22/07/2026
SHUKRANI ZA DHATI
Kwa niaba ya familia ya marehemu Agness Joseph Assenga, mfiwa (Dr. Prophetess Oliver Edward Mwiga) pamoja na familia nzima, tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kila mmoja aliyesimama nasi katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mama yetu mpendwa, Agness Joseph Assenga, aliyefariki dunia tarehe 14 Julai 2026 katika Hospitali ya Amana akiwa anapatiwa matibabu.
Tunatoa shukrani za pekee kwa Wachungaji, Mitume, Manabii, viongozi wa dini mbalimbali, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndugu, jamaa, marafiki, majirani, wafanyakazi wenzetu, na wote mliojitokeza kutufariji kwa maombi, salamu za pole, michango ya hali na mali, pamoja na uwepo wenu kuanzia kipindi cha kuugua, msiba, mazishi hadi baada ya mazishi.
Upendo, mshikamano na faraja mlizotuonyesha vimetupa nguvu kubwa katika kipindi hiki cha majonzi. Kwa hakika, hatuna uwezo wa kuwataja mmoja mmoja, lakini kila mchango na kila neno la faraja limegusa mioyo yetu na litabaki kuwa sehemu ya kumbukumbu zetu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu awabariki kwa wingi, awalinde, awaongezee afya njema, amani, neema na mafanikio katika kila hatua ya maisha yenu.
Tunawaombea mrejeshewe mema mara nyingi zaidi kwa yote mliyotutendea.
Mungu awabariki sana.
Imetolewa na: Dr. Prophetess Oliver Edward Mwiga
(Mfiwa)
Pamoja na Familia ya Marehemu Agness Joseph Assenga.