Pastor Xavier

Pastor Xavier Ukurasa huu ni maalumu kwa ajili ya kujifunza neno la Mungu.

Day 2 Prophetic Visit
29/07/2025

Day 2 Prophetic Visit

Day 1 of Prophetic Visit To Mwanza
28/07/2025

Day 1 of Prophetic Visit To Mwanza

Thank you for being our Pastor
15/06/2025

Thank you for being our Pastor


USILEWE KWA MVINYOWaefeso 5:18[18]Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;Ili mlevi aendelee katik...
27/03/2025

USILEWE KWA MVINYO

Waefeso 5:18
[18]Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;

Ili mlevi aendelee katika ulevi wake anahitaji kunywa kile Kila mara/Kila wakati ndipo ataendelea kubaki kwenye hali ya kulewa kwake.
Ili Roho Mtakatifu aendelee kujaa ndani yako, inapaswa kujazwa naye Kila siku kila mara.

Aliyelewa Kwa kilevi, matendo yake na tabia zake huongozwa na kilevi kilichoko ndani yake, na wakati mwingine hufanya mambo ambayo ni kutokana na ushawishi wa kile kilevi, hali kadhalika Kwa yeye ambaye amejawa na Roho Mtakatifu muda wote, tabia na matendo yake huongozwa na Roho Mtakatifu.

Aliyelewa Kwa kilevi haogopi kufanya jambo lolote kwani kilevi ndicho kinacho mwongoza, hali kadhalika aliyejawa na Roho Mtakatifu anapewa ujasiri wa kufanya jambo lolote kwani Roho ndiye anayemuongoza kufanya Kila anachotaka kufanya.

Tunapokea Roho Mtakatifu mara moja, swala la ujazo wa Roho Mtakatifu ni endelevu.
Hivyo tamani kujawa na Roho Mtakatifu Kila wakati.

Matendo ya Mitume 4:31

[31]Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. 

Hawa waliojaa Roho Mtakatifu hapa wengi wao walikuwepo kwenye Matendo Sura ya 2, hivyo walijazwa tena Kwa mara nyingine tena.

Tamani kujazwa upya na Roho Mtakatifu, usikubali kubaki kwenye viwango vilevile.

Exavery Nduye
Mchungaji
0757-754176

KILA MTU ATABEBA MZIGO WAKE.Ezekieli 18:20[20]Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba ya...
25/03/2025

KILA MTU ATABEBA MZIGO WAKE.

Ezekieli 18:20

[20]Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.

Kila mtu atalipia gharama ya matendo yake mwenyewe mbele za Mungu.

Kila mtu atatoa maelezo kuhusu maisha yake alipokuwa hapa duniani siku hiyo mbele za Mungu.

Hakuna ambaye atasimama badala ya mtu mwingine.

Kuwa mcha Mungu ni swala binafsi na ni swala la kuamua wewe mwenyewe, siyo swala la kuangalia mbona fulani hamwabudu Mungu, la hasha.

Ezekieli 18:21

[21]Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa. 

Kwa kuwa Mungu ni wa msamaha, huwa anasamehe watu ambao wako tayari kumrudia yeye Kwa kuziacha njia zao mbaya(dhambi).

Mungu anataka kutenda Kwa halali na haki, siyo Kwa dhuluma na kuzishika amri zake.

Ezekieli 18:22

[22]Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi. 

Mungu anapomsamehe mtu, huwa anaamua kuziweka mbali kabisa dhambi hizo za awali na kuamua kuanza ukurasa mpya na mtu aliyefanya toba, hivyo ni wajibu wa mtu husika kufanya toba ya kweli na kuamua kuishi Kwa kumwelekea Mungu.

Exavery Nduye

0757-754176

Mchungaji

JE UNAYE MCHUNGAJI?Zaburi 23:1[1]BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Kazi ya mchungaji ni;1. Kutafuta ma...
24/03/2025

JE UNAYE MCHUNGAJI?
Zaburi 23:1
[1]BWANA ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu.

Kazi ya mchungaji ni;
1. Kutafuta malisho Kwa ajili ya kondoo (wanyama)wake.
2. Kuhakikisha usalama wa mifugo yake.
3. Kuiongoza mifugo ili kuelekea sehemu sahihi Kwa ajili ya malisho, maji na mahali pa kupumzika.
4. Kuhakikisha usalama wa afya ya mifugo yake pale wanapopatwa na magonjwa.
5. Kuhakikisha wanazaliana na kuongezeka ili kuwa kundi kubwa.
Mungu alimtuma Yesu ulimwenguni ili aje kuwa mchungaji mwema wa maisha yetu na roho zetu, naye hufanya majukumu yote ya mchungaji mwema Kwa wale ambao wamemwamini na kuishi sawasawa na neno lake.
Mchungaji huwa anajishughulisha na kundi lake tu kwani anawajibika Kwa wale ambao amekabidhiwa kuwatunza, hali kadhalika Yesu ndiyo anavyofanya. Wale waliomwamini ndio wanaofaidika kwanza na uwepo wake.

Yohana 10:11
[11]Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.

Yesu Kwa kuwa ni mchungaji mwema alikubali kuutoa uhai wake Kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa kondoo zake yaani wale ambao wanamwamini, hivyo kifo chake pale msalabani kilikuwa Kwa ajili ya kukomboa uhai wa watu wote ambao wamepotea kwenye dhambi, Kwa kumwamini Yesu unaingia kwenye kundi la kondoo wake hivyo kufaidika na uwepo wake kwako k**a mchungaji wake.

Yohana 10:14,27
[14]Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi;
[27]Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.

Wajibu wa kondoo;
1. Kumjua mchungaji wao.
2. Kuijua sauti ya mchungaji wao.
3. Kumfuata mchungaji wao.
4. Kufanya kile mchungaji wao anaelekeza wakati wote.
Kumjua mchungaji kunawasaidia kondoo kuto bebwa na mtu mwingine ambaye siyo mchungaji wao, hii husaidia kuepuka kupotezwa na kupata madhara kutoka Kwa huu ambaye siyo mchungaji.
Kondoo anaweza tu kumjua mchungaji, kuitambua sauti yake na kumfuata, endapo tu atakuwa na mahusiano ya muda mrefu na ya kudumu kati yake (kondoo) na mchungaji wake.
Yesu k**a mchungaji wetu, ili uweze kumjua, kuijua sauti yake na kumfuata kikamilifu, ni lazima kukubali kujifunza neno lake, Kwa kusoma maandiko Matakatifu, kusikiliza mahubiri na nyimbo za kikristo Kwa muda mrefu

OVERCOMING TEMPTATIONMatthew 4:3  And when the tempter came to him, he said, If thou be the Son of God, command that the...
16/12/2024

OVERCOMING TEMPTATION

Matthew 4:3 And when the tempter came to him, he said, If thou be the Son of God, command that these stones be made bread.

Hello family!

The faithfulness of God allows every man to be tempted within his ability; therefore, God does not allow us to be tempted beyond our ability to overcome.

He provides a way for us in his Word to win over temptation, therefore, instead of complaining what one needs to do is to find that way of escape in the midst of the temptation.

If you don't find it what do you do? What you do is to pray for God to show you that way of escape.

Quote the scripture above to him and He will give you an answer.

He also gives us the grace to bear temptations just us He gave Jesus Christ the grace to endure and overcome his temptations.

We should also understand that God tests us but the devil tempts us.

The intention of God in testing is to promote us but the intention of the devil in temptation is to discredit and run us down.

Dear beloved, what did you learn from this article?

I celebrate you!

Pastor Xavier

Zaburi 25:1[1]Ee BWANA, nakuinulia nafsi yangu, Katika hali zote, mtazame Mungu pekee wala usizitegemee akili zako na wa...
13/12/2024

Zaburi 25:1
[1]Ee BWANA, nakuinulia nafsi yangu,

Katika hali zote, mtazame Mungu pekee wala usizitegemee akili zako na wala usiweke matumaini yako Kwa watu.

Mpe nafasi Mungu ya kushughulikia mambo yako, ruhusu majibu ya changamoto zako yatoke Kwa Mungu mwenyewe.

Ukiweka tumaini Kwa wanadamu au kwenye vitu ipo siku utavunjwa moyo na kuumizwa kwani uwezo wa binadamu na vitu huwa vinamwisho.

FINISH STRONG

Isaya 53:5[5]Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kw...
25/11/2024

Isaya 53:5
[5]Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,
Alichubuliwa kwa maovu yetu;
Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake,
Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
But he was wounded for our transgressions, he was bruised for our iniquities: the chastisement of our peace was upon him; and with his stripes we are healed.

24/11/2024

JUMAPILI ASUBUHI 24.11.2024.

SOMO: UMUHIMU WA KUA NA MCHUNGAJI

UTANGULIZI.

-Wote ambao tunamwamini Mungu tunahitaji kua na mchungaji k**a kiongozi wetu na mtu wa kutuhudumia.
-Sababu ni nyingi na faida ni nyingi za wewe kua na mchungaji.
-Mchungaji hatumtazami kwa muonekani au umri au namna ya jinsi ilivyo bali tunatazama namna ambavyo Mungu amempa hiyo nafasi kusimama kwetu.
-Mchungaji kwako anasimama k**a kiongozi kwako na kwaajili ya kigezo cha kimbingu.
-Mungu huwachagulia watu wachungaji kwa kusudi lake Mungu yeye mwenyewe.
-Wajibu wetu ni kutii na kuitikia kile ambacho Mungu ametupa.

Waefeso 4:11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;

-Mungu ndie anayechagua mchungaji licha ya mifumo ambayo binadamu huitumia kujipatia wachungaji.

Yeremia 3:15-16 nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo wangu, watakaowalisha kwa maarifa na fahamu.
16 Kisha itakuwa, mtakapoongezeka na kuwa wengi katika nchi hiyo, asema Bwana, siku zile hawatasema tena, Sanduku la agano la Bwana; wala halitaingia moyoni; wala hawatalikumbuka, wala hawatalizuru, wala hayatafanyika hayo tena.

-Mungu anapohitaji mtu akue na kuongeza humuwekea kwake mbele mchungaji ilikusudi apandwe kwake na kuona na kujua kile kilichomo ndani yake kwaajili ya kukua na kustawi kwa mtu huyo.
-Ukikataa kua na mchungaji kwenye hilo eneo maana yake umekataa kustawi na kuongezeka na kukua pia.

Yeremia 23:4 Nami nitaweka juu yao wachungaji watakaowalisha; wala hawataona hofu tena, wala kufadhaika, wala hatapotea hata mmoja wao, asema Bwana.
-Mungu ndie anaeweka wachungaji juu yetu na jukumu lao kuu ni kutulisha kwa mafundisho mazuri.

NINI WAJIBU WA MSHIRIKA KWA MCHUNGAJI.

1. Kuwatii.
Waebrania 13:17 Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, k**a watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.

-Biblia inatia msisitizo wa kuwa tii na kuwaheshimu wachungaji wetu aliwaweka mbele yetu na huo ndio moyo wa mshirika kwa Mungu.

Waefeso 6:1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.

2. Kuwaombea.
Wakolosai 4:2 Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani;*
3 mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa

-Ilikusudi wadumu na kubaki kwenye maono na maeneo ambayo Mungu amewapa.
-Ni wajibu wetu k**a washirika kusimama na kuomba kwaajili ya wachungaji wetu.
-Maombi yetu yanaweka hekima kwao na kuisema ile siri ya Mungu kwa ujasiri.

Wakolosai 4:4 ili niidhihirishe, k**a inipasavyo kunena.

-Ni wajibu wetu kuwaombea hawa watu ambao Mungu amewaweka mbele yetu.

3. Kuwaheshimu.
1 Petro 2:17 Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.

-Tuwaheshimu wachungaji wetu hata k**a hatuko karibu nao lazima tuwajibike katika hilo.
-Weka mipaka ya kimahusiano wewe na mchungaji wako mazoea yasipite zaidi.

4. Kuwahudumia.
Wafilipi 4:14-19 Lakini mlifanya vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu.
15 Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu.
16 Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja.
17 Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.
18 Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.
19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.

-Shiriki katika matukio yao,changamoto zao au mahitaji yao kwa kuwahudumia vyema.
-Matokeo ya huduma nzuri kwao kwa kugusa mioyo yao huleta furaha na amani mioyoni mwao.
-Sisi k**a vyombo vya Mungu tutumike kuwahudumia wachungaji wetu.

NINI HUTOKEA TUNAPOTAMBUA NAFAZI YA MTUMISHI WA MUNGU KWENYE MAISHA YETU.?

1. Unakua umegusa moyo wa Mungu.

2. Lango la baraka kutoka kwa Mungu.
-Na ndipo wanapobariki watu kwa kutamka na baraka hizo huja.

Hesabu 6:22-24 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
23 Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo mtakavyowabarikia wana wa Israeli; mtawaambia;
24 Bwana akubarikie, na kukulinda;

-Mchungaji ni lango la baraka kwako maana yeye ndie anachofungua kile ambacho Mungu amekusudia kifike kwako.

Waebrania 7:7 Wala haikanushiki kabisa kwamba mdogo hubarikiwa na mkubwa.

-Wachungaji ni wakubwa kwetu,wazazi na walezi wetu wao huachilia baraka kwetu sisi wadogo.

3. Kifuniko/ulinzi kwako wa Kiroho.
-Itambue nafasi ya mchungaji kwemye maisha yako kwa kushikisha wao mema na changamoto zako.

4. Mchungaji ni utambulusho wako kwake katika ulimwengu wa Roho.

Matendo ya Mitume 19:14-16
[14]Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hiv
[15]Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani?
[16]Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.

-Kuna namna tu ambavyo kwenye maisha yako unahitaji mchungaji na maisha yako yanakupa dhamani pale tu unapotambua nafasi ya wachungaji kwako.
-Tambua nafasi ya mchungaji kwenye maisha yako na kwa kadri amabavyo Mungu anakupa nafasi na kufanya kwenye maisha yako.
-Nguvu ya mchungaji ni washirika na viongozi wake na sisi tunao wajibu wa kua bora kwa watumishi wa Mungu.

HITIMISHO.

Mawasiliano: 0757754176

Address

Dodoma
255

Telephone

0757754176

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Pastor Xavier posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Pastor Xavier:

Share