Mwl Thomas Mhina

Mwl Thomas Mhina Mafundisho ya Neno la Mungu
Akaniambia "Lisha kondoo zangu"

Bwana Yesu asifiwe Sana.Tunapenda kukukaribisha kwenye Semina ya Neno la Mungu wewe na jirani yako, tunakuombea update n...
06/02/2026

Bwana Yesu asifiwe Sana.
Tunapenda kukukaribisha kwenye Semina ya Neno la Mungu wewe na jirani yako, tunakuombea update nafasi ya kufika. Kumbuka kumshirikiasha na mwingine.Tunakuombea tuombeane.
Mungu akubariki. Amen.

SASA VINAPATIKANA.KARIBU UJIPATIE CHAKULA KITABU.Ukue kiroho.Ukiwahi ni vizuri zaidi tuna nakala chache kidogo.Gharama z...
20/01/2026

SASA VINAPATIKANA.
KARIBU UJIPATIE CHAKULA KITABU.
Ukue kiroho.

Ukiwahi ni vizuri zaidi tuna nakala chache kidogo.
Gharama za usafiri ni juu yako ikiwa uko mbali

KARIBU NA MUNGU AKUBARIKI.

Bwana Yesu asifiwe milele hapo ulipo.Nipende kukutakia heri ya Krismasi wewe na familia yako hapo ulipo. Katika kipindi ...
25/12/2025

Bwana Yesu asifiwe milele hapo ulipo.
Nipende kukutakia heri ya Krismasi wewe na familia yako hapo ulipo.
Katika kipindi hichi Mungu anapenda tukumbuke msaada wa Mungu kwaajili ya utumishi wako kwa Mungu hapa duniani.
Somo linaenda kwa kichwa kinachosema….
Pokee upako wa kuzaa kwaajili ya kusudi la Mungu.
neno litakalo kusaidia kupokea anachokiachilia katika msimu huu kwaajili yako na ulimwengu mzima kutuvusha mahali tulipo kwama.
Tunapotazama somo hili Mungu ametupa tutazame kutokea kwenye kile kitabu cha Luka 1:26-38,
“Mwezi wa sita , malaika Gabrieli alitumwa na Mungu Kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,27kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.28Akaingia nyumbani kwake akasema,Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe.29Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani?30Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.31Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.32Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake.33Atamiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.34Mariamu akamwambia Malaika, litakuwaje neno hili, maana sijui mume?35Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika k**a kivuli: kwa sababu hiyo hicho kitakcho zaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. 36Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa;37kwa kuwa hakuna neno lisilo wezekana kwa Mungu.38Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu k**a ulivyosema.” Luka 1:26-38.
1) Upako uliokuja juu ya Mariamu ni matokeo ya kuitikia wito wa utumishi toka kwa Mungu.
Embu tusome Luka 1:34-35
Malaika hakuwa anamjibu mariamu swali lake bali alikuwa anamfunulia kilichoko ndani ya wito wa utumishi alioitiwa na Mungu.
Nirahisi ukaona Jibu la malaika k**a vile lilitokana na swali la mariamu pekee, lakini hapana! Mungu alishaweka hilo jibu ndani ya ule wito wa utumishi wake. Malaika alimfunulia mariamu aone msaada wa Mungu ndani ya wito wa utumishi wake kwa Mungu.
Mahali Mungu alipokuweka unawezakuwa mtumishi wa Mungu na amekukusudia umtumike Yeye. Ndiyo maana imeandikwa” … Hamwezi kumtumika Mungu na mali.” Mathayo 6:24. Huu upako hauji kwa mtu ambae anatumika kwaajili ya mali bali yeye amtumikiae Mungu.

Ndiyo maana Mungu kanituma nikwambia anataka umtumikie hapo alipokuweka ili upokee upako huu wa kukusaidia kuzaa kitakatifu (matokeo yanayomtambulisha Mungu kwenye eneo alilokuweka). Ooh halleluya!
Mariamu aliambiwa ukikubali utumishi huu “……..Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika k**a kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, …” kwanini? kwasababu hakiwezi kuzaliwa kitakatifu bila Roho mtakatifu na nguvu zake kutakasa mazingira yanayopitisha na kubeba kitakatifu. Unapopokea wito wa utumishi huu unapokea na upako unaokutaka wewe na mfumo wako unaotakiwa kupitisha kitu Mungu anachotaka kupitisha kwenye hilo eneo la utumishi wako. Unajua huwezi ukatoa maneno matakatifu k**a “Roho mtakatifu na nguvu hajikojuu yako”.

K**a Mariamu alipata neema kwa Mungu na wewe umepata neema kwa Mungu kukuletea wito wa kubeba kusudi lake ili umtumikie mahali ulipo; Upokee na upako wa kuzaa kitakatifu kwaajili ya kutimiza kusudi lake.
Haijalishi eneo lipi Mungu amekuweka ni polisi, mwanajeshi, Mwalimu, daktari n.k. Mungu anataka ukubali wito wa kumtumikia mahali ulipo ili upokee upako wake, uzae kitakatifu (utendaji mtakatifu na matunda matakatifu kwaajili ya kusudi lake).
Utauliza, sasa ndo naitikaje? Unaitikia kusudi la Mungu kukuweka hapo na kutumika kwasababu hiyo. Utumishi wako kwa Mungu ni kukubali kutumikia kusudi lake mahali ulipo kwanza kabla ya matakwa yako binafsi. Haleluyah apo ulipo!!!

2) Upako uliokuja juu yake ulijibu na mahitaji yake pia.
Wakati Mungu anamletea mariamu wito huu, Mariamu alikuwa na mahitaji yake binafsi na Yusufu pia. Walikuwa bado ni wachumba kwahiyo walikuwa na hitaji la kufunga ndoa yao pia. Sasa
Mungu anamuita mariamu kubeba ujauzito ambao sio wa Yusufu na Yusufu kulea ujauzito ambao siyo wake, unaweza kuelewa maswali waliyokuwa nayo.

Mariamu alipoamua kukubali kubeba wito wa utumishi wa kubeba ujauzito Mungu aliamua kumjibu mariamu hitaji lake la kuolewa. Wakata malaika anaongea na Mariamu alikuwa ni mchumba wa Yusufu. Lakini baada ya mariamu kumbeba Yesu ndipo Mungu akamwambia Yusufu mchukue mkeo (Mathayo 1:20). Maana yake hakuwa mke wake kabla ya hapo. Unasema nani aliwafungisha ndoa? Ni Mungu mwenyewe, aliposema mchukue mkeo. Haleluya!
-Unajua unapoamua kumbeba Yesu moyoni mwako au kusudi lake moyoni mwako Mungu anashuhulika na Yusufu wako pia asikuache.
-Kunamtu anapatashiba kubeba cha Mungu au kusudi lake akimuogopa Yusufu wake! nataka nikwambie usiogope! wewe mbebe Yesu na Mungu atashuhulika na Yusufu wako.
-Kunamtu anaogopa kubeba cha Mungu ofisini akimuogopa bosi wake au wafanyakazi wenzake! nataka nikwambie usiwaogope hao wewe beba cha Mungu na Mungu atashuhulika nao, na muda si mrefu watageuka kukusaidia k**a Yusufu alivyo banwa na Mungu mpa akakubali kumsaidia mariamu.
Kunamtu amemuacha Yesu ili aolewe, Kumbuka mariamu alimbeba Yesu akaolewa.

Na kwako ni hivyo hivyo unapokubali kumtumikia Mungu mahali ulipo unapokea na upako wake unakusaidia kuzaa kwaajili ya Mungu na Mungu kujibu mahitaji yako.
Kubali kufanya kazi na Mungu ushiriki na upako wa kukusaidia kutimiza kusudi la Mungu.
Mungu anakuita itika poke ana upako wa kukusaidia kuzaa kitakatifu ili Mungu atukuzwe mahali alipokuweka kupitia hicho ufanyacho. Haleluya milele!
Mungu wangu na Baba yangu mtakatifu wa Yakobo akubariki na kukutunza mtaka Yesu arudipo tena. Ameni.

24/10/2025

Bwana Yesu asifiwe hapo ulipo ndugu yangu!
Tunamshukuru Mungu tena kwa kutupa nafasi ya kusikia kutoka kwake.

Ujumbe Mungu aliyotupa leo, unasema

Usiruhusu nuru yako izimishwe na nyakati unazopitia.

shetani anashida na nuru yako kuliko kile unachopitia. Anatafuta kuzima nuru yako iliafanye kazi kwa uhuru bila kuonekana.
Mara nyingi huju panya wanafurahi kwa kiasi gani taa ikizimila nyumbani. Kwasababu taa nitishio kwa shuhulizao.

Tutazame Ile;
Mathayo 5:14-16, unasema hivi
[14]Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.
[15]Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
[16]Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Nataka useme maneno haya wakati tunaweka utangulizi wa somo hili,
Sema "Mimi ni nuru mahali Mungu aliponiweka na ulimwengu mzima."

Mistari hii inatuwekea muunganiko mzuri sana kati ya nuru na matendo na utukufu wa Mungu. Kwa muunganiko huu, unaona nuru inamatendo (yanayoitwa mema). Ukifanikiwa kuzima nuru umezima matendo yanayotegemea nuru kuonekana.
Kwahiyo ukizima nuru unazima na matendo yake, yanayofanya Mungu asionekane na atukuzwa na watu. Unapoamua kuficha nuru unaficha matendo ya nuru ili nuru isiwafikia watu.

Ujawahi kuona mtu akiwa na rafiki zake na wanfanya vitu ambavyo havijakaa sawa, Ili asigombane nao au kutendana nao anaamua kutokufanya au kusema kile kinachopingana na dhambi yao.

Au mtu akiwa na shida anaamua kuficha nuru yake asijulikana k**a ameokoka Ili apate msaada.
Hivi ni vitu vipo na madhara yake ni makubwa.
Haijalishi nyakati unazopitia hakikisha Nuru yako haizimikia kabisa. Kumbuka u apopoteza nuru yako unapoteza na muelekeo wa maisha yako. Bwana Yesu asifiwe Sana.


Tutazame jambo la,

1) Wako wanaotegemea nuru yako, hata k**a wote mnapita mahali pa kufanana.

Mungu anapokupa kuwa nuru mara nyingi siyo kwaajili yako peke yako. Hivyo ni muhimu kuwa makini na mamuzi unayofanya unapopita kwenye nyakati ngumu.

Tutazame mfano huu wa Yesu akiwa malabani pamoja na wale wanyang'anyi wawili, ile Luka 23:39-43
[39]Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi.

[40]Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo?

[41]Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa.

[42]Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.

[43]Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.

Unaposoma habari hii, unamuona Yesu amesulubiwa msalabani pamoja na Wany'ang'anyi wawili, tunaweza sema wote walipita kwenye hali za kufanana.

Wote tunajua Yesu ni nuru na mwokozi wa ulimwengu, usingefikiri angepita kwenye mazingira ya namna hiyo pamoja na watu aliopita nao.

Sasa tazama wale wanyang'anyi walichokiona kwa Yesu waliekuwa wanapita nae kwenye nyakati ngumu, ule mistari wa [39]"Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi".
Mmoja aliamua kumtukana akifikiri ile kwamba anapita mahali wanapopita hawezi kuwamsaada kwao pia.
Sasa angalia Yule wa pia kitu alisema, " [40]Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo?
[41]Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa.
[42]Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. "

Wa pili alijua kabisa hata k**a tunapita na Yesu katika mazingira ya kufanana, hatufanani nae kunamsaada aliobeba kwaajili yetu . Alimjua Yesu anapita anapopita kwaajili yao waokolewe, kwahiyo alijua anaweza kumsaidia katikati yamazingira yaleyale wanayopitia.
Alijua wote wanapita kwenye giza lakini Yesu ni nuru yao.

Unajua ni kazi kuomba masaada kwa mtu amabae wote mnapita kwenye hali ngumu. Lazima Mungu akufunulie uone kilichondani yake. Na ukiona mtu anaomba msaada kwa mtu ambae anapita kwenye hali hiyo hiyo, ujue kunakitu maeona kwake k**a msaada.

Yesu angeamua kunyamazi ombi la yule mnyang'anyi kwasababu ya hali anayopitia, lakini alijua alichobeba kwaajili yao. Hivyo hakuruhusu Hali anayopitia izimishe kile alichobeba kwaajili yao.

Ile kwamba unapita kwenye hali ngumu haina maana huwezikuwa nuru kwa wengine. Ndiyo maana ni lazima kulinda Sana moyo wako, Ili Hali unazopitia isizimishe Nuru yako na watu wanaokutegemea wakakosa msaada wa Mungu. Ukosoma habari ya Naomi na wakwe zake kwenye kile kitabu cha Ruthu 1-2, utaona Naomi alijaribu kufanya kosa la kujaribu kumzuia Ruthu asipate msaada Mungu alioweka ndani yake.

Kunawatu Mungu anawapitisha pamoja na wewe kwenye hali mbayo uliyonayo siyo kwasababu wamekosea au walistahili kupita hapo, bali kwasababu yako upate msaade wa kutoka. Sasa unajua ni rahisi kuwadharau kwasababu wote mnapita kwenye hali za kufanana, ukafikiri hawezi kuwa masaada kwako. Hili ndolokosa alilofanya yule mnyang'anyi namba Moja! Usije ukaingia kwenye kosa k**a hili.

Unajua ni kwanini Yule wa kwanza alianza na kumtukana Yesu? Ili tujue yule wa pili hakuangalia yule wa kwanza anamuonaje Yesu au anamsemaje Yesu , lakini alisikia Mungu anachomsemesha moyoni mwake juu ya masaada alioweka ndani ya Yesu.
Yule mwizi wa pili angeungana na mwenzake asingepata masaada kabisa wa kutoka.
Jifunze kusema k**a yule ndugu alieponywa na Yesu,
"........Kwamba yeye ni mwenye dhambi sijui. Najua neno moja, kuwa mimi nalikuwa kipofu na sasa naona. "Yohana 9:25.

Ni rahisi sana ukawatazama watu Mungu aliowabebesha masaada kwaajili yako kwa maneno ya watu wanayosema juu yao. Jifunze kusikia moyoni mwako, Mungu anachokuwekea kuhusu mtu aliembebesha msaada wako.
Wengine wanaweza wasione masaada wao bali wewe unakaonamsaada wako, k**a yule mwizi wa pili.
Usifanye kosa k**a la yule mtu wa Isaya 53:4-5
[4]Hakika ameyachukua masikitiko yetu,
Amejitwika huzuni zetu;
Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa,
Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

[5]Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,
Alichubuliwa kwa maovu yetu;
Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake,
Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

Wao walidhani Yesu amepigwa na Mungu, wakapishana na uponyaji wao.
Maana yake hawakuona uponyaji wao kupitia kupigwa kwake kwasababu walidhani amepigwa na Mungu. Wakati wengine wanaona uponyaji kwakupigwa kwake wao waliona anaadhibiwa na Mungu kwa makosa yake mwenyewe.

Japo Yesu alipita pamoja na wanyang'anyi msalabani lakini alikuwa nuru yao.
Jifunze kwa Yesu, mazingira yasizimishe nuru yako, Yesu alijua Yeye ni nuru hatak**a amesulubiwa katikati ya wanyang'anyi, hakuruhusu nuru yake izimishwe na mateso na kipigo na maumivu na kudharauliwa pamoja na wanyang'anyi. Yule mwizi wapili asingeona nuru kwa Yesu K**a angeamua kumezwa na hali anayopiti. Yesu alijua msaada aliobeba kwaajili yao.

Ikiwa Mungu amekubebesha masaada kwaajili ya wengine, usidharau ulichobebeshwa kwasababu ya mahali unapopita. Yesu hakudharau alichobeba kwasababu ya hali anayopitia na wewe pia uusidharau ulichobeba kwasababu ya mazingira unayopitia. Bado unaweza kuwamsaada hatak**a umewekwa msalabani na wanyang'anyi. Haleluya!!!

2) Ile kwamba mnapita mahali pa kufanana, haina maana mnafanana.

Tutazame mfano wa kutoka 14:1-31.
Hii ni habari ya wana wa Israeli walipokuwa walivuka bahari ya Shamu, bahari ya Shamu ilikuwa ni mlango wa kuvuka kwa Wana wa Israeli kutoka misri. Lipo jambo nataka tujifunze hapa. Ukosoma Ile habari utagundua,

Wamisri walipowafuatia wana wa Israeli ungefikiri k**a vile Wamisri wangevuka bahari ya shamu kwasababu walivuka pamoja na wana wa Israeli. Lakini unaona waisraeli wanatokeza upande wa pili na Wamisri wanazama baharini. Walifikiri kwasababu Israeli wamevuka bahari ya Shamu na wao watavuka bahari ya Shamu.

Wasijue bahari walipovuka Israeli inaweza ikawameza wao. Kwa sababu swala siyo kuvuka bali ni nani anaevuka pamoja na wewe. Haleluya!!
Ndiyo maana usijaribu kuiga watu wengine hakikisha una Imani yako kwa Mungu wako, atakutoa.
Ile kwamba unaona mtu anavuka mahali usiige kwanza, tafuta kujua anavuka na nani. Bwana Yesu asifiwe milele.

Jambo jingine ninalotaka uwone hapa,

Mungu alipowafungulia wana wa Israeli mlango kwenye bahari ya Shamu, Wamisri walifikiri umefunguliwa na kwaajili yao pia na wanaweza kuutumia kuvuka kwenda ng'ambo nyingine.
Mlango haukuwa kwaajili ya kila mtu bali kwa Israeli peke yao.

Unajua mlango ukifunguliwa haina maana ni kwaajili ya kila mtu. Utagundua unapoona wengine wamepita wewe ukifika unafungwa, kwanini kwasababu haukufunguliwa kwaajili yako.
Vivyo hivyo mlango ukifungwa siyo kwaajili ya kila mtu.
Ndiyo maana ukiona mlango umefungwa usikasirike muulize Mungu kwanini umefunga, kwasababu unaweza kutaka kwenda kwa mkumbo au kimazoea usijue Mungu anaufungulia mlango mwingine kwaajili yako.

Tutazame tena ule mfano wa Luka 23:39-43.
Kosa alilofanya mwizi wa kwanza ni kujifananisha na Yesu kwasababu wote wanapita mahali pa kufanana. Walisulubiwa watatu msalabani lakini mbinguni walienda wawili tu!
Wote walipita msalabani lakini sio wote waliingia mbinguni.

Nirahisi ukaona wote mnapita mahali pa kufanana lakini mlivyobeba havifanani hivyo hatma zenu hazifanani pia.

Usije ukafanya hili kosa kabisa, kwakufikiri mazingira mnayopitia kwakufanana ni kwasababu mnafanana.

- Ukisikiliza yale maneno ya mwizi wa pili pale msalabani utagundu alijiua Siri ya ajabu sana,
Jambo la I) Alijua japo wamesulibiwa wote wao walikuwa na makosa kweli ila Yesu hakukosa neno lolote. Ndani yake alipata ujumbea uliomsaidia kupata msaada kwa Yesu.
Ok alipata ujumbea gani; alipata kujua hakusulubiwa kwaajili ya makosa yake bali kwaajili ya makosa yao.
Baada ya kujua hivyo akapata hekima: isemayo, huyu mtu Mungu ameamua kumpitisha mahali tunapopita na sisi Ili tupate msaada alioweka ndani yake kwaajili yetu, asingependa tuangamia hata k**a dhambi imetufikisha hatua hii Bado kunatumaini la maisha mengine baada ya hapa.

Jambo la 2) Alijua wakifa wote watatu saa ile Yesu haendi kule watakapoenda wao, bali anaenda mbinguni kwenye ufalme wake. Ndiyo maana akasema unikumbuke "...utakapoingia katika ufalme wako" niende na wewe.
Ujumbe aliopata ni kuwa! hata k**a wote tunapita mahali pa kufanana, tulichobeba havifanani na hatma zetu hazifanani (tunapoenda hakufanani)
Akapata hekima: akasema naeweza kuamua hatma yangu kwakukubali alichobeba huyu Ndugu kwaajili yangu hapa msalabani. Kwasababu hata k**a dhambi imenifikisha hatua hii ya msalaba siruhusu inifikishe jehanamu ya moto; nitaenda na wewe katika ufalme wako huko uwendako.

Ndani yake yalizaliwa maamuzi ya ajabu sana. Aliamua hata k**a Mimi na mwenzangu tumekuja wote msalabani, sikotayari kwenda anapotaka kwenda Yeye. Mimi nimeamua kwenda na wewe Yesu kwenye ufalme wako, kwahiyo nikumbuke.
Najaribu kusema kilichokuwa moyoni mwake na kupelekea maamuzi aliyofanya.
Hayasiyo mahesabu mepesi sana, lakini ni na uhakika Mungu alimsaidia kabisa.

Najaribu kufikiri yule mwizi wa kwanza laipomuona mwenzie yuko mbingu alijisikiaje? Lazima aliwaza, yaani nilifikiri wewe ni mwizi mwenzangu aisee! Akifikiri kwasababu wote wamepita kwenye uwizi basi wataenda wote jehanamu ya moto.

Imani ya yule mwizi wa pili ilimtenganisha na wizi na mwizi mweziwe na kumuunganisha na Yesu.

Imani yako kwa Yesu Kristo uliyonayo inaweza kukutofautisha na watu wengine hata k**a mnapita kwenye hali za kufanana. Unaweza kufanya maamuzi k**a yule mnyang'anyi; je mazingira ninayopitia yaamua hatma ya nuru yangu, yaamue kesho yangu au Imani yangu kwa Mungu?
Haya ni maamuzi yako binafsi usiyafanye kwa mkumbo! Tenga muda na kaa peke yako.
Na Mungu wangu awe nawe hapo! Uvukekatika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Amen.
Mungu na akubari sana.
Ninakuombea.

SEMINA YA NENO LA MUNGU-CHATO MJINI
04/08/2025

SEMINA YA NENO LA MUNGU-CHATO MJINI

SEMINA YA NENO LA MUNGU.Mungu akubariki unapoendelea kusikiliza.Subscribe kuendelea kufuatilia masomo zaidi.

04/08/2025

Kusudi la toba linafanyakazi ndani yako kuzaa mkakati wa mabadiliko.

Address

Chato
Geita

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mwl Thomas Mhina posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Mwl Thomas Mhina:

Share