KPMC Church

KPMC Church The Kingdom of God is Our first Priority (Matthew 6:33)

18/06/2026
Wasiliana nasi kwa msaada waIBADAMAFUNDISHO YA NENO LA MUNGUMAOMBI NA MAOMBEZIUSHAURI
18/04/2026

Wasiliana nasi kwa msaada wa
IBADA
MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU
MAOMBI NA MAOMBEZI
USHAURI

Je uko Dodoma na unatafuta mahali Sahihi pa kuabudu?Unaweza ukachagua kuabudu nasi!Karibu sana kwenye Ibada ya Jumapili ...
18/04/2026

Je uko Dodoma na unatafuta mahali Sahihi pa kuabudu?
Unaweza ukachagua kuabudu nasi!

Karibu sana kwenye Ibada ya Jumapili hii
Dkt Mwamtobe Aam

03/04/2026

JESUS PAID IT ALL.... WITH HIS STRIPES WE ARE HEALED

Isaya 53:1-12
1 Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?

2 Maana alikua mbele zake k**a mche mwororo, Na k**a mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.

3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na k**a mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.

4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

6 Sisi sote k**a kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.

7 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; K**a mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na k**a vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.

8 Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.

9 Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa na hila kinywani mwake.

10 Lakini Bwana aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake;

11 Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.

12 Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.

Hivi unaelewa kwamba mwanadamu haamimiki? Basi haifai kabisa kumtegemea.Hivi unafahamu kwamba mwanadamu aweza kubadilika...
02/04/2026

Hivi unaelewa kwamba mwanadamu haamimiki? Basi haifai kabisa kumtegemea.
Hivi unafahamu kwamba mwanadamu aweza kubadilika? Basi haifai kabisa kumtegemea.
Hivi unafahamu kwamba Wanadamu aweza kufa wakati wowote? Basi haifai kabisa kumtegemea.
Hivi unafahamu mwanadamu aweza kuyakana maneno yake mwenyewe? Basi haifai kabisa kumtegemea.

YUKO mmoja tu aliye mwaminifu, ashikaye maagano yake, asiyebadilika na aliye wa milele, YESU KRISTO! Huyu anafaa kutegemea.

Kwa hiyo hata maandiko tu yangenyamaza kwamba libaki kwetu wenyewe, bado haifai kabisa kumtegemea mwanadamu.

02/04/2026

BIBLE STUDIES
TITLE: MFANO WA MWANA MPOTEVU
NA DR. MWAMTOBE AAM
MAANDIKO: LUKA 15:11-32

Luka 15:11-32 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹¹ Akasema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili;
¹² yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia. Akawagawia vitu vyake.
¹³ Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati.
¹⁴ Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji.
¹⁵ Akaenda akashik**ana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe.
¹⁶ Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu.
¹⁷ Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.
¹⁸ Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako;
¹⁹ sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye k**a mmoja wa watumishi wako.
²⁰ Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana.
²¹ Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena.
²² Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni;
²³ mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi;
²⁴ kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia.
²⁵ Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo.
²⁶ Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini?
²⁷ Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima.
²⁸ Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi.
²⁹ Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu;
³⁰ lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona.
³¹ Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako.
³² Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.

MAFUNZO KUTOKA KATIKA MFANO WA MWANA MPOTEVU
1. Ukiwa mwana, unayo haki kuirithi vitu vya ufalme wa Mungu. The moment ukiokoka wewe ni mwana wa Mungu na hivyo una sehemu katika familia ya Mungu na una haki ya kuirithi Baraka zote zilizoahidiwa na Mungu. Ni haki yako....... Mst 11-12.
2. Baraka zote unazorithi kutoka kwenye ufalme wa Mungu zinakuwa salama tu pale unapoendelea kubaki ndani ya ufalme. Ukitaka hizo Baraka ulizorithi kwenye ufalme wa Mungu ziendelee kuwa Hai na kuongezeka sharti ni kwamba uendelee kuwa ndani ya ufalme.....mst 13
3. Kwenda mbali na ufalme ni kupoteza Baraka zako zote. Tunapaswa kuwa makini sana, wakati mwingine mafanikio hutufanya kwenda mbali na Mungu jambo ambalo ni hatari sana maana ni ngumu kuendelea kuwa na mafanikio hayo nje ya uwepo wa Mungu. - Mst 13-14.
4. Kuwa nje ya ufalme humfanya mtu kuzalisha tabia ambazo hakuwa nazo kabisa, kijana aliyekuwa mzuri kabisa chini ya Usimamizi wa baba yake alipoenda mbali alianza tabia ya uasherati.... Mst 13.
5. Kukaa nje ya ufalme husababisha uhitaji, ukame na njaa ambayo humsukuma mtu kufanya mambo ambayo angekuwa ndani ya ufalme asingeweza kufanya... Mst 13-16.
6. Hata mtu aliye nje ya ufalme, Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yake ya kumshawishi kurudi kwenye ufalme isipokuwa kazi inakuwa ni kuzingatia moyoni mwake na kurudi kwenye ufalme... Mst 17.
7. Kuna wakati kibinadamu tunaona hatustahili kusamehewa na Mungu kwa sababu ya dhambi zile tulizozitenda, lakini Mungu yuko tayari kutusamehe tukiamua kurudi kwake bila kujali tumefanya dhambi kubwa au ya ajabu kiasi Gani.... Mst 18-20.
8. Malaika mbinguni hushangilia pale ambapo mwenye dhambi mmoja anatubu na kurudi kwa Mungu.... Mst 22-24.
9. Kukaa mbali na Mungu ni kufa na kurudi kwa Mungu ni kuwa Hai tena.... Mst 24.
10. Sisi tuliookoka tayari hatuna haki sana zaidi ya hao ambao hawajaokoka k**a wataamua kuokoka hata leo... Mst 25-28.
11. Ukiwa kwenye ufalme wa Mungu, chochote kilicho kwenye ufalme wa Mungu ni haki yako wewe; Mst 29-31.
12. Kila mmoja anapaswa kushangilia na kufurahi mtu mmoja anapoamua kuacha dhambi na kumwamini Mungu - Mst 32.

MAPITO AU SHIDA AU MATATIZO YANA TABIA YA KUKUONDOLEA IMANI KWA MUNGU - BE WATCHFULLHebu imagine Yohana Mbatizaji aliyet...
28/03/2026

MAPITO AU SHIDA AU MATATIZO YANA TABIA YA KUKUONDOLEA IMANI KWA MUNGU - BE WATCHFULL

Hebu imagine Yohana Mbatizaji aliyetabiri ujio wa Yesu...

Luka 3:15-17 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁵ Basi, watu walipokuwa wakingoja yatakayotokea, wote wakiwaza-waza mioyoni mwao habari za Yohana, k**a labda yeye ndiye Kristo,
¹⁶ Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto;
¹⁷ ambaye pepeo lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake, na kuikusanya ngano ghalani mwake, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.

Yohana 1:25-27 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁵ Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?
²⁶ Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi.
²⁷ Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake.

Pia alithibitisha ujio wa Yesu na yeye ndiye aliyemtambulisha kwa watu akisema ameshuhudiwa hivyo na Roho wa Mungu.

Yohana 1:29-35 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁹ Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
³⁰ Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.
³¹ Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji.
³² Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka k**a hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake.
³³ Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.
³⁴ Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.

Lakini baada ya kupitia lile jaribu la kutupwa gerezani anawatuma wanafunzi wale wale ambao aliwatambulisha kwao kwamba huyu ni Yesu, kumuuliza k**a huyo aliyemtambulisha ndiye Kristo au wamngojee Mwingine?

Luka 7:19-20 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁹ Ndipo Yohana alipowaita wawili katika wanafunzi wake, akawatuma kwa Yesu akiuliza, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?
²⁰ Nao walipofika kwake, walisema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?

Mungu ni yule yule, hajabadilika. Bado anatenda hata sasa...... Majibu ya Yesu

Luka 7:21-23 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²¹ Na saa ile ile aliwaponya wengi magonjwa yao, na misiba, na pepo wabaya; na vipofu wengi aliwakirimia kuona.
²² Ndipo alipojibu, akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana hayo mliyoyaona na kuyasikia; vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa habari njema.
²³ Naye heri mtu ye yote asiyechukizwa nami.

Niseme k**a Abihudi Mishori kwenye wimbo wake unaoitwa "WEWE NI MUNGU"...

"Mungu kumwelewa ni kazi sana lakini endelea kumwamini".

The moment Mungu akieleweka basi atakosa sifa ya kuwa Mungu. Wewe endelea kumwamini na wala usiwe na mashaka naye hata kidogo, ni huyo huyo kweli kweli.

Mungu akubariki sana,
Ninakutakia Jumamosi yenye Baraka za Bwana.

Ni mimi ndugu yako katika Kristo

Rev. Dr. Mwamtobe Aam
KPMC Church HQ
Dodoma, Tanzania
Simu: 0754776076 /0783663621

27/03/2026

KINGDOM PRIORITY MISSION CHURCH
SEMINA YA NENO LA MUNGU MTANDAONI
MACHI 24-27, 2026 (JUMANNE - IJUMAA)
SOMO: THE MIGHT OF GOD IS UNQUESTIONABLE / UWEZA WA MUNGU SI WA KUULIZA
MNENAJI: DR. MWAMTOBE AAM - ASKOFU MKUU WA KPMC NA MCHUNGAJI KIONGOZI WA KANISA LA KPMC DODOMA
SIKU YA NNE - IJUMAA MACHI 27, 2026

Jana nilikueleza sifa tatu za Mungu na uhusiano wake na The Might of God is UNQUESTIONABLE. Katika sifa hizo Tuliona kwamba Mungu wetu (1) Yupo kila mahali kwa wakati wote (2) Mungu anajua yote, Na (3) Mungu ni wa milele na asiyebadilika.

Leo tuanze kwa kuangalia sifa ya nne ya Mungu na uhusiano wake na The Might of God is UNQUESTIONABLE.

SIFA YA NNE: MUNGU NI MUWEZA YOTE (OMNIPOTENCE)
Nilieleza katika moja ya kipindi kilichopita kwamba Wanadamu tuna kiwango fulani cha uwezo, uwezo wetu una ukomo. Hata k**a tungepambana kiasi Gani, bado uwezo wa Mwanadamu una ukomo wake.

Mungu ni Mungu mwenye uweza wote, ni Mungu mwenye uwezo wa kusababisha jambo lolote litokee, hata k**a linaonekana gumu kiasi Gani. Kuna mambo ambayo yako nje kabisa ya mawazo ya wanadamu, Mungu anaamuru na mambo hayo yanatokea bila shida yoyote.

Sifa hii ya Mungu pamoja na sifa zingine ambazo nilizifafanua siku ya Jana zote zinatuthibitishia kwamba Mungu uweza wake uko juu sana, uweza wake ni beyond human imagination, uweza wake ni unquestionable.
Umewahi kufikiri jambo lolote gumu, Mungu anaweza kufanya jambo hilo. Unapitia jambo fulani gumu, Mungu anaweza kufanya jambo hilo. Unapitia hali fulani ngumu ambayo umehangaika nayo kwa muda mrefu, kwa Mungu ni jambo dogo sana maana analiweza kabisa. The Might of God is UNQUESTIONABLE.

BAADHI YA MAMBO YANAYOONYESHA THE MIGHT OF GOD IS UNQUESTIONABLE KATIKA MAANDIKO

Kuna maandiko mengi sana yanayothibitisha The Might of God is UNQUESTIONABLE. Kwa kweli ni mambo ambayo kabisa ni ngumu kuingia kwenye akili za damu na nyama na yakakubalika.
Hii ndiyo sababu hata watu wengine wamedhani ni stori za kawaida lakini ukweli ni kwamba ni mambo ambayo yalitendeka waziwazi kwa mkono wa Mungu.
Baadhi ya mambo haya ni haya yafuatayo....

Mambo haya matatu Niliyaelezea nilipokuwa nafunua ile mistari ya msingi ya somo letu
1. Mariam alipata ujauzito (mimba) kwa uweza wa Roho Mtakatifu (Yaani bila kumjua Mwanaume) - Luka 1:26-35, 37.
2. Elizabeth alipata ujauzito alipokuwa mzee; Luka 1:5-26, 36-37.
3. Uwezekano wa ngamia kupenya katika tundu la sindano; Mathayo 19:24-26 Ling. Marko 10:17-27,Luka 18:18-27 (Ambwene Mwasongwe ameimba wimbo anasema Mungu anaweza kuvunja jiwe kwa yai, kupiga mluzi akiwa amefumba maji mdomoni, kupandisha mlima na baiskeli isiyo na mnyororo.

Nafasi na muda visingelitosha kueleza kwa kina kila tukio, rejea maandiko yaliyotajwa;
4. Sara kupata mtoto katika umri wa miaka 90; Mwanzo 18:1-2, 9-14; 21:1-3.
5. Mungu aweza kufanya mambo yote na wala makusudi yake hayawezi kuzuilika; Ayubu 42:2; 10-12.
6. Mungu hurejesha amani na utajiri kwa mji (au nafsi ya mtu) ulio ukiwa; Zekaria 8:4-6.
7. Mungu alileta kware wa kutosha kundi lote la wana wa Israeli (watu 600,000); Hesabu 11:4-6, 11-24; 31-32.
8. Mungu hukausha bahari na mito ya maji huifanya kuwa jangwa; Isaya 50:2, Kutoka 14:13-16, 21-22, Yoshua 3:14-17, Luka 8:23-24.
9. Lolote ambalo amelinena, ametimiza; Ezekiel 12:21-25; 24:14, Habakuki 2:3, Isaya 14:24.
10. Hakuna neno gumu asiloliweza Mungu; Yeremia 32:27, 17; 36-44.

NI WAKATI GANI MZURI WA KUTANGAZA UWEZA WA MUNGU?

Wakati mzuri sana wa kutangaza uweza wa Mungu siyo wakati wa shangwe, siyo wakati wa furaha, siyo wakati wa amani, siyo wakati wa ushindi, siyo wakati ambao mambo yamekunyokea.
Bali wakati mzuri wa kutangaza uweza wa Mungu ni wakati ule unaona mambo hayaendi kabisa, muda ule unapoona kwamba mambo yamesimama. Wakati ule ambao unaona juhudi zako hazizai matunda, huoni nuru, huoni mlango, huoni uwezekano wa kuwa na kesho njema, huu ndiyo wakati wa kutangaza uweza wa Bwana.

Wakati ambao huoni kesho, wakati ambao unaona kwamba umefika mwisho, wakati ambao umekata tamaa kabisa, huu ndiyo wakati mzuri wa kutangaza uweza wa Bwana. Tujifunze kwa Ayubu na manabii wengine katika maandiko ambao walipokutana na magumu ndipo walipotangaza uweza wa Bwana.

“Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika.”
— Ayubu 42:2 (Biblia Takatifu)

Je unajua matokeo yake? Walipotangaza uweza wa Bwana katikati ya vita amani ilitokea, walipotangaza uweza wa Bwana katikati ya magonjwa uponyaji ilitokea, Walipotangaza uweza wa Bwana katikati ya kukata tamaa na hofu nyingi walitiwa nguvu na Bwana.
“Kisha Bwana akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; Bwana naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza.”
— Ayubu 42:10 (Biblia Takatifu)

Kilichoanza kabla ya kuwaombea wale rafiki zake ni kutangaza uweza wa Bwana. Kwa hiyo wakati mzuri wa kutangaza uweza wa Bwana ni pale unapoona mambo hayaendi kwenye maisha yako. Tangaza uweza wa Bwana sasa.
Nimefika mwisho wa semina yetu, Mungu akupe neema ya kuyaishi haya.
Mungu awabariki sana

KINGDOM PRIORITY MISSION CHURCH SEMINA YA NENO LA MUNGU MTANDAONIMACHI 24-27, 2026 (JUMANNE - IJUMAA) SOMO: THE MIGHT OF...
26/03/2026

KINGDOM PRIORITY MISSION CHURCH
SEMINA YA NENO LA MUNGU MTANDAONI
MACHI 24-27, 2026 (JUMANNE - IJUMAA)
SOMO: THE MIGHT OF GOD IS UNQUESTIONABLE / UWEZA WA MUNGU SI WA KUULIZA
MNENAJI: DR. MWAMTOBE AAM - ASKOFU MKUU WA KPMC NA MCHUNGAJI KIONGOZI WA KANISA LA KPMC DODOMA
SIKU YA TATU - ALHAMISI MACHI 26, 2026

Watumishi wa Mungu, Bwana Yesu Asifiwe sana. Ninawasalimuni nyote katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Bwana na mwokozi wa maisha yetu. Hallelujah.
Ninazo shukrani nyingi kwa Mungu kwa kutupa neema tena ya kuendelea na somo letu na leo ni siku ya tatu. Lakini Nitumie nafasi hii kukukaribisha tena na tena kuendelea kufuatilia somo hili nikiamini kwamba kuna jambo la kwako kabisa ambalo Mungu anataka kusema na wewe.
Umekaribishwa sana.

Katika siku hizi mbili Tumefanikiwa kuona dhana za ndani kabisa za mistari yetu ya msingi ambayo ni Luka 1:37 na Luka 18:27. Mungu hasubiri tumalize somo ndiyo upate jambo la kujifunza na la kuondoka nalo, na kwa sababu hiyo naamini kwamba kupitia mistari hiyo ya msingi na maelezo yaliyotolewa vimekutoa mahali kwenda mahali pa juu na pazuri zaidi katika safari yako ya maisha na safari ya Utumishi pia.
Leo ninataka tutoke hapo sasa tuangalie jambo jingine ndani ya THE MIGHT OF GOD IS UNQUESTIONABLE. Karibu sana tuendelee kujifunza pamoja.

Katika siku hizi mbili Tumefanikiwa kuona dhana za ndani kabisa za mistari yetu ya msingi ambayo ni Luka 1:37 na Luka 18:27. Mungu hasubiri tumalize somo ndiyo upate jambo la kujifunza na la kuondoka nalo, na kwa sababu hiyo naamini kwamba kupitia mistari hiyo ya msingi na maelezo yaliyotolewa vimekutoa mahali kwenda mahali pa juu na pazuri zaidi katika safari yako ya maisha na safari ya Utumishi pia.
Leo ninataka tutoke hapo sasa tuangalie jambo jingine ndani ya THE MIGHT OF GOD IS UNQUESTIONABLE. Karibu sana tuendelee kujifunza pamoja.

SIFA ZA MUNGU (ATTRIBUTES OF GOD)
Sifa za Mungu ziko nyingi sana, katika masomo yangu ya Theolojia niliwahi kusoma kozi moja yenye Jina la ATTRIBUTES OF GOD na mwandishi wa ile manual amechambua karibu sifa 40 za Mungu. Sitaki kusema zote hizo ila nataka nikuonyeshe sifa kuu nne za Mungu ambazo humtafautisha kabisa yeye na miungu mingine.
Sifa hizi nne siyo kwamba zenyewe ni bora na muhimu kuliko zingine bali na zenyewe ni sehemu ya kuendelea kutafsiri mada yetu ambayo ni THD MIGHT OF GOD IS UNQUESTIONABLE.

SIFA YA KWANZA : YUPO KILA MAHALI (OMNIPRESENCE)
Mungu wetu yupo kila mahali, yupo hata mahali pale ambapo hatujawahi kufikiri kwamba yupo. Fikiria popote unapoweza kufikiria, Mungu yupo. Na, si tu kwamba yupo sasa bali yupo wakati wote.
Hapo ulipo Mungu yupo, hapa nilipo Mungu yupo, na, kule kwingine yupo, ile kwamba humuoni haina maana kwamba Hayupo kwa sababu ni vitu vingi sana hatuvioni lakini vipo. Ile kwamba huoni madhihirsho yake haina maana kwamba Hayupo, maana Mungu kujidhihirisha mahali ni jambo jingine tena.

Kwa kuwa Mungu yupo kila mahali, hakuna namna unaweza kumkimbia. Ndiyo, unaweza kukimbia kivuli chako lakini huwezi kumkimbia Mungu. Umewahi kujiuliza swali hili katika wakati fulani wa maisha yako?

“Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?”
— Zaburi 139:7 (Biblia Takatifu)
Mtu mmoja baada ya mambo yake kuwa magumu alikusudia kwenda mbali kabisa na wanadamu, lakini siyo mbali na Mungu kwa sababu huwezi kumkimbia Mungu.

Je wewe umewahi kufikiria kwenda wapi? Daudi aliwahi kufikiria hivi;
Zaburi 139 (Biblia Takatifu)
⁸ K**a ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
⁹ Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari;
¹⁰ Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika.

Daudi aliwahi hata kufikiria kwenda kuzimu, aligundua kwamba Mungu na huko pia yuko. Umewahi kukutana na hali ile wanasema unatamani ardhi ipasuke ikumeze? Ardhi inaweza kukumeza kweli lakini na huko utakakowenda Mungu yupo. Wapi tena?

Zaburi 139 (Biblia Takatifu)
¹¹ K**a nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;
¹² Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza k**a mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.

Kwa nini maovu mengi hufanyika usiku? Hata hivi ninavyoandika Kuna watu na inawezekana wengine wanapitia ujumbe huu wanasubiri usiku uingie vizuri ili waweze kufanya maovu yao kwa Uhuru. Ni kwa sababu wakati wa giza/usiku ni ngumu kuonekana na watu, lakini siyo ngumu kuonwa na Mungu kwa sababu kwake yeye ni mwanga na giza ni sawasawa.

Kwa hiyo unaweza kudhani kwamba umefanya kwa siri kabisa lakini ninakupa uhakika kwamba wakati unafanya Mungu alikuwepo na amekuona. Ndiyo, hata k**a ulikuwa peke yako.

Daudi alipozini na mke wa Uria maandiko hayatuelezi kwamba Kuna mtu yeyote aliyeshuhudia kile kitendo, lakini tunaelezwa Mungu akimtuma Nathani kwenda kuzungumza na Daudi juu ya tukio lile lililofanyika kwa siri sana.
Nataka kusema nini? Hakuna mahali ambapo Mungu Hayupo, yupo kila mahali. K**a Kuna jambo baya umefanya na ukafikiri kwamba uko salama kwa sababu mchungaji wako hajui, wazee wa kanisa hawajui, wazazi na watu wengine hawajui, ninakufahamisha kwamba hauko salama. Salama yako ni kutubu tu.

Hii sifa ya Mungu kuwa kila mahali inaendelea kuatamia uweza wa Mungu na kuufanya uwe unquestionable. Sasa k**a anaweza kuwa kila mahali kwa wakati wote ni jambo gani litamshinda kulifanya? The Might of God is UNQUESTIONABLE.

SIFA YA PILI: MUNGU ANAJUA MAMBO YOTE (OMNIPRESENCE).
Wanadamu tumepewa uwezo fulani wa kujua mambo, lakini hatujui mambo yote. Ndiyo, hata tunfeunganisha fahamu na uelewa na ujuzi na elimu zetu wote kabisa, bado Kuna mambo mengi sana ambayo hatuyajui. Ndiyo, Kuna mambo mengi sana yasiyo na idadi ambayo hatuyajui, labda tutayajua tukifika mbinguni.
Nabii Isaya anapoandika kwa ulinganifu yale ambayo sisi tunayajua na yale ambayo Mungu anayajua anasema hivi.....

Isaya 55 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁸ Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.
⁹ Kwa maana k**a vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.

Mimi Nimesoma Geography, haya mambo ya umbali tulisoma sana mpaka umbali wa kutoka kwenye jua mpaka kwenye dunia kwamba ni takribani kilometa million 149.6. Ni umbali mrefu sana lakini hak

Lakini umbali kati ya dunia na mbingu hakuna anayejua isipokuwa Mungu mwenyewe. Kwa hiyo Mungu anaposema kwa kinywa cha Isaya kwamba mawazo (Biblia zingine zimeandika though, knowledge, power, plans) yake yako mbali sana la mbingu ilivyo mbali na dunia maana yake uwezo wake wa kujua mambo ni mkubwa kiwango ambacho hausemeki zaidi ya kusema anajua mambo yote.
Daudi anasema...

Zaburi 139 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Ee Bwana, umenichunguza na kunijua.
² Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
³ Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, Umeelewa na njia zangu zote.

Zaburi 139 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Maana hamna neno ulimini mwangu Usilolijua kabisa, Bwana.
⁵ Umenizingira nyuma na mbele, Ukaniwekea mkono wako.
⁶ Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi, Hayadirikiki, siwezi kuyafikia.

Je Mungu anayejua mambo yote kutakuwa na jambo la kumshinda kweli? Ni muhimu ufahamu kwamba uwezo wa kufanya mambo umefungwa kwenyw uwezo wa kujua mambo, yule anayejua zaidi atafanya mambo mengi na makubwa zaidi.

Sifa hii nayo inaendelea kuatamia the Might of God is UNQUESTIONABLE.

SIFA YA TATU: WA MILELE ASIYEBADILIKA (ETERNAL AND UNCHANGING)
Kitu chochote ambacho wewe unakijua kina mwanzo wake, na chenye mwanzo lazima kitakuwa na mwisho wake (kanuni ya asili). Chochote chenye mwanzo kina historia yake ambayo inaweza kwenda umbali mrefu inavyowezekana lakini kuna wakati utafika mwisho. Pia chenye mwanzo kina tabia ya kubadilika kulingana na mazingira na muda.

Lakini kuna Mungu ambaye hana mwanzo, habadilili, hakui, hazeki, na nini Tena? Ni yeye yule Jana Leo na hata milele.

“Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.”
— Malaki 3:6 (Biblia Takatifu)

“Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.”
— Waebrania 13:8 (Biblia Takatifu)

Umewahi kufikiria mtu ambaye ameishi miaka mingi zaidi? Methusela aliishi miaka 969. Waswahili husema kuishi kwingi ni kuona mengi, na k**a ni hivyo basi kuishi kwingi ni kuweza mengi yaani kuwa na uwezo mkubwa. K**a hii ni kweli basi Methusela kwa kizazi chake alikuwa na uwezo mkubwa kuliko walio wengi.
Sasa Kuna Mungu ambaye hana mwanzo na hana mwisho, hii nayo inaendelea kuatamia the Might of God is UNQUESTIONABLE.

Sifa ya nne tutaangalia kesho ambapo tutahitimisha na mambo mengine makubwa ambayo yanaendelea kukoleza the Might of God is UNQUESTIONABLE.

Bwana Yesu akubariki sana.

Address

Dodoma
2158

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when KPMC Church posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share