19/05/2024
*Ujumbe muhimu kwa wanaotaka kufanikiwa*
_Sehemu ya *kwanza*_
✓Nguvu Ya Kuanza Na Ulicho Nacho
Kila siku jua linapo chomoza na kuzana ni ishara ya kwamba siku imesha isha.
Ukweli ni kwamba kila siku inapopita katika macho yetu imebeba Baraka kwaajili kila kiumbe chenye uhai.
Kumbuka: Maisha ni fursa na kila mmoja hufanikiwa kwa kadri ya uwezo wake wa kufikiri na kutenda. Na kila siku mpya inapokuja mbele ya mtu ni fursa,sasa inategemea wewe unaitumiaje katika matumizi ya muda ili kufikia NDOTO zako.
Ukweli ni kwamba kila siku mpya inapokuja machoni kwa mtu kwa neema ya Mwenyezi Mungu imebeba fursa ya mafanikio kwa mtu.
Changamoto ni kwamba watu wengi wamekuwa na visingizio vingi sana, kila siku mpya inapokuja mbele yao wakati wanapotekeleza majukumu kila siku.
Na ndomana watu wengi wanapo anza mwaka mpya huwa na mipango||malengo||mawazo makubwa sana, ambayo mtu binafsi hujiwekea na kusema nataka mpaka itakapo fika mwakani niwe nimesha yatimiza.
*Mfano* wengine walikuwa na wazo la kifungua duka, biashara,kujenga, kuweka akiba labda 1M n.k
Cha ajabu mpaka sasa tunaelekea nusu mwaka yawezekana hakuna chochote ulicho kifanya kwasababu ya visingizio ambavyo unavyo
*Kitu unachotakiwa kufanya ni kuanza na ulicho nacho ili upate unacho kihitaji