Pastor Erasto Msuka

Pastor Erasto Msuka ▪️ Apostle,Pastor & Teacher at MAABARA YA YESU CHURCH - Dodoma, Tanzania
▪️Mentor
▪️Life Coach.

Wafuata miujiza badala ya kumfuata YESU mtenda miujiza waliandamana kwenda kwa haka kajinga. Walitoa laki 5 k**a sadaka ...
28/07/2026

Wafuata miujiza badala ya kumfuata YESU mtenda miujiza waliandamana kwenda kwa haka kajinga. Walitoa laki 5 k**a sadaka ya kumuona nabii kiboko ya wachawi na maombezi ya "KUPOKEA"😂😂.

Sijui hao wafuasi wake wako wapi siku hizi!! Au ndo hao wanaosumbua makanisani leo na mapepo yao ya umala** wa makanisa, ni magumegume hao.

2 Timotheo 4:3-4

"Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; 4nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo".

Mithali 12:1 SUV

"Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa; Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni k**a mnyama".

NB: Utatapeliwa sana usipomruhusu YESU KRISTO kuwa BWANA ili akutawale, akuongoze na kukutiisha kwenye KWELI (NENO).

Apostle & Pastor Erasto Msuka
CMF-MAABARA YA YESU PENTECOST CHURCH, Nzuguni Dodoma.
28.07.2026.



HAPPY ABSENCE DAY Leo *4.4.2026* ingekuwa *Birthday* yako mke wangu kipenzi, lakini kwa mapenzi ya *MUNGU* akaona vyema ...
04/04/2026

HAPPY ABSENCE DAY

Leo *4.4.2026* ingekuwa *Birthday* yako mke wangu kipenzi, lakini kwa mapenzi ya *MUNGU* akaona vyema ukaisherehekee *PARADISO*.

Kwa mara ya kwanza, ninasherehekea siku yako ya kuzaliwa bila uwepo wako mama wa watoto wangu wazuri.

Siku k**a hii, tulizoea kuitumia kwa pamoja kumtafakari MUNGU kwa zawadi ya maisha kwetu.

Endelea Kumsifu MUNGU huko uliko, endelea kuinama na kuinuka mbele za MWANA-KONDOO WA BWANA pamoja na Makerubi, Maserafi na Malaika, ukiuimba wimbo wa *Musa*, "Wastahili MWANA-KONDOO uliyechinjwa.

Bado nitaendelea kukuenzi kwa kuwa mwaminifu kwa maisha yangu yote, mpaka hapo MUNGU atakaponifungulia mlango wa agano jingine kwa UAMINIFU wangu. Vitoto vyako *Miracle na Melvin* wanakukumbuka, ila picha zako kwenye SIMU zetu imekuwa faraja kwao, Miracle anauliza baba *"mama atarudi lini?, akipona atarudi?".* Watoto hawa wananifariji sana mke wangu.

"*_Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika k**a na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye_ "* (1 The 4:13-14)

Tunakukumbuka mama yetu.

04/04/2026
05/03/2026

Ministering and Mastering Birthday Ceremony.

*MC kazini.*

Shepherd Erasto

HAPPY BIRTHDAY HELLEN (MRS OMAR) 1/3 miaka kadhaa iliyopita, ndio siku iliyokubali kukuleta duniani mtoto wangu mrembo  ...
04/03/2026

HAPPY BIRTHDAY HELLEN (MRS OMAR)

1/3 miaka kadhaa iliyopita, ndio siku iliyokubali kukuleta duniani mtoto wangu mrembo HELEN binti JOSEPH.... Masha'Allah.....

K**a Mchungaji wako na baba yako wa Kiroho, ninayo furaha kubwa sana kwa Neema ya MUNGU kukuona ukiongezewa mwaka (1+ ) mwingine tena.

Najua mwanangu umepitia nyakati nyingi za furaha, maumivu, misukosuko, amani, magonjwa, mafanikio, kudharauliwa na kuthaminiwa n.k.

Umekuwa na nyakati pia za kumiliki vitu vingi vizuri na vya thamani kwenye maisha yako ikiwemo mume, watoto, fedha, nyumba, mavazi, biashara n. k, hakika hayo yote ni mema sana mbele za MUNGU, lakini nikuhakikishie tu, siku uliyofanya maamuzi ya kupokea "WOKOVU (YESU)" ndicho kitu cha THAMANI sana ulichokipokea katika maisha yako yote MWAKA JANA. Ninakufurahia sana mwanangu kukuona ukizidi kuongezeka kumpenda YESU kwa IMANI ya MATENDO na unazidi kumtegemea Yeye kila iitwapo leo.

Yeremia 17:7

“Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake”

Umefanyika BARAKA kubwa kwenye Kanisa lako la CMF-MAABARA YA YESU PENTECOST CHURCH , SADAKA zako na majitoleo yako yote ni HARUFU NZURI YA MANUKATO YA KUPENDEZA MBELE ZA MUNGU. MUNGU azikumbuke SADAKA zako na kuyaangaza maisha yako k**a tafsiri ya jina lako " Helen/Hellen" - yaani mwangaza au Nuru au mng'ao(Light or Shining).

Abarikiwe mume wako kipenzi Mr. Omar , wabarikiwe mabinti zako wazuri, Mariam na Zuhura (Zuu).

Umemheshimisha MUNGU na familia yako kwa kufanyia BIRTHDAY PARTY yako ndani ya KANISA. Libarikiwe tumbo lililokuzaa.

Hesabu 6: 24-26

“Bwana akubarikie, na kukulinda; Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; Bwana akuinulie uso wake, na kukupa amani”

Happy birthday to you my lovely spiritual daughter, mwanangu kipenzi, Hellen wangu, kipenzi cha Omar mwenyewe, shangazi na bibi wa MIRACLE na MELVIN. Melvin ameniambia akija nyumbani akute misosi ya kutosha na masotojosotojo yake.... 😂😂😂. Enjoy your day daughter.

Pastor Erasto Msuka

NINI KINATAWALA AKILI YAKO?Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.” Yakobo ...
24/02/2026

NINI KINATAWALA AKILI YAKO?

Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.” Yakobo 1:22

Mojawapo ya funguo muhimu ya kuishi maisha ya ushindi ni kuwa mtendaji wa Neno la Mungu. Kwa maana yeyote aliyelisoma neno kisha akalichukua Neno na kuliishi,alitembea kwenye baraka siku zote za maisha yake. Faida ya Neno la Mungu haipo katika kusoma na kutafakari pekee,bali faida ipo katika kuliishi Neno la Mungu.

Neno la Mungu likitawala akili yako, litaathiri mwenendo na tabia yako.

Kuwa mtendaji wa Neno ni:

•Kuweka Neno katika matendo ya kila siku
•Kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu
•Kutii hata sauti ya Mungu
•Kuruhusu Neno litawale maamuzi na tabia

Luka 11:28 “Heri walisikiao neno la Mungu na kulishika.”

Kumbuka;

Silaha na funguo kubwa ya ushindi ni kuwa mtendaji wa Neno. Hebu kumbuka kile ambacho Bwana alichowaambia Israeli kwenye Kutoka 19:5, aliwaambia ikiwa wataitii sauti yake kweli kweli, na “kulishika agano langu,” hapo ndipo watakapokuwa tunu kwake kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yake.

Vita na Mapigano ni ya kawaida. Imani ni tofauti. Wale wasio na Neno hutukuza adui lakini wale walio na Neno hutangaza ahadi za ushindi.

Acha mazoezi ya kushindwa bali anza kutangaza ushindi. Mfariji yuko pamoja nawe. Ahadi yake bado ipo.

Ushindi wako unaanza pale Neno linapotawala akili yako.

Shepherd Erasto Msuka

24.2.2026.

Yamkini Mwaka 2025  haukuwa mzuri kwako  ulipata MISIBA Umelia sana 😭😭.......... Umehuzunika Sana kiasi cha Imani yako k...
23/12/2025

Yamkini Mwaka 2025 haukuwa mzuri kwako ulipata MISIBA Umelia sana 😭😭..........

Umehuzunika Sana kiasi cha Imani yako kwa Mungu kutikiswa hata kushuka kabisa kwa sababu ya mapito mengi lakini, naomba kusema neno Moja NAWE rafiki yangu......

MUNGU BADO YUPO NA WEWE, ANAJUA MAPITO YAKO YOTE uliyopitia, unayopitia na yajayo, HIVYO HATA K**A HAJAJIBU UNAVYO TAKA YEYE BABO NI BABA YAKO.

Jambo moja jema kwako ni kwamba, 2026 ni MWAKA BORA ZAIDI KWAKO......... NEEMA MPYA, KIBALI KIPYA, MIPENYO MIPYA , BARAKA MPYA ZIPO NJIANI ZINAKUJA. AMINI TU.

Isaya 43:19

"Tazama, nitafanya jambo jipya! Sasa litachipuka, je, hamtalitambua? Nitafanya njia jangwani na vijito vya maji katika nchi kame".

👉Mwaka 2026 Simama na MUNGU....... UTAFANIKIWA KILA JAMBO UTAKALO LIFANYA KWA IMANI.

✍️Andika "NINAPOKEA"

Erasto .

Address

Dodoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Pastor Erasto Msuka posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Pastor Erasto Msuka:

Shortcuts

Share