05/02/2019
WAEBRANIA 2:18 Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa. Ni ahadi ya Mungu mwenyewe kuwa hawezi kumwacha mwanadamu aliyemfanya kwa mfano wake akajaribiwa kuliko uwezavyo, yapo mambo mengi ambayo yanatesa watu kwa sababu yamezidi uwezo wao kifikra/ kifedha n.k...Mwana wa Mungu; Yesu Kristo alikubali kuithibitisha ahadi ya Baba kupitia msalaba, akateswa ili nasi tupate msaada tujaribiwapo. NI HERI KUMKABIZI YESU MAPITO YAKO ILI AKUSAIDIE