vijana_kkkt_dmp

vijana_kkkt_dmp Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from vijana_kkkt_dmp, Religious organisation, Dodoma.

Wewe ni kijana unayependa vibe la maana, mafundisho ya wakati ya Neno la Mungu, sifa zisizo na mipaka na unataka kuugawa...
29/04/2026

Wewe ni kijana unayependa vibe la maana, mafundisho ya wakati ya Neno la Mungu, sifa zisizo na mipaka na unataka kuugawa mwaka wako kwa kishindo cha kiroho... basi kituo chako ni kimoja tu: TANGANYIKA PACKERS, KAWE📍Tarehe 13.06.2026 📌

​Tamasha la Twen’zetu Kwa Yesu 2026 linarudi tena likiwa na moto zaidi! Hapa ndipo tunapokutana ili kuwa "Mastar" katika utukufu wa Mungu. Njoo uwaone na usifu pamoja na wakali k**a:

​🎤 Rose Mhando (Mama wa Vibe!)
🎤 Boaz Danken
🎸 AGAPE GOSPEL BAND
🎶 NEEMA GOSPEL CHOIR
🎹 KWAYA ZA VIJANA KKKT - DMP na vionjo kibaaaaaao.

​Hii si ya kukosa! Ni sehemu ya kukutana na vijana wenzako, kubadilishana mawazo, na kupokea baraka zitakazokufanya ung’ae mwaka mzima.

​✅ Save the Date: 13 June 2026
✅ Location: Tanganyika Packers | Kawe
✅ Mission: Be The Star! ✨

​Wa tag marafiki zako hapa chini ambao lazima uambatane nao katika Twen'zetu ya mwaka huu ili tukamsifu Yesu wetu kwa style ya kipekee! 🔥🙌





24/04/2026

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Makao Makuu, imewakutanisha Wenyeviti wa Vijana wa Dayosisi na Waratibu wao kutoka Dayosisi zote 28 za Kanisa hilo, ili kujadilii masuala yanayohusu kundi la vijana katika ustawi wa Kanisa na jamii kwa ujumla.

Katika ufunguzi wa warsha hiyo, Mwakilishi wa Askofu wa KKKT DKMs, Dkt. Msafiri Mbilu, Mchg. Jeremiah Mboko, ambaye ndiye Mchg. Kiongozi wa Usharika wa Mikanjuni, pamoja na kuwakaribisha washiriki, amesema warsha hiyo imekuja wakati muafaka na kuwahimiza viongozi kuitumia kwa manufaa.

Askofu mlezi wa vijana KKKT, Dkt. Syprian Hilint, akizungumza katika Ibada ya ufunguzi, amesema ni muhimu kila mshiriki akatoka na kitu muhimu kutoka kwenye semina hiyo, ambacho kitasaidia ustawi wa Dayosisi yake na jamii, jambo ambalo ndilo dhamira ya Kanisa kuandaa mafunzo hayo.

Warsha hiyo ya siku nne, inafanyika KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (DKMs), Usharika wa Mikanjuni jijini Tanga ambapo Katibu Mkuu wa KKKT, Rogath Mollel na Naibu Katibu Mkuu Misioni na Uinjilisti KKKT, Godfrey Walalaze wanahudhuria.


KKKT Marathon 2026
23/04/2026

KKKT Marathon 2026

.k.k.t_vijana_taifa
23/04/2026

.k.k.t_vijana_taifa

Vijana - DMP Jimbo la Kati 2026
23/04/2026

Vijana - DMP Jimbo la Kati 2026

Vijana - DMP Kusini Magharibi 2026
23/04/2026

Vijana - DMP Kusini Magharibi 2026

23/04/2026

Twen'zetu kwa Yesu 2026
📌 Vijana KKKT DMP - Kitunda Relini

Tutaonana baadaye...!
25/03/2026

Tutaonana baadaye...!

📍 KKKT UKONGA
25/03/2026

📍 KKKT UKONGA

2 Timotheo 4:7
24/03/2026

2 Timotheo 4:7

Rest Easy Man of God... Mr. Emmanuel Josia. Poleni vijana wa KKKT Ukonga, poleni vijana wa Jimbo la Kati, poleni vijana ...
22/03/2026

Rest Easy Man of God... Mr. Emmanuel Josia. Poleni vijana wa KKKT Ukonga, poleni vijana wa Jimbo la Kati, poleni vijana wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Umoja wa Vijana DMP tumepoteza mjumbe wa Kamati Kuu ya Vijana Dayosisi. Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe, Amen

Shalom...Wapendwa, haya ndo matokeo ya jumla ya Mtihani wa kupima Ufahamu wa Biblia Dayosisi 2026. Nitumie nafasi hii ku...
22/03/2026

Shalom...
Wapendwa, haya ndo matokeo ya jumla ya Mtihani wa kupima Ufahamu wa Biblia Dayosisi 2026.

Nitumie nafasi hii kuwapongeza na kiwashukuru wawakilishi wote wa vituo vilivyoshiriki mtihani huu kwa mwaka huu.

Shukrani kwa Wachungaji, Wainjilisti, Watendakazi, na viongozi wa vijana na wote mlioshiriki kuwaandaa watahiniwa kwa namna yoyote kuanzia Mtihani wa Jimboni hadi Dayosisi.

Tunageukia Uimbaji sasa...!

Nawatakia Ibada njema.

- Mwenyekiti Uv DMP

Address

Dodoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when vijana_kkkt_dmp posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share