Efatha Church - Ukombozi

Efatha Church - Ukombozi Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Efatha Church - Ukombozi, Religious organisation, Iringa, Iringa.

NAIBARIKI IJUMAA YANGU. Jina la BWANA ni Ngome Imara; Mimi ni Mshindi.
22/05/2026

NAIBARIKI IJUMAA YANGU.

Jina la BWANA ni Ngome Imara; Mimi ni Mshindi.

Karibu sana katika semina ya kipekee itakayofanyika Efatha Church Iringa - Wilolesi kuanzia tarehe 09 mpaka 11 April, 20...
08/04/2026

Karibu sana katika semina ya kipekee itakayofanyika Efatha Church Iringa - Wilolesi kuanzia tarehe 09 mpaka 11 April, 2026. Ni wakati wa kuvunja vifungo na kupokea hatua mpya ya mafanikio kwa familia yako na uchumi wako kupitia mtumishi wa Mungu, Kuhani Zebedayo Sanga.

πŸ“… Tarehe: 09 - 11 Aprili, 2026
πŸ•˜ Muda: Saa 9:30 Alasiri – 12:00 Jioni
πŸ“ Mahali: Wilolesi, Iringa

Usipange kukosa! Mkaribishe na ndugu, rafiki au jirani ambaye anahitaji kuguswa na mkono wa Mungu. Tuonane hapo! πŸ™Œ

NAIBARIKI ALHAMISI YANGU. Mimi ni Mtakatifu wa BWANA, Mimi ni Mbarikiwa wa BWANA; Kwangu hakutapungua Kicheko, Sherehe, ...
19/02/2026

NAIBARIKI ALHAMISI YANGU.

Mimi ni Mtakatifu wa BWANA, Mimi ni Mbarikiwa wa BWANA; Kwangu hakutapungua Kicheko, Sherehe, Furaha, Tafrija, Karamu na Utele.

NAIBARIKI JUMAMOSI YANGU. Mimi ni Mtakatifu wa BWANA, Mimi ni Mbarikiwa wa BWANA; Mimi sifi kwa magonjwa au ajali wala k...
14/02/2026

NAIBARIKI JUMAMOSI YANGU.

Mimi ni Mtakatifu wa BWANA, Mimi ni Mbarikiwa wa BWANA; Mimi sifi kwa magonjwa au ajali wala kwa mapenzi ya yule mwovu ama ya wanadamu.

NENO LA SIKUNa Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la EfathaTarehe 13/02/2026SOMO: NI WAKATI WA KUPOKEA BARAK...
13/02/2026

NENO LA SIKU

Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha

Tarehe 13/02/2026

SOMO: NI WAKATI WA KUPOKEA BARAKA ZAKO USISINZIE

Waefeso 5: 14-17 β€œHivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza. Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si k**a watu wasio na hekima bali k**a watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana”.

Wakati wa Maachilio au Marejesho ya baraka zako, uponyaji, miujiza na mengine uliyotamani kwa muda mrefu umewadia. Amka kaa katika nafasi yako ili iwe rahisi kuyapokea kwa maana Mungu hatakawia na watu watajua umekutana naye. Kuwa macho ni ile hali ya kukiri Neno, kuomba bila kukoma, kutangaza Ushindi uliopata katika Yesu Kristo na kudumu katika imani.

Kusinzia ni kulala pasipo ridhaa yako kwa sababu ya nguvu inayokuzuia ushindwe kukaa macho. K**a ilivyo unaposinzia kimwili, unakuwa haujui kinachoendelea; ndivyo ilivyo kiroho unapotazamia jambo lakini unashindwa kulisubiri huko ni kusinzia. Unaweza ukasinzia katika ndoa, matoleo, kusoma au kuomba kwa sababu ya hiyo nguvu. Kusinzia huletwa na uchovu, uvivu, kutokumaanisha na kutokuzingatia jambo unalotazamia. Unasinzia kwa kuishi maisha ya kujichanganya, mashaka na kutoliamini Neno la Mungu.

Baraka au tarajio lako linapochelewa unasinzia kwa sababu moyo wako unashindwa kutazamia au kusubiri. Shetani akijua kuwa unao ufahamu kuhusu Mungu, ufahamu huo ni tishio kwake kwani anakuwa hana uwezo wa kukuzuia wala kukushambulia kwa maana ufahamu huo unakupa kuwa macho kiroho. Hivyo ili aweze kukupata atakuletea nguvu inayopingana na huo ufahamu ili usinzie kiroho, ukate tamaa na kupoteza changamko lako ili aweze kufanya kile anachokitaka katika maisha yako.

Ili kupokea uliyoandaliwa amka uwe macho wala usikubaliane na maisha duni uliyonayo maana huo siyo mpango wa Mungu kwako. Mungu anakusubiri uamke ili akupe taraja lako.

NAIBARIKI IJUMAA YANGU. Mimi ni Mbarikiwa wa BWANA, Mimi ni Mtakatifu wa BWANA; adui zangu wote wamewekwa chini ya miguu...
13/02/2026

NAIBARIKI IJUMAA YANGU.

Mimi ni Mbarikiwa wa BWANA, Mimi ni Mtakatifu wa BWANA; adui zangu wote wamewekwa chini ya miguu Yangu, Mimi ni Mshindi.

NENO LA SIKUNa Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la EfathaTarehe 12/02/2026SOMO: MUNGU HULIANGALIA NENO LAK...
12/02/2026

NENO LA SIKU

Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha

Tarehe 12/02/2026

SOMO: MUNGU HULIANGALIA NENO LAKE ILI ALITIMIZE

Yeremia 1:12 "Ndipo BWANA akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize."

Chochote hapa Duniani kina Mipaka na kina Mwisho wake. Chochote kinachofanyika hapa Duniani ni tukio kwa hiyo kuna Muda wa kuanza na kuna Muda wa kukoma, hivyo usisukumwe na vitu vilivyo na Mwisho. Kuna jambo moja lisilo na mwisho nalo ni Neno la Mungu; Mungu ana Neno lake, analituma kwetu ili tupate kuponyeka. Neno halina mwisho lakini mara zote lina jambo la kutimiza. Neno likitumwa kwa mtu au mahali lina kuwa na Kazi maalum ya kufanya, kwa hiyo Neno la Mungu linapoenea inamaana kuna kitu cha kutendea Kazi.

Neno la Mungu linaponenwa kwako linakuwa na Nguvu ya kutekeleza kile kilichotamkwa; hivyo uwe na Amani, Uwe tayari kukamilisha Kazi ya Mungu kwa sababu Mungu anataka ukamilishe. Hakuna anayeweza kumzuia Mungu anachotaka kufanya kwako.

Wakati wote tamani kusoma Neno la Mungu na uombe sawa sawa na hilo Neno kwani hapo ndipo zilipo ahadi za Mungu; ukiomba sawa sawa na Neno Mungu atatenda kwako kwani Yeye mara zote huliangalia Neno lake ili apate kulitimiza.

12/02/2026

The wisdom that speaks

NAIBARIKI ALHAMISI YANGU. Mimi ni Mtakatifu wa BWANA, Mimi ni Mbarikiwa wa BWANA; Mimi sitapungukiwa na kitu.
12/02/2026

NAIBARIKI ALHAMISI YANGU.

Mimi ni Mtakatifu wa BWANA, Mimi ni Mbarikiwa wa BWANA; Mimi sitapungukiwa na kitu.

Address

Iringa
Iringa

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church - Ukombozi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share