WE Belong to JESUS

WE Belong to JESUS Penda ukurasa huu ili uweze kukua kiroho zaidi na zaidi ili tuendeleee kutangaza Neno la Mungu, Maana kila Neno la Mungu litatimia K**a lilivyo andikwa

Nyakati ngumu kwenye maisha huwa ni za kitambo Kidogo . Mwamini Mungu sana
12/11/2025

Nyakati ngumu kwenye maisha huwa ni za kitambo Kidogo . Mwamini Mungu sana

22/10/2025

Yesu ni Mfalme

Mimi ni mwanamke mjane ninaishi mjini Arusha. Huu ni ushuhuda wangu wa maisha yangu.Miaka 21 iliyopita nilifunga ndoa na...
21/03/2025

Mimi ni mwanamke mjane ninaishi mjini Arusha. Huu ni ushuhuda wangu wa maisha yangu.

Miaka 21 iliyopita nilifunga ndoa na mume wangu mpendwa kanisani, baadaye tukajaliwa kuwa na watoto wa2 mmoja wa kiume Alfred na mwingine wa k**e Minza. Mimi nimesomea mambo ya uuguzi MD, nimefanya kazi muda mrefu ktk hospitali za wilayani karatu na Arusha mjini mpk nilipolazimika kuacha kutokana na udhaifu wa mwili na mambo yaliyonipata katika maisha. Mume wangu alikua ni askari polisi mpk baadaye alipojiunga na ajira zingine mpaka alipokutwa na mauti k**a nitakavyoeleza baadaye hapo chini.

Tulipooana na mume wangu,maisha yalikua ya furaha sana na tulikua na mipango mingi mizuri ya kujiendeleza kiuchumi na kihuduma kwani tulikua tunampenda Mungu na tulikua waimbaji na waombaji kanisani. Baada ya muda mrefu katika maisha ya ndoa na familia, baadaye maisha yalianza kuwa magumu kutokana na mishahara yetu kuwa midogo ukilinganisha na mahitaji. Mume wangu alijisikia vibaya sana zaidi yangu hasa pale alipoona wengine hasa marafiki zake wanafanikiwa lkn yeye hafanikiwi. Kuna maaskari walikua wakipandishwa vyeo haraka na kuhamishiwa mijini ikiwemo Daressalaam na Arusha- hali hiyo ilimpa shida sana akawa anaomba na kufunga kwa muda mrefu lkn hakuona mafanikio.

Wakati fulani ilitokea akakutana na rafiki yake askari mwenzie, akamualika nyumbani kwake. Mume wangu aliporudi akaja akiwa mwenye mawazo makubwa sana, sikujua ni kwanini na hukuniambia hata nilipomuuliza.

Baada ya siku kadhaa mume wangu akaacha kwenda kanisani wala huduma hakufurahia tena. Akawa ni mkimya na mwenye mawazo mengi sana. Siku moja akaniambia atasafiri kikazi kwa muda wa siku tatu. Baada ya siku tatu akarudi akiwa hoi sana na mgonjwa km mtu mwenye malaria. Nikajaribu kumshawishi twende hospitali hakukubali kbs akaniambia ni uchuvo tu wa safari na kazi na atakuwa salama. Kesho yake, kweli akaamka vzr na kwenda kazini bila kuugua km hapo jana. Ikapita muda mrefu bila kujua hasa nini kinachoendelea kwa mume wangu kwani hakuniambia chochote hata nilipomuuliza.

Baada ya muda, mume wangu akapata nafasi ya kwenda masomoni Moshi. Alipomaliza masomo hayo,haikuchukua muda mrefu tukapata barua ya uhamisho wa mume wangu kikaz kuelekea Arusha mjini.

Binafsi nilifurahi sana, nikajua Mungu ameanza kujibu maombi yetu ya siku nyingi. Kwa hiyo na mimi nikaanza mipango ya uhamisho. Tulipofika Arusha tukapata makazi mapya na kanisa zuri la kuabudia. Baada ya muda niligundua mume wangu hakupenda mambo ya Mungu km siku za zamani. Wakati huu mimi nilikua mjamzito nikijandaa kupata mtoto wa pili.

Tulizungumza sana na mwenzangu lkn sikujua hasa kitu gani kulikua kinamsumbua. Baada ya muda niligundua mume wangu alikua mlevi wa pombe na tabia yake ilibadilika sana hasa kuhusu mambo ya kiimani na kushirikishana mipango. Aligeuka kuwa mtu wa mambo mengi,kuamrisha na msiri sana- kutokana na aina ya kazi zao nikajua ni kawaida.

Nilipojifungua mtoto wetu wa pili akaniletea zawadi ya gari mark2-mimi nilikua miongoni mwa wanawake wachache kuendesha mark2 wakati miaka ya90 mwishoni. Tulijisikia vzr sana na mambo ni k**a yalikua yananyooka.

Mwaka 2001 mume wangu alipata nafasi ya kwenda tena chuoni kusoma kwa muda mfupi huko Dar, nikabaki na familia na nikawa naendelea vzr na kazi zangu. Alipomaliza masomo akarudi na maisha yakaendelea kwa muda km kawaida. Baada ya miezi km sita kutoka chuo ni, mume wangu akaniambia anataka kuacha kazi- nilishangaa sana nikamuuliza maswali mengi lkn hukunijibu vzr. Wiki moja baadaye akaniambia ameacha kazi na ameajiriwa shirika moja kubwa la UN hapa Arusha.

Kweli akaanza kuvaa sare mpya za kazi hiyo mpya. Kazi hiyo mpya ilituletea mafanikio makubwa sana ya kifedha na kujieneza kwa mali. Wakati huo pia mimi nilipata nafasi ya kwenda kusoma chuoni muhimbili Dar kwa muda wa miaka mitano. Nikaenda Dar nikaiacha familia ikiendelea vzr kbs.

Nikiwa Dar chuoni nilipata nafasi ya kwenda nje ya nchi kufanya seminar ya health exhibitions (mafunzo ya maonesho)- nikiwa huko nilipigiwa simu kuwa mtoto wetu mdogo amefariki dunia. Nilichanganyikiwa nikarudi nyumbani kwa kuchelewa, nikakuta wameshamzika Alfred mwanangu sikumuona tena. Ilisemekana alifariki ghafla sana bila kujua hasa ni ugonjwa gani au alipatwa na nini mwanangu. Niliongea na madaktari, wakanieleza kuwa mwanangu alitokwa na damu nyingi sana mpk ndani ya jeneza. Uchungu mkubwa na kuchanganyikiwa vilinipata bila kujua hasa nini cha kufanya.

Niliporudi msibani nilishangaa kumkuta mume wangu akiwa na pete kubwa ya dhahabu yenye kinakshi cha tanzanite katikati mkono wa kuume. Nilipomuuliza akaniambia amenunua mjini bei ghali sana na pia ameninulia na mimi aina km hiyo ya pete. Sikujua chochote nikaipokea ile pete km zawadi nikawa naivaa.

ITAENDELEA maana ni ndefu sana...

06/01/2025

😅😅😅

07/12/2024

Eti Kuna ukweli wapendwa

God's Names 🙏
13/09/2024

God's Names 🙏

Kuna siku Mungu atakupa furaha kuu.Isaya 55:22
27/06/2024

Kuna siku Mungu atakupa furaha kuu.
Isaya 55:22

27/06/2024

Address

Dodoma

Telephone

+255657537249

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when WE Belong to JESUS posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to WE Belong to JESUS:

Share