Efatha Eden Dodoma

Efatha Eden Dodoma Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Efatha Eden Dodoma, Religious organisation, Nkuhungu, Chama, Dodoma.

Kwa nini Mungu alifanya mwanadamu awe wa mwisho katika umbaji?-Mwanadamu apate makao salama-Mungu alikuwa na makusudi ya...
23/08/2026

Kwa nini Mungu alifanya mwanadamu awe wa mwisho katika umbaji?
-Mwanadamu apate makao salama
-Mungu alikuwa na makusudi ya kumuweka mwanadamu juu ya umbaji wote awe wa kipeke ametupa thamani ya katika umbaji
-Mungu aliumba mwanadamu wa mwisho hili kuwafundisha kumtegemea yeye

Tamanio la mungu ni kuwa na ushirika na mwanadamu aliyemuumba kwa sura na mfano wake
Toka agano la kale Mungu anamtafuta mwanadamu awe shIrika pamoja nae
●KUTOKA 19:10-15
●KUMBUKUMBU LA TORATI 4:10
Kwa nini Mungu anataka akutane na sisi kwa sababu kuna viti anataka aseme na sisi anataka kutufundisha jinsi ya kumcha Mungu
●KUMBUKUMBU LA TORATI 31:12
Mungu anatamani kukutana na watu wake kwa ajili ya kumcha yeye

IBADA YA JUMAPILITAREHE 23.08.2026MT:MARTHA MAKAHAWIASOMO:NJIA ZA MUNGU AZICHUNGUZIKINjia za mungu azichunguziki lakini ...
23/08/2026

IBADA YA JUMAPILI
TAREHE 23.08.2026
MT:MARTHA MAKAHAWIA
SOMO:NJIA ZA MUNGU AZICHUNGUZIKI

Njia za mungu azichunguziki lakini kila njia imewekwa kwa majira na wakati wake
●MWANZO 1:26
-Kila kitu Mungu alikifanya kwa makusudi hakuna mahali alikurupuka kufanya kitu aliweka mipanga na mtiririko wa kazi yake yote aliyofanya na kila alichokifanya alijua kinafaha kwa kitu gani
Mungu aliumba mwanadam kwa kusudi la kutawala na kumiliki
Kila alichokiumba Mungu ni kwa kusudi.

Kuna mambo ya kujifunza kuhusu umbaji wa Mungu
●MWANZO 1
-Mungu alijitengenezea Mbingu
-Alitenga mahali pakavu akapaita nchi
●ZABURI 115:16
Mungu alitengeneza nchi kumuwekea binadamu makao salama.kazi yote alifanya hili kumuandalia mwanadamu mahali,mungu alifanya kazi yote hiyo kwa mtu anayeitwa mwanadamu

Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake; Kwa kuwa BWANA ndiye m...
23/08/2026

Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini jina lake;
Kwa kuwa BWANA ndiye mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi.

Zaburi 100:4-5

Mfanyieni BWANA shangwe, dunia yote; Mtumikieni BWANA kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba; Jueni kwamba BWANA ndiye ...
23/08/2026

Mfanyieni BWANA shangwe, dunia yote;
Mtumikieni BWANA kwa furaha;
Njoni mbele zake kwa kuimba;
Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.

Zaburi 100:1-3

Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema, ...
23/08/2026

Akusamehe maovu yako yote,
Akuponya magonjwa yako yote,
Aukomboa uhai wako na kaburi,
Akutia taji ya fadhili na rehema,

Zaburi 103:3-4

Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi ...
23/08/2026

Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.
Naam, vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi jina lake takatifu.
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA,
Wala usizisahau fadhili zake zote.

Zaburi 103:1-2

"Baba yetu wa mbinguni, tunakuja mbele zako mioyo yetu ikiwa imejaa shangwe na shukrani, tukisifu wema wako uliotufikish...
16/08/2026

"Baba yetu wa mbinguni, tunakuja mbele zako mioyo yetu ikiwa imejaa shangwe na shukrani, tukisifu wema wako uliotufikisha hapa; tunaliadhimisha jina lako kwa kuwa wewe ni ngome yetu na mwamba wetu wa wokovu, na sifa za vinywa vyetu ziwe harufu ya manukato inayopanda mbele ya kiti chako cha enzi."

​Zaburi 95:1-2 — "Oya, njoni tuimbie Bwana kwa furaha; tumfanyie kelele za shangwe Mwamba wa wokovu wetu. Na tuje mbele zake kwa shukrani, tumfanyie kelele za shangwe kwa zaburi."

●MWANZO 18:1-15-Ukikosa subira umekosa imani usikatishwe tamaa na kitu chochote kileUsiruhusu moyo wako kuinama●LUKA 1:5...
16/08/2026

●MWANZO 18:1-15
-Ukikosa subira umekosa imani usikatishwe tamaa na kitu chochote kile
Usiruhusu moyo wako kuinama

●LUKA 1:5
-Mungu ana majira na wataki wake anapokusubirisha katika nyakati jua kusubiri kuchelewesha kwako kupata kile unachoitaji ni kwa sababu ya majira ya Mungu dumu katika subira
-mngojee Mungu anaratiba yako njema usichoke wala kukata tamaa endelea kumuamini pasipo kukata tamaa siku yako njema yaja na itakuwa maana Mungu sio muongo na awezi kukuacha yeye yu hai anaishi

●ZABURI 40
-Sio muda wote wa kupambana kuna wakati jifanye mdhaifu sio kila vita ya kupigana jifunze kumngoja Bwana

● YAKOBO 5:9-11
-Yeyote mwenye kusubiri huyo ni heri kwa Mungu,wanaheri wanaojifunza kumsubiri Bwana

IBADA YA JUMAPILI KATIKA KITUO CHA EFATHA NALATAREHE 16.08.2026MCH:DEBORAH UDIBOSOMO:SUBIRA KATIKA MUNGU●DANIEL 11:32-Wa...
16/08/2026

IBADA YA JUMAPILI KATIKA KITUO CHA EFATHA NALA
TAREHE 16.08.2026
MCH:DEBORAH UDIBO
SOMO:SUBIRA KATIKA MUNGU

●DANIEL 11:32
-Watu wamjuhao Mungu wao watakuwa hodari na kutenda mambo makuu
Na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana
-Ukimpenda Mungu utakuwa na subira ya kumgoja Bwana,tujifunze kusubiri katika haki zake(GOD timing is always the best)

-Subira ndio inayoumba imani yoyote aliye na imani ni mtu wa subira anajifunza kumsubiri yeye na kumuamini Mungu katika nyakati zote,dumu siku zote katika kumuamini Mungu
-Subira siku zote inajenga imani na kufanya usipoteze miaka yote uliyomcha Mungu, Mungu achelewagi anayo siku njema kwako.

"Ee Bwana Mungu Mkuu wa majeshi, tunakuinua na kulihimidi jina lako leo kwa kuwa Wewe ndiwe Mungu wa pekee; tunalitukuza...
16/08/2026

"Ee Bwana Mungu Mkuu wa majeshi, tunakuinua na kulihimidi jina lako leo kwa kuwa Wewe ndiwe Mungu wa pekee; tunalitukuza fadhili zako zisizopimwa na ukuu wako usiosemekana, tukitangaza sifa zako katikati ya kusanyiko hili kwa sababu unastahili heshima na utukufu wote."

​Zaburi 145:3 — "Bwana ni mkuu, mwenye kusifiwa sana, wala ukuu wake hautafutiki."

Address

Nkuhungu, Chama
Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Eden Dodoma posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Efatha Eden Dodoma:

Shortcuts

Share