TAG ZIZI

TAG ZIZI Tunamshukuru Mungu kanisa la TAG Z**I kwasasa tunapatikana kupitia ukurasa wetu huu wa Face book, Tu

Hizi ni baadhi ya picha za matukio katika Mkutano wa Injili, uliofanyika kuanzia Tarehe 16-23-08-2020, katika Viwanja Z*...
27/08/2020

Hizi ni baadhi ya picha za matukio katika Mkutano wa Injili, uliofanyika kuanzia Tarehe 16-23-08-2020, katika Viwanja Z**I CHRISTIAN CENTRE.

Karibuni sana kwenye semina, itakayo anza jumatatu hadi jumapili, hapa TAG-Z**I CHRISTIAN CENTRE(ZCC).
22/08/2020

Karibuni sana kwenye semina, itakayo anza jumatatu hadi jumapili, hapa TAG-Z**I CHRISTIAN CENTRE(ZCC).

Karibuni sana watu wote, Mwalike na Rafiki yako, Kupitia Mkutano huu, Mungu anaenda kukutana na mahitaji yako kwa viwang...
04/08/2020

Karibuni sana watu wote, Mwalike na Rafiki yako, Kupitia Mkutano huu, Mungu anaenda kukutana na mahitaji yako kwa viwango vya tofauti sana. Kwa Maelekezo zaidi wasiliana nasi: 0767 469 595, 0784 469 595, 0673 469 585

SOMO: UKIAMINI YOTE YAWEZEKANAIMANIMaandiko: Marko 9:19-2319 Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi h...
30/07/2020

SOMO: UKIAMINI YOTE YAWEZEKANA

IMANI

Maandiko: Marko 9:19-23

19 Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Nichukuliane nanyi hata lini? Mleteni kwangu 20 Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu. 21 Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto. 22 Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia. 23 Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. 24 Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu.

Imani ya kweli katika Yesu ni msingi imara katika maisha ya kiroho. Ni jibu la mambo yote. Ni mkono unaochukua majawabu ya mahitaji yetu kutoka ulimwengu usioonekana na kuyafikisha kwenye ulimwengu wa mwili, tukaona kwa macho na kushika kwa mikono yetu.

Imani ni nini?
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
(Ebr 11:1)

Imani inakuthibitishia kuwa kitu unachokihitaji kimepatikana sasa wakati kinatarijiwa; imani inakiona:kitu halisi na kukik**ata wakati hakipo.

Nchi ya Israeli ilikumbwa na ukame mbaya sana, ikatokea njaa kali, ikasababisha watu kula watoto wao, punda na mavi ya njiwa. Katika nyakati hizo za ukame nabii Elisha aliyekuwa na imani katika Mungu alitangaza kuwa kesho kutapatikana unga tele na nafaka mbalimbali. .Imani iliona mbali ikavuka mipaka ya ufahamu wa kibinadamu. Askari wa mfalme aliona kmwili Elisha aliona kiroho.
Elisha akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria (2Fal 7:1)
Kesho yake kweli yote yalitimia; soma (2Fal 7:1-20) Askari wa mfalme alikufa kwa kutokuamini.

Imani inazaliwa na inakua.
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. (Rum 10:17)
Imani ya kweli inazaliwa kwa kusikia Neno la Kristo. Imani inakua kila wakati inapotumika kuleta majibu ya mambo magumu. Yesu alifundisha somo la imani inayoleta matokeo.
(Mathayo 17:20) Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amini, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.

Imani inayoweza kuhamisha milima ya matatizo yako yote, inanza na kiasi cha punje ya haradali iliyo ndogo kuliko punje ya mchicha. Fahamu kuwa punje hiyo ikipandwa inaota na kukua hadi kuwa mti mkubwa. Na imani yako itakua kwa kadiri unavyoitumia kutatua matatizo yanayokukabili siku kwa siku.

Daudi alikuwa na ujasiri wa kukabiliana na Goliathi kwa sababu imani yake ilikua katika Bwana kwa kuwaua simba na dubu.

(1Sam17:36 ) Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa k**a mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.

Baba wa kijana tuliyemsoma hapo juu alimwomba Yesu kwa mashaka akisema, “lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia”. Bwana Yesu alimjibu kwa maneno yake , “Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye”. Yule baba alitambua haraka kosa lake akatubu na kuamini. Yesu akamponya mwanawe saa ileile.

Kizazi chetu tunafanana na baba huyo; tunafahamu kuwa Yesu anaponya, anaokoa na kutenda miujiza mingi. Inapokuja kwenye mahitaji yako wewe binafsi imani inapungua. JiulizeYesu amekufanyia nini? na unamtarajia akufanyie nini katika matatizo yako? Je unaamini kweli anaweza? Je moyoni mwako mna mahangaiko na kutangatanga kutafuta ufumbuzi?. Kutokuamini ni dhambi na kunakukosesha majibu ya mahitaji magumu ya moyo wako. Mungu hashindwi na neno lolote.

Ushuda wa kweli : Umetokea katika nyanda za juu kusini mwa Tanzania.
Mama mmoja alikuwa na tatizo katika kizazi, akafanyiwa upasuaji wa kukiondoa. Hakuwa amejaliwa mtoto yeyote. Alihuzunika sana kukosa mtoto. Akaamua kumwamini Mungu atendaye miujiza kupita fahamu za kibinadamu. Akatamka nitazaa mtoto kwa tumbo langu na kumnyonyesha kwa matiti yangu. Madaktari walimkanusha na watu wakamdhihaki. Muda si mrefu akayaona anabadilika , miezi tisa akazalishwa mtoto mzuri na daktari yuleyule aliyeondoa tumbo la uzazi. Mungu ni wa kushangaza ndiyo sababu anaitwa MUNGU anafanya njia pasipo na njia.

Alimpa mtoto mama asiye na tumbo la uzazi, atakosaje wewe mtoto uliye na tumbo? muujiza ni wako wewe, gharama ni imani ya kweli kwa Yesu , anakwambia,” Yote yawezekana kwake aaminiye.”

Rev. Mwl. F.M.Swenya
Mawasiliano:
+255 67 469 595, 0784 469 595
Email: [email protected]

SOMO: USIOGOPE MWAMINI YESUHofu nini?Hofu ni hisia inayosababishwa na hatari au tishio.Hofu huanzia kwenye ubongo baada ...
11/07/2020

SOMO: USIOGOPE MWAMINI YESU

Hofu nini?
Hofu ni hisia inayosababishwa na hatari au tishio.

Hofu huanzia kwenye ubongo baada ya kupata taarifa ya hatari au tishio kupitia milango mitano ya fahamu: yaani kuona, kusikia, kunusa, kuonja na kugusa. Mwitikio huu wa hofu huenea mwili mzima.

Hisia hizi zina nguvu sana, husababisha athari mbaya za kiakili, kimwili na kiroho.

Kiakili:- Hofu inamwondolea mtu utulivu wa mawazo, umakini na busara ya maamzi mazuri. Mtu anaweza kukimbia hovyo, kujificha na kufeli masomo katika mitihani.

Kimwili:- Hofu inasababisha maumivu ya kifua au tumbo, midomo kukauka, kichefuchefu, mapigo ya moyo kwenda mbio, kupumua kwa shida, kutetemeka, kukosa usingizi nk

Kiroho:- Hofu inasababisha mtu kusahau ahadi za Mungu, matendo makuu aliyotendewa na mwisho kupoteza kabisa imani kwa Mungu.

Vyanzo vya hofu ni vingi sana kutegemea mhusika na mazingira yake. Hatari na matisho yanaweza yakalenga: afya, familia, uchumi, masomo, hatima ya maisha nk. Mungu anajua mapito yako na yupo karibu nawe akusaidie.

Bwana Yesu anasema hivi katika (Yn 14:1) Msifadhaike mioyoni mwenu; mwaminini Mungu, niaminini na mimi. Jibu la hofu zako ni kumwamini Mungu katika Jina la Yesu. Mungu ndiya msaada wa kweli katika hatari na majanga ya aina zote .Kwa sababu Mungu mwenyewe ameahidi katika Neno lake anasema:-
Kwa maana mimi, Bwana, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia. (Isaya 41: 13)
Bwana, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, ... (Isaya 44: 2)

Mpendwa msomaji wangu, unapopita katika majaribu mazito, usiogope maana Mungu yupo kukusaidia. Haijalishi ukubwa wa jaribu wala uhalisia wa madhra yanayoweza kutokea.

Nimekwambia hofu huanzia kwenye ubongo, unaweza kuona au kusikia maafa makubwa yaliyotokea mahali fulani yakakuogopesha na kupoteza imani. Mfano covid 19 ilipolipuka ilitikisa dunia na kuua watu wengi sana katika nchi zilizoendelea tofauti na Tanzania nchi changa kiuchumi, kitekinolojia na hata kiutaalam. Ukweli corona iliingia Tanzania lakini madhara yake hayakuwa makubwa k**a ilidhaniwa na shirika la afya la dunia WHO. Siri yake ni nini?

Mheshimiwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania alilitia moyo taifa letu lisiogope corona kupitiliza na alipiga mbiu ya maombi ya kitaifa ya siku tatu. Alisisitiza imani kwa Mungu zaidi ya dawa madaktari na barakoa, bila kupuuza tahadhari za wataalamu wa afya.

Tunamshukuru Mungu aliyeingilia kati kuliponya taifa letu la Tanzania na covid 19 ikiwa ni matokeo ya majibu ya maombi yaliyofanyika nchi nzima na baadhi ya madhehebu yaliendelea kuliombea taifa bila kukoma. Mataifa ya ya nje yanaishangaa Tanzania kulikoni ? Jibu kuna Mungu aliyesikia maombi ya watanzania waliyoomba kwa imani bila hofu wala mashaka.
Ahadi za Mungu ni kweli, tukilishika Neno na kufanya maagizo yake anatuponya kabisa.

Ee nchi, usiogope; furahi na kushangilia; kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu. (Yoel 2: 21)
Akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye. (Kutoka 15:26)

Mpendwa wangu, katika matatizo yako magumu ya kutisha, usiogope, sikiliza Neno lake, tenda maagizo yake na umwamini Yesu Kristo kwa kumaanisha kuwa yeye ni mwokozi hutaangamia. Neno la Mungu linakwambia:-

Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu. Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza. ( Zaburi 91:14-15) Tena anasema
Naye Bwana, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike. (K*m 31:8)

Kwa ahadi za uhakika namna hii unayo sababu gani ya kuogopa? Kwa nini umwache Mungu, ujiingize kwenye ushirikina ukidhani utapata msaada kwa waganga wa kienyeji?. Unapopita katika nyakati ngumu ni vita, usipokuwa jasiri utashindwa. Mungu anasema:-

Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako. (Yos 1: 9)

Mungu ni msaada wako wa karibu, unaopatika tele wakati wa mateso. Mwite atakuitikia. Mtwishe mizigo yako atakuchukulia na umwamini katika vita vyako atakupigania. Anapenda kukuona unaishi maisha ya amani na utulivu ndiyo sababu ya Yesu kuja duniani. Ubarikiwe.
Rev. F. M. Swenya
Wasiliana nami: 0767 469 595/0784 469 595/0673 469 585

Address

P. O. BOX 2255
Iringa

Telephone

+255767469595

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TAG ZIZI posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to TAG ZIZI:

Share