Love Network Tz

Love Network Tz program pekee Tanzania ambayo inashirikisha project zote Tanzania ambazo zina uhusiano wa karibu kati ya viongozi wake na hadhira.

LOVE NETWORK TZ
‘Friends Yet Family’
1 YOH 4 : 8
Ni program ambayo inashirikisha project zote ambazo zina uhusiano wa karibu kati ya viongozi wake na hadhira kwa pamoja kwa nia la kuwasilisha dhamira ya kila huduma. Love network inalengo la kudumisha umoja baina ya vikundi kadhaa ambavyo vina malengo tofauti kwa kushirikishana changamoto ambazo zinawapata

kila mmoja pamoja na mafanikio ili kujifunza vitu mbalimbali vitakavyotusaidia kukua kihuduma. Madhumuni:
LN imedhamilia kuweka msisito kuhusu tunda la roho, (UPENDO) kwa kuwa asili ya upendo ni Mungu mwenyewe, (Mungu ni Upendo) 1 Yoh 4:8 na alituonesha mfano kwa kumtoa mwanae wa pekee Yoh 3:16

LN ipo kuwafariji vijana wenye ndoto za kuanzisha huduma ambazo zitamtukuza Mungu, hivyo itawakutanisha na watu wenye mafanikio makubwa kwenye taasisi zao ili watoe mawazo au hatua za kufanya ili kuweze kufikia viwango wanavyovitarajia. Kufanya charity kwa kuwatembelea wafungwa, yatima na watu wasiojiweza kwa kuwaonesha upendo kwamba bado Mungu ana nafasi kubwa kwenye maisha yao ndio maana anatumia LN kuwakumbusha. Kuandaa event kubwa zitakazohusisha vikundi mbalimbali ambavyo vitapenda kushirikiana nasi ili kuwasilisha huduma ambazo wanazifanya na kutoa zawadi/tuzo kwa waasisi wa hizo pgm ili waendelee kumtumikia Mungu kwa viwango vya juu. Kusambaza habari njema kwa kupeleka injili mijini na vijijini kwa sehemu zisizofikika kirahisi ili kuitangaza kweli ya Mungu, watu wakapate kuona upendo kamili wa Mungu kwenye maisha yao kupitia LN mwisho wapate wokovu. Kubadilisha mitazamo ya jamii iliyotuzunguka kwa kupitia jumbe za picha, video na nyaraka mbalimbali tutakazozitoa kwenye mitandao ya kijamii ambazo zitaelezea thamani ya upendo wa Mungu kwenye maisha yetu. Historia ya NL kwa ufupi:
Hapo awali ilikuwa ipo ndani ya taasisi ya Testimony Tale, lakini kufikia Tar 1 Oct, imejitoa rasmi hivyo itakuwa ni project inayojitegemea wala haitokuwa tena chini ya viongozi wa TT na haitohusika tu na vijana, bali ni kila mtu ambaye anaweza kuungana nasi kufanikisha hili.

CO – Founder of LN

Address

Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Love Network Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Love Network Tz:

Shortcuts

Share