Discipleship International Ministry - Dim

Discipleship International Ministry - Dim Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Discipleship International Ministry - Dim, Religious organisation, Iringa.

TUNABADILISHWA KUTOKA UTUKUFU HATA UTUKUFU.Apostle Elia.(c.mkuchu).
30/01/2023

TUNABADILISHWA KUTOKA UTUKUFU HATA UTUKUFU.
Apostle Elia.(c.mkuchu).

09/01/2023

KWABIDII ZOTE ULIZOFANYA/UNAZOFANYA KUHAKIKISHA KUWA WATOTO WAKO WANAKWENDA SHULE,JE BIDII GANI ZA KIMADHABAU YA MUNGU UNAYEMWAMINI UMEFANYA ILI KUWAKABIDHI HUKO KWA IBADA NA SADAKA ILI HUYO MUNGU AKAWAPIGANIE HUKO WAKATI WEWE HAUKO PAMOJA NAO.
HUKO MASHULENI WATAKUTANA NA WENZAO WALIOTOKA KWA BIBI NA BABU ZAO AMBAKO WAMESHAFANYIWA TAMBIKO NA IBADA ZA MIUNGU LKN WEWE UNAWAPELEKA KIENYEJI!
YAKIWAKUTA MTASEMA HATUWAAMBII,NDIYO NIMEWAAMBIA SASA.MTOTO AMEJAZA MAVITU KIBAO YA SHULE YENYE GHARAMA KUBWA LKN KWENYE MADHABAU YA MUNGU UNAYEMWAMBUDU HUJAMWEKEZEA SADAKA YA MADHABAU!KWA LUGHA NYINGINE UTAJIKUTA UNASEMA MTOTO WANGU YUKO SHULE LAKINI MUNGU HATAMBUI KUWA YUKO SHULE MANA SADAKA INAYOMNENEA KUWA YUKO SHULE HAIPO MADHABAUNI.
Mika 4:5
[5]Kwa maana mataifa yote watakwenda, kila moja kwa jina la mungu wake, na sisi tutakwenda kwa jina la BWANA, Mungu wetu, milele na milele.
For all people will walk every one in the name of his god, and we will walk in the name of the LORD our God for ever and ever.

Religious organisation

01/08/2019

AUGUST2019.
MWEZI WA MUNGU KUTEMBEA KATIKATI YETU.
"K**a Mungu alivyosema,ya kwamba,Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea,nami nitakuwa Mungu wao,nao watakuwa watu wangu."(2koritho6:16b).
Huu ni mwezi wa mtembeo wa Mungu katika maisha yako.Mungu anataka atembee kupitia miguu yako,anataka kugusa vitu mbalimbali kwenye maisha yako na ya wengine kupitia mikono yako.!
Ukiwa mwenyewe tu ukitembea hakuna matokeo,ukishika vitu wala huoni badiliko lakini kwa imani ukijua kuwa si wewe tena bali ni Kristo ndani yako,ukitembea Mungu anatembea,ukigusa vitu Mungu ameshika,ukisema ni Mungu amesema,utaona matokeo ambayo hujawahi kuyaona,na siyo wewe tu utakaye yaona bali hata wanaokuzunguka wataona!
Ngoja nikuoneshe matokeo ya Yesu kuwa anatembea:-
Katika nchi ya wagerasi kulikuwa na mtu mwenye mapepo mengi(region)na makao yake yalkuwa makaburini na hakuna mtu aliyeweza kumfunga tena ,hata kwa minyororo.kwasababu alikuwa mara nyingi kwa pingu na minyororo lkn aliikata ile minyororo,na kuzivunjavunja zile pingu na minyororo,wala hakuna mtu aliyeweza kumshinda!
Lakini siku Yesu amakanyaga tu katika aridhi kwa miguu yake biblia inasema"Alipomwona Yesu kwa mbali ,alipiga mbio,akamsujudia"!(marko5:1-13).
Yesu akianza kutembea ndani yako impact yake itasababisha yaliyoshindikana kwa wanadamu yawezekane kwako,Mungu amekufanya kuwa jawabu la matatizo ya watu katika Jina la Yesu.
Unaweza ukatumia ufunuo huu kuombea nyumba yako,ofisi yako,mashamba yako,na chochote kwa kutembea maana ukikanyaga si wewe unayekanyaga bali ni Kristo ndani yako,na kwa njis ya Kristo,miguu yako imepewa mamlaka ya kukanyaga nge na yoka na nguvu zote za yule adui(luka10:19),kila mahali zitakapokanyaga nyayo za miguu yako nimewapa kumiliki(joshua1:3)-miguu yetu imepewa umiliki kwa jina la aliye ndani yetu.Miguu yetu inafanya mazingira yasiyovukika yaweze kuvukika mbele yako kwa jina la Yesu,mfano katiƙa mto yordani maji yalitii wakavuka salama"basi hao waliolichukua hilo sanduku,walipofika yardani,na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa katika maji ya ukingoni,ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama,yakainuka yakawa kichuguu mbali sana....
Watu wakavuka kukabili yeriko"(yoshua3:15-17).
Nakuombea kwa jina la Yesu,kokote utakapokanyaga wakajue kuwa umefika siyo watu tu bali ata ufalme wa giza wakajue kuwa amafika aliyemkuu kuliko sisi na wakusujudie siyo wewe ila Yesu Kristo ndani yako,Kila mikono yako itakachogusa,Mungu amegusa,ukinena ni Kristo amenena,maneno yako yawe na neema huku yakiwa yamekolea munyu yamfae kila muhitaji katika jina la Yesu.
Yesu Kristo atembee ndani yako,katikati yako na kwa watu kupitia wewe katika jina la Yesu!
Shalom.

20/04/2018

Somo la leo:
Sharoom,sharoom, wanafunzi wa Yesu.Yesu Kristo asifiwe. Leo tutakuwa na somo linalosema:-ILI UISHI MAISHA YA USHINDI UNAHITAJI KUWA MTU WA KUSAMEHE.
Mathayo18:21"Kisha petro akamwendea akamwambia, Bwana ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimi nimsamehe?Hata mara saba?22Yesu akamwambia, sikuambii hata mara saba,hata saba mara sabini."
Yesu anajibu swali la petro juu ya kiasi gani naweza kumsamehe mdeni wangu(mkosaji).Yesu anampatia majibu ambayo hakuyatazamia-7*70!!hii inamaanisha kuwa kusamehe uwe ni mfumo rasmi ambao ni endelevu,kwasababu katika maisha tunayoishi tunakutana na vitu mambo na watu wa aina tofauti tofauti wenye mira na desturi tofauti tofauti ambapo kuishi pasipo kukoseana ni vigumu lakini kukiwa na mfumo wa kuchukuliana na kusameheana maisha yatasonga na wengi watapata kujirekebisha na kubadilika.
Kwa wanafunzi wa Yesu ni muhimu tena ni lazima kusamehe(hata k**a mkosaji hajaja kukuomba msamaha)kwaajili ya faida yako mwenyewe kwani pasipo kusamehe Mungu wa mbinguni hawezi kutusamehe wala kupokea na kuyajibu Maombi yatu.mathayo 6:12"utusamehe deni zetu(makosa)kam sisi nasi tunavyowasamehe wadeni wetu(wanaotukosea).mathayo 6:14"kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao,na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi! Kwahyo ili tupate msamaha mbele za Mungu lazima tusamehe waliotukosea.
Usiposamehe huwezi kuishi maisha ya ushindi kwani huwezi kumshinda adui yako. Kumbuka adui yatu mkubwa ni shetani kwahyo hata inapotokea mtu amekukosea siyo yeye aliyepanga kukufanya vibaya bali ni roho ya shetani nyuma yake iliyomsukuma kufanya vile,sasa huwezi kumshinda shetani kwa kumwekea mtu aliyekukosea kisasi lakini kwa njia ya kumsamehe na kumwombea utakutana na adui halisi na kumshinda na hatimaye hata yeye aliyekufanyia ubaya utakuwa umemsaidia kujitambua.Neno katika mathayo5:44"wapendeni adui zenu,waombeeni wanao waudhi ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni....! Umeona,tunaambiwa tuwapende adui zetu na kuwaombea wanaotuudhi kwanini, kwasaba

12/04/2018

NENO LA LEO:-
NGUVU YA UUMBAJI KATIKA KINYWA CHAKO.
Mithar18:20-21."Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake, Atashiba mazao ya midomo yake.Mauti na uzima huwa Katika uweza wa ulimi,na wao waupendao watakula matunda yake."
Nakusalimu mwanafunzi wa Yesu katika jina la Yesu Kristo aliye hai!
Utangulizi wa neo la Mungu unatuambia kuwa maisha ya mtu yatakuwa na utele(kushiba)katika kila eneo Kwa kutegemea namna ya kutumia kinywa chake(maneno) kwasababu ndani ya kinywa cha mtu kuna uwezo wa kuua(mauti)na pia kuna uwezo wa kuuisha(kufanya uhai hata kwa vitu vilivyo kufa) kwahyo namna unavyoweza kutumia kinywa chako ndo namna utakavyopata matunda yake!ndomana akasema wao waupendao watakula matunda yake.
Asilimia kubwa ya namna ilivyo hali ya watu iwe kiroho au kimwili ni matokeo ya namna walivyotumia vinywa vyao! Wewe hujawai kujiuliza kwanini ukiomba kazi katika taasisi nyingi watakufanyia usaili na moja kati ya kipengele watakachokufanyia ni kwenye eneo la kujieleza wakiamini kuwa maneno yako yanabeba utambulisho wa kuwa wewe ni nani na unauwezo gani hata kuwafaa Katika kufanya nao kazi!!
Ni namna gani maneno yana nguvu ya uumbaji?
Mwanzo1:1-3"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi, nayo nchi ilikuwa ukiwa tena utupu,na giza lilikuwa juu ya vilindi vya uso wa maji,Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa Maji.Mungu akasema,iwe nuru, ikawa nuru."
Mungu alipoona nchi imekuwa ukiwa tena utupu(formless),giza limetanda,hakuna hali ya kuvutia,ingawa ndani yake(Mungu)alikuwa na picha ya vile anavyotaka dunia iwe.alikuwa na picha ya milima na mabonde,picha ya inchi kavu na bahari, jua na mwezi ...!lkn akaona kuwa ili iwe rahisi kuumbika lazima airuhusu Roho yake itulie juu ya uso wa maji kwani alijua kuwa Roho yake ikitulia juu ya uso wa maji haitakuwa kazi ngumu kuzitoa zile picha zilizopo ndani yake za namna anavyotaka dunia iwe kwani atazitoa nje Kwa kutamka neno tu,kwanini, kwasababu Roho wa Mungu(Roho Mt) tayari yuko juu ya uso wa Maji kwaajili ya kuumba.kumbuka k

10/04/2018

NENO LA LEO:UMEZALIWA ILI UISHI MAISHA YA USHINDI.
"Kwa maana kila kilichozaliwa na Mungu,huushinda ulimwengu,na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu,hiyo imani yetu.(1yohana5:4).
Neno la Mungu ndiyo kioo cha kutuonesha uhalisia wetu ulivyo katika Kristo Yesu.Hii ndiyo inayonipa ujasili wa kusema kuwa wewe siyo vile watu wanavyosema bali ni vile neno la Mungu linavyokuita na kukuona kwani neno la Mungu ni Mungu mwenyewe.(yohana 1:1).Neno linatuambia kuwa sisi tumezaliwa si kwa mbegu inayoharibika,bali isiyoharibika,neno LA uzima ambalo linadumu milele(1petro1:23).Pia neno ndani yake limebeba roho inayoleta uhai wa mtu au kitu hata kuweza kuishi(yoh6:63),ndiyomaana hata petro alipokuwa amechoka asubh baada ya kufanya kazi ya kujichosha ya kutafuta samaki usiku kucha bila kupata chochote,baada ya kuambiwa na Yesu"nenda mpaka kilindini mkatwike nyavu,"akamjibu kuwa Bwana tumefanya kazi ya kujichosha usiku kucha lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu".biblia inasema baada ya kwenda na kufanya kwa neno la Yesu lenye uhai(roho),petro alipata samaki wengi sana(luka5:1-6).
Katika fungu letu la kwanza la 1yohana5:4 tunaambiwa kuwa kila kitu kilichozaliwa na Mungu kinauwezo wa kuushinda ulimwengu,anavyosema ulimwengu maana yake vitu,watu pamoja na mifumo yoote ambayo kwa namna moja inaweza kuleta changamoto au ukinzani wa kukuzuia kufikia mafanikio yako iwe kiroho au kimwili!
Mungu ameamua kuzungumzia kitu(kila kitu)ilimladi kina roho wa Mungu ndani yake ambayo imekuwa imparted kupitia wewe,kina uwezo wa kushinda changamoto mbalimbali hata kufikia malengo ndiyo maana hata mifupa mikavu katika bonde kipindi cha ezekiel baada ya kupata roho(uhai)kwa neno la Mungu kupitia nabii ezekiel iliweza kuungana na kuanza maisha.
Niseme jambo hapo kwako wewe mwanafunzi wa Yesu Kristo,K**a neno linasema kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu,je wewe si zaidi ya kitu! Wewe siyo kitu,wewe ni Mtu ni zaidi ya kitu kwahyo ushindi katika kila hali ya maisha ni lazima katika

07/04/2018

We are ordered by our Lord Jesus Christ to make people disciples through the gospel,then teach them the true word of God after being baptized by the holy spirit. This is the foundation of our Ministry. Methew 28:19-20,John8:31-32.

Address

Iringa

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Discipleship International Ministry - Dim posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Discipleship International Ministry - Dim:

Share