28/01/2026
WA MUME MKRISTO NA MKE MKRISTO KIBIBLIA
Mnenaji: Mwl.Imani Mwanyingi| FGG|Bezaleli Media Tanzania|IBADA YA JUMAPILI| TOCC DODOMA|Januari 04, 2025
Rejea:
- BIBLIA
- Wajibu wa Mme Mkristo (Frank R. Parish - 2003)
""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Familia ni taasisi ya kwanza kabisa aliyoanzisha Mungu, na ili iwe imara, kila mwenza anapaswa kutimiza wajibu wake kikamilifu. Baba na mama wana nafasi za kipekee katika malezi, uongozi, ujenzi p mm maadili, na ustawi wa kiroho, kijamii na kiuchumi wa familia. Biblia inaelekeza wazi majukumu yao, huku jamii ikitegemea mchango wao katika kuunda kizazi chenye heshima, bidii na kumcha Mungu.
~ Uongozi wa Ki-Mungu huanzia nyumbani; Kwa ajili hiyo maandiko yote yanayohusu maisha ya Ukristo yamekusudiwa yaonekane kwanza NYUMBANI.
“tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane k**a na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.”
— Waefeso 4:32
A: WAJIBU WA MUME MKRISTO (BABA)
1. KUMTII KRISTO KWA BIDII ILI KUPATA MSAADA WA KUONGOZA FAMILIA (KICHWA)
“Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana akili njema, Sifa zake zakaa milele.”
— Zaburi 111:10
“Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, k**a chombo kisicho na nguvu; na k**a warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.”
— 1 Petro 3:7
2. KUMPENDA MKE WAKE NA KUMPA HESHIMA KWA MOYO WA KUJITOA
• K**a Kristo alivyoipenda Kanisa.
“Enyi waume, wapendeni wake zenu, k**a Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;” — Waefeso 5:25 (22-33)
• Kutenda Kila jambo Kwa Upendo
“Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.”
— 1 Wakorintho 13:13
• Kumpenda Mke SI Kwa jinsi anavyotii au asivyotii; Bali KWA KULITII LILE AGIZO LA MUNGU.
Angalia HAPA, maneno KUMPENDA MKE yanarudiwa mara Tatu k**a msisitizo!
Waefeso 5:25,28, 33
²⁵ Enyi waume, wapendeni wake zenu, k**a Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
²⁸ Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao k**a miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
³³ Lakini kila mtu ampende mke wake k**a nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.
• Kwa KUAMUA (UAMUZI), Siyo KUJISIKIA
Kumpenda Mke kunapaswa kufanyika Kwa uamuzi wa dhati kutoka moyoni badala ya kuongozwa na Hisia.
K**a vile Kristo alivyolipenda Kanisa, akautoa upendo wake Wote bila kujali kungetokea NINI.
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”
— Yohana 3:16
“Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.”
— Wakolosai 3:19
• Kuwa tayari KUMSAIDIA MKE KATIKA HALI ZOTE
Mfano:
- Mahitaji ya Kimwili: madeni, kuyumba biashara, matatizo ya kifamilia kwao, nk.
- Shughuri za nyumbani: Kufua, kupika, kumwagilia bustani, kwenda sokoni, nk Kila inapobidi.
3. KUTUNZA NA KUMHESHIMU AGANO TAKATIFU LA NDOA
Mwanaume anapoamua kuoa, anafanya AGANO LA KUJITOA KWA MKEWE mbele za MUNGU. Huu unafananishwa na mkataba wa kimbingu ambao kamwe hautanguki. Ni jukumu zito ambalo mwanaume hapaswi KUINGIA bila maandalizi ya Kutosha!
Angalia,
“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”
— Mwanzo 2:24
“Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”
— Marko 10:9
“Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.”
— Malaki 2:16
4. KUTOA UONGOZI WA KIROHO/DIRA KWA MKE NA FAMILIA
– Kuwaongoza kwa hofu ya Mungu.
“Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, k**a Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.”
— Waefeso 5:23
“akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo”
— Waefeso 1:22
“Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.” — 1 Wakorintho 11:3
5. KUWAFUNDISHA WATOTO KUMPENDA MUNGU (IMANI)
– Kupandikiza maadili, misingi ya Imani na kumcha Mungu.
“nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.”
— Kumbukumbu 6:6-7
“Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.”
— Mithali 22:6
Mfano: MAOMBI, Utoaji, Adabu na Heshima Kwa WATU wengine, Ukarimu, Matunda ya Roho Mtakatifu, Umuhimu wa ELIMU(maarifa), nk.
6. KUWAPENDA NA KUWAHESHIMU WATOTO
– Kuwapenda na Kuwalea kwa nidhamu na maonyo ya Bwana.
“Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.”
— Waefeso 6:4
- Kuwaletea Zawadi Mke na Watoto ili wafurahie kukupokea unapokuja nyumbani. SI TU upokelewe Kwa kuwa una zawadi, lakini kwamba Watoto na mke wafurahie unapoonekana kwamba wewe ndiye mtunzaji wa Familia Katika Hali zote!
- Kuwaadabisha Kwa Fimbo ya adhabu. Unapomchapa Mtoto Kwa kuwa amekosa, unadhihirisha kwamba unampenda na unataka aje kuwa Mtu mzuri.
“Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.”
— Mithali 13:24
- KUTOA adhabu Kwa Hekima na Kiasi, WASIJE Wakakata Tamaa!
“Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.”
— Wakolosai 3:21
7. KUTUNZA NA KULEA FAMILIA(MKE NA WATOTO)
MUME MKRISTO anawajibika Kutoa mahitaji ya kifamilia; kuhangaikia mahitaji ya nyumba na familia.
“Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.”
— 1 Timotheo 5:8
KUTUNZA: Kuileta mahitaji ya nyumbani na mahitaji ya familia mfano: SAMANI ZA NDANI, CHAKULA,MAVAZI, CHAKULA, MALAZI, ELIMU NA MATIBABU.
KULEA: Ni kusimamia tabia na mwenendo wa familia (Mke na Watoto).
Mfano:
• Kufundisha Watoto tabia njema, bidii ya kazi, Adabu na Heshima, nk
• Kusimamia tabia ya Mtoto: Kupongeza anapofanya vizuri(zawadi) na kuadibu anapokengeuka!
• Kuangalia na Kusimamia mwenendo wa Mke na KUMSAIDIA inapobidi.
Mfano: Anarudi nyumbani Usiku, anachelewa Kanisani, anakwepa MAOMBI, hatoi fungu la kumi, anavaa isivyofaa, nk. Mme ana nafasi kubwa ya kusaidia, Kwa MAOMBI, maonyo na mafundisho Katika neno la Mungu!
8. KUSAMEHE NA KUWA MVUMILIVU
– Afundishe familia neema na upendo wa kweli.
Wakolosai 3:12-13
¹² Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,
¹³ mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; k**a Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
9. KUDUMISHA TABIA NJEMA (MFANO WA KUIGWA) NYUMBANI NA KATIKA JAMII
– Kwa tabia njema, uadilifu na maisha ya kiroho.
“Mnifuate mimi k**a mimi ninavyomfuata Kristo.” — 1 Wakorintho 11:1
Mfano:
TUNDA LA ROHO
"Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo k**a hayo hakuna sheria"
--- Galatia 5:22-23
10. KUWA MLINZI WA FAMILIA
Hili linawezekana Kwa MAOMBI, ili MUNGU aistawishe familia na kuiepusha na Majanga! Mfano: UGOMVI, KUTOELEWANA, TALAKA, nk.
• Mme MKRISTO anapaswa kuwa chanzo na SABABU ya familia kuwa na amani!
Waebrania 12:14-15
¹⁴ Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
¹⁵ mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.
• Kumlinda Mke na Watoto dhidi ya mashambulizi ya WATU wengine k**a vile Ndugu wabaya, majirani wabaya, mawifi wabaya, nk.
Yaani, KUMTETEA MKE HADHARANI ili KUMUONYA NYUMBANI!!
• KUWATIA MOYO MKE NA FAMILIA
Kwa kuwa wao ni mawili MMOJA, Matendo ya Mme na Mke yanaweza ama KUMTIA MOYO MKE Kujua KIROHO au Kumkwamisha!
“Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.”
— Waefeso 5:31
TAZAMA!
Mhubiri 4:9-10
⁹ Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.
¹⁰ Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!
B: WAJIBU WA MKE MKRISTO KIBIBLIA*
“Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.” — Mwanzo 2:18
WAJIBU KIBIBLIA:
1. Kuyatoa Maisha yake Kwa Kristo na KUMCHA MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI
“Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.”
— Kumbukumbu 6:5
“Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa.”
— Mithali 31:30
“Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.”
— Mithali 31:10
2. KUMPENDA MUME NA WATOTO WAKE
– Maisha ya mama yaonyeshe upendo wa kweli.
"...ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe"
- Tito 2:4-5
KWA NAMNA GANI?
• Kukubali Kuongozwa na Mme wako. Kwa kutii unaonesha wazi kwamba unampenda na unatambua nafasi yake Kwa MUNGU na Kwa familia.
“Enyi wake, watiini waume zenu k**a kumtii Bwana wetu.”
— Waefeso 5:22
“Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, k**a Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.”
— Waefeso 5:23
“Lakini k**a vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.”
— Waefeso 5:24
• Kumtendea Mema k**a Ipasavyo Wajibu wa Mke Kwa Mme.
“Lakini ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema.”
— 2 Wathesalonike 3:13
• KUTUNZA Mme na Watoto: Kuandaa chakula, Kusafisha nyumba, Kufua nguo, nk.
• KULEA MME NA WATOTO: Mwanamke anawajibika kusimamia tabia na mwenendo wa Mme wake ili KUTOA USHAURI Kwa Hekima na kujenga NDOA Imara!
3. MKE NI MLEZI WA FAMILIA
MKE anapaswa Kuungana na Mme wake KUSIMAMIA TABIA ZA WANAFAMILIA Wote nyumbani.
Mama ni Mwalimu na Mlezi nambari Moja, kabla ya Mme wake k**a hakimu inapobidi.
“Mwanangu, shika maagizo ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako.”
— Mithali 6:20
“Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.”
— Mithali 23:22
• Kufundisha Familia UKARIMU NA KUSAIDIA WATU. Mama mtoani na mkarimu atafunza wanaye kuwa wakarimu, na kinyume chake ni kweli!
“Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.”
— Mithali 31:27
“Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.”
— Mithali 31:20
• Kulea watoto katika adabu ya Bwana*
– Awe mlezi wa kwanza wa kiroho kwa watoto.
*(Mithali 1:8; 2 Timotheo 1:5)*
• Mlezi wa watoto* – Kuwa mstari wa mbele kulea watoto katika maadili.
*(2 Timotheo 1:5, Mithali 1:8)*
• *Mlinzi wa afya ya familia* – Yeye hufuatikia lishe, usafi, na matibabu Kwa Watoto wakati Wote!
Mama yu karibu zaidi na Watoto na anapatika a Kwa urahisi, Hali ambayo Watoto huihitaji zaidi!
4. KUMTII MME KATIKA KILA JAMBO
Kutii MME_Ni kujiweka chini ya Uangalizi, Kuhifadhiwa na kupokea UPENDO wake na Hali yake ya Kiungu (KICHWA CHA MKE).
KUTII _Ni Kukubali kufuata uongozi.
• Neno KUTII_Latokana na maneno mawili ya Kigiriki;
~ HUPO = Chini ya
~ TASSO = Katika Utaratibu mzuri, ulioteuliwa.
KUMBE, KUTII MME ni kuishi chini ya utaratibu maalum uliotolewa na Mungu, yaani kuishi chini ya Uongozi WA MUME wake Katika Utaratibu uliowekwa na MUNGU mwenyewe.
“Lakini k**a vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.”
— Waefeso 5:24
• KWA KUWA MME NI KICHWA CHA MKE (KIONGOZI)
"Enyi wake, watiini waume zenu k**a kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, k**a Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili"
--- Efeso 5:22-23
• ILI WASIOAMINI NENO, WAVUTWE!!
“Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;”
— 1 Petro 3:1
• ILI WATUNZWE NA KULINDWA
“Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, k**a chombo kisicho na nguvu; na k**a warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.”
— 1 Petro 3:7
“Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,”
— 2 Wakorintho 6:18
5. MSAIDIZI WA MME WAKE* – Hii ni Kazi ya awali aliyokabidhiwa na Mungu. MKE husaidia na kuhakikisha Mipango, malengo, na MAONo ya Mme wake Kwa familia yanafanikiwa.
“Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”
— Mwanzo 2:18
“Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.”
— 1 Wakorintho 11:9
• KUMUOMBEA MME WAKATI WOTE
• KUMTIA MOYO MAMBO YAKE YANAPOENDA MRAMA NA YANAPOENDA VIZURI
• KUSIMAMIA SHUGHURI ANAZOAGIZWA NA MME KWA UAMINIFU, nk.
6. KUWA NA TABIA NJEMA NA KUMCHA MUNGU
• Kutafuta SIFA Njema (MKE Mwema)*(Mithali 31:10–31,
• UPENDO wa dhati Kwa Mme na Watoto.
Tito 2:3-5
⁴ ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao;
⁵ na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.
7. MAMA NI FUNDI, MJENZI WA FAMILIA YENYE MAADILI MEMA
• Mama hufundisha lugha, heshima, ibada
“Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.”
— Mithali 10:1
8. *Kushiriki shughuli za kiuchumi* – Mama anaweza kufanya kazi au biashara kusaidia familia.
• Mjasiriamali, SI MVIVU/MZEMBE!
Mithali 31:16-19
¹⁶ Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
¹⁹ Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.
9. *Kusimamia nyumba kwa hekima*
– Mama ndiye mlinzi wa mazingira ya nyumbani.
“Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.”
— Mithali 31:27
- Msimamizi wa nyumbani* – Kusimamia shughuli za ndani; USAFI WA MAZINGIRA, VYOMBO VYA CHAKULA, MPANGILIO WA SEBULE,
10.. *Kuwa mwenye busara, safi, mpole na mtulivu*
– Maisha yake yawe mfano kwa jamii.
*(Tito 2:5)*
• Kumstahi/KUMSITIRI MME wake.
“Lakini kila mtu ampende mke wake k**a nafsi yake mwenyewe; WALA MKE ASIKOSE KUMSTAHI MUMEWE ”
— Waefeso 5:33
KATIKA UDHAIFU, MKE amuombee Mme wake, Amtunzie Siri na Kutafuta namna nzuri ya KUMSAIDIA Mme badala ya KEJELI, DHARAU NA MASENGENYO!!
• Aweze kuwatumia Kwa Hekima maneno MATATU MUHIMU Katika NDOA
A. ASANTE
B. SAMAHANI
C. NISAMEHE
Baba na mama kila mmoja Kwa wakati wake ana nafasi ya kipekee kimaandiko, kijamii na kiuchumi. Familia ikiongozwa kwa ushirikiano wa wajibu hawa, huleta jamii imara yenye heshima kwa Mungu.
“Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila.”
— 1 Petro 3:8-10
JE, NDOA yako Ina changamoto? Hakuna amani na utulivu wa kweli!? Yupo MUNGU, muasisi wa NDOA! Yeye aliyewaunganisha, Atawasaidia kuishi PAMOJA Kwa amnlani, furaha na UPENDO! Bado tunaweza kumwamini TU, nyakati nzuri zinakuja! Usiondoke! Usiombe TALAKA, SI mpango wa MUNGU!
MUNGU akujaalie Amani, UPENDO na Furaha ya kweli mwaka huu Mpya 2026
MUNGU AKUBARIKI, AMEN!!!
FGG|Mwalimu wa Neno la Mungu|Mwandishi| Media Tanzania| TOCC DODOMA|MAGHARIBI Mwa Jiji la Dodoma|Ibada ya JUMAPILI|Januari 04, 2025
©©©©©©©©©©©©©©©©©©©©©©©©