Bethel Gospel Assembly-Tanzania

Bethel Gospel Assembly-Tanzania Ni taasisi ya kiroho inayo husika na kumtangaza Yesu kristo kuwa ni Bwana na mwokozi wa ulimwengu...

*VITA YA KIROHO*Katika sehemu ya 4 niliongelea sana juu ya kuwa na macho ya rohoni.Macho ya rohoni yanakusaudia wewe kuu...
07/01/2026

*VITA YA KIROHO*
Katika sehemu ya 4 niliongelea sana juu ya kuwa na macho ya rohoni.

Macho ya rohoni yanakusaudia wewe kuujua hiyo Vita unayopigana nayo ni aina gani na hao unaopigana nao ni akina nani na Wana uwezo kiasi gani?

✍️Macho ya rohoni yanakusaidia ujue jinsi utakavyopigana Vita yako

*EFESO 1:17-18>>Mungu wa BWANA wetu YESU kristo awape ninyi roho ya hekima na ufahamu....macho ya mioyo yenu yatiwe nuru mpate kujua......*

Ona hapo anasema tupewe roho ya ufahamu na hekima.
🖕Ufahamu ni uwezo wa kutambua kile unachopigana nacho ninkitu gani na kina uwezo kiasi gani.?
🖕Hekima ni ujuzi wa kukusaidia namna ya kuchukua maamuzi ktk Vita unayopigana.

Mfano tukisoma *Efeso 6:12* inasema Kushindana kwetu si juu ya damu na nyama Bali ni juu ya Falme, mamlaka, wakuu wagiza hili, na majeshi ya pepo wabaya......
✍️Sasa k**a mtoto wa Mungu unapaswa kujua hizo Falme NI kutu gani na kina uwezo kiasi gani. Pili unapaswa kujua hao wakuu wa giza ninakina nani na wakija kupigana na nami wanakuja kwa sura ipi?

✋Tunasoma Bible inasema shetani alipomwendea Adamu na Hawa ktk Bustani ya Edeni alivaa mwili wa nyoka hiyo tunaipata *MWANZO 3:1-8*

Sasa k**a ni hivyo hivi akija kwangu na kwenye biashara au nyumba yangu huwa anakuja akiwa na mwili wa namna gani⁉️

Christian wengi hawana uelewa wa kujua hapa ndo shetani kaja aua vipi na k**a amekuja je amevaa sura ya namna gani hawajui. Matokeo yake wanashindwa Vita kirahisi.

*UFUNUO 17:3-6>>Akanichukua ktk roho hata jangwani nikaona mwanamke ameketi naye ana majina ya makufuru.....*

Ukisoma mistari hiyo yote kwa uaminifu utagundua kwamba Yohana alipewa macho ya rohoni akaanza kuona ile Vita iko nyuma ya mwanamke fulani aliyekuwa amevaa mavazi mekundu sijui ana jina la Siri nk. Soma hiyo mistari utaelewa.

Hiyo macho ya rohoni ni mhimu saana ktk Vita unayopigana.

🔥Mfano Vita yako labda inapitia ktk ndoto zako. Ni mhimu kuomba Mungu akupe macho ya ufahamu wa kutambua maana ya ndoto hizo ili uweze jua namna ya kupigana au kuomba.

🖕Angalia unaweza ukaota *Nyoka mkubwa Mweusi tii* aidha unaopigana naye au anatembea nk Hapa unapaswa kujua kuwa Nyoka Mweusi ni nguvu ya uchawi unaopambana ktk maisha yako kiuchumla yaani kila eneo la maisha yako.

🖕Ukiona Nyoka wa kijani maana yake ni nguvu ya uchawi inayopambana na Uchumi wako

👏Ukiona Nyoka wa kijivu maana yake unapambana na roho ya mauti ktk maisha yako. Ninaposema roho ya mauti simaanishi kifo cha *Fa fe fi fo fuuu* hapana hapo ni roho ya mauti ktk maisha yako labda kwenye Uchumi, afya, ndoa, kazi nk

Sasa tunapokuwa hatuna macho ya rohoni inatuwia vigumu saana kujua namna ya kupigana Vita yetu.

🔥Kuna mtu alikuja kwangu akanambia Nabii niombee nateswa na roho ya uzinzi saana nikamuuliza inakutesaje? Akanambia kila mara naota nafanya mapenzi na ndugu zangu wa karibu mfano dada au shangazi zangu nk

Nikamwambia mpendwa hapo hauteswi na roho ya uzinzi Bali unasumbuliwa na roho za Mizimu ya kwenu ambazo zimekuozesha mke wa kichawi.
Yaani inakuwa hivi Mizimu ya kwenu inakupa mke au mume wa kiroho na huyu ndo anakuwa mtawala wa maisha yako. Unaweza ukawa na mke/ mume wa duniani lkn kiroho mizimu imekupatia mke/ mume na huyu ndo anasababisha usiweze kuishi na huyo uliyenaye kwa Amani.

Watu wengi hukosea saana hapo anaanza kuvunja roho ya Uzinzi kumbe ni Mizimu.

👆Ukitaka kujua unateswa na roho ya uzinzi na uasherati utaona ukiota Maumbwa kila mara aidha yanakukumbiza au unayafukuza hayatoki. Tambua hapo vita yako iko kwenye roho ya uzinzi na uasherati.

Somo lifuatalo nitafafanua saana juu ya Ndoto na tafsiri zake na jinsi ya kupigana Vita

**
+255654881958

Address

Kongwa
Dodoma

Telephone

+255654881958

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bethel Gospel Assembly-Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Bethel Gospel Assembly-Tanzania:

Shortcuts

Share