AICT Iringa

AICT Iringa Kumwabudu Mungu kwa roho na kweli tukiishi katika maisha utoshelevu.

Kanisa linalohubiri na kufundisha Injili ya Yesu Kristo kwa usahihi na kumhudumia mwanadamu katika ukamilifu wake kwa msingi wa Neno la Mungu.

10/05/2024

Naitwa Emmanuel Nyamalya, ni Mchungaji wa AICT na Mratibu wa Community Bible Study (CBS) kwa nchi ya Tanzania, naishi Iringa.

CBS ni huduma ya Kujisomea Biblia isiyo ya kidhehebu iliyoanza mwaka 1975 na darasa moja huko Marekani. Leo ni huduma inayokua kwa kasi sana kwa watu wa marika yote katika nchi zaidi ya 120 na lugha 92. Maelfu ya watu wanajihusisha na Mungu na Neno lake. Maono yetu ni maisha yanayobadilishwa kupitia Neno la Mungu. Utume wetu ni kufanya wanafunzi wa Bwana Yesu Kristo katika jumuia zetu kwa kujali na kujisomea Biblia kwa kina, hupatikana kwa watu wote.

Karibu katika Mwezi huu wa 5 tulioutenga kuwa Mwezi wa Ukarimu.

Lengo ni kushirikisha fursa ya kusaidia kifedha kuenea kwa Biblia na matokeo yake nchini na barani Afrika. Tunaamini kwamba makanisa ya Tanzania, washiriki wa CBS na akina kaka na dada wengine wenye moyo wa ukarimu, mna uwezo wa kipekee na fursa hii ya kuimiliki huduma kifedha, na kuendelea kwa uendelevu kutetea utume wa CBS kimataifa. Watanzania tunaweza kutoa kile tulichonacho kuwabaraki watu wengine nchini kwetu na ulimwenguni kote.

Mwezi wa Ukarimu unakupa fursa ya kuwezesha mtu angalau mmoja aliye na shauku ya kujifunza zaidi kuhusu Mungu na tumaini Analoleta, kupata Biblia na kitabu chake cha kujifunzia. Kila shilingi unayochangia itatumika kwa uaminifu kumnunulia mtu mmoja kitabu au Biblia. Mwaka jana, 2023 wafungwa 133 walipokea Biblia 63 na vitabu 485 vya Kujifunzia Biblia. Tumeona maisha ya watu yaliyobadilika yakiwa chachu ya jamii nzima kubadilika. Unapotoa kwa ukarimu mwaka huu 2024 utasaidia kuleta mwamko wa Neno la Mungu kwa watoto na vijana na wasiojiweza.
Unafikiri kwa nini utoe?
1. Kuwezesha kuwanunulia Biblia na vitabu vya masomo watu wasio na uwezo wa kununua k**a vile wafungwa, yatima, wanafunzi, wakimbizi na kadhalika. Kwa mfano, ukitoa TZS 24,000 utakuwa umempatia mtu mmoja Biblia. Ukitoa 1,000 utakuwa umemnunulia mtu mmoja kitabu cha kujifunzia.

2. Kufikia maeneo ambayo hayajafikiwa ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Hapa Tanzania CBS haijafika mikoa ya Kagera, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Kigoma, Tanga na mikoa yote ya Zanzibar. Unapotoa unapeleka huduma ya Kujifunza Biblia kwa kina katika mikoa mingine. Kwa kuwa umepokea agizo la utume mkuu, basi, una fursa ya kuunga mkono utume mkuu.

3. Unapotoa kile ulichonacho unashiriki kuwekeza katika ufalme wa Mungu; hivyo, kuwezesha huduma za CBS kuendelea kupanuka na kustawi. Naomba usiache nafasi hii inayopatikana na ya heshima kufanya kazi na Mungu ikupite. K**a unacho kitu cha kula kila siku, basi tayari unacho kitu cha kutoa kwa Mungu kila siku. Mungu akujalie, utoapo kwa ukarimu.

Basi nakuomba tafadhali sana utumie fursa hii kushiriki baraka hizi. Inaweza kuwa TZS 1,000/ 2,000/ 5,000/ 10,000/ 50,000/ 100,000/ 1,000,000/ 5,000,000/ 10,000,000 au zaidi. Vinaweza kuwa vitu k**a vile: Kuku, Mbuzi, Ng’ombe, mahindi, maharage, viazi, mihogo, miti, madini au kingine chochote.

Unaweza kuchangia kupitia akaunti ya huduma iliyoko BANK YA CRDB
AKAUNTI NAMBA: 015C 493 655 800
JINA: AICT COMMUNITY BIBLE STUDY IRINGA
AU MPESA 0762 032 766
JINA: EMMANUEL BWIRE NYAMALYA
Baada ya kuchangia unaweza kutuma fomu ya kuweka fedha au ujumbe ili kupata stakabadhi.
Mungu akubariki kwa sadaka yako ya moyo wa ukarimu unaposhiriki baraka hizi ambazo Mungu amekupa nafasi. Amina.
Kwa maelezo zaidi unaweza kupiga namba 0736 998 144

21/04/2023

Welcome to our AICT Iringa Church Page. We have eligible theologians who serves you with pure theology.

Rev. Nyamalya is attending the ordination of Bishop Katoto and the inauguration of the AICT Kati Diocese at AICT Kizota ...
27/11/2022

Rev. Nyamalya is attending the ordination of Bishop Katoto and the inauguration of the AICT Kati Diocese at AICT Kizota in Dodoma.

Rev. Emmanuel Nyamalya is travelling to Dodoma for the ordination of Bishop Katoto
26/11/2022

Rev. Emmanuel Nyamalya is travelling to Dodoma for the ordination of Bishop Katoto

03/10/2022
Juma la wanawake AICT Iringa limehitimishwa kwa Mgeni Rasmi Mheshimiwa Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Iringa, Dora Nz...
25/09/2022

Juma la wanawake AICT Iringa limehitimishwa kwa Mgeni Rasmi Mheshimiwa Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Iringa, Dora Nziku, kupiga picha pamoja na wachungaji na mjumbe wa Sinodi. Hitimisho liliandamana na changizo la kutunisha mfuko wa idara na kuchangia ujenzi wa choo bora.

Asante sana mliotuombea na kutushika mkono.

24/09/2022

Karibu Africa Inland Church Mshindo, Iringa barabara ya Ipogolo

20/09/2022

Kichwani mwa mtu mna mipango mingi, lakini anachokusudia Mwenyezi-Mungu ndicho kitakachofanyika.
Methali 19:21 BHN

21/08/2022

Watoto, Vijana na walimu wao wakihitimisha kambi ya Neno la Mungu kanisani leo Jumapili 21/08/2022.

Mch Emmanuel B. Nyamalya involved in training leaders in Christian Education and CBS at AICT Iringa today Friday 5 Augus...
05/08/2022

Mch Emmanuel B. Nyamalya involved in training leaders in Christian Education and CBS at AICT Iringa today Friday 5 August, 2022.

Mch Kiongozi wa Pastoreti ya Iringa, Emmanuel Nyamalya, akitambulisha huduma ya kujisomea ya Biblia isiyo ya kidhehebu (...
11/07/2022

Mch Kiongozi wa Pastoreti ya Iringa, Emmanuel Nyamalya, akitambulisha huduma ya kujisomea ya Biblia isiyo ya kidhehebu (Community Bible Study) kwa maaskofu, wachungaji na viongozi wengine wa madhehebu ya Kikristo. Semina iliyofanyika mjini Tabora 8-9/7/2022 ambayo ilihudhuriwa na washiriki zaidi ya 156.

Address

Ruaha
Iringa

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 15:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00
Saturday 08:00 - 15:00
Sunday 07:00 - 18:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AICT Iringa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share