23/11/2021
Somo: upendo kwa adui wako.
Rev: Sam Arnold
BWANA YESU asifiwe ndungu wapendwao , Leo napenda tuwe na somo juu ya kuwapenda watu ambao nafsi zetu ziliwaona k**a maadui zetu.
Rumi 12:20 lakini adui yako akiwa na njaa mlishe ; akiwa na kiu mnyweshe; maana ufanyapo hivyo utampalia makaa ya moyo
Kuna wakati mtu alikuuzi kiasi ambacho mlivunja mpaka ukaribu mliokuwa nao haupo Tena. Hii Ni kutokana na ukweli kwamba qliumiza moyo wako
Umewahi pokea taarifa za kuwepo kwa watu wenye tabia mbaya mtaani kwako K**a vile waizi, wachawi, watu wanojiuza mashoga matapeli na tabia zinazo endana na hizo . Watu hawa wameumiza moyo wako kwa matendo yao machafu, hata K**a haukuumizwa nao Basi nduguyo amewahi kutana nao.
Katika kukuumiza ulifika wakati uliwachukia hata kuto kuwathamini hata kugoma kukaa karibu nao pengine umefikia kumwombea hata kwa Mungu ili awaondoe ukiamini Mungu anakulipizia kisasi kwa adui zako.
Ikumbukwe Mungu huwapenda wenye dhambi kiwango Cha kuwafia msalabani, na haujawahi kuwaona kuwa Ni adui kwake .
Waombee wanao kuudhi tutaendelea panapo neema