30 Farao akaondoka usiku, yeye na watumishi wake wote, na Wamisri wote; pakawa na kilio kikuu katika Misri; maana hapakuwa na nyumba hata moja asimokufa mtu.
31 Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, Ondokeni tokeni katika watu wangu, ninyi na wana wa Israeli; enendeni, kamtumikieni Bwana k**a mlivyosema.
^^Mungu akakujalie kupendelewa kupewa vyote unavyohitaji k**a alivyowapendelea wanna wa Israeli kutoka 12:35-36 Wana wa Israeli wakafanya k**a neno lile la Musa; wakataka kwa Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu, na mavazi. 36 Bwana akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara.
1 nyakati 20:1Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Yoabu akawaongoza mashujaa wa jeshi, akaiteka nyara nchi ya wana wa Amoni, akaja akauhusuru Raba. Lakini Daudi akakaa Yerusalemu. Naye Yoabu akaupiga Raba akauangamiza
^^Omba Bwana akupe kuteka nyara na kumiliki katika ulimwengu was roho
2 Kisha Daudi akamtwalia mfalme wao taji toka kichwani pake, akaona ya kwamba uzani wake ni talanta ya dhahabu, na kulikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani; akazitoa nyara za mji, nyingi sana.
Omba Bwana akupe nyara nyingi na taji yenye thamani nyingi.
"Ombeni nanyi mtapewa tafuteni nanyi mtaona bisheni nanyi mtafunguliwa"mathayo 7:7
Mungu akubariki

07/01/2020

OMBA VIZURI 2020…

💥 SAMSONI alimuomba MUNGU alipize kisasi kwa KUJIUA pamoja na Wafilisti; Mungu akamtia nguvu na Samsoni akafa pamoja na Wafilisti 3000 (Waamuzi 16:26-30).

💥 MASIKINI LAZARO alitamani MAKOMBO; hivyo MUNGU akamletea tajiri mwenye roho nzuri aliyeruhusu Lazaro akae chini ya meza na kula MAKOMBO (Luka 16:20-21).

🔥 JABEZI akamuomba MUNGU amwondolee balaa, mikosi, maumivu, na aipanue mipaka yake; MUNGU akamsikia na akampa haja ya moyo wake (1 Nyakati 4:9-10).

🔥 HANNA akamuomba MUNGU ampe mtoto wa kiume na kwamba angemtoa amtumikie MUNGU; ombi lake likasikiwa, Mungu akampa mtoto SAMWELI (1 Samweli 1:10-11).

UNATAKA MUNGU AKUTENDEE NINI 2020??

✨ Usiombe MAKOMBO au kutamani KUFA na adui zako.

✨ Omba MAONGEZEKO, omba KUFUNGULIWA, na KUZIDISHWA!!

ZABURI 20:1,4; “BWANA akujibu siku ya dhiki, Jina la MUNGU wa Yakobo likuinue… 4 Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, na kukutimizia mipango yako yote.”



Pastor Zakayo Nzogere

25/12/2019

FURAHA NDANI YA CHRISTMAS
Unapokumbuka siku ya kuzaliwa kwake Yesu tunapata mambo makuu 3 yanayohuhisha maisha yetu ya kiroho na kimwili.
1. Maisha yetu yajawe na utukufu wa Mungu na huo utukufu ukatung'arie pande zote kuanzia rohoni Hadi mwilini.
Luka 2: 8 -9 Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku.9 Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.
2. Tutembee kwenye majira mapya kwasababu ukombozi umetujilia mwambie bwana haya ni majira mapya nataka kutembea kwenye huu ukombozi uliokuja kwaajili yangu, maisha yako yabadilike Anza kuona bwana amefanya kitu kwaajili yako acha kuona kilio Tena ona kuburudika kwakuwa bwana amekukumbuka K**a wale wachungaji waliotokewa na malaika wakasema haya twendeni bethelehemu tukaone bwana aliyotwambia luka 2:13 Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,14 Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.15 Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana.
BWANA amekuridhia uuone utukufu wake katika maisha yako
3. Upokee kutoka bwana Yale Mambo aliyoyakusudia upate kwa mapenzi ya bwana K**a wale mama jusi walipomletea Yesu dhahabu, uvumba na manemane Mungu alijua anachohitaji ndio maana akampa vile vitu kupitia mama jusi na pia upokee na utamani kumjua Mungu kuishi K**a yeye apendavyo
%% uwe na krismas yenye baraka bwana akufurahishe ufurahie kutoka moyoni mpaka mwilini%%merry Christmas 🍉🍉

22/12/2019

BWANA ASEMA HIVI
Onyo kwa habari ya manabii uwe makini manabii wengine hawakutumwa na Bwana Yeremia 23: 21 Mimi sikuwatuma manabii hao, lakini walikwenda mbio; sikusema nao, lakini walitabiri.
∆∆Yeremia 23:15 Basi Bwana wa majeshi asema hivi, katika habari ya manabii, Tazama, nitawalisha pakanga, nitawanywesha maji ya uchungu; kwa kuwa kutoka kwa manabii hao wa Yerusalemu kukufuru kumeingia katika nchi yote.
∆∆Bwana anasema usisikilize kuwa maakini
Yeremia 23: 16 Bwana wa majeshi asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wakiwatabiria; huwafundisha ubatili; hunena maono ya mioyo yao wenyewe; hayakutoka katika kinywa cha Bwana. Angalia vizuri maana siku hizi mpaka p**i ya upako,unga wa upako hayo ni maono yao sio ya Mungu.
∆∆Hawawasikilizishi watu neno la Bwana Bali maneno yao.
Yeremia 23:18 Maana, ni nani aliyesimama katika baraza la Bwana, hata akalifahamu neno lake na kulisikia? Ni nani aliyelitia moyoni neno langu, na kulisikia?
∆∆hawawaelekezi watu kuacha uovu Bali kupata vitu vya dunia hii sio kutubu dhambi kanisa ambalo halikemea dhambi maana yake lipo kwa maslahi ya alieanzisha
Yeremia 23:22 Lakini k**a wangalisimama katika baraza yangu, ndipo wangaliwasikizisha watu wangu maneno yangu, na kuwageuza waziache njia zao mbaya, na uovu wa matendo yao.
Yeremia 23:23 Mimi ni Mungu aliye karibu, asema Bwana, mimi si Mungu aliye mbali.
%%%nimenawa mikono%%%
NB: nimetoa K**a nilivyopokea.

29/11/2019

Nimeipenda hii unaweza pia kushea kwa wenzako:-
👇👇👇👇👇👇
MASOMO MATATU
SOMO LA KWANZA.
Nilikuwa kanisani nikimsikiliza muhubiri mmoja maarufu, muhibiri alitoa mfukoni noti za shilingi elfu kumi kumi zilizokuwa na jumla ya Tsh laki moja, akauliza, "ni nani miongoni mwenu anataka nimpe hii laki moja?"
Watu wengi waliokuwa mle kanisani walinyosha mikono, kila mmoja alikuwa akishauti mimi! Mimi!. Nikaanza kushangaa ni nani atakuwa na bahati ya kupewa ile pesa kati ya mamia ya watu waliohudhuria ile ibada.
Pia nikajiuliza kwa nini (ambapo bila shaka na baadhi ya wahudhuriaji wengine nao walijiuliza) atoe kitita cha shilingi laki moja kirahisi rahisi hivyo.
Wakati watu wakiendelea kupiga kelele kusema nipe mimi, nipe mimi huku wamenyosha vidole vyao, kutokea nyuma akaibuka msichana mdogo mwenye umri k**a miaka 18 hivi, akaenda mbele kule aliko yule muhubiri akafika mbele na kuchukua ile laki moja kutoka mkononi mwa yule muhubiri.
"Safi sana, msichana! Umefanya vema," alisema yule muhubiri.
"Wengi wetu tunapenda kukaa tu na kusubiri mambo mazuri yaje yenyewe. Hii haitaweza kuwasaidia hata kidogo, unatakiwa kuinuka na kutafuta mafanikio. Mafanikio hayawezi kuja k**a umekaa tu.
Na maisha yetu ndivyo yalivyo, tunaziona fursa nyingi sana zikiwa zimetuzunguka, kila mtu anahitaji mambo mazuri. Ila tatizo hatutaki kusimama na kuzifuata hzo fursa. Simama sasa na ufanye kitu, usisubiri mafanikio huku umekaa, kamwe hayatakuja. Usijali kuhusu watu watasema nini. Chukua hatua.
SOMO LA PILI.
Baadae yule muhubiri akatoa tena noti ya shilingi 10000 na akainyanyua ili wote tuione. Nikafikiri anarudia k**a mwanzo tena. Lakini akauliza swali jepesi. "Noti hii inathamani gani?" Waumini wakajibu "shilingi elfu kumi". "Mko sahihi" akawajibu.
Akaichukua ile noti akaifinyanga finyanga na kuwauliza tena noti ile inathamani ya shilingi ngapi!? "shilingi elfu kumi" wakajibu wale wauminii!
Akaitupa chini ipe noti, akaikanyaga kanyaga sana, akaichukua na kuuluza tena noti hii ina thamani ya kias kuikanyaga noti ya fedha, thamani ya noti itabaki pale pale."
"Maisha yetu ndivyo yalivyo, tunatakiwa tuwe k**a noti ya shilingi elfu kumi. Ktk maisha kuna kipindi tutasalitiwa, tutakanyagwa, tutaonewa na kupigwa. Ila usiache thamani yako ipotee, kwa sababu mtu amekuumiza tu, hiyo haimaanishi ndio thamani yako imepotea. Wewe ni wa thamani mno jinsi ulivyo. Usiache thamani yako ipotee kwa sababu ya wachache!
SOMO LA MWISHO.
Njia tofauti, jibu moja.
2+5=7
6+1=7
3+4=7
7-0=7
7+0=7
9-2=7
8-1=7
Point

Address

Iringa

Telephone

+255673706717

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Askari Wa Yesu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Askari Wa Yesu:

Share