01/09/2026
IBADA MAALUM YA FAMILIA | TAREHE 1/9/2026 | KANISA LA EFATHA KISASA, DODOMA
KUHANI FRIDA GILBERT
SOMO: NAFASI ZA MUNGU KATIKA FAMILIA
Familia ni mtu pia familia ni watu. Mungu mwenyewe ana familia
1. Mungu mwenyewe
- Kumruhusu Mungu awe wa kwanza katika familia maana yake umemruhusu Mungu aitawale familia yako
- Mungu ndiye anamiliki na anatawala katika familia
2. Ndoa; yaani ni mume na mke
3.Watoto; kwa sababu watoto wanatokana na baraka ya ndoa.
4. Wazazi ambao wamemzaa mwenza wako
5. Ndugu
- Yule ambaye hajafikia nafasi ya pili ya watoto ambayo ipo katika ndoa mtu anagawanya kutokana hali anayopitia kwa wakati ule.
- Pia k**a umezifikia nafasi zote, je unasimama na kuwajibika katika nafasi hizo ulizopo? Maana kila nafasi ukiitekeleza ina baraka zake.
- Lakini Kuna mtu akishatoka kwa wazazi, anasahau kabisa nafasi ya wazazi ambayo siyo sawa
- Pia kuna watu wanatakiwa kutubu kwa sababu wamesahau nafasi za wazazi wao upande wake na upande wa wenza wao.
Wakolosai 3:18-21
"Ninyi wake, watiini waume zenu, k**a ipendezavyo katika Bwana. Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao. Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana. Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa."
- Neno la Mungu linatuongoza kwa kila ujumbe ambao tunatakiwa kuufuata, ili kila familia iweze kupata furaha na baraka
- Tunaposema nafasi ya kwanza ni Mungu ni k**a Joshua alivyosema kwamba Mimi na nyumba yangu tutamtukia bwana,maana yake Joshua familia yake alimkabidhi Mungu.
- Yawezekana sisi tulikozaliwa hatukutamkiwa maneno haya ila Mfano haya maneno akiyatamka baba ndani ya familia yake maana yake ni agano ambalo baba ameliweka.
- Familia inaanzia ndani ya mtu.
Yohana 6:33
"Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima."
Tukiyafuata haya yote hatutayahangaikia. Kwahiyo tufundishe utakatifu ndani ya familia zetu.
Familia ya kwanza ambayo Mungu aliiweka ni ya Adamu na Hawa na ni familia ambayo ilikuwa na baraka Mungu aliibariki, lakini familia hiyo iliingia katika dhambi kwa sababu ya kutokutii baada ya hapo vizazi na vizazi vikaingia katika dhambi na uovu
- Chanzo cha mambo yote yanayosababisha kuingia katika maumivu ni dhambi na uovu.