13/03/2026
SOMO: *"MADHARA YA KUACHA KUOMBA KWASABABU YA KUKATA TAMAA"*
*📖Luka 18:1........ imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tamaa.*
*Sehemu ya 2*
✍️Katika utangulizi wa somo hili, nilisema kwamba kuna madhara makubwa ya kuacha kuomba kwasababu ya kukata tamaa, ingawa si watu wengi wanajua jambo hili.
✍️Katika sehemu sehemu ya 1 ya somo hili, tulianza kuangalia madhara ya kuacha kuomba kwasababu ya kukata tamaa. K**a haujapata nafasi ya kufuatilia sehemu ya 1 ya somo hili, jitahidi ufuatilie kwasababu kuna vitu muhimu ambavyo nilifundisha.
✍️Siku ya leo naomba tuangalie madhara mengine ya kuacha kuomba kwasababu ya kukata tamaa 👇👇
*MADHARA YA 2: KUKOSEKANA KWA NGUVU AMBAYO INAHITAJIKA NA MUNGU ILI AITUMIE KATIKA KUJIBU MAOMBI YAKO*
✍️Unapokuwa unaomba, kuna kiasi/kiwango fulani cha nguvu za Mungu zinazotoka ndani yako (kiwango fulani cha nguvu za Mungu zinazofanya kazi muda huo kutoka ndani yako), na hicho kiwango cha nguvu za Mungu ndicho ambacho Mungu anakitumia katika kujibu maombi yako.
✍️Kwahiyo ukikata tamaa na kuacha kuomba, maana yake ni kwamba, *kunakosekana nguvu za Mungu kutoka ndani yako ambazo zipo kazini, ambazo Mungu ndizo anazotakiwa kuzitumia katika kujibu maombi yako.*
📖Waefeso 3:20 *Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu.*
*MSISITIZO:* Msisitizo mkubwa kwenye huo mstari sio tu nguvu, bali nguvu itendayo kazi ndani yetu (nguvu iliyopo kazini).
✍️Kwenye huo mstari, unaona wazi kabisa kwamba Mungu anafanya mambo ya ajabu mno kuliko yale tuyaombayo au tuyawazayo, *kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu.*
✍️Nguvu itendayo kazi ndani yetu, ni kiwango cha nguvu za Mungu kilichopo kazini wakati husika. Yaani kiasi cha nguvu za Mungu kutoka ndani yetu ambacho kinatumika wakati husika.
*✍️Hiyo nguvu itendayo kazi ndani yetu, ndiyo nguvu ya Mungu ambayo Mungu anaitumia katika kujibu maombi yetu wakati tunaombea jambo fulani.*
*KUMBUKA:* Wakati wewe umekata tamaa na kuacha kuomba na huku unasema kwamba unamuachia Mungu, fahamu ya kwamba kunakuwa hakuna kitu kinachoendelea ambacho kitasukuma majibu ya maombi yako kuja kwako. Maana kunakuwa hakuna nguvu itendayo kazi ndani yako, ambayo Mungu ataitumia katika kujibu maombi yako.
‼️Ni hasara kubwa sana kukata tamaa na kuacha kuomba, na huku unasubiri majibu kutoka kwa Mungu, wakati hakuna nguvu ya Mungu kutoka ndani yako ambayo itasukuma majibu yako kutoka kwa Mungu kuja kwako.
🔺Mara nyingi mtu ukikata tamaa na ukaacha kuomba, Roho Mtakatifu anakuwa anakuletea himizo la kukutaka uendelee kuomba, kwasababu anajua kwamba hakuna kitakachoendelea, zaidi ya kujichelewesha tu kuja kupata majibu ya maombi yako.
* AKIWA GEREZANI*
✍️Petro akiwa gerezani na amefungwa minyororo, alikuwa amekata tamaa na anasubiri tu kuuwawa na Herode.
✍️Kutokana na kwamba Petro alikuwa amekata tamaa ya kuishi, hivyo kule gerezani alikuwa haombi, bali analala tu.
✍️Kitendo cha Petro kutokuomba, maana yake ni kwamba kilikuwa hakifungui mlango wa msaada wa Mungu kuja kwake.
* ya juhudi ya Kanisa kwa ajili ya Petro:*
✍️Kilichomsaidia Petro kutoka gerezani ni *maombi ya juhudi,* ambayo kanisa liliomba kwa ajili yake.
📖Matendo ya Mitume 12:4-5
[4] Alipokwisha kumk**ata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu. [5] Basi Petro akalindwa gerezani, *nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.*
✍️Maombi ya juhudi, sio maombi ya kawaida, bali ni maombi ambayo ndani yake yamebeba bidii, kuomba bila kukoma na kutokata tamaa, haijalishi mazingira ya anayeombewa yakoje au jambo linaloombewa yakoje.
✍️Maombi ya juhudi ambayo yaliombwa na kanisa kwa ajili ya Petro, ndiyo yaliyoachilia nguvu za Mungu kutoka ndani ya waombaji, ambazo Mungu alizitumia katika kumtoa Petro gerezani kwa kumtuma malaika.
📖Matendo ya Mitume 12:7-8
*[7] Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi. [8] Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate.*
✍️Kumbuka ile Waefeso 3:20 ya kwamba *"Mungu anajibu yale tuyaombayo au tuyawazayo kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu"*. Kwahiyo Mungu alitumia nguvu zilizokuwa kazini wakati kanisa linaomba kwa juhudi, kwa ajili ya kumwokoa Petro dhidi ya mikono ya Herode.
*ZINGATIA:* K**a kanisa lisingemwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili ya Petro, ni wazi kabisa kwamba Petro angeuwawa na Herode, kwasababu yeye binafsi alikuwa amekata tamaa na haombi, *hivyo hakukuwa na nguvu zilizokuwa kazini kutoka ndani yake, ambazo Mungu angezitumia katika kujibu maombi yake na kumwokoa.*
🔺Hili jambo la Mungu kujibu maombi yako kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yako, ni moja ya kanuni za kiroho, ambazo zinahusisha ushirikiano wa Mungu na mwanadamu kiutendaji.
✍️NI HASARA KUBWA SANA KUKATA TAMAA NA KUACHA KUOMBA, HALAFU HUKU UNAJIFARIJI KWAMBA MUNGU ATAJIBU TU KWA WAKATI WAKE.
✍️KUSUBIRI MAJIBU KWA MUNGU WAKATI UMEKATA TAMAA NA HAUOMBI, NI SAWA NA KUENDELEA KUJIPOTEZEA MUDA WAKO.
🔺KILA WAKATI INAPOKUJA HALI YA KUKATA TAMAA NA KUACHA KUOMBA, NI LAZIMA UJIULIZE KWAMBA SASA MUNGU ATAJIBU MAOMBI YANGU KWA KUTUMIA NGUVU GANI WAKATI HAKUNA NGUVU INAYOACHILIWA, AMBAYO MUNGU ANATAKIWA AITUMIE KUJIBU MAOMBI YAKO??
🔺K**A KUNA JAMBO ULIKUWA UMELIKATIA TAMAA NA UMEACHA KULIOMBEA, NAKUSHAURI ANZA KULIOMBEA TENA KWA JUHUDI KUBWA, BADALA YA KUSUBIRI MAJIBU HEWA.
*Somo litaendelea sehemu ya 3......*
ujumbe huu, nina amini umepata kitu cha kukusaidia.
+Mungu akupe nguvu ya kuendelea kuombea vitu bila ya kukata tamaa.
°Ni sisi ndugu zako katika mwili wa Kristo,
* , Mwl Mandela & Devotha Mwambeso*
0752197065
Dodoma, Tanzania
Email: [email protected]