12/02/2023
THEME: JESUS WILL ASTOUND YOU
SOMO: YESU ATAKUSHANGAZA
Teacher: Pastor J Lekeni
Luka 5 :1-11 (Luke 5 : 1 -11)
1 Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti,
2 akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa, lakini wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao.
3 Akaingia katika chombo kimoja, ndicho chake Simoni, akamtaka akipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni.
4 Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.
5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.
6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;
7 wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama.
8 Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini pa Yesu, akisema, Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana.
9 Maana alishikwa na ushangao, yeye na wote waliokuwa pamoja naye, kwa sababu ya wingi wa samaki walioupata;
10 na kadhalika Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, waliokuwa washirika wa Simoni. Yesu akamwambia Simoni, Usiogope, tangu sasa utakuwa ukivua watu.
11 Hata walipokwisha kuviegesha pwani vyombo vyao, wakaacha vyote wakamfuata.
Wafilipi 4:6 (Philipians 4:6)
Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
Zaburi 34:4 (Psalm 34:4)
Nalimtafuta Bwana akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote.
Zaburi 37:5 (Psalm 37:5)
Umkabidhi Bwana njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.
Zaburi 55:22 (Psalm 55:22)
Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.
Zaburi 123:1-4 (Psalm 123:1-4)
1 Nimekuinulia macho yangu, Wewe uketiye mbinguni.
2 K**a vile macho ya watumishi Kwa mkono wa bwana zao K**a macho ya mjakazi Kwa mkono wa bibi yake; Hivyo macho yetu humwelekea Bwana, Mungu wetu, Hata atakapoturehemu.
3 Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu sisi, Kwa maana tumeshiba dharau.
4 Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha, Na dharau ya wenye kiburi.