Kelvin Chambua-H.L.M

Kelvin Chambua-H.L.M Mahali pa kutano na Mungu
Hapa ni mahali pa mguso
Mahali watu wanageuzwa kwa neno la Mungu

SHALOMNAJUA TUPO KWENYE JUMA AMBALO TUNAKUMBUKA KILE YESU ALIKIFANYA PALE MSALABANI KWA AJILI YA MWANADAMUTAMBUA:-Kazi y...
29/03/2024

SHALOM
NAJUA TUPO KWENYE JUMA AMBALO TUNAKUMBUKA KILE YESU ALIKIFANYA PALE MSALABANI KWA AJILI YA MWANADAMU

TAMBUA:-Kazi ya Yesu Masalabani Kufa na Kufufuka kwetu waamini ni ya kukumbukwa na kutangazwa wakati wote sio kwenye wiki ya pasaka tu.Huu ndio ujumbe wetu.

WELL MIE LEO NASUKUMWA KUZUMNGUMZIA USALAITI WA YUDA NA KILE UMENIFUNZA BINAFSI NAAMINI NAWE ITAKUJENGA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE.

TUANZIE HAPA:-
MOJA K**A UMEFWATILIA NA KUSOMA UTAGUNDUA JAMBO HILI YESU ALIWAFAHAMU WANAFUNZI WAKE WOTE NA TABIA ZAO PASIPO MTU KUMWAMBIA KITU CHOCHOTE

Yohana 6:70.,71.
70. *Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?* 71. Alimnena Yuda, mwana wa Simoni Iskariote; maana huyo ndiye atakayemsaliti; naye ni mmojawapo wa wale Thenashara.

BWANA YESU ALIMJUA YUDA NA KITU ALICHONACHO NDANI YAKE HATA KABLA HAKIJA DHIHIRIKA ILA ALIJUA YUPO PALE KWA KUSUDI(KUMSALITI-KUWA CHANZO CHA YESU KUK**ATWA) KWASABABU WANAFUNZI WAKE ALIWAPATA KUTOKEA KWENYE MAOMBI YA MKESHA.

HAKUCHAGUA ILI MRADI ILA ALIPATA NAFASI YA KUKAA KWENYE MAOMBI NA KUMUULIZA MUNGU ILI AMPE WATU SAHIHI ALIOWAKUSUDIA KWA AJILI YAKE.MAANA YAKE HATA WEWE KABLA HAUJASHIRIKIANA NA MTU IWE NI HUDUMA/BIASHARA N.K SPEND TIME NA MUNGU ILI MWENYE ENZI AKUFUNULIE WATU SAHIHI WA KUAMBATANA NAO SAWA?

TAZAMA HAPA...
Luka 6:12-16.
12. Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. 13. Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume; 14. Simoni, aliyemwita jina la pili Petro, na Andrea nduguye, na Yakobo na Yohana, na Filipo na Bartolomayo, 15. na Mathayo na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Simoni aitwaye Zelote, 16. na Yuda wa Yakobo, na Yuda Iskariote, ndiye aliyekuwa msaliti.

Nataka ufahamu Yesu aliwajua na ndio maana aliwagawa kwa makundi(Alichukua tahadhari )

Utagundua 1(Yohana ni Mwanafunzi aliyependwa sana na Yesu hata akalala kifuani mwake)

Alafu walikuja 3(Yohana,Petro,Yakobo) Hawa kuna siri walikuwa wanazijua kumuhusu Yesu hadi udhaifu aliokuwa anaufunua wakiwa mahali pa siri pa Maombi.

Kuna mambo akina Petro walikuwa wanayajua kuhusu Utukufu wa Mungu na hawakusema kwa watu(Wanafunzi) wengine mpaka Yesu alipoondoka Duniani.

Alafu the 12(Na wao walikuwa wana mambo yao pia)

Alafu 70(Wale waliotumwa wawili wawili kuhubiri)Then Makutano

Ukifwatilia utagundua aliwatenga kwa makusudi kabisa kiasi kwamba wayahudi walipotaka kumuua haikua raisi kumpata Unless amekuwa betrayed na watu wake wa karibu na as you read your Bible una gundua walifanana na Yesu vibaya mno kwasababu ya nguvu ya kuathiri aliyokuwa nayo Yesu ikambidi mpaka Yuda amsaliti tena kwa kwenda kumbusu ili wamjue Yesu ni yupi this is Amazing .Eeh Mungu nipe nguvu ya kuwathiri watu kwa kiwango hiki aisee

Iko hivi Ukiona Adui yako anataarifa zako ujue Mtu wako wa karibu au Rafiki yako anashirikiana na Adui zako/yako.

Niliwahi kusema hivi kipindi fulani kwamba "Ni Panya wa ndani ndio amjurishaye Panya wa nje mahali unafichaga chakula"

Hata mwizi hawezi kuingia mahali ambapo hajajikusanyia taarifa za kutosha ili asik**atwe na watoa taarifa ni watu wa Nyumbani humo humo atakapo kuiba.

My point ni hii kuwa makini na watu waliokaribu nawe sio kila Mtu anapaswa kuwa karibu sana na kufahamu kila kitu chako sawa huwezi kusalitiwa na wa mbali wasaliti wa kwanza ni wanaokujua na uharibifu wao huwa mkubwa sana kuliko wa mtu wa nje.

Kosa kubwa wengi hufanya ni kushare important staff na Rafiki yako ambaye ni Rafiki wa Adui yako pia...K**a upo kwenye hili fungu nikwambie tu umeishwa shindwa vita kabla hata haijaanza



Nikutakie Heri ya Siku kuu ya Pasaka ikawe njema sana kwako mtu wa Mungu.Umebarikiwa sana

Kelvin Chambua Ck
Heaven Light Ministries Intl
Dodoma
Tanzania

22/01/2024

Shalom shalom
Unaendeleaje???

Daka hii...

‭‭Mat‬hayo ‭9:2‭-‬8‬ ‭SUV‬‬
[2] Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; *naye Yesu, alipoiona imani yao,* alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako. [3] Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. [4] Naye Yesu, hali akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu? [5] Kwa maana rahisi ni lipi, ni kusema, Umesamehewa dhambi zako, au ni kusema, Ondoka, uende? [6] Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako. [7] Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake. [8] Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii.

‭‭Mt‬ ‭9:2‬ ‭SUV‬‬
[2] Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; *naye Yesu, alipoiona imani yao,* alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako.

1) IMANI INAWEZA KUONEKANA.

2/MTU ANAWEZA KUSAIDIKA SIO KUPITIA IMANI YAKE BALI IMANI YAKO.

Yesu hakuiona Imani ya Mgonjwa ila aliona Imani ya Watu waliompeleka Mgonjwa na Kwasababu yao mgonjwa akapata msaada kutoka kwa Yesu

Kuna wakati acha watu wasimamie kwenye Imani yako na kupokea msaada kutoka kwa Mungu ikibidi.
can stand for them and pray

3) IMANI INAWEZA KUONEKANA.
Nataka uone yakwamba imani inaweza kuonekana Kabisa kwa Macho

*Inaonekanaje sasa????*
-Inaonekana kupitia Matendo(Hatua unazochukua)...Hawa Ndugu walikosa nafasi mlangoni wakaenda kupita darini.

Sasa utaelewa kwanini Mtume Yakobo Anaandika imani pasipo Matendo imekufa Yakobo 2:26

Endelea kuamini katika Mipango yako ya 2024 uliyoweka hata k**a mengine hayakufanikiwa 2023.Safari hii tutachukua hatua na kuweka kwenye Matendo yale ambayo tumepanga Nakwambia 2024 tunatoboa

#2024 NI YETU.
Umebarikiwa sana
Kelvin Chambua CK
Heaven Light Ministries Intl
Dodoma
Tanzania

01/01/2024

Shalom Shalom
Heri ya Mwaka 2024....
Karibu Darasani na Nimesukumwa kuanza na Ujumbe huu Mwaka huu

KICHWA:- MUNGU ANAWEZA KUWA MWALIMU WAKO AKAKUFUNDISHA NA KUKUONGOZA KATIKA NJIA SAHIHI.

Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini k**a mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na k**a yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.
1 Yoh 2:27 SUV

Haya mafuta yanayotajwa hapa sio mafuta tu ila ni Alama yake Roho Mtakatifu.Ni Alama moja wapo kati ya alama zake Roho Mtakatifu kwahiyo badala ya kusema Mafuta/Anointing sema Roho Mtakatifu aliyeko ndani yenu atawafundisha habari za Mambo yote na kuwapasha habari juu ya Mambo yajayo.

Sasa Roho afundishi kila mtu ila wale waliojiachilia na wako tayari kufundishwa na yeye.Kujiachilia maana yake umemtambua na kumpa nafasi yake anayoistahili

Lakini Hatua ya kwanza unaanzia kwenye kuokoka kisha unampokea akae ndani yako akiishakaa NDANI YAKO hapo ndipo anaanza kukufundisha.Maana yake ili aweze Kukufundisha lazima awe ndani yako na wewe uwe tayari kujiachilia Mikononi mwake na kutii Maelekezo au Neno lake au maongozi yake anayokupa.

Tenga Muda nae na umpe Nafasi ya Kwanza kwenye jambo lolote unalotaka kulifanya atakushangaza kwasababu Roho Mtakatifu anautashi usio wa kawaida kwasababu YEYE ni Mungu

Ona pia Mstari huu....
Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
Zab 32:8 SUV

➡️Nitakufundisha(Hapa Mungu anakuwa Mwalimu wako wa kwanza kwasababu anajua yote na ndiye alikuumba na alikuleta Duniani kwa kusudi lake maalumu jiachilie kwake akufundishe mwenyewe kuyatekeleza Mapenzi yake)

➡️Nitakuonyesha Njia...Acha ayafungue Macho yako akuonyeshe njia sahihi ya kuiendea ili usije kukosea njia wala kupotea
na Mungu kamwe hawapotei Njia wala hutasikia wako njia panda kamwe

➡️Nitakushauri...Peleka na Mipango yako na Mambo yako kwake na acha Yeye akushauri lipi utekeleze lipi liache au usubiri kwasababu sio wakati wake sahihi KUMBUKA hajawahi kumuonyesha Mtu njia na kumuacha aende peke yake bali humuongoza na kumuelekeza kwa upole mpaka aifikie Kanani yake salama. and Obey Him

MKAZO WANGU:-
Moja Mungu anajua yote kwahiyo anaweza kukufundisha vyema haswa yale yasiyo dhambi...Kwasababu Mambo ambayo ni dhambi hasili yake sio Mbinguni

Pili Anaijua njia unayopaswa kuiendea ndio maana Biblia ya King James Version inamtaja Roho Mtakatifu k**a ni GUIDER SIO LEADER akiwa ana maana anaijua Njia amekwisha kuipita kabla yako Mungu anajua wapi unatakiwa kutulia au kuendelea au wapi ukimbie wapi utembee au wapi upumzike...nk

Kasome Hesabu 9:18- Utaona wakati Mungu anawaongoza wana wa Israeli kwa lile Wingu mahali lilipotulia na wao walitulia lilipoelekea ndipo walipo elekea n.k

Nini nakwambia Mungu anajua direction ya Maisha yako na njia yako sio ya wengine kuna mizunguko ipo kwenye njia yako ni kwa ajili ya kukutengeneza kuwa mtu bora sana...Usitake kwenda k**a wengine wewe sio wao Wewe umetengwa...Wewe ni wa tofauti...Wewe ni wa Bwana.
Wingu usifwate watu

Na kinachonishangaza zaidi hata ukianza kuiendea njia bado ataenda na wewe na atakuwa anakushauri ili usifanye Maamuzi yasiyo sawa ukiwa kwenye Njia(Utatembea kwenye Mapenzi yake)

God is so so careful na maisha yetu anatuwazia yaliyo mema sana

Ona na hii...
Basi sasa, enenda, *nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena.* Nawe utasema naye, na kuyatia maneno kinywani mwake; nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na pamoja na kinywa chake, na *kuwafundisheni mtakayofanya.*
K*t 4:12‭, ‬15 SUV

Nimesoma sana na kusikia watu wakifundisha kuhusu wito wa Musa na namna Bwana alimtuma ila leo mistari hii imerudi sana Moyoni mwangu kwa namna ya ajabu

Katikati ya mabishano ya Musa kuogopa kurudi Misri Mungu hakuahidi kuwa nae tu ila anahidi kumfundisha nini cha kufanya na nini cha kusema katika utumishi wake oooh Glory...Angalia hakuishia hapo alipomfundisha ni k**a alimuwekea uwezo pia wa kwenda kumfundisha na Haruni kile alifundishwa na haya ni Maombi yangu Mambo ambayo Bwana atakufundisha sirini, Mungu akawekee na huo uwezo wa kufundisha na wengine kwa jina la Yesu Kristo aliye hai.amen

NOTE:Na hiki ndicho kitafanya hata wewe utumishi wako uwe tofauti ikiwa Bwana ndiye atakuwa anakufundisha na kukuelekeza nini cha kufanya .Huwezi Kufundishwa na Bwana na ukawa Mtu wa kucopy vya wengine.

Gharama ya uanafunzi ni kutoa muda wako wa kusikiliza na kutunza kwenye maandishi hicho anachokufundisha hata k**a unaona ni kitu kidogo tunza kuna wakati hayo Maarifa utayahitaji.
kwenye Maandishi

Kumbuka hujaitwa kuiga cha Fulani k**a ni kweli umeitwa maana yake MUNGU anayo Maelekezo specific kwa ajili ya utumishi wako na akitaka ufundishwe na Mtu atakudirect(kuelekeza) kwa huyo mtu au kukuletea huyo Mtu ili apate kuachilia kile kitu chako ambacho Mungu amekiweka ndani yake kwa ajili yako.

ukapoteza kile ulichopewa sawa sawa

We are different (Tuko tofauti)

Chochote unachotaka kukifanya kwenye Huduma yako iwe ni strategy irudishe kwenye Mizani ya Maombi ili kutaka kusikia Bwana anasemaje kuhusu Mawazo uliyonayo utakuja kushangaa sana namna ataanza kusema na Wewe.Hatujui kila kitu ila tupo tayari Kujifunza kwake kila siku iitwapo leo.

Ona na hii...
BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, *nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.*
Isa 48:17 SUV

Bwana akikufundisha kamwe huwezi kupata Hasara....Bwana ni Mtu wa Faida.Huwezi kupata Hasara kwasababu Mungu huutangaza mwisho kabla ya mwanzo maana yake anaujua Mwisho.Aliishapita ndio akaja kukuchukua kukupitisha Wewe anajua kila kitu.Anaona kila kitu hata yaliyo Sirini kwasababu Giza na Nuru kwake yote ni sawa.


Alafu atakuongoza katika njia ikupasayo kuifuata sio Njia yeyote utakayoiona au uitakayo hakuna kwasababu kuna njia Bwana amekukusudia kuipita tangu kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu na ndiyo atakayo kuongoza kupita kwayo.

Kwahiyo Notice jambo hili k**a unataka kupata faida lazima ukubali kuwa Mwanafunzi na ukubali awe Kiongozi wako maana anaijua Njia sahihi ikupasayo uifwate sio uipite(Fwata ile njia ambayo Yeye tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu alikuandalia kuipita usipite popote)... Gharama yako ni kujiachilia na kusikia Sauti na Kuona kile anakusemesha(UFUNGUO WA KULA MEMA YA NCHI NI UTII JUU YA NENO LA KIMAELEKEZO ALILOLITOA BWANA)

KUTII maana yake kukubali na kuliweka kwenye matendo lile Neno alilokwambia.Unapokea Maelekezo yake na kuyafanyia Kazi tena kwa wakati.

Ona na hii kutokea kwenye Upande wa familia na malezi
*Na watoto wako wote watafundishwa na BWANA;* na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.
Isa 54:13 SUV

Unaweza kumwamini na kumkabidhi watoto wako na Yeye akawa Mwalimu wao maisha yao yote.Ukimkabidhi watoto wako ataanza kuwaongoza na kuwafundisha.

Wewe k**a mzazi pamoja na kwamba Mungu amekuamini kuwa Mwalimu wao kuwafundisha mema lakini kuna mahali wataenda hautakuwa pamoja nao wakabidhi mikononi mwake ili awafundishe mwenyewe na kuwalea na kuwatunza.

Sikia ukimpa Bwana Watoto wako ndio pale utashangaa kila wanapoenda Bwana atawainulia watu ambao watajitoa kuhakikisha wanawalea k**a vile ni watoto wao wa kuwazaa na kuwekeza Maarifa yasiyo ya kawaida ndani yao alafu unakuja kugundua ni BWANA alikuwa kazini akiwafundisha Watoto wako mwenyewe.

Embu jimilikishe huu Mstari kwasababu ni moja ya mistari yenye ahadi ya amani ndani yake akikufundisha Wewe na familia yako moja ya Matokeo mtayaona ni kukaa katika Amani(Pasipo vita/Maneno-Maneno/shida/Majanga/Mawazo n.k)

Kumjua Mungu pia ni moja ya chanzo cha Mtu kukaa katika Amani

Hekima ya Kimungu pia itakufanya ukae katika amani nyingi k**a ilivyokuwa kwenye mipaka ya sulemanj.Nimekuongezea haya kwasababu katika Kukufundisha moja ya Matokeo yatakuja juu yako ni Kumjua Mungu zaidi lakini pia Hekima na Maarifa ya Kimungu yatafunuliwa kwako/Ndani yako by default.

Umebarikiwa sana tuishie hapa kwa leo mpaka wakati mwingine tena.Asante sana kwa kujifunza nasi

Hongera kwa kuingia 2024 lakini amua ya kwamba ndani ya Mwaka huu Mpya kuongozwa na kufundishwa na Mungu katika chochote kile ufanyacho.Umebarikiwa

2024 NI YA KWETU


Min. Kelvin & Jenipher Chambua CK
Heaven Light Ministries Intl
+255715242566
Dodoma
Tanzania

10/11/2023

SIFA ZINAZOMFANYA MTU KUWA MWANAFUNZI WA KRISTO KWELI KWELI

*Mwanafunzi wa Kristo ni nani?*
Mwanafunzi ni Mwamini au Mtu ambaye amemwamini Kristo na amekubali kukaa na kujifunza kumuhusu Mungu na Kristo wake aliyemtuma

hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.
Mdo 11:26 SUV

Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Mathayo 28:19‭-‬20 SUV
-Kuwafanya Mataifa au Watu kuwa Wanafunzi ni kazi endelevu aliyopewa Muamini kwenye Agizo kuu

-Ni kazi ya kumuandalia BWANA watenda kazi

-Ni kazi ya kulijenga Kanisa (Mwili wa Kristo) la Mungu.... Fahamu Kanisa ni Darasa tunenda kujifunza kuhusu Mambo yamuhusuyo Mungu sio kuburudishwa.

ni jambo la Lazima...msiminye Muda wa Mafundisho ya Neno la Uzima

Nikisema hivi namaanisha Viongozi wahakikishe wanapata Muda wa kujiandaa kuja kufundisha na wawe Watu wanaosoma na kujifunza ili wawe na Chakula/Neno.(Tenga Muda wa kumtafuta Mungu ili akupe kitu cha kusema na watu wake).

Wajibu wa Pili unaenda kwa wasikiaji moja k**a Wewe ni Mwanafunzi makini lazima uwe na Mahali pa kuandika na hautakaa mahali ambapo haita sikia vyema utajua namna ya kujiposition,lakini pia kuwaombea wanaokuja kufundisha wafundishe/waseme k**a inavyowapasa kunena

Kanisa ni SHULE inanayotufundisha mambo yamuhusuyo Mungu (YESU)

Uanafunzi ni Maisha ya Mkristo...Tunatakiwa kujifunza na kukua katika kumjua Yeye(Mungu/Yesu ma Uweza wa kufufuka kwake)

Don't create followers but create disciples(Usitengeneze Wafuasi tengeneza Wanafunzi).Na usijitengenezee Wanafunzi wako bali Wanafunzi wa Kristo.

*Je ni nani anaweza kuwa Mwanafunzi?(Ninawezaje kuwa Mwanafunzi)*
-Kwa kuhubiriwa Injili ya Kristo
-Kuiamini kazi yote ya Msalaba(Kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo)
-Kukaa Chini ya Fundisho la Kristo(Ufundishwe yote ambayo Yesu aliwamuru Mitume kuyashika).

☑️Kasome Agizo Kuu utayaona haya yote.

*SIFA ZA WANAFUNZI WA KRISTO*
➡️SIFA YA KWANZA:- MWANAFUNZI NI MTU ALIYEJIKANA NA KUJITWIKA MSALABA WAKE NA KUMFWATA KRISTO YESU.
-Its No longer about You but Christ-Its all about Christ(Hakuna tena kuhusu Wewe ila Kristo)-Upotee aanze Yeye kuonekana kupitia Wewe
-Kujitoa Mzima Mzima hakuna kuangalia Nyuma tena
-Ni Mtu aliyeacha vyote kwa ajili ya Kristo

K**a mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Luka 14:26‭-‬27‭, ‬33 SUV

➡️SIFA YA PILI:- MWANAFUNZI NI MTU WA NENO(MTU ALIYEKAA CHINI YA FUNDISHO LA KRISTO Mfano Mitume akina Petro)
-Amejaa Neno la Mungu
-Ameshika Neno la Mungu
-Anaishi kwa Neno la Mungu

Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, *Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;*
Yohana 8:31 SUV

➡️SIFA YA TATU:- MWANAFUNZI NI MTU ANAYETEMBEA KATIKA PENDO
-Amejifunza Kumpenda Mungu na kuwapenda Watu walioumbwa na Mungu(Jamaa ya Waaminio na Adui pia)
-Ni katika Pendo pekee ndio tutawajua Wanafunzi halisi wa Kristo
-Sio kuhubiri kuhusu Upendo ila kuuishi na lazima Ufahamu Upendo hauthibitiki kwa Maneno ila kwa Matendo.

Amri mpya nawapa, Mpendane. K**a vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. *Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.*
Yohana 13:34‭-‬35 SUV

➡️SIFA YA NNE:-MWANAFUNZI NI MTU ANAYEMZALIA BWANA MATUNDA
-Ni Mtu mwenye Matokeo chanya kila alipo
-Ni Mtu anayewaleta wengine kwa Yesu yaani anafanya kazi ya Muhubiri Injili
-Ni Mtu aliyeunganishwa na Kristo na anatembea katika Usafi/Utakatifu... Mwanafunzi Yeye ni Tawi la Mzabibu yaani Kristo kuzaa kwake kunategemeana sana na Ushirika wake na Kristo.

Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. *Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.* Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. K**a vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje k**a tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. *Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.*
Yohana 15:1‭-‬8 SUV

➡️SIFA YA TANO:- MWANAFUNZI NI MTU ALIYEKUWA KAJAA ROHO MTAKATIFU NA IMANI N.K
-Kawatazame Mitume au akina Stefano walikuwa ni watu wa Imani haswa na watu waliokuwa wamejaa Roho Mtakatifu haswa.

Najua ziko nyingi ila izo kadhaa hapo zikufunze jambo unapoendelea kujifanyia tathimini binafsi Mwisho huu wa mwaka

HITIMISHO:-Nimalize kwa kusema hivi

Fahamu jambo hili Hapo kwanza Wakristo wote tuliitwa Wanafunzi au Waamini kabla ya Matendo 11:26

Jambo la pili kwa kadri Injili inavyohubiriwa na kufundishwa ndivyo idadi ya Wanafunzi inavyoongezeka

Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.
Matendo 6:7 SUV

*Hata walipokwisha kuihubiri Injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi,* wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia,
Matendo 14:21 SUV

-Kwa Kadri NENO LA MUNGU LINAVYOENEA VIVYO HIVYO NA WANAFUNZI WANATAKIWA KUONGEZEKA.

MAANA YAKE KWA KADRI WATU WENGI WANAVYOSIKIA NENO LA MUNGU TUNATEGEMEA WABADILISHWE NA ILE KWELI WANAYOISIKIA NA HATIMAYE KUONGEZEKA KWA JAMII YA WAAMINIO(WAKRISTO AU WATU WANAOMWAMINI KRISTO YESU)
THE GOSPEL UNTIL SOMETHING HAPPEN(ENDELEA KUHUBIRI INJILI MPAKA VITU VIANZE KUTOKEA).

-SASA LENGO LETU LISIWE KUONGEZEKA BALI KUWAFIKIA WATU NA HABARI NJEMA ZA YESU KRISTO. NAANDIKA HAYA KWASABABU LENGO SASA LIMEBADIRIKA SIO TENA KUOKOA NAFSI ZA WATU BALI WATU WANAANDAA MIKUTANO NA SEMINA K**A SEHEMU YA HARAMBEE ZA KUPATA PESA NA MASHINDANO KWAMBA K**A MTUMISHI FULANI ANAFANYA NA MIMI LAZIMA NIFANYE HIZO WRONG MOTIVES (NIA MBAYA/MBOVU) ZIMETULETEA WRONG RESULTS (MATOKEO MABAYA).

UMEBARIKIWA MTEULE.AMEN

Min.Kelvin & Jenipher Chambua CK
Heaven Light Ministries Intl
H.L.M-H.L.A.N
DODOMA.
TANZANIA.

19/09/2023

*HEAVEN LIGHT MINISTRIES INTL*

Shalom Nakusalimu kwa jina lipitalo majina yote ninayo Mambo machache natamani tuaangalie leo...

*NIFANYE NINI NINAPOMTUMIKIA MUNGU CHINI YA MTUMISHI MWINGINE WA MUNGU ALIYENITANGULIA KIHUDUMA*

Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa Neema yake ya Ajabu na kunipa kupita chini ya Huduma kadhaa na mpaka leo bado natumika na Huduma pia na humu ndani nimepewa kujifunza mambo kadhaa ya muhimu sana kwenye Maisha ya UTUMISHI na Mimi leo nataka nishare na wewe Mambo machache ya Msingi ambayo yatakusaidia sana.

*HAPA NASEMA NA WATU HAWA*
1/WATOTO WA KIROHO WANAOLELEWA NA MTUMISHI.

2/ASKARI WENGINE WANAOHUDUMU PAMOJA NA MTUMISHI KWENYE HUDUMA(WATUMISHI WA MUNGU WANAOTUMIKA CHINI YA KIONGOZI)-NASEMA NA WATENDA KAZI WOTE WANAOFANYA HUDUMA CHINI YA MTUMISHI YEYOTE WA MUNGU.
-Wenye Huduma za masaidizano i.e waombaji waimbaji, partners,K**ati n.k

*MAMBO YA MUHIMU YA KUJIFUNZA UNAPOTUMIKA CHINI YA MTU*
1/Muheshimu na Hakikisha unakuwa MTII juu ya Maelekezo Mtu wa MUNGU anayatoa ili uwe salama katika leo yako na kesho yako ya Huduma.

Naelewa kibinadamu kuna wakati unaweza kuona k**a amekosea mambo lakini lazima ujue hajifanyii tu ila na Yeye anapokea Maelekezo kutoka kwa aliyemuita incase unapata shida na Maamuzi au Maelekezo nenda peke yako kazungumze kwa kumshauri k**a unaona kuna namna ingefanyika na kuleta ufanisi zaidi na akikataa tii na mwisho ukumbuke mwenye huduma ni Yeye(Yeye ndiye Mungu amemwamini na kumpa na wewe pale upo kujifunza)

MFANO:Elisha na Geazi
-Geazi Mtumishi wa Elisha alipatwa na ukoma kwa kutokutii Neno lililosemwa na Mtumishi la kutokupokea Fedha kutoka kwa Naamani.K*tii ni tabia ya Watu wanyenyekevu

Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako. Lakini akasema, K**a BWANA aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa. Naamani akasema; K**a sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala wawili; kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa BWANA. Jambo hili BWANA amwachilie mtumwa wako; bwana wangu akiingia nyumbani mwa Rimoni ili aabudu humo, naye akitegemea mkononi mwangu, nami nikijiinama nyumbani mwa Rimoni, hapo ninapojiinama nyumbani mwa Rimoni, BWANA amwachilie mtumwa wako jambo hili. Akamwambia, Enenda kwa amani Basi akamwondokea mbali kidogo. Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema, Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta; k**a BWANA aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu kwake. Basi Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio anakuja nyuma yake, alishuka garini amlaki, akasema, Je! Ni amani? Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana na manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili. Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamshurutisha, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakayachukua mbele yake. Naye alipofika kilimani, alivitwaa mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha wale watu kuondoka, nao wakaenda zao. Lakini yeye akaingia, akasimama mbele ya bwana wake. Elisha akamwambia, Watoka wapi, Gehazi? Akanena, Mtumwa wako hakuenda mahali. Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng’ombe, na watumwa, na wajakazi? Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma k**a theluji.
2 Fal 5:15‭-‬27 SUV
-Kosa dogo la kutokutii kukamcost akapata ukoma na hakupokea tena hata upako uliokuwa juu ya Elisha(Kosa likamcost Maisha usifanye hili kosa)

-Hapa ndipo nilijifunza hata k**a Mtumishi atakukwaza kiasi gani na kukuumiza nitaenda kulia kwa Bwana ila nitajitahidi sana kunyamaza ikibidi kuondoka kabisa hilo eneo ili usije ukakosea Nakwambia tena ni mambo ya kujifunza

*As we learn we grow in it(Tunapozidi kujifunza tunakuwa)*

-Neno la MUNGU linasema kutii ni bora kuliko dhabihu
1Samweli 15:22

Unapogusa Eneo la fundisho la Utii moja ya jambo utagundua ni kwamba Mungu kwenye maandiko yake matakatifu amekuagiza kuwatii na kuwaombea wale wanaotuongoza
Warumi 13:1-

K*tokutii ni dhambi na ndio dhambi waliyoitenda Adamu na Hawa pale bustanini shida haikuwa kula ila shida ilikuwa walikula walichoambiwa wasile umeipata Point yangu hapo...Ukiambiwa usifanye alafu wewe ukafanya maana yake umeasi au haujatii agizo/Neno....Umekaidi

Na kwenye UTUMISHI ni hivyo KIONGOZI Mkuu ni mmoja Yeye ndiye anatoa Maelekezo wengine tunafuata maelekezo yaliyotolewa unless k**a alikukaimisha na hapo lazima utafute kujua anasemaje juu ya kile unataka kukifanya...Maana yake lazima uwajibike kumpa taarifa.

2/. TEMBEA/TUMIKA KATIKA UNYENYEKEVU, UAMINIFU NA UPOLE.

-Biblia inamuonyesha Elisha akimimina maji juu ya mikono ya Elia na huoni akinung'unika Mahali popote.... Au kaangalie Nafasi alikuwa nayo Daudi baada ya kupelekwa Ikulu alikuwa ni mbeba silaha lakini wakati huo huo MUNGU alikuwa anampa shule kuhusu Ikulu.

Hapa namaanisha k**a unataka kupokea kile kilichoko juu ya Mtumishi lazima Ujifunze kumtumikia na kuwa Mwaminifu ndipo Bwana atakupa cha kwako.

Maana yake unapoona Mungu amekupeleka sehemu lazima utambue moja ya sababu za msingi za Mungu kukuweka chini ya Mtumishi mwingine ni wewe kujifunza na hakikisha kwa jitihada zote unawekeza katika kujifunza sana.Moja ya mambo utajifunza ni mwendo wa namna ya kutumika n.k

Mtumishi wa Mungu T.D Jakes aliwahi kusema You can't Receive the Anointing that you don't serve(Huwezi kupokea Upako wa Mtumishi ambaye hujautumikia/Hujatumikia chini ya Mtumishi aliye nae huo upako).

The Mantle is transferable(Vazi/Upako unamishika)Ila hauendagi kwa yeyote.Kumbuka wana wa Manabii walikuwepo ila aliyepokea upako uliokuwa juu ya Elia ni mmoja tu Elisha chanzo ni nidhamu aliyokuwa nayo.

3/Hakikisha unapata MUDA wa Kumuombea na kutoa Mali au fedha zako(sadaka) kutegemeza HUDUMA YAKE.

Nisikilize k**a Yeye anakesha kukuombea nawe muombee tena kwa bidii sana....KUMUOMBEA NI LAZIMA SIO OMBI HATA K**A HUTAKI MUOMBEE

Pia Neno linasema atampiga Mchungaji na kondoo watatawanyika...
Marko 14:27

Shetani akitaka kuwavuruga anampiga Kiongozi wenu,na akipigwa kundi lote hutawanyika na hamtaendelea Mbele tena...

kwahiyo kumuombea kwenu ndio usalama wenu pia.Kumuombea kutawafanya mmpende na kunyenyekea zaidi...K**a hujui moja ya jambo Maombi hufanya ni kushughulikia hali yako ya ndani(Mtu wako wa ndani pia)

Kasome namna Paulo alikuwa anayaombea makanisa yaliyoenda kuhubiri pamoja nae kwa Mali zao Mfano Kanisa la Filipi nilikuwa nasoma mpaka Nashangaa... anawatamkia Maneno Mazito ya Baraka

Unajua Mungu anatufundisha ni hili Jifunze kujiungamanisha na SADAKA kwenye HUDUMA ya MTUMISHI unayetumika chini yake.Kuna wakati unakuta umepata kujua kuna Mambo yanamsumbua na anahitaji FEDHA au assistance fulani be there saidia pasipo kutaka kuonekana na Watu uone k**a kutakuwa na Milango iliyofungwa Mbele yako.

Usisubiri partners watoke Nje kuja kusupport HUDUMA yenu lakini anzeni nyinyi kujitoa watu wa nje wakija waje kusupport tu.Chota Baraka chap chap hahaa hapa najua kuna aina ya watu hawapendagi kusikia habari za Sadaka ila kasome biblia yako Zawadi itakupa kibali mbele za wakuu Wewe endelea kwendaga mikono mitupu tu hayaa sisi Wengine haya tulijifunza in a hard way hatukupataga Mtu wa kutuambia mapema ila Namshukuru Mungu amenipaga nidhamu ya kujifunza kwa watu iwe kwa kutazama au hata kuuliza inapobidi na hiki moja ya watu walitumika kupanda mbegu ni Mke wangu pamoja na Mtumishi wa Mungu Rehema tena huyu ndio aliniambia wazi wazi Mungu awabarikini sana kokote mlipi

Ile kwamba mpo ndani ya Huduma sio guarantee ya ninyi kupokea kile alichobeba Mtumishi hata k**a atawawekea mikono kila Mara na kuwaombea.

Nakwambia ukweli Mtu yeyote anayesimama na Mtumishi kwenye jambo lolote analolifanya huwa anaenda pamoja nae kokote aendapo, na kiukweli huwa anakuwa kwenye Moyo wa Mtumishi kasome habari za Mama Mshunami na Elisha nawaza tu k**a yule mama asingelipata wazo la kujenga kile chumba yamkini Elisha asingelipata mzigo wa kumuombea ili apate Mtoto.

*Iguse madhabahu nayo ikuguse*

Madhabahu ambayo huipelekei sadaka haiwezi kukusaidia.Iguse madhabahu ya Mtumishi unayetumika nae kwa SADAKA ZAKO acha kupeleka Nje au Mbali majibu yako yapo hapo hapo Tulia Unless umeongozwa na Bwana...Hii inaenda mpaka kanisani maana wengi hiwa wanawadharau wachungaji wao sana leo upone kwa jina la Yesu.

Jifunze kujichotea baraka,kwani hujawahi kufwatilia na kujiuliza kwanini watu wa nje ndio hubarikiwa/kupata msaada kwa wepesi kuliko walioko ndani ya Huduma/Kanisa

4/KATAA KUJILINGANISHA NAE HATA K**A NA WEWE NI MTUMISHI.

-Upako huwa hautembei horizontal (ulalo) ila Vertical (kutoka juu kwenda chini).Ukitaka kupokea jishushe kujishusha sio dhambi ila itakufaidia wewe ujishushae.

Kujilinganisha nae wakati wengine huwa ni matokeo ya kiburi cha uzima/Ujeuri n.k

Kuna Watu wa Mungu wana mahusiano ya ndani sana unaposhindana nao Bwana atakachokuja kufanya ni kukublock wewe ukajikuta hukui wala uendelei kamwe au hata kupigwa kabisa na Mungu kwa ujinga wako.

MAFANO:
MUSA /HARUNI V.S AKINA KORA
Hesabu 16:
-Kora alimchallenge Musa na Haruni kwamba na wao ni makuhani Mungu hawezi kusema na akina Musa tu peke yao na wao ni Watumishi ...alafu aliyeita akaja kuamua kesi ndipo Ardhi ikafunguka na ikawameza akina Kora na wenzie wote.

Soma hapa....
nao, pamoja na watu kadha wa kadha wa wana wa Israeli, watu mia mbili na hamsini, Wakuu wa mkutano, waliokuwa wateule wa mkutano, watu wenye sifa, wakainuka mbele ya Musa; nao wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, BWANA naye yu kati yao; n’nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa BWANA? Musa aliposikia maneno haya, akapomoka kifudifudi; kisha akanena na Kora na mkutano wake wote, akawaambia, Asubuhi BWANA ataonyesha ni kina nani walio wake, kisha ni nani aliye mtakatifu, tena ni nani atakayemkaribisha kwake; maana, yeye atakayemchagua ndiye atakayemsongeza kwake. Fanyeni neno hili; twaeni vyetezo, ninyi Kora na mkutano wake wote; vitieni na moto, mkaweke na uvumba juu yake mbele za BWANA kesho; kisha itakuwa ya kwamba mtu BWANA atakayemchagua, yeye atakuwa mtakatifu; inawatosha ninyi, enyi wana wa Lawi. Je! Mwaona kuwa ni jambo dogo kwenu, kuwa Mungu wa Israeli amewatenga ninyi na mkutano wa Israeli, ili apate kuwakaribisha kwake; ili mfanye utumishi wa maskani ya BWANA, na kusimama mbele ya mkutano ili kuwatumikia; tena ya kuwa amekuleta uwe karibu, na ndugu zako wote wana wa Lawi pamoja nawe? Nanyi, je! Mwataka na ukuhani pia? Kwa sababu hii wewe na mkutano wako wote mmekusanyika kinyume cha BWANA; na Haruni, je! Yeye ni nani hata mkamnung’unikia? Musa akakasirika sana, akamwambia BWANA. Usiikubali sadaka yao; mimi sikutwaa hata punda mmoja kwao, wala sikumwumiza hata mtu mmoja miongoni mwao. Kisha Musa akamwambia Kora, Wewe na mkutano wako wote iweni hapa mbele ya BWANA kesho, wewe, na wao, na Haruni; mkatwae kila mtu chetezo chake, na kutia uvumba juu yake, mkavilete mbele za BWANA, vyetezo mia mbili na hamsini; wewe pia, na Haruni, kila mtu na awe na chetezo chake. Basi wakavitwaa kila mtu chetezo chake, wakatia na moto ndani yake, wakatia na uvumba juu ya moto, na kusimama pale mlangoni pa hema ya kukutania, pamoja na Musa na Haruni. Kisha Kora akakutanisha mkutano wote kinyume chao mlangoni pa hema ya kukutania; na utukufu wa BWANA ukatokea mbele ya mkutano wote. Kisha BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja. Nao wakapomoka kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote? BWANA akasema na Musa, na kumwambia, Nena na mkutano, na kuwaambia, Ondokeni ninyi hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani, na Abiramu. Basi Musa akainuka na kuwaendea Dathani na Abiramu; na wazee wa Israeli wakaandamana naye. Akasema na mkutano, na kuwaambia, Nawasihi, ondokeni penye hema za hawa watu waovu, wala msiguse kitu chao cho chote, msiangamizwe katika dhambi zao zote. Basi wakaondoka hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani na Abiramu, pande zote; nao kina Dathani na Abiramu wakatoka nje wakasimama mlangoni mwa hema zao, pamoja na wake zao, na wana wao na watoto wao wadogo. Musa akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kwamba BWANA amenituma, ili nifanye kazi hizi zote; kwa kuwa mimi sikuzifanya kwa akili zangu mwenyewe. K**a watu hawa wakifa kifo cha sikuzote, k**a watu wote wafavyo, au k**a wakipatilizwa kwa mapatilizo ya watu wote; hapo basi BWANA hakunituma mimi. Lakini BWANA akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau BWANA Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka; nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshik**ana na Kora, na vyombo vyao vyote. Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni. Nao Israeli wote waliokuwa kando-kando yao wakakimbia kwa ajili ya kilio chao; kwa kuwa walisema, Nchi isije kutumeza na sisi. Kisha moto ukatoka kwa BWANA, ukawateketeza hao watu mia mbili hamsini waliofukiza uvumba.
Hes 16:2‭-‬7‭, ‬9‭-‬11‭, ‬15‭-‬35 SUV

*MFANO WA PILI NI MWENDELEZO WA HIKI NI HESABU 17*

Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia, Nena na wana wa Israeli, kisha upokee kwao fimbo, fimbo moja kwa ajili ya nyumba ya kila baba, katika wakuu wao wote, k**a nyumba za baba zao zilivyo, fimbo kumi na mbili; kisha andika jina la kila mtu katika fimbo yake. Na katika fimbo ya Lawi utaliandika jina la Haruni; maana, itakuwa fimbo moja kwa kila kichwa cha nyumba za baba zao. Nawe utaziweka katika hema ya kukutania mbele ya huo ushahidi, hapo nikutanapo pamoja nanyi. Kisha itakuwa, mtu huyo nitakayemchagua, fimbo yake itachipuka; nami nitayakomesha kwangu manung’uniko ya wana wa Israeli, wanung’unikiayo juu yenu. Basi Musa akawaambia wana wa Israeli, ndipo wakuu wao wote wakampa fimbo, fimbo moja kwa kila mkuu, k**a nyumba za baba zao zilivyokuwa, fimbo kumi na mbili; na fimbo ya Haruni ilikuwa kati ya fimbo zao. Kisha Musa akaziweka hizo fimbo mbele za BWANA katika hema ya kukutania. Ilikuwa siku ya pili yake, Musa akaingia ndani ya hema ya ushahidi; na tazama, ile fimbo ya Haruni iliyokuwa kwa nyumba ya Lawi ilikuwa imechipuka, imetoa michipukizi, na kuchanua maua; na kuzaa malozi mabivu. Kisha Musa akazileta nje hizo fimbo zote kutoka hapo mbele za BWANA na kuziweka mbele ya wana wa Israeli wote; nao wakaangalia, na kila mtu akaitwaa fimbo yake. Kisha BWANA akamwambia Musa, Irudishe fimbo ya Haruni mbele ya ushahidi, ili itunzwe iwe ishara juu ya hawa wana wa maasi; ili uyakomeshe manung’uniko yao waliyoninung’unikia, ili wasife. Basi Musa akafanya vivyo; k**a BWANA alivyomwagiza, ndivyo alivyofanya. Kisha wana wa Israeli wakanena na Musa, na kumwambia, Angalia, sisi twafa, twaangamia, sote twaangamia. Kila mtu akaribiaye, aikaribiaye maskani ya BWANA, hufa; je! Tutakufa pia sote?
Hesabu 17:1‭-‬13 SUV

-Mungu akachipuza fimbo bila kupandwa wala Maji ili kusignify aliowachagua na Mungu akakomesha Maneno yote.

-Chunga sana Mdomo wako na Matendo yako ifahamu nafasi yako na tumika kwa uaminifu mahali ambapo MUNGU amekupa ukiona umeshindwa toka ila usimobilize watu against Mtumishi ili utake Nafasi aliyonayo....Hiki kitu ndio kile alichotaka kufanya shetani pale Mbinguni alitaka kufanya mapinduzi yeye ndio aanze kurun show pale kilichompata mpaka leo anasimulia,akajua yeye si chochote si lolote.

Kuna wakati Utukufu unaouona uko juu yako ni kwasababu ya Mahali ulipojiungamanisha napo Dont forget that...Siku utakapoyakoroga na ule Utukufu utaondoka juu yako maana Utukufu ni Vazi.

5/MPOKEE MOYONI MWAKO NA TAMBUA MAFUTA YALIYOKO JUU YAKE ILI UWEZE KUYAFAIDI.

-Nataka utambue Mtumishi yeyote hata yule unayemuona niaje niaje pia anamafuta ya Roho Mtakatifu juu yake na hayo Mafuta huwa hayatoki kiholela Neno la Mungu linasema Ampokeae Nabii hupata Thawabu ya Nabii

Maana yake nini hatak**a Mtumishi anaupako mkubwa kiasi gani ukimdharau huwezi kupata msaada kutoka kwake kamwe

MFANO:YESU NA WATU WA NYUMBANI KWAKE
-Wagalilaya walikosa kufaidi kile kilichokuwa juu ya Yesu kwa ajili yao kwasababu walipofushwa na roho ya mazoea (the spirit of familiarity-Walijikuta wanamjua sana wakidhani ni Mtoto wa Yusufu na ndio wakapishana na Muujiza yao)

Soma hapa...
Na alipofika nchi yake, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, *Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii?* Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda? Na maumbu yake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote? Wakachukizwa naye. Yesu akawaambia, *Nabii hakosi kupata heshima, isipokuwa katika nchi yake, na nyumbani mwake mwenyewe. Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwao.*
Mt 13:54‭-‬58 SUV

Kwenye Mfano huu kuna Mambo mengi ya kujifunza
-Hawa ndugu hawakumuamini Yesu kisa ni walikuwa wanamfahamu pamoja na Ndugu zake.Nakwambia fwatilia Ndugu au watu wowote wanaomfahamu Mtumishi tangu akiwa mdogo k**a huwa wanapokea kile amebeba,Hawa hata akiwepo kwenye Huduma anakuja kumsupport Ndugu yake unless Mungu ameingilia kati...

GROUP jingine ambalo huwa halipokei au huwa ni kazi wao kupokea au kumpokea ni Marafiki zake ambao walikuwa wanamjua tangu zamani nakwambia fuatilia na hawa nao ni mpaka Bwana awaponde ponde kwanzaa ndio utaona kuvunjika na wanaanza kumtazama k**a Mtumishi wa Mungu.

Kamwe usiruhusu Mahusiano yako ya nje na MTUMISHI yakuzuie kupokea Neno au Upako au Thawabu aliyobeba Mtu wa MUNGU Jifunze kubadirika ili uweze kufaidia upako juu ya Mtumishi kuna Muda hata k**a ni Rafiki yako ukiona tu kaanza kuongea kwenye Nafasi ya kitumishi na Wewe hama harakaa ili uweze kupokea sawa sawa haya Mambo sio mepesi lakini jifundishe jilazimishe mpaka uweze ni Rafiki yako sawa,Ni mume wako sawa lakini bado ni Mtumishi wa Mungu na akiama Nafasi hama nae.

Ivi umegundua pia hata wake za Watumishi au Watoto(biological) na wao huwa mara nyingi hawafaidiki na upako uliopo juu ya Watumishi wa Mungu.

Nakumbuka niliwahi kusikia ushuhuda Mmoja wa Mama Mchungaji mmoja ambaye alikuwa kanisani kwenye Ibada na mume wake alikuwa akiwahudumia watu na Wingu au Upako Ulikuwa Mkubwa sana na watu walisaidika sana wakawa wanatoa shuhuda kuu yule mama akainuka katikati ya ibada akarudi nyumbani akapika chakula kizuri akipendacho Mume wake na akatoa sahani za wageni akatenga Mezani akimsubiria Baba Mchungaji arudi...Sasa na Baba Mchungaji kule akawa anahudumu huku akitafakari kuna kitu gani kimetokea mbona Wife kaondoka ghafla alipofika nyumbani akakuta yale Mazingira akakaribishwa na kuketishwa Mezani...Sasa familia yao ilikuwa inapitia changamoto fulani na walikuwa wameomba lakini hakuna Matokeo yeyote yule Mama akapiga magoti akamwambia Baba Mchungaji familia yangu inapitia hili naomba uniombee yule Pastor anasema Upako ule ule uliokuwa kanisani ukashuka juu yake saa ile ile pale nyumbani akaweka mikono juu ya mke wake nae akaenda chini kwa Nguvu za Mungu...Hapa nikajifunza Upako wa Roho Mtakatifu unatabia usipomheshimu Mtumishi haukusaidii kamwe....

Unajua kilichotokea ni hivi yule Mama alitambua Nafasi ya Mume wake k**a Mtumishi wa Mungu na kwamba Mungu ameweka kitu juu yake kwa ajili ya watu na yeya ni mmoja ya watu waliowekwa chini yake....Mama akaama kutoka kwenye Nafasi ya mke wa Mtumishi akawa Kondoo katika kundi la Bwana ambalo Mtumishi ameaminiwa kwalo akahusiana na Mume wake k**a Mtumishi wa Mungu na alipofanya hivyo Mungu akayasikia Maombi yake.

Umenielewa ewe Mama Mtumishi si ndio ? Ubarikiwe sana

SOMA PIA MFANO HUU:
➡️MUSA, HARUNI NA MIRIAM
Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi. Wakasema, Je! Ni kweli BWANA amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? BWANA akasikia maneno yao. Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi. BWANA akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje. BWANA akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili. Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa? Hasira za BWANA zikawaka juu yao; naye akaenda zake. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe k**a theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma. Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi. Nakusihi, asiwe k**a mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake. Musa akamlilia BWANA, akasema, Mpoze, Ee Mungu, nakusihi sana. BWANA akamwambia Musa, Je! K**a baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena. Basi Miriamu alifungwa nje ya kambi muda wa siku saba; wala watu hawakusafiri hata Miriamu alipoletwa ndani tena.
Hes 12:1‭-‬15 SUV

-Nataka nikuonyeshe Ndugu za Musa ambavyo walijikwaa kuhusu kuoa kwa Musa na wakamsema na Mungu akasikia na akaja kuamua jambo hili Miriam akapigwa na ukoma Haruni akanusurika kwasababu alikuwa na Mafuta ya kikuhani siku ile juu yake

tena Chunga kimya chako sometimes unaweza kuumizwa lakini jizuie usiongee kwa watu kaongee kwa Mungu hata k**a unaona madhaifu yake jitahidi kuyaficha unayaona kwasababu upo karibu na Mungu ameruhusu uyaone ili umuombee sawa sawa Acha Maneno Maneno.

Kumbuka hata WATOTO wa Nuhu kuna mmoja aliufunua uchi wa Baba yake badala ya kuufunika k**a wale wawili waliopata Hekima akapokea Laana kwa generation yake na wenzie wakavuna baraka kwasababu walimstahi Baba yao na kufunika uchi wake.

not Unveil the Nakedness of Your father/Man of God (Usifunue uchi wa Baba yako... Mtu wa Mungu)

Kumbuka kwasababu ya ukaribu ulionao nae ndio maana umeyajua hayo Madhaifu k**a unaona huwezi kuhandle(kustahimili) jiweke mbali sio lazima umzoee na sio dhambi kujiweka mbali ni nidhamu njema kwa ajili ya afya yako ya kiroho.

Soma hapa...
Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao. Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea. Akasema, Na alaaniwe Kanaani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake. Akasema, Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu; Na Kanaani awe mtumwa wake. Mungu akamnafisishe Yafethi. Na akae katika hema za Shemu; Na Kanaani awe mtumwa wake. Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini. Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa.
Mwa 9:20‭-‬29 SUV

*UNAPOTUMIKA MAMBO HAYA NAOMBA USIAYASAHAU*

1/Unapotumika kuna Kitu k**a Kiongozi unatakiwa kukiachilia kwa walio chini yako

MFANO Yesu aliaachilia NENO LA MUNGU kwa Mitume 12 na PAULO pia aliachilia NENO LA MUNGU kwa akina Timotheo tena akawaagiza na wao wawafundishe watu wengine waaminifu lile Neno.

Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.
2 Timotheo2:2 SUV

-Nataka Ufahamu wewe k**a Kiongozi ni kielelezo kwa walio chini yako kuna watu wanakufwata na wanajifunza chini yako.

Wewe ni barua kuna watu wanakusoma kwa kadiri unavyoonyesha ubora katika UTUMISHI wako unafanya na Watu walioletwa chini yako Kesho kuja kuwa bora zaidi yako maana wamejengwa kwenye Msingi bora.

Jambo la Mwisho wekeza kwa kuwafundisha NENO LA MUNGU kwa ufasaha kumbuka MUNGU amekuamini na amekupa dhamana na kuna muda akiwataka anategemea wawe wameiva na wamekomaa.
hayo tu

2/Kwa wale wanaotumika chini yako(Mtumishi ) naomba niwaambie Mambo mawili ya kutoa
-Moja Muda wako na kupokea kile unapewa yaani Neno ukiwa na mtazamo kwamba unabeba NENO kwa ajili ya generation itakayofuata...Unabeba NENO kulipeleka kwa Watu wengine watakaokuwa waaminifu.

Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.
2 Tim 2:2 SUV

Jambo la Pili ujitoe Kwa Vitu vyako Mali kuhakikisha unasupport Huduma ambayo unamtumikia Mungu kwayo

na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, *waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.*
Luka 8:3 SUV

-Je Wewe unamtumikia Mtumishi Kwa Mali zako(unatumika pamoja nae kwa fedha zako?)
-Kwasababu ya Uwepo wako hakikisha kuna maeneo Mtumishi wa Mungu asistruggle ndio maana Mungu alikupeleka hapo ili Yeye akupandie vya Rohoni naye avune vya Mwili ni Kanuni ya kimungu though Paulo akasema aliamua kufanya kazi ili asije akamlemea Mtu yeyote umenielewa
1Wakoritho 9:11

ANGALIZO LA MUHIMU:
-Jifunze kujitoa zaidi Mfano ni kweli umekuja k**a Partner wa Huduma ila kuna muda unaona kuna kitu/Vitu unaweza kufanya na wanahitaji mtu hakikisha unakuwa tayari kujitoa kwa hari yote na kuyafanya yote kwa uaminifu na kwa moyo wako wote k**a kwa Bwana.Maana wengi wanaotoa Fedha huwa hawajitoi.... 2Wakoritho 8:5

Tena walitenda hivi si k**a tulivyotumaini tu, bali kwanza walijitoa nafsi zao kwa Bwana; na kwetu pia, kwa mapenzi ya Mungu.
2 Kor 8:5 SUV

na kishaToa

Nimekupa baadhi tu ya Siri za ndani ila naamini yapo mengi waweza kujifunza kutokea kwa Watumishi Wengine na kwenye Neno la Mungu na kuweka kwenye Matendo kile tunajifunza ili kuwa bora Asante kwa kukaa Darasani kujifunza pamoja nami.Umebarikiwa sana Mtumishi wa Mungu.
Chambua generations

Kelvin & Jenipher Chambua CK
Heaven Light Ministries Intl
Dodoma.
Tanzania.

Address

Dodoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kelvin Chambua-H.L.M posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Kelvin Chambua-H.L.M:

Share

Category