Ufahamu Katika NENO

Ufahamu Katika NENO Ufahamu utakusaidia kuijua kweli na kweli itakuweka huru

06/04/2024

Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;
Mithali 9:9

KIWEKEE AZINA KWA SIKU YA TAABU YAKO"Utukufu wangu utakuwa mpya kwangu, Na uta wangu hurejezwa upya mkononi mwangu."    ...
09/11/2023

KIWEKEE AZINA KWA SIKU YA TAABU YAKO
"Utukufu wangu utakuwa mpya kwangu, Na uta wangu hurejezwa upya mkononi mwangu."
Ayubu 29:20
- Kila ukitendacho duniani unaniwekea hazina Yako
- Kusitiriwa kwa mtu kunategemea Jinsi Yeye anavgosimama kusitiri wengine
- Kiwango chako Cha kuwatendea wengine kinaamua Nini utendewe na kwa Kiwango Gani
- Kadri mtu anavyowatendea watu yaliyo mema ujiwekea ulinzi, akiba ha mema na Azina ya kurejeza utu wake
- Biblia inasema Ezekia alimkumbisha Mungu mema aliyowahi kiyatenda, Mungu akamsikia akamwongezea Miaka 15
Isaya 38:3
Kumbe wema ni akiba na ubaya ni akiba pia.
Mwandishi wa kitabu Cha Ayubu anajaribu kutukumbusha Tumaini la Ayubu siku ya TAABU yake
- Ayubu alitumainia wema wake kwa watu Kuwa msaada kwake siku ya TAABU yake.
Na alitarajia kurudishiwa utukufu na heshima aliyokuwa nayo mara dufu kwa azina aliyoiweka kwa watu
Anasema
"Utukufu wangu utakuwa mpya kwangu, Na uta wangu hurejezwa upya mkononi mwangu. Ayubu 29:20
KWA NINI AYUBU ALIPATA UJASIRI KUTARAJIA
KURUDISHIWA HESHIMA NA UTUKUFU ALIOKUWA NAO?
Ayubu 29:11
11 Maana sikio liliponisikia, ndipo likanibarikia; Na jicho liliponiona, likanishuhudia.
12 Kwa sababu nalimwokoa maskini aliyenililia; Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia.
13 Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia; Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.
14 Nalijivika haki, ikanifunika, Adili yangu ilikuwa k**a joho na kilemba.
15 Nalikuwa macho kwa kipofu, Nalikuwa miguu kwa aliyechechemea.
16 Nalikuwa baba kwa mhitaji, Na daawa ya mtu nisiyemjua naliichunguza.
17 Nami nilizivunja taya za wasio haki, Na kumpokonya mawindo katika meno yake.
21 Watu walitega masikio kunisikiliza, na kungoja, Wakanyamaa kimya wapate sikia mashauri yangu.
22 Hawakunena tena baada ya kusikia maneno yangu; Matamko yangu yakadondoka juu yao.
23 Walikuwa wakiningojea k**a kungojea mvua; Wakafunua vinywa vyao sana k**a mvua ya masika.
24 Walipokata tamaa nikacheka nao; Na mwanga wa uso wangu hawakuuangusha.
25 Niliwachagulia njia, nikakaa k**a mkuu wao. Nikakaa k**a mfalme katika jeshi la askari, Mfano wa awafarijiye hao waombolezao.
KATIKA MAANDIKO HAYO TUNAPATA SIFA ZA AYUBU ZILIZOSABABISHA KURESHWA
KWA UTUKUFU NA HESHIMA YAKE
1. Aliwasaidia maskini na Yatima
2. Aliwafariji wajane na kuwatunza
3. Alikuwa mteteze wa haki na alisimamia maadili
4. Alifanya kazi ya advocacing, kuwasemea wasioweza kusema, kuwaonesha na kuwaongoza wasioweza kuona Ili wapate kuona.
5. Aliwasaidia wahotaji, Tena si tu wale aliowajua bali hata wale hasiowajua aliwasaidia
6. Alitetea waliodhurumiwa na kulinda haki zao
7. Aliwashauri watu wakamsililiza
8. Alicheka na waliokata tamaa wakapata tumaini la kurejezwa kwa furaha yao
9. Aliwaongoza watu katika mema hata walayafikia.
10. Aliwafariji waombolezao.
KURURUDISHWA KWA UTUKUFU KWA AYUBU KULITEGEMEA SANA AZINA YAKE NA IVUMILIVU WAKE WAKATI WA TAABU.
Rejea
Mathayo 19:21
Marko 10:31
Luka 18:22
Mathayo 6:14-20
HITIMISHO
".. jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; "
Mathayo 6:20

WARAKA MAALUM KWA MTU MAALUM"Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, k**a vile roho yako ifaniki...
01/11/2023

WARAKA MAALUM KWA MTU MAALUM

"Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, k**a vile roho yako ifanikiwavyo.
3 Yohana 1:2

Huu ni waraka uliowahi kuandikwa na Mzee Yohana kwa kijana wake ampendae aitwae GAYO

Kwa GAYO MPENZI...

Kwa Nini GAYO?
GAYO ni mtu maalum aliyeumbwa kwa kusudi maalum

GAYO alistahili kutamkiwa maneno ya Baraka k**a yale, kwa kuwa alikuwa ni mtu mwenye huruma juu ya kazi ya Mungu,
pale alipoona kuna uhitaji wa injili kupelekwa mbele, alijitoa kikamilifu kuichangia kazi ya Mungu,

Aliwasafirisha wale watumishi wa Mungu kuipeleka injili kila mahali palipohitajika pasipo kujali kupungukiwa kwa namna yoyote,tofauti na wakristo wengi waliokuwepo katika makanisa yale.

alikuwa anawakaribisha pia wageni (wakristo) waliokuwa wanatoka mbali kwa ajili ya kwenda kuifanya kazi ya Mungu.

Ilifikia mpaka hatua wale wote waliokuwa wanaifanya kazi ya Mungu ambao walikuwa katika maeneo yale aliwasaidia kiasi kwamba wakawa hawana uhitaji wowote kutoka kwa watu wasioamini,
aliwahudumia kwa vyote Hadi unaweza kutengeneza picha kuwa hakukuwa na kikwazo chochote cha kifedha na kimazingira kilichokwamisha kazi ya Mungu maeneo yale,
alifanya hivyo kwa bidii mpaka sifa zake zikavuma katika makanisa yote ya Kristo, na habari kumfikia Mtume Yohana.

Ninakuletea waraka huu wewe mtu maalum uliyeumbwa kwa kazi maalum
Tuna kazi ya Mungu ni kazi mpya. Ilipo
Eneo KITASENGWA - IRINGA MJINI
Jina la kanisa: FPCT- IRINGA GLORIOUS TEMPLE
inahitaji sana mkono wako nawe utapokea baraka za rohoni zitakazo sababisha baraka zako za Mwilini.
Mahitaji ya msingi.

Bati 150 ili kukamilisha hema la kuabudia.linajengwa full bati na mbao baadhi ya sehemu

Mbao 1x4 , 100 au 1x6 ,70

Mirunda 35

Linajengwa kwa bati full suit

Mbao 1x4 , 100 au 1x6 ,70

Misumari kg 10

Vitambaa vya kupambia jora 3

Mimbari 1
Viti vya plastic 50
Speaker mid 2 base 1
Mic 2
Cement mifuko 12
Mchanga trip 2
Umeme unahitaji nguzo 2
Kiwanja tayari tunacho.
Shiriki chochote unachoweza
Kwa namba
0768797612
X-MASS SOLOMON MWAKANYAMALE
Mungu atakubariki sana
Taja kitu unachotamani ununue utakikuta kwa Jina lako.aidha hema kitasomeka au risiti ya ununuzi wa kitu hicho.
Hapana dini wala udhehebu shiriki kuijenga madhabahu ya Mungu.

Ninaibariki kazi ya Mikono na Afya Yako k**a roho yako ifanikiwavyo.
Mimi niwe Yohana wewe uwe GAYO mpendwa wangu katika ujenzi wa Kazi ya Mungu IRINGA MJINI

Maisha ni Yako, lakini msiba ni wa kwetu, hapa ndipo waswahili husema mchuma janga kulila hula na wakwao.Ndoa ni Yako la...
24/04/2022

Maisha ni Yako, lakini msiba ni wa kwetu, hapa ndipo waswahili husema mchuma janga kulila hula na wakwao.
Ndoa ni Yako lakini sherehe ni yetu.

Uongozi ni wako ila Maamuzi ni yetu, na maamuzi ni Yako furaha ni yetu
Hii ni kanuni ya maisha, tumeumbwa kwaajili ya wengine hivyo Kila tulifanyalo tukumbuke wengine.

UKOMBOZI KWA NJIA YA DAMU YA YESUWarumi 5:9"Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na gh...
04/05/2020

UKOMBOZI KWA NJIA YA DAMU YA YESU

Warumi 5:9
"Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye."
Waefeso 1:7
"Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake."
Waefeso 2:13
"Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo."
Halelleya.
UKOMBOZI ni tendo linalofanywa ili kulipa gharama iliyofanya kitu flani kiwe chini ya milki ya Mwingine.
Dhambi ilimfanya Mwanadamu kuwa chini ya kongwa la uasi chini ya Shetani.
Ili kumtoa Mwanadamu katika kifungo hiki Yesu alijitoa awe gharama atukomboe
Tito 2:14
" ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema. "
Hivyo kukombolewa ni kulipiwa gharama na Mungu ili kupokea haki,
Inawezekana ni kweli hukustahili kupona lakini Kwa kuwa Mungu amekuridhia anakuponya na kukupa Nafasi nyingine ili uoneshe juhudi katika mema na kumpendeza Mungu.
Kazi kubwa ya Damu ya Yesu ni kulipa gharama.
Tunapoomba na kutaja damu ya Yesu tunafunua hati ya umilki ya uzima wetu ambayo tumepewa na Yesu.
Kumbuka Mwenye haki hana haki mpaka hajue haki yake. Ukijua haki ya Uzima na kulindwa katika damu ya Yesu Kristo utajikuta unajizingira kila wakati na hiyo damu ya Yesu iki iwe alama. Ajapo adui anakuta alama kuwa huyu si milki yako ni Mali ya Yesu Kristo.
Damu ya Yesu ni alama ya Usalama baada ya kutukomboa,
Ishara hii ya Damu Mungu aliitoa tangu zamani kwa wana wa Izrael
Kutoka 12:13
"Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri"
Damu ya Yesu hata Sasa inatumika k**a alama ya umilki. Anayejua kuitumia damu ya Yesu kwa Kukiri kwa kuwa amejua haki yake ya ukombozi ujizingira kwa hiyo asipatwe na dhara lolote.
Malaika alipopita Misri alipoiona damu kwenye miimo na vizingiti katika nyumba za Wanna wa Izraeli alipita hakuruhusu dhara lolote kuongia Izraeli.
Je utajiukiza kwa wana wa Izraeli ambao hawakupaka damu katika miimo na vizingiti ilikuwaje,? Jibu ni kwamba nao madhara yaliwakuta.
Pia utajiuliza ilikuwaje kwa wamisri waliokuwa katika nyumba za Izraeli ? Jibu ni kwamba kwa gharama ya Damu ya ukombozi hata chenye hatia ufanyiwa haki. Hivyo wageni waliokuwa katika nyumba zilizopakwa Damu walisalimika
Itumie Damu ya Yesu kuiweka familia yako salama katika wakati huu. Hii ikufanyie haki na kukupa thamani upokee Uzima na kuwa salama.
DAMU YA YESU UKOMBOA JINA LAKE LINAOKOA.

TAFAKARI  Mwanzo1: 1-311. Wakati wote Roho wa Mungu huwa juu ya nchi akiwatazama wanadamu wote na vyote vilivyomo dunian...
29/04/2020

TAFAKARI
Mwanzo1:
1-31
1. Wakati wote Roho wa Mungu huwa juu ya nchi akiwatazama wanadamu wote na vyote vilivyomo duniani. Hata magumu Mungu anayaona. ( Utupu na Ukiwa)
2. Ili Mungu afanye Jambo neno hutangulia( lazima useme unachotaka kiwe ili kiwe( akasema iwe Nuru) soma pia Yohana 1:1-3 pasipo neno hakikufanyika chochote
3. Mungu huandaa mazingira kabla ya kukuleta Duniani au kukupeleka mahali, Vyote vilifanyika lakini ni kwaajili ya Mwanadamu ( kwajili yako).
Hivyo fahamu Mazingira yoyote utakayokuwepo ukifanya ya Mungu ni milki yako na unahaki hapo kumiliki
4. Mungu ni wa Maongezeko, vyote alivyovifanya alitaka viongezeke.. Ulifanyalo liongezeke haya ndiyo mapenzi ya Mungu
5. Mwanadamu aliumbwa kwa Mfano wa Mungu, ( spiritual being) Mwanadamu ni kiumbe cha Kiroho mwenye mawasiliano na Mungu utashi, na uwezo wa kuchagua( free will)
6. Mwanadamu alikabidhiwa Mamlaka juu ya viumbe vyote na hii humpa Nafasi nyingine ya kufanana na Mungu kwa kuwa na Mamlaka juu ya viumbe
7. Kwa asili Nuru na giza hutengana palipo Nuru giza hujitenga.
8.Uumbaji huanzia Rohoni, kufanya kitu kiwe inategemea sana dhamira ya ndani ya Mtu. Mungu alikusidia kuundoa ukiwa katika nchi akasema ikawa. Ukidhamiria Jambo ukasema, itakuwa
TU WANA WA MUNGU TUNA MAMLAKA

Tukiwatanguliza wengine Mungu anatutanguliza kwa wengine.Mungu akuandalie njia katika kila jema ulitendalo
14/02/2020

Tukiwatanguliza wengine Mungu anatutanguliza kwa wengine.

Mungu akuandalie njia katika kila jema ulitendalo

Neno huongeza maarifa na Ufahamu katika Mungu. Maombi Huongeza nguvu za kiroho. OMBA SANA, SOMA NENO UKAUSHANGAZE       ...
12/01/2020

Neno huongeza maarifa na Ufahamu katika Mungu. Maombi Huongeza nguvu za kiroho.

OMBA SANA, SOMA NENO UKAUSHANGAZE ULIMWENGU

Mwaka 2020 tunakuletea Add value of life program. Kwa wakazi wa Iringa mjiandae kutupokea .Nimepata kibali kuinua vipaji...
21/12/2019

Mwaka 2020 tunakuletea Add value of life program. Kwa wakazi wa Iringa mjiandae kutupokea .Nimepata kibali kuinua vipaji mbali mbali mwaka 2020. Kinywa changu kina nguvu ya Mungu iwezayo kufufua kipawa na kila kilichokufa ndani yako. Watu wa dini zote kabila zote Mungu atawahudumia kipitia program hii. Itakapokufikia huduma hii usiache kushare story na wengine. May God bless u.

Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshi...
10/11/2019

Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
Yohana 12:26
Ukimtumikia Mungu tarajia heshima Maana akikuheshimu Mungu wanadamu wanapisha tu.

30/09/2019

ukijua umepata unachokitaka

"Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii."

Kumbukumbu la Torati 29:29
ili kupata unachokitaka lazma ujue kiliko

Address

Iringa

Telephone

+255768797612

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ufahamu Katika NENO posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Ufahamu Katika NENO:

Share