02/07/2026
https://www.facebook.com/share/p/1GVdv2AzZF/
Ujumbe wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini kuhusu suala la ndoa baada ya kusema ana Degree 4 hivyo hawezi kuishia kupika na kufua.
"Tatizo la zama hizi ni kwamba tunawasilisha ndoa kana kwamba ni gereza la ndoto, wakati ukweli ni kwamba ndoa bora ni mahali ambapo ndoto za pande zote mbili hukua. Lakini juu ya ndoto zote kuna ndoto moja kuu zaidi, kuishi kwa furaha, upendo, heshima na unyenyekevu"
"Kufua boxer au kupika ukiwa na degree nne si udhaifu, k**a ambavyo elimu si kipimo cha ubora wa ndoa wala thamani ya mtu. Mambo haya yanaweza kuishi pamoja bila mgongano"
"Elimu haimfanyi mtu kuwa mkubwa kuliko huduma, na huduma haipunguzi hadhi ya mtu. Mtu anaweza kuwa na shahada nyingi, akaongoza na kubadilisha jamii, na bado akachagua vitendo vya upendo ndani ya ndoa. Hilo si kushushwa hadhi, ni uchaguzi wa upendo"
"Tatizo huanza pale majukumu ya kifamilia yanapoonekana k**a adhabu badala ya kujitoa. Ndoa si mashindano ya vyeo au vyeti, bali ni safari ya kuulizana, Leo nita