Newjerusalem.chc

Newjerusalem.chc ๐–๐ก๐š๐ญ๐ฌ๐€๐ฉ๐ฉ โ˜๏ธŽ +255 692107628
(2)

25/04/2026

VILIO VYA TAWALA MAMA Upendo Nkone Akimshukuru Mungu

25/04/2026

ANDIKA EE MUNGU wangu usiruhusu adui zangu wafurahie anguko langu โœ…

23/04/2026

KILA MAUMIVU UNAYOPITIA NI YA MUDA MFUPI TU โ€“ MUNGU ATAKUSAIDIABwana Yesu Kristo Asifiwe, Mwana wa Mungu aliye hai.Inawe...
22/04/2026

KILA MAUMIVU UNAYOPITIA NI YA MUDA MFUPI TU โ€“ MUNGU ATAKUSAIDIA

Bwana Yesu Kristo Asifiwe, Mwana wa Mungu aliye hai.

Inawezekana leo moyo wako umejaa huzuni na maumivu. Inawezekana umechoka kwa sababu ya mambo unayopitia. Labda umeomba sana lakini bado hali haijabadilika. Labda umefika mahali unasema moyoni, โ€œJe Mungu kweli ananiona?โ€

Leo nataka nikutie moyo kwa Neno la Mungu:
Maumivu unayopitia si ya milele โ€” ni ya muda mfupi tu. Mungu atakuinua.

Biblia inasema:
โ€œMaana mateso yetu mepesi yaliyo ya muda mfupi yatutengenezea uzito wa utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana.โ€
(2 Wakorintho 4:17)

Hii ina maana kwamba maumivu yako hayataishi milele. Kuna siku yataisha na Mungu atageuza hali yako.

1. MAUMIVU YA MAHUSIANO

Kuna watu wanaumia sana kwenye mahusiano.
Labda uliwapenda watu kwa moyo wako wote lakini walikuumiza. Labda uliamini mtu lakini akakusaliti.

Maumivu ya mahusiano yanaweza kumfanya mtu akate tamaa kabisa.
Lakini Biblia inasema:

โ€œBwana yu karibu na waliovunjika moyo, huwaokoa waliopondeka roho.โ€
(Zaburi 34:18)

K**a moyo wako umevunjika leo, ujue Mungu yupo karibu sana na wewe.
Ana uwezo wa kuponya moyo wako na kukupa mwanzo mpya.

2. MAUMIVU YA KUCHEKWA NA KUDHARAU

Watu wengi wanaumia kwa sababu ya kudharauliwa.

Labda watu wanasema:

โ€œHuyu hawezi kufanikiwa.โ€
โ€œHuyu hana kitu.โ€
โ€œHuyu maisha yake yameharibika.โ€

Lakini kumbuka: watu waliomcheka Yusufu walikuja baadaye kumuinamia.
Biblia inasema:

โ€œBwana huwainua maskini kutoka mavumbini, na mhitaji humwinua kutoka jalalani.โ€
(Zaburi 113:7)

Wale wanaokucheka leo wanaweza kushangaa kesho Mungu atakapokuinua.

3. MAUMIVU YA KUONEWA NA KUSINGIZIWA

Kuna maumivu makubwa sana ya kuonewa au kusingiziwa.

Unaweza kuwa hujafanya kosa lolote lakini watu wanakusemea vibaya.
Wengine wanakupaka matope ili kukuharibia jina.
Lakini Mungu anaona na anajua ukweli.

Biblia inasema:
โ€œSilaha yoyote itakayofanyika juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa.โ€
(Isaya 54:17)

Mungu mwenyewe atasimama kutetea haki yako.

4. MAUMIVU YA KUKATALIWA NA KUBEZWA

unaweza ukawa ni miongoni mwa watu wengi ambao wamekataliwa katika maisha.

Wengine walikataliwa na ndugu zao.
Wengine walikataliwa kwenye kazi.
Wengine walikataliwa kwenye mahusiano.
Lakini hata Yesu Kristo alikataliwa.

Biblia inasema:
โ€œJiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni.โ€
(Zaburi 118:22)

Hata k**a watu wamekukataa, Mungu anaweza kukufanya uwe wa thamani kubwa sana.

5. MAUMIVU YA UMASIKINI

Umasikini unaweza kumfanya mtu ajisikie hana thamani.
Lakini ujue Mungu hubadilisha hali za watu.

Biblia inasema:
โ€œBaraka ya Bwana hutajirisha, wala haiongezi huzuni pamoja nayo.โ€
(Methali 10:22)

Mungu anaweza kubadilisha maisha yako ghafla.

6. MAUMIVU YA MAGONJWA

Kuna watu wanaumizwa na magonjwa ya muda mrefu.
Wengine wamezunguka hospitali nyingi bila kupata majibu.

Lakini Biblia inasema:
โ€œYeye ndiye ayaponyae magonjwa yako yote.โ€
(Zaburi 103:3)

Hakuna ugonjwa uliomshinda Mungu.

7. HATA HILI LITAPITA

Kila hali ya maisha huwa na mwisho.
Biblia inasema:

โ€œKilio chaweza kukaa usiku kucha, lakini asubuhi furaha huja.โ€
(Zaburi 30:5)

Usiku unaweza kuwa mrefu, lakini asubuhi lazima ifike.

HITIMISHO
Kwenye hitimisho Nataka ujue jambo moja muhimu sana:
Hali yako ya sasa si mwisho wa maisha yako.
Mungu anaweza:
~kubadilisha maisha yako
~kukuponya
~kukutetea
~kukufanikisha
~kukurudishia furaha yako

Biblia inasema:
โ€œNayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.โ€
(Yeremia 29:11)

Kwa hiyo USIKATE TAMAA.
Mungu bado ana mpango mzuri juu ya maisha yako.

MAOMBI
K**a unapitia maumivu yoyote katika maisha yako, nataka kukuombea.

Tuma ombi lako la maombi au maelezo ya changamoto unayopitia kupitia WhatsApp:

+255 692 107 628
Pastor Frank Mgaya

Tutakuombea, na Mungu atakusaidia.
Kumbuka:

Maumivu yako ni ya muda mfupi tu. Mungu atakuinua.
Bwana akubariki sana.

By PASTOR FRANK MGAYA

22/04/2026

WIMBO UNAITWA SAUTI NDANI YA MACHOZI kutoka kwake Rev.

MAOMBI YA LEO โ€“ IMANI KWA YALIYOSHINDIKANABaba wa mbinguni,Nasimama mbele zako leo nikikiri kwamba Wewe ni Mungu wa yasi...
22/04/2026

MAOMBI YA LEO โ€“ IMANI KWA YALIYOSHINDIKANA

Baba wa mbinguni,
Nasimama mbele zako leo nikikiri kwamba Wewe ni Mungu wa yasiyowezekana. Wewe ndiye unayesema kwenye utupu na kuleta uhai palipokuwa hapana kitu.

Kuna hali katika maisha yangu zinazoonekana kuwa ngumu, zisizoeleweka, na zilizo nje ya uwezo wangu. Kuna mambo siwezi kuyatatua kwa nguvu zangu mwenyewe. Lakini leo nakumbushwa kwamba hakuna jambo gumu kwako, ee Bwana.

NENO LA MUNGU
Mathayo 19:26
โ€œKwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu yote yanawezekana.โ€
Yeremia 32:27
โ€œTazama, mimi ndimi Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! kuna neno lolote gumu lisilowezekana kwangu?โ€

MAOMBI
Ee Bwana,
Imarisha imani yangu pale mashaka yanapotaka kuingia. Nisaidie nisiangalie yale ninayoyaona kwa macho ya mwili tu, bali niamini yale uliyoniahidi.

Wakati hali zinaonekana hazibadiliki, nikumbushe kwamba bado unatenda kazi, bado unasonga, na bado una uwezo wa kufanya zaidi ya ninavyofikiri au kuwaza.

Nifundishe kukuamini kwa moyo wote, na nisaidie kuachilia mipaka yote niliyoweka juu ya uwezo wako. Ondoa mashaka yangu, ujaze ndani yangu imani thabiti.

Badilisha kusitasita kwangu kuwa ujasiri.
Badilisha hofu yangu kuwa tumaini.
Badilisha kutokuamini kwangu kuwa imani isiyotikisika.

TAMKO LA IMANI
Leo nachagua kuamini kwamba:
Mungu anafanya kazi hata nisipoona
Mungu hajachelewa
Mungu ana uwezo wa kubadilisha kila hali
Najua tayari unatenda kazi nyuma ya pazia kwa ajili yangu.

Nachagua kuamini, kuamini, na kuendelea mbele kwa imani.

Kwa maana Wewe unaweza kufanya zaidi sana kuliko yote niombayo au nifikiriyo.

Katika jina la Yesu Kristo,
Amina.

WITO WA IMANI

K**a umebarikiwa na maombi haya, andika kwa imani:

๐Ÿ‘‰ โ€œMUNGU WA YALIYOSHINDIKANA ANATENDA KAZI KWANGU SASAโ€

BY PASTOR FRANK MGAYA
Huduma: Newjerusalem Church of Holy Christians

๐Ÿ“ Makao Makuu: Dodoma, Tanzania

UJUMBE WA KINABII โ€“ USIKU HUU MUNGU ANABADILI HATIMA YAKO ๐ŸŒ™๐Ÿ”ฅUsiku huu si wa kawaida. Ni usiku ambao Mungu anaingilia kat...
21/04/2026

UJUMBE WA KINABII โ€“ USIKU HUU MUNGU ANABADILI HATIMA YAKO ๐ŸŒ™๐Ÿ”ฅ

Usiku huu si wa kawaida. Ni usiku ambao Mungu anaingilia kati safari ya maisha yako. Kuna mambo yaliyokuwa yamepangwa dhidi yako, lakini Mungu anayavunja kimya kimya. Kuna kilichokuwa kimechelewa, lakini usiku huu kinaanza kusogezwa mbele.

๐Ÿ“– Zaburi 30:5
โ€œMaana hasira hudumu kwa kitambo kidogo, lakini fadhili hudumu maisha yote; kilio huja kukaa usiku, lakini asubuhi huwa furaha.โ€

Hii ni kauli ya Bwana kwako: kile kilichokufanya ulie muda mrefu, usiku huu kinapoteza nguvu yake. Mungu anabadili simulizi yako; anayageuza mapambano kuwa ushuhuda, aibu kuwa heshima, na kuchelewa kuwa kasi ya ghafla.

Usiku huu, Mungu anafanya kazi mahali ambapo macho yako hayawezi kufika. Anarekebisha yaliyochakaa, anafungua yaliyofungwa, na anakuandaa kwa asubuhi mpya. Usilale na hofuโ€”lala na imani.

Tamka kwa sauti:

> โ€œUsiku huu Mungu anabadilisha hatima yangu. Ninapokea amani, ulinzi, na mabadiliko ya ghafla kwa jina la Yesu.โ€ ๐Ÿ™๐Ÿ”ฅ

Lala kwa amani. Asubuhi yako haitakuwa k**a jana. By PASTOR FRANK MGAYA

18/04/2026

USIKU WA LEO UTATETEWA NA MUNGU
13/04/2026

USIKU WA LEO UTATETEWA NA MUNGU

13/04/2026

MWAMINI MUNGU

12/04/2026

1 Wakorintho 9:14
Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.

Address

Dodoma

Telephone

+255622510770

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Newjerusalem.chc posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Newjerusalem.chc:

Share