03/02/2026
YESU NISAIDIE KUTOA KIBANZI KATIKA JICHO LANGU,,,,,!
Luka 6 ;42---45
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴² Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako.
⁴³ Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri;
⁴⁴ kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu.
⁴⁵ Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
Ilikuwa ni wakati wa kuandaa msosi wa mchana, jua kali kwa ncha zake hii ilinifanya nitembee huku naangalia chini k**a mtu anayehesabia hatua
Bpiiiiiip... bpiiiiiiip...! Honi za onyo zililia . Macho yangu aliitanzama ile range rover nyeusi kuanzia chini hadi kwenye taa za mbele ... huku miguu ikikosa nguvu .. maamuzi yalichelewa kutoka..
gonga tu huyo ....!
Makusudi hayo...! Alisikika mpita njia wa baiskel,, aliyetupita hapo bado nimeduwaa...! Miguu ilikuwa mizito sana. Kutokana na kustuka na honi ya gari ile!
Dogo usiwe na makuu .. wapishe watumia barabara waendelee na mambo yao,, sogea hapa... alikuwa ni mbaba mmoja wa k**a hamsini hivi...mwenye masharubu na ndevu nyingi ila sio ndefu.
Macho yangu yalihama kutoka kwenye kumtazama usoni na kuhamia miguuni ambapo ilikuyo ilikuwa na suruali ya kaki mpauko tena mtumba ngumu viatu vya wazi na kimoja kilishapita kwa fundi ...
Hujambo rafiki,,,, unaitwa nani,,,? Haloo,,,!Aliniongelesha. Eh naam,,,! Niliitikia kwa kulopoka..." kwani una shida? Hapana sina shida!! Nilijibu kabia hajamaliza hata kuuliza,
Okay naitwa gaspari ni mwinjilisti wa kipentekoste kutoka mtaa wa nne kulia kwetu.. samahani ( inaendelea kesho.....)