30/07/2023
Yesu asifiwe mpendwa Ibada ya Leo ilikuwa Njema Sana. Matangazo yalikuwa k**a ifuatavyo:
✓ Aliesimama leo ilikuwa ni familia ya Joseph David (Mkombozi) na Piniel Hosea
✓ Atakaesimama wiki ijayo Ibada ya Asubuhi ni Witness na Mchana Elibariki Saruni.
✓ Mchungaji alimshukuru Mungu K**a alivyotangaza.
✓ K**ati ya kanisa itabaki baada ya Ibada
✓ Wamama nao watanaki baada ya Ibada
✓ Mchungaji ameomba watu waende Jumuiya kwa mitaa yao.
MAHUBIRI: SOMO; KUSITASITA KTK SAFARI YA KIROHO
1Wafalme 18:21, Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni, bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno.
2 Wafalme 17:41, Basi mataifa hawa wakamcha BWANA, tena wakaziabudu sanamu zao za kuchongwa; na wana wao vile vile, na wana wa wana wao; k**a walivyofanya baba zao, wao nao hufanya vivyo hivyo hata leo.
Mchungaji amendelea kwa kusema tuache kumchanganya Mungu na Miungu utachelewesha Baraka zako mwenyewe.
Tuchague tutakae mtumika K**a ambavyo yoshua alivyochagua.
UKISOMA
Yoshua 24:14, Basi sasa mcheni BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye BWANA.
15, Nanyi k**a mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.