TAG CCC Chato

TAG CCC Chato TAG Chato Christian Centre (CCC)
We invite everyone to join us in Worshipping Our most hight God.

Tunamshukuru Mungu tumekuwa na Mkutano wa baraka sana na wengi wamempokea Yesu Kristo.
26/05/2024

Tunamshukuru Mungu tumekuwa na Mkutano wa baraka sana na wengi wamempokea Yesu Kristo.

IBADA YA TAREHE 07/04/2024MNENAJI: Pst. Zephirine kahigwaSOMO: KUMTUMIKIA MUNGU KWA NJIA YA SADAKA KWA MOYO WA KUPENDAma...
07/04/2024

IBADA YA TAREHE 07/04/2024
MNENAJI: Pst. Zephirine kahigwa
SOMO: KUMTUMIKIA MUNGU KWA NJIA YA SADAKA KWA MOYO WA KUPENDA

mathayo 6:19-3

Mambo mawili ya kuelewa kabla ya kumtolea Mungu sadaka

1. Elewa cha utoaji
Zaburi 24:1
Kutoka 19:5
Zaburi 50:10

Kiini cha utoaji ni kua Mungu Ndie anae miliki vitu vyote

2. Elewa Sheria ya utoaji

Mungu ana tuamuru kumrudishia kila ambacho Alitupa

07/04/2024
Praising God
07/04/2024

Praising God

Jerusalem choir ministeringTAG CCC Chato
07/04/2024

Jerusalem choir ministeringTAG CCC Chato

  Tarehe 31/0/2024Na,Rev. Zephrine Kahigwa Ujumbe: Ushindi ulio katika Ufufuo wake KristoMathayo 28:1-28, Luka 23:50-56U...
01/04/2024


Tarehe 31/0/2024

Na,
Rev. Zephrine Kahigwa
Ujumbe: Ushindi ulio katika Ufufuo wake Kristo
Mathayo 28:1-28, Luka 23:50-56

Utangulizi;
👉🏾Ufufuo wa Yesu Kristo ni moja ya kweli kuu za Injili. Yesu ni tofauti kabisa na mtu mwingine yeyote na utofauti wake mkubwa ni kule kufufuka na kuacha kaburi.
👉🏾Kufufuka kwake kunathibitisha kuwa, yeye ndiye mwana wa Mungu kweli kweli.

📌Matukio Makuu yanayotokana na Ushindi ulio katika kufufuka kwake Yesu;
1. Yeye Yesu, aliizika mauti na akaleta uzima alipofufuka kutoka kwa wafu.
Yohana 11:25 - 26, 32-44
👉🏾Uzima wa Yesu unafanya mambo mengi mbali na kutuingiza mbinguni, hapa duniani bado uzima huu hufanya vitu vingi vya kutufanya tuishi k**a washindi.

2. Yeye alibeba dhambi zetu ili sisi tusiishi katika dhambi tena.
Warumi 5:8, 6:6
👉🏾Dhambi hubebwa nau hukaa ndani ya utu wa kale
👉🏾Utu wa kale, ni utu wa mtu ambaye hajaokolewa, utu huu wa lake hufa pamoja na kristo msalabani ili mwamini apokee uzima mpya ndani ya Kristo.
Wagalatia 2:20
👉🏾Sisi tuliosulubiwa pamoja na Kristo, sasa tunaishi pamoja naye katika maisha yake ya ufufuo. Yeye Yesu akifanyika, chanzo na kiini cha mawazo, akili, maneno na matendo yetu.
👉🏾Ule utumwa wa mwili kutumikia dhambi, umevunjwa. 2Wakorintho 5:17,
👉🏾Ili uhamishwe kutoka kwenye utumwa huo wa dhambi, ni lazima mtu akubali kununuliwa na Kristo kwa damu yake. Ukisha kununuliwa, utawajibika kuishi maisha ya yule (yaani Mungu) aliye kununua (lazima ubadilike). Ufunuo 5:9-10
👉🏾Kuanzia sasa waamini wanapaswa kutokukubali maisha yaliyopita kutawala maisha yako ya sasa ndani ya Kristo (ishi katika maisha yaliyobadilika na yanayodhihirisha ushindi aliotupatia Yesu)

Katika Ibada ya Tarehe 24/03/2024Na,Rev. Zephrine KahigwaUJUMBE: KUTAFUTA KUMJUA KRISTO VIZURIAndiko la Msingi;Wafilipi ...
24/03/2024

Katika Ibada ya Tarehe 24/03/2024

Na,
Rev. Zephrine Kahigwa

UJUMBE: KUTAFUTA KUMJUA KRISTO VIZURI
Andiko la Msingi;
Wafilipi 3:1-16

Utangulizi;
👉🏾Ufahamu wa mtu katika Kristo, ni jambo la msingi sana la kumfanya mkristo kuweza kuendelea mbele katika wokovu.
Paulo ni mfano mkubwa na mzuri wa aina ya mtu ambaye anaonyesha moyo wake wa kutaka kumjua sana Mungu katika viwango vikuu sana. Paulo anatamani kupata ufahamu wa kuujua uweza Mungu uliomfufua Kristo katika wafu.
👉🏾Ukimjua Kristo, utajua unakokwenda, utajua faida za huko, uzuri wa huko na thamani/ubora wa huko na ukishajua haya, hakuna mtu yeyote atakayekuzuia katika njia yako.

📌Mambo Makubwa Matatu ya kuyafahamu katika Kumjua Kristo;
👉🏾1. Kumjua Kristo binafsi na asili zake.
Wafili 3:7-8
✓Unapoishi k**a mkristo, tafuta kumjua huyu Kristo ni wa namna na jinsi gani. Asili ya Kristo ni Mungu mwenyewe na ndiyo maana kufufuka kwa Kristo halikuwa jambo gumu kwake. Ni lazima tumjue Kristo na asili zake kwa viwango ambavyo amefunuliwa kwetu kwa neno.
✓Kristo amefunuliwa kwetu kwa neno la Mungu, hivyo ili kupata ufunuo wake, ni lazima tupate muda mwingi wa kulisoma neno na kuomba.
Kumjua Kristo, ni uzuri usiopimika kwa mizani.
Kumfuata Kristo kwa Roho wake Mtakatifu.
✓Roho Mtakatifu yupo kila mahali na kila wakati huzungumza ndani yetu na kutufunulia mengi namna ya kuishi.
✓Hivyo ni lazima umtafute na kujiweka kwenye mahusiano na makusudi yake ya milele.

2. Kuujua Uweza wa Kufufuka kwake
Wafilipi 3:10 - 11, Waefeso 1:28-20
✓Tamani kujua uweza wa Mungu wa ufufuo, kwa kuwa huu ni uwezo usio wa kawaida. Paulo anataka kujua siri iliyopo kwa kufufuka kwa Kristo (kupata ujuzi wa maisha yaliyofanywa upya).
✓Kuujua huu uweza kutakuwezesha kuingia katika ufalme wa Mungu mbinguni.

3. Ni lazima tujue ya kuwa msingi wa wokovu wetu na tumaini lake ni dhabihu ya kifo na damu ya Kristo iliyomwagika.
Waebrania 9:13-14

Mungu akubariki!

24/03/2024

Kumsifu Bwana kunawapasa wanyoofu wa moyo zab 33:1

Jerusalem kwaya wakihudumu
24/03/2024

Jerusalem kwaya wakihudumu

SUNDAY SERVICE @ tagccchato
24/03/2024

SUNDAY SERVICE @ tagccchato

24/03/2024

Address

Geita/Chato
Geita
161CHATO

Telephone

+255753206788

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TAG CCC Chato posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category