Jeshi La Mawaridi

Jeshi La Mawaridi •Jeshi La Mama Bikira Maria | Jeshi La Mawaridi �
•Salini Rozari na Moyo Wangu Safi Utashinda~Bikira Maria
•Sali, tumaini na Usiogope ~ Mt.

Pio
•Mawaridi � yetu ni Rozari Takatifu
•Bikira Maria Imakulata ... Utuombee �

Tunakubudu Ee Yesu na Tunakubariki wa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako Mtakatifu 🙏🏼
11/06/2025

Tunakubudu Ee Yesu na Tunakubariki wa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako Mtakatifu 🙏🏼

TAFAKARI: SEHEMU YA PILITendo la mafarisayo kunung'unika baada ya Kristo kukaa na Lawi na watoza ushuru wenzake ni tendo...
05/03/2022

TAFAKARI: SEHEMU YA PILI

Tendo la mafarisayo kunung'unika baada ya Kristo kukaa na Lawi na watoza ushuru wenzake ni tendo la kulikwepa sana sisi. Wanakosa unyenyekevu na wao kujiona bora zaidi kuliko watoza ushuru, wanajipa usafi na haki. Sisi k**a Wakristo hatupasi kuwa hivyo hata k**a tunadumu katika sala na kujitahidi kutenda mema, tutambue hiyo ni kwa neema tu za Mungu bali tunachoweza kufanya ni kuwaombea wale wakosefu neema ya uwongofu lakini pia kuendelea kujiombea sisi neema ya Mungu isitupungukie, tudumu katika sala na matendo mema. Mtakatifu wangu mpendwa, Mt. Pio alisema " Kumbukuka, mdhambi ambaye hujutia dhambi zake yupo karibu na Mungu kuliko mtu yule ambaye hujisifu au kujikweza kwa matendo yake mema"

Kristo anatoa jibu zuri sana kwa manung'uniko ya mafarisayo, jimbo ambalo linatakiwa litupe nguvu ja faraja sisi wakosefu, Kristo amekuja kwa ajili yetu na si kwa ajili ya wale wajionao k**a mafarisayo. Yesu ni mwenye Huruma, anajua majeraha yetu kutokana na dhambi zetu na anataka kutuponya. Sisi ni wadhambi na hoe haye. Tuitikie sauti yake naye Yesu atatuponya na majeraha ya dhambi zetu.

Tumsifu Yesu Kristo, niwatakie Jumamosi njema Mungu awabariki sana.

🙏🌹 ✝️

TAFAKARI: Kristo...Tumaini Letu🙏.Katika Somo la Injili siku ya leo tunaona Yesu anamuita Lawi, mtoza ushuru na anamwambi...
05/03/2022

TAFAKARI:

Kristo...Tumaini Letu🙏.

Katika Somo la Injili siku ya leo tunaona Yesu anamuita Lawi, mtoza ushuru na anamwambia nifate. Lawi anamfata Kristo na anamuandalia karumu nyumbani kwake, lakini pia anawaalika watoza ushuru wenzake ambao mbele ya macho ya mafarisayo walikua ni watu waovi, watu wenye dhambi.

Tutafakari tendo la Lawi kuitikia wito wa Kristo na kuacha yote na kumfaata, katika kipindi hiki cha kwaresma Kristo anatuina tena tuache yote ya kidunia na kumfata yeye, k**a alivyofanya Lawi, ambaye pia toka kwake tunajifunza kuwa wanyenyekevu mbele za Mungu. Jambo ambalo Lawi analitenda baada ya kuitikia wito wa Yesu ni jambo ambalo tunatakiwa sote kurishiki kwa upendo mkubwa zaidi, injili inasema akamfanyia karamu kubwa nyumbani kwake na palikua na mkutano wa watoza ushuru wengine. Baada ya Lawi kuitikia wito wa Yesu ni k**a alishakombolewa katika kifungo, katika dhambi, anatambua uzuri/raha wa kuwa karibu naye hataki kushiriki ile faraja peke yake, kwa maana mafarisayo waliwatenga kwa kuwa ni watu waovu, anawaalika wenzake kuishiriki ile furaha ya Kristo.

Vilevile sisi katika maisha yetu hasa kipindi hiki cha kwaresma, tunaalikwa kuwashika mkono wengine na kuwasogeza karibu na Mkombozi Yesu Kristo k**a alivyo fanya Lawi mara tu tunapo itika sauti ya Kristo. Tunapobatizwa tunaitwa kumfata Kristo, tunakua wafuasi wa Kristo lakini katika safari yetu mara kadhaa tunapotea njia au kuzama katika giza na kuacha nuru naye ndiye Kristo, lakini Kristo hatuachi anatuita tena tumfate hasa katika kipindi hiki cha kwaresma. K**a vile ule wimbo usemanvyo "Lakini hata sasa asema Bwana nirudieni mimi kwa moyo yenu yete" Kristo anatuita tena mimi na wewe, yupo tayari kutupokea na kutuonjesha tena upendo na Huruma yake kuu.

Tumsifu Yesu Kristo

INAENDELEA POST INAYOFATA 🙏.

TAFAKARI: Kristo...Tumaini Letu🙏.Katika Somo la Injili siku ya leo tunaona Yesu anamuita Lawi, mtoza ushuru na anamwambi...
05/03/2022

TAFAKARI:

Kristo...Tumaini Letu🙏.

Katika Somo la Injili siku ya leo tunaona Yesu anamuita Lawi, mtoza ushuru na anamwambia nifate. Lawi anamfata Kristo na anamuandalia karumu nyumbani kwake, lakini pia anawaalika watoza ushuru wenzake ambao mbele ya macho ya mafarisayo walikua ni watu waovi, watu wenye dhambi. Tutafakari tendo la Lawi kuitikia wito wa Kristo na kuacha yote na kumfaata, katika kipindi hiki cha kwaresma Kristo anatuina tena tuache yote ya kidunia na kumfata yeye, k**a alivyofanya Lawi, ambaye pia toka kwake tunajifunza kuwa wanyenyekevu mbele za Mungu. Jambo ambalo Lawi analitenda baada ya kuitikia wito wa Yesu ni jambo ambalo tunatakiwa sote kurishiki kwa upendo mkubwa zaidi, injili inasema akamfanyia karamu kubwa nyumbani kwake na palikua na mkutano wa watoza ushuru wengine. Baada ya Lawi kuitikia wito wa Yesu ni k**a alishakombolewa katika kifungo, katika dhambi, anatambua uzuri/raha wa kuwa karibu naye hataki kushiriki ile faraja peke yake, kwa maana mafarisayo waliwatenga kwa kuwa ni watu waovu, anawaalika wenzake kuishiriki ile furaha ya Kristo. Vilevile sisi katika maisha yetu hasa kipindi hiki cha kwaresma, tunaalikwa kuwashika mkono wengine na kuwasogeza karibu na Mkombozi Yesu Kristo k**a alivyo fanya Lawi mara tu tunapo itika sauti ya Kristo. Tunapobatizwa tunaitwa kumfata Kristo, tunakua wafuasi wa Kristo lakini katika safari yetu mara kadhaa tunapotea njia au kuzama katika giza na kuacha nuru naye ndiye Kristo, lakini Kristo hatuachi anatuita tena tumfate hasa katika kipindi hiki cha kwaresma. K**a vile ule wimbo usemanvyo "Lakini hata sasa asema Bwana nirudieni mimi kwa moyo yenu yete" Kristo anatuita tena mimi na wewe, yupo tayari kutupokea na kutuonjesha tena upendo na Huruma yake kuu.

Tendo la mafarisayo kun

MT. JOHN JOSEPH WA MSALABA. John Joseph alikuwa anajinyima sana hata akiwa kijana. Alijitolea hata katika umri wake mdog...
05/03/2022

MT. JOHN JOSEPH WA MSALABA.

John Joseph alikuwa anajinyima sana hata akiwa kijana. Alijitolea hata katika umri wake mdogo kwa maisha ya umaskini na kufunga. Akiwa na miaka 16 alijiunga na Wafransisko huko Naples; alikuwa Mtaliano wa kwanza kufuata harakati za mageuzi za Mtakatifu Peter Alcantara. Sifa ya John ya utakatifu ilisababisha wakubwa wake wamuweke katika jukumu la kuanzisha kasisi mpya hata kabla ya kuwekwa wakfu.

Utii ulimchochea John kukubali kuteuliwa k**a bwana mdogo kiongozi, mlezi na, mwishowe, kiongozi wa jimbo. Miaka yake ya kufidia ilimwezesha kutoa huduma hizi kwa makasisi kwa hisani kubwa. K**a mlezi, alijiona hana upendeleo wa hali ya juu na alisisitiza kufanya kazi jikoni au kubeba kuni na maji yanayohitajika na makasisi.

Wakati muda wake k**a Kiongozi wa jimbo ulipomalizika, John Joseph alijitolea kusikia maungamo na kufanya unyogofu. Alikua na karama za unabii na uponyaji.

John Joseph alitangazwa mtakatifu mnamo 1839 na ndiye mtakatifu mlinzi wa Ischilia, Italia, mahali ambapo alizaliwa.

Kuzaliwa

15 Agosti 1654 huko Ischia, Naples, Italia k**a Carolo Gaetano Calosirto

Alikufa

5 Machi 1734 ya sababu za asili

Imetangazwa kuwa mtakatifu

Tarehe 26 Mei 1839 na Papa Gregory XVI

Mtakatifu John Joseph, wenye Heri na watakatifu wengine wa leo; Mtuombee 🙏

🙏🌹 ✝️

 🙏🌹  ✝️
04/03/2022

🙏🌹 ✝️

KITUO CHA SITAVERONIKA ANAPANGUSA USO WA YESUEe Yesu Tunakuabudu, tunakushukuru; kwa kuwa umewakomboa watu kwa Msalaba w...
04/03/2022

KITUO CHA SITA
VERONIKA ANAPANGUSA USO WA YESU

Ee Yesu Tunakuabudu, tunakushukuru; kwa kuwa umewakomboa watu kwa Msalaba wako Mtakatifu.

Veronika akisukumwa na ibada na huruma analeta kitambaa chake ili kupangusa uso wa Yesu ulioharibika, na Yesu alichapa juu yake sura yake: zawadi kubwa kwa huduma ndogo. Na wewe unaweza kumpatia Mwokozi wako nini kwa fadhila nyingi ulizopata kutoka kwake? Ee Yesu wangu Mwenye Huruma! Nikupe nini kwa neema zote ulizonijalia mimi? Tazama, mimi ninajitolea kabisa kwa utumishi wako. Ninakutolea moyo wangu: uchore ndani mwake picha yako Takatifu, na isifutwe tena na dhambi

Baba Yetu...Salamu Maria...Atukuzwe Baba.

TAFAKARI: Veronika anafanya tendo la Huruma kwa Yesu kwa kumpangusa uso wake bila kujali na kuogopa macho ya watu na askari. Anaamua kufanya jambo sahihi, na Yesu anamzawadia picha ya uso wake katika kitamba. Linaonekana ni tendo dogo lakini zawadi yake ni kubwa, lakini ni kubwa kiimani. Tutafakari leo ni jinsi gani sisi tunakua na Huruma kwa wale wanaoteseka au wahitaji, je huwa tunaogopa macho wa watu kuwasaidia au kuwafariji wale ambao jamii huwaacha peke yao au huwatesa na wakiwa hawana hatia? Kipindi hiki cha kwaresma kiwe kwetu cha kuguswa ndani kabisa na tendo hili la Veronika, nasi tufanye vile vile kwa wengine hasa wanaohitaji huruma yetu.

Katika Shajara yake Mtakatifu Faustina Kowalska, mtume wa Huruma ya Mungu anaandika hivi

"...Mtu anatkiwa kufanya angalau tendo moja la huruma kwa siku; angalau moja; lakini yaweza kuwa zaidi,matendo haya yanaweza kufanywa na kila mmoja kwa urahisi,hata yule maskini sana. Kwa kuwa kuna njia tatu za kufanya matendo ya huruma.

Ya Kwanza ; Maneno ya huruma kwa kusamehe na kufariji.

Ya Pili; K**a huwezi kutoa maneno, basi Sali, hiyo nayo ni huruma.

Ya Tatu; Matendo ya huruma.

Na siku ya mwisho ikifika, tutahukumiwa kulingana na haya, na misingi hii tutapokea hukumu ya milele. " ( Shajara 1158).

Hatuna kisingizio cha kushindwa kuonyesha Huruma, tubadilike na tuwe watu wa kuwagusa wengine kwa Huruma.

SALA: Ee Yesu, utujalie moyo k**a wa Mt. Veronika, bila woga na kwa ujasiri tuwe vyombo vyako vya huruma kwa watu wote. Amina.

🙏🌹 ✝️

✝️TAFAKARI YA NJIA YA MSALABA✝️KITUO CHA TANOSIMONI WA KIRENE ANAMSAIDIA YESUEe Yesu Tunakuabudu, tunakushukuru; kwa kuw...
04/03/2022

✝️TAFAKARI YA NJIA YA MSALABA✝️

KITUO CHA TANO
SIMONI WA KIRENE ANAMSAIDIA YESU

Ee Yesu Tunakuabudu, tunakushukuru; kwa kuwa umewakomboa watu kwa Msalaba wako Mtakatifu.

Simoni wa Kirene alilazimishwa kumsaidia Yesu kuubeba Msalaba wake, na Yesu alikubali msaada wake. Yeye pia angekubali bila kusita wewe uubebe Msalaba wake: Yeye anakuita lakini wewe husikii,Yeye anakualika lakini wewe unakataa. Ni aibu kubwa kubeba msalaba kwa kukaidi! Ee Yesu! Asiyechukua msalaba wake na kukufuata, hakustahili. Tazama, mimi ninajiunga nawe
katika Njia ya Msalaba. Nitakuwa msaidizi wako nikifuata nyayo zako zenye damu ili niweze kuungana nawe katika uzima wa milele.

Baba Yetu...Salamu Maria...Atukuzwe Baba.

TAFAKARI: Katika kituo hiki Simoni wa Kirene anamsaidia Yesu kuubeba msalama mzito wa ukombozi. Kristo pia anatualika kuubeba Msalaba wa ukombozi, japo anasema kuwa kila mtu abebe msalaba wake na kumfata, sisi k**a Wakristo tunaowajibu wa kusaidia katika safari ya ukombozi. Tutafakari ni mara ngapi tumekua daraja au kikwazo kwa watu wengine katika kuelekea ukombozi? Kwa kuishi maisha safi ya Kikristo tunakua mfano kwa wengine na kuwavuta karibu na Yesu na kwa njia hiyo tunashiriki katika ukombozi. Tunapo kuwa katika kipindi hiki cha kwaresma, tutafakari ni njia gani tunaweza kusaidia katika safari ya ukombozi kwa wengine. Tunaweza fanya hivyo kwa kuwaombea na kuwashirikisha katika Sakramenti mbalimbali za Kanisa k**a Ubatizo na Kitubio.

SALA: Ee Yesu, mimi pia nataka nishiriki katika safari ya ukombozi, nifanye chombo chako cha kuwaletea wengine hasa wale waliopotea katika maisha ya kidunia habari njema ya uwongofu wa roho. Amina.

🙏🌹 ✝️

TAFAKARI Mapendo 🙏Katika somo la injili, Yesu anathibitisha thamani ya kufunga kwa muda baada ya kufa na kufufuka kwake,...
04/03/2022

TAFAKARI

Mapendo 🙏

Katika somo la injili, Yesu anathibitisha thamani ya kufunga kwa muda baada ya kufa na kufufuka kwake, wakati wa kanisa, 'Wakati utafika wa kuondolewa kwao bwana-arusi, ndipo watakapofunga'. Ni Jumatano ya Majivu na Ijumaa Kuu pekee zinazosalia k**a siku za mfungo na kujinyima, lakini msimu mzima wa Kwaresima umefahamika kitamaduni k**a wakati wa kufunga. Tunajinyima kitu ili tuweze kujitoa kikamilifu zaidi kwa njia ya Bwana. Msemo wa 'hapana' unaohusisha kufunga ni daima katika kusema 'ndiyo' kubwa zaidi kwa Bwana na watu wake. Hivi ndivyo nabii Isaya anasisitiza katika somo la kwanza la leo. Anafanya uhusiano thabiti kati ya kufunga na huduma ya Bwana kupitia utunzaji wa walio hatarini zaidi, kuvunja pingu zisizo za haki, kuwaacha huru waliokandamizwa, kushiriki mkate wetu na wenye njaa. kuwalinda maskini wasio na makazi, kuwavisha walio uchi. Yesu anatangaza katika injili kwamba chochote tunachofanya kwa wale walio na uhitaji mkubwa tunamfanyia, na chochote tunachomfanyia tunamfanyia Mungu, kwa sababu yeye, Yesu, ni Mungu-pamoja nasi. Ndani ya mapokeo ya Kikristo, Kwaresima, msimu wa mfungo, pia ni majira tunapojitoa kwa namna ya pekee kwa wale wenye uhitaji mkubwa. Kuonyesha ukarimu wakimbizi wa vita, k**a vile iliyopo Ukraine, ni wonyesho mwingine wa utunzaji wa wahitaji ambao Isaya na Yesu wanakazia sana. Isaya anawatangazia watu katika somo hilo la kwanza kwamba ikiwa wanawajali walio hatarini, wale waliojeruhiwa kwa namna fulani, jeraha lao wenyewe litapona. Sisi wenyewe tunaponywa tunapofanya kazi ya uponyaji wa wengine.

Tumsifu Yesu Kristo 🙏.

🙏🌹 ✝️

MT. CASIMIR WA POLAND Machi 4, Kanisa Katoliki linamheshimu Mt. Casimir Jagiellon, mkuu ambaye maisha yake ya kumtumikia...
04/03/2022

MT. CASIMIR WA POLAND

Machi 4, Kanisa Katoliki linamheshimu Mt. Casimir Jagiellon, mkuu ambaye maisha yake ya kumtumikia Mungu yamemfanya Mt. Mlinzi wa Poland, Lithuania, na vijana.

Mwaka 1984, Papa John Paul II Alisema kuwa Kanisa "lilimtangaza Casimir mtakatifu na kumuweka mbele yetu sio tu kuabudiwa tu bali pia kwamba tunaweza kuiga sifa zake za kishujaa na kufuata mfano wake wa utakatifu. Ushuhuda wake wa imani kubwa na uchamungu wa dhati unaendelea kuwa na maana maalum kwetu leo, haswa "wito mgumu" anaotoa kwa vijana."

"Maisha yake ya usafi na maombi yanakuita utekeleze imani yako kwa ujasiri na bidii, kukataa vivutio vya udanganyifu vya jamii ya kisasa inayojiruhusu, na kuishi imani yako kwa ujasiri bila woga na kwa furaha."

Casimir Jagiellon alizaliwa mnamo 1458, wa tatu kati ya watoto kumi na tatu waliozaliwa na Mfalme Casimir IV wa Poland na mkewe Elizabeth wa Austria. Yeye na kaka zake kadhaa walisoma na kuhani na mwanahistoria John Dlugosz, ambaye uchamungu wake wa kina na utaalam wa kisiasa ulimshawishi Casimir katika malezi yake

Toka mchanga alikataa maisha ya anasa na badala yake alichagua njia ya kujinyima na kujitolea. Alivaa nguo za kawaida, alilala chini mara kwa mara, na alitumia muda mwingi wa usiku katika sala na kutafakari juu ya mateso na kifo cha Kristo

Casimir alionyesha upendo wake kwa Mungu kwa kujitolea, pia kuwasaidia masikini. Alijulikana k**a kijana mwenye huruma sana ambaye alihisi maumivu ya wengine vizuri

Casimir alikataa kuoa, alipendelea kuishi maisha ya kumtumikia Mungu na watu wake

Baada ya kupata dalili za ugonjwa wa kifua kikuu, Casimir alitabiri kifo chake na akajitayarisha kwa kukuza ibada yake kwa Mungu. Alikufa njiani kuelekea Lithuania mnamo Machi 4, 1484, na alizikwa na nakala ya wimbo wa Marian aliousoma mara kwa mara.

Papa John Paul II alikumbuka jinsi Mt. Casimir "alivyokubali maisha ya useja, alijitiisha kwa unyenyekevu kwa mapenzi ya Mungu katika mambo yote, alijitolea kwa upendo kwa Bikira Maria na akaanzisha mazoezi mazito ya kumuabudu Yesu wa Ekaristi

Mt. Casimir; Utuombee 🙏

🙏🌹 ✝️

✝️TAFAKARI YA NJIA YA MSALABA✝️KITUO CHA NNEYESU ANAKUTANA NA MAMA YAKEEe Yesu Tunakuabudu, tunakushu; kwa kuwa umewakom...
03/03/2022

✝️TAFAKARI YA NJIA YA MSALABA✝️

KITUO CHA NNE
YESU ANAKUTANA NA MAMA YAKE

Ee Yesu Tunakuabudu, tunakushu; kwa kuwa umewakomboa watu kwa Msalaba wako Mtakatifu.

Bila shaka kituo hiki kilikuwa chenye kuumiza na kusikitika kwa Maria Mama Huzuni, kumwangalia Mwanawe Mpendwa sana akilemewa na mzigo wa Msalaba! Moyo wake ulizoea maumivu mengi yasiyosemeka. Alitamani sana kufa badala ya Yesu au pamoja naye. Umsihi Mama huyu wa Huzuni akusaidie katika saa ya kufa kwako. Ee Yesu, ee Maria, mimi ni sababu ya maumivu mengi na
makubwa ambayo yanachoma mioyo yenu! Moyo wangu pia uweze kuhisi na kozoea hata kidogo cha maumivu yenu. Ee Mama qa Huzuni, uniwezeshe kushiriki katika mateso uliyovumilia wewe na Mwanao kwa ajili yangu, na unijalie nizoee huzuni yako, ili nikiumizwa nayo niweze kufurahia msaada wako saa ya kifo changu.

Baba Yetu...Salamu Maria...Atukuzwe Baba.

TAFAKARI:- Katika kituo hiki inakutana Mioyo miwili mitakatifu lakini iliojaa Uchungu mwingi sana kwa ajili ya dhambi zetu. Mama Maria anahuzunika kutokana na mateso ya mwanae ambaye hana hatia. Ni dhambi zetu ambazo zinasababisha maumivu Haya. Lakini tutafakari jinsi gani Mama Maria, Mama wa Mateso mengi alivyo na upendo kwetu! Sisi ndio tunasababisha mwanaye mpendwa ateseke asulubiwe na afe kifo cha fedhea msalabani. Pamoja na kusababisha maumivu haya bado Mama Maria siku zote hutuombea kwa Mwanaye Yesu Kristo neema nyingi, ni upendo kiasi gani!? Anatufariji, anatupa amani, furaha n.k Ni wa kushangaza upendo wake. Tafakari je wewe unaweza kumuombea au kumsaidia mtu ambaye anasababisha maumivu kwako moja kwa moja au kupitia mtu wako wa karibu unayempenda? Wengi wetu hatuwezi kuvumilia. Basi tutafakari katika siku ya leo, ni dhambi zetu zipi ambazo zinaendelea kuumiza Mioyo ya Yesu na Maria, na tuombe neema ya Mungu kupitia kwa Mama Maria ili tuachane na dhambi hizo ambazo ni sababu ya maumivu kwa Yesu na Mama Maria.

SALA: Ee Yesu na Maria, nisaidie niweze kupata uchungu juu za dhambi zangu. Nijaze na huzuni ile ile mlioipata baada ya kukutana katika njia ya Msalaba ili nisiweze kutenda dhambi tena. Amia.

🌹🙏 ✝️

Address

Dodoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jeshi La Mawaridi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Jeshi La Mawaridi:

Share