06/05/2026
MFUNGO WA SIKU 40:DAY 5.
👉KUOMBEA WAZAZI.
Tunamshukuru Mungu Kwa baraka zake kuifikia Siku ya Leo.Hili jambo la kuwaombea WAZAZI ni k**a halifanyiki mara Kwa mara maana mara nyingi utasikoa KUOMBEA watoto,mabinti wasioolewa n.k ila ni mara chache sana kuandaa MAOMBI kwaajili ya KUOMBEA WAZAZI wetu.Kwa neema ya Mungu Leo Siku yetu ya 5 tunapata muda WA kuwaombea WAZAZI wetu.
Mungu AMETUPA WAZAZI Bora sana na hii haijaalishi wapo hai ama hawapo ila ninachokiamini ni kwamba kila Mtu ametokana na WAZAZI katika kuzaliwa kimwili.Hivyo tenga muda wako KATIKA kuwaombea WAZAZI wako.
VITABU VYA KUSIMAMIA KATIKA MAOMBI.
YOHANA 19:25-27Â Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene.
26 Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao.
27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.
1 TIMOTHEO 5:8 Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
MITHALI 23:22 Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.
LUKA 1:41-42 Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu;
42 akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.