Jecafu Assemblies of God -Jag

Jecafu Assemblies of God -Jag YOHANA 10:10b' "Yesu alikuja kwa ajili yako" "Jesus Came for You" (JECAFU).

10/06/2025
Mapishi ya Ijumaa 23/06/2025 yanaendelea katika eneo la tukio. Ewe mkazi wa Dodoma hii sio ya kukosađź•“
05/06/2025

Mapishi ya Ijumaa 23/06/2025 yanaendelea katika eneo la tukio. Ewe mkazi wa Dodoma hii sio ya kukosađź•“


Askofu, makamu askofu pamoja na baadhi ya wachungaji wa kanisa la JECAFU Assemblies of God katika picha za pamoja wakiwa...
05/09/2024

Askofu, makamu askofu pamoja na baadhi ya wachungaji wa kanisa la JECAFU Assemblies of God katika picha za pamoja wakiwa kwenye kongamano la mwaka lililokutanisha waumini kutoka matawi yote. Kongamano hili lilifanyika katika kanisa la JECAFU makao makuu, Ihumwa, Dodoma.

Mungu ametupa wachungaji wazuri wa roho zetu.
God bless our pastors.

Karibuni nyoote.
20/08/2024

Karibuni nyoote.

19/08/2024


Yesu Juu watumishi wa Mungu! Kwa Neema ya Mungu tumepata nafasi tena ya kuandaa Ibada hii kwa msimu wa pili mfululizo, n...
25/07/2024

Yesu Juu watumishi wa Mungu! Kwa Neema ya Mungu tumepata nafasi tena ya kuandaa Ibada hii kwa msimu wa pili mfululizo, naomba kuwaletea Tangazo hili, sasa ni rasmi tarehe 30 Agosti 2024 tutakuwa na Mkesha huu Mkubwa, tafadhali usipange kukosa, mwalike na rafiki yako.


Pokea salamu za mwaka mpya kutoka Mwaka 2024 ukawe mwaka utakaoutumia kumtafuta na kuhusiana na Mungu kibinafsi.Ukawe ni...
01/01/2024

Pokea salamu za mwaka mpya kutoka

Mwaka 2024 ukawe mwaka utakaoutumia kumtafuta na kuhusiana na Mungu kibinafsi.

Ukawe ni mwaka wa kutimiza malengo ya kusoma neno zaidi, kusikiliza mafundisho zaidi, kufunga na kuomba zaidi, kuongozwa na Roho Mtakatifu zaidi na kuongeza kiwango chako cha imani na utakatifu zaidi.

Mungu hatakuacha ikiwa utatembea katika mapenzi yake. Amen

Uwe na mwaka uliobarikiwa sana.

See you at the top.



Mratibu wa Vijana  akizungumza, kuomba, kuombea na kuongoza vijana na watu wote kumshukuru Mungu kwa mambo aliyoyatenda,...
31/12/2023

Mratibu wa Vijana akizungumza, kuomba, kuombea na kuongoza vijana na watu wote kumshukuru Mungu kwa mambo aliyoyatenda, anayoyatenda na atakayoyatenda.

Kati ya mambo mengi aliyozungumza, mratibu hakuacha kuwakumbusha waumini kote duniani kumshukuru Mungu pasipo kujalisha hali wanazopitia maana biblia imetuasa kumshukuru Mungu katika kila jambo.

Je, umeacha kumshukuru Mungu kwa sababu ya hali unazozipitia! Usiache maana katika mambo yote twajua kwamba Mungu hutenda kazi na wale wampendao ILI KUWAPATIA MEMA.

Heri ya Mwaka mpya mwanafamilia wetu. Tunakupenda.




Asante Mungu kwa kutuwezesha kuwa na ibada ya mkesha wa vijana kurudisha shukurani kwa yale yote uliyotutendea katika mw...
31/12/2023

Asante Mungu kwa kutuwezesha kuwa na ibada ya mkesha wa vijana kurudisha shukurani kwa yale yote uliyotutendea katika mwaka mzima. Sisi vijana na watoto wako Ee Mungu tuna shukurani nyingi kwako. Tusingeweza pekeetu Bwana. Afya zetu, uchumi wetu, familia zetu, kazi zetu na kila kila kitu chetu ni ushuhuda wa udhihirisho wa utukufu wako Mfalme wa wafalme.

Idara ya Vijana JECAFU ASSEMBLIES OF GOD tumeazimia kukupa ibada hii kwa kutambua na kuthamini uwepo wa Mwanao Yesu Kristo katika kututendea mema siku zote. Sifa zote zina Mungu wetu aliye JUU milele na milele, Amen.

Address

Elshadai
Dodoma

Telephone

+255625655004

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jecafu Assemblies of God -Jag posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share