31/08/2017
SIRI ILIYOFICHWA KATIKA TALANTA
Bwana Yesu Asifiwe mpendwa wa Mungu leo ni siku nyingine ambayo Mungu katupa kibali kujifunza Neno lake katika siku hii ya le.
Kila Mtu ameshawahi kusikia na kusoma habari na mfano alioutoa Yesu Kristo kuhusu Talanta na watumwa, Leo tumepata Neema nitakueleza siri iliyopo katika Mfano wa Talanta.
Unaweza ukakubaliana nami kuwa BIBLIA NI UNABII KWA YALE YALIYOTOKEA, YALIYOPO NA YAJAYO.
Talanta Kibiblia imezungumzwa k**a Fedha hila leo Tutaiangalia Talanta k**a Huduma, Karama au wito wa Kristo.
Tutaanza Kuangalia Mstari hu, Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. Mathayo 25 :14
Mfano wa Mtu atakaye kusafiri hapa ni Yesu Alikuwa anajizungumzia mwenyewe kabla ya kurudi kwa Baba na akawaita WATUMWA WAKE( WATEULE&WATUMISHI) na kuweka kwao mali zake,Kibiblia tunaona Yesu Kristo aliweka kwa watumishi wake mali yake na zaidi ya alivyo navyo ndio I maana akasema NILIYOYAFANYA NANYI MTAYAFANYA NA KUBWA ZAIDI YANGU.
Baada ya Yesu kutaka kusafiri alianza kugawa mali kwa watumwa wake na ilikuwa hiv, Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri-Mathayo 25 :15
Hapa Yesu Kristo alitoa Talanta kwa kila mtu kulingana na UWEZO WA UWEZO WA MTU. Halafu yeye akasafiri hii safari ni ya yeye kurudi kwa Babaye Mbinguni. Nini kiliendelea kwa wote waliopewa Talanta? Fatana nami, Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.-Mathayo 25 :16
Huyu aliyepokea Talanta 5 kutoka kwa Yesu Kristo alifanya biashara nazo akazalisha zingine tano,Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida.-Mathayo 25 :17 Unaona mtu wa pili naye alichuma zingine Mbili mbali na alizopewa.
Shida inaanzia hapa sasa Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake.-Mathayo 25 :18
Huyu baada ya kupewa akaificha chini binafsi wengi sana tupo kwa huyu aliyefukia talanta yake chini na kujiona kuwa tupo sawa na hakuna shida kabisa tunaishi maisha ya Amani.
Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.Mathayo 25 :19
Siku iliwadia sasa wakati ambao mwenye mali anakuja kuchukua mali zake ambaye huyu anayekuja si mwingine ni YESU KRISTO WA NAZARETH. Huyu Yesu anakuja kufanya hesabu na WOTE ALIOWAPA TALANTA SAWA UWEZO WAO.
Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida.-Mathayo 25 :20 Waoooooo Huyu alimpendeza Yesu sana kwa hicho alichopewa na kukizalisha na mwisho anarudisha vile alivyopewa na faida juu.
Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.Mathayo 25 :21
Sasa tunaenda kwa aliyepewa mbili, Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida, Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.Mathayo 25 :22-23
Sasa hao tunaona Yesu anawakaribisha hao waliopewa talanta na kuzalisha.
Tumuangalie huyu aliyepewa Talanta moja na akaifuki, Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya; basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.Mathayo 25 :24-25
Umeona majibu ya huyu mtu yani alipewa kitu kwaajili ya kuzalisha yeye anafanya akiinacho ni sawa ambocho ni tofauti na alichopewa nini matokeo yake?
Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.Mathayo 25 :26-30
Nafikiri umeona adhabu iliyomtokea aliye fukuia Talanta yake.
Awali nimesema Leo tunaangalia Talanta k**a Huduma, Karama, Kusudi au Wito ambao ulipewa na Yesu Kristo na Mungu ukiwa Tumboni mwa mama yako na baada ya kumpokea Roho Mtakatifu. Je hiyo umeifukia au umeiwekeza izae mara mbili? wako wengi wanaishi k**a hawakupewa Talanta na Yesu Kristo wanasema wanawasindikiza wengine hii si kweli kila mmoja kapewa kulingana na uwezo wake, wewe uwezo wako ni wa 5,2 au 1? Je Talanta yako inakua au inasubiri kufufuliwa? haya maswali tunapaswa kujiuliza sote.
Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. Yohana 15 :8
Unaona kuwa Mungu anapendezwa na namna ambavyo watu wanamzalia matunda?
Hiyo huduma uliyopewa unaifanya ni ya familia shauri yako vunja mipaka mzalie Mungu aliye hai matunda ya kiroho yaani umsogezee watu zaidi ya aliokupa.
HUDUMA KARAMA NI KWAAJILI YA WATU NA HUO NI MKOPO AMBAO YESU ALIKUKOPESHA URUDISHE NA RIBA NA HAKUNA MSAMAHA WA RIBA KATIKA MKOPO HILA KUNA FIDIA YA KULIPA KWA KUCHELEWESHA AU KUTOKUTOA MKOPO.
MUNGU AKUBARIKI NAKUTAKIA UVUNAJI WA MAZAO MEMA.
Mt. Suleiman S Swai
HUDUMA YA BONDE LA BARAKA TANZANIA.
0745993259/0653053514