Nzuguni B SDA Church Dodoma +255

Nzuguni B SDA Church Dodoma +255 words of God

18/09/2022

( MAKAMBI 2022)
NITAKWENDA
KWA
UWEZO WA NGUVU
ZA
MUNGU

Baadhi ya vijana Wa kanisani letu LA nzuguni b SDA wakiwa wmewatembelea watoto ambao ni yatima hapa ni kijiji cha matuma...
20/03/2022

Baadhi ya vijana Wa kanisani letu LA nzuguni b SDA wakiwa wmewatembelea watoto ambao ni yatima hapa ni kijiji cha matumaini kampasi ya kisasa karibu na Shule ya martin Luther takribani 5.5 km kutoka Viwanja vya kanisani kwetu na hii nikunogesha juma LA vijana likiambatana mafundisho pamoja na matendo ya huruma

19/03/2022

*Kisa cha Mke Aliyefumaniwa katika Uzinzi*

1 [Walikwenda kila mtu nyumbani kwake; naye Yesu akaenda mpaka mlima wa Mizeituni.

2 Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha.

3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.

4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.

5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?

6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumsh*taki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.

7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.

8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.

9 Nao waliposikia, wakash*takiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.

10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale wash*taki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?

11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]

Yohana 8:1 - 11

19/03/2022

*Baba Anayejali*

27 Ndipo askari wa liwali wakamchukua Yesu ndani ya Praitorio, wakamkusanyikia kikosi kizima.

28 Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu.

29 Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!

30 Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule mwanzi, wakampiga-piga kichwani.

31 Walipokwisha kumdhihaki, wakalivua lile vazi, wakamvika mavazi yake, wakamchukua kumsulibisha.

Mathayo 27:27 - 31

*Baba Anayejali* 27 Ndipo askari wa liwali wakamchukua Yesu ndani ya Praitorio, wakamkusanyikia kikosi kizima. 28 Wakamv...
19/03/2022

*Baba Anayejali*

27 Ndipo askari wa liwali wakamchukua Yesu ndani ya Praitorio, wakamkusanyikia kikosi kizima.

28 Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu.

29 Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!

30 Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule mwanzi, wakampiga-piga kichwani.

31 Walipokwisha kumdhihaki, wakalivua lile vazi, wakamvika mavazi yake, wakamchukua kumsulibisha.

Mathayo 27:27 - 31
# # # # # nukuu kutoka kwa mwinjilisti Fanueli kupitia neno LA Mungu # # # #

Vijana wa sda kwenye kipindi cha shule ya sabato
22/01/2022

Vijana wa sda kwenye kipindi cha shule ya sabato

Ibada Kuu - Nzuguni B SDA ChurchNa Mzee Kiongozi, Fadhili Daudi *KICHWA CHA SOMO: TUKO KWENYE UWANJA WA VITA*Ni pambani ...
22/01/2022

Ibada Kuu - Nzuguni B SDA Church
Na Mzee Kiongozi, Fadhili Daudi

*KICHWA CHA SOMO: TUKO KWENYE UWANJA WA VITA*

Ni pambani kati ya Yesu na Shetani. Tunapojifunza katika Biblia, tunaona Mungu mara zote amekuwa mshindi katika pambano hili. Na hata mara nyingi aliporuhusu siyo kwamba huyo shujaa aliyefia vitani amekufa akiwa upande wa shetani, La Hasha.

2 Mambo ya Nyakati 32: 7 - 8
7 Iweni hodari, na wa moyo mkuu, msiogope, wala msifadhaike kwa sababu ya mfalme wa Ashuru, wala kwa majeshi yote walio pamoja naye; kwa maana yupo mkuu pamoja nasi kuliko aliye pamoja naye;

8 kwake upo mkono wa mwili; ila kwetu yupo Bwana, Mungu wetu, kutusaidia, na kutupigania mapigano yetu. Na watu wakayategemea maneno ya Hezekia, mfalme wa Yuda.

Matengenezo yanamfanya shetani anyanyuke na kupigana na yule alitushindia kupitia sisi.

Soma pia:
_2 Mambo ya Nyakati 32: 1 - 23_

Yeremia 33:3
3 Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.

Hap tunajifunza somo kubwa sana kwani kila mmoja hapa anapitia pambano fulani la aina yake wengine la magonjwa, uchumi, elimu n.k. lakini ukilitambua hili kwamba katika mapambano haya yupo yule ambaye alikwisha shinda kila aina ya pambano na uwezo huyo ametupatia basi siku zote tutapambana kupitia yeye. Yesu amekuwa akitupambania hapa sote tu mashahidi. Hivi karibuni ukame ulitupiga ila tukapiga magoti kuomba na Mungu akatupa Neema ya Mvua. Tukitilia kwa Mungu basi Mungu anashughulika na majeshi yake kwa niaba yetu. Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote aliyemchagua kwa lengo la kutupatia ushindi.

_*Endelea tu na matengenezo. Unapoondoa ibada za sanamu, unapoondoa taratibu ambazo hazimtukuza Mungu basi Mungu wetu wa Mbinguni ataendelea kupigana kwa ajili yetu k**a ilivyokuwa kwa Hezekiel.*_

01/10/2021
28/05/2021

Kuelekea sabato ya wageni idara ya vijana wadogo trh 29 mei 2021 kwapamoja tunasema yesu anatoshaaaa!!!!!

Address

Nzuguni B
Dodoma

Telephone

+255767725522

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Nzuguni B SDA Church Dodoma +255 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share