Viwawa Parokia Mt.stephano Shaidibuguruni DSM

Viwawa Parokia Mt.stephano Shaidibuguruni DSM Kwenye page hii tutapata taarifa mbalimbali kutoka viwawa wa Parokia ya Mt.stephano shahidi Buguruni

Tumezaliwa kwenye moja, Kanisa moja, Katoliki Takatifu la Mitume. Tujivunie Ukatoliki wetu ⛪🙏
14/01/2026

Tumezaliwa kwenye moja, Kanisa moja, Katoliki Takatifu la Mitume.

Tujivunie Ukatoliki wetu ⛪🙏

07/01/2026

K**a kawaida, Vijana tulikiwasha haswa na kujivunia Ukatoliki wetu kupitia nyimbo halisi za Kikatoliki.



.Yoseph

Baadhi ya picha za Matukio katika siku ya VIJANA ambayo ilifana vilivyo katika ukumbi wetu wa Parokia.
05/01/2026

Baadhi ya picha za Matukio katika siku ya VIJANA ambayo ilifana vilivyo katika ukumbi wetu wa Parokia.

FAHAMU  KWA UFUPI  HISTORIA  NA  KIFO  CHA  MT.  PETRO HUKU  KICHWA  CHAKE  KIKITAZAMA  ARDHINI:Mtume Petro aliuawa kish...
03/01/2026

FAHAMU KWA UFUPI HISTORIA NA KIFO CHA MT. PETRO HUKU KICHWA CHAKE KIKITAZAMA ARDHINI:

Mtume Petro aliuawa kishahidi mjini Roma mnamo mwaka 64 BK, wakati wa utawala wa Kaisari Nero.

​Kifo chake kilikuwa hivi:

✍️ Aliihukumiwa adhabu ya kusulubiwa.

✍️ Petro aliomba asisulubiwe k**a Yesu Kristo, kwa sababu alijiona hastahili kufa kwa namna sawa na Bwana wake.

✍️ Maombi yake yalikubaliwa, hivyo alisulubiwa kichwa kikitazama chini na miguu juu.

✍️ Aliuawa katika eneo la Circus of Nero (karibu na vilima vya Vatican). ​Mwili wake ulizikwa karibu na eneo hilo, na sasa hivi Basilika la Mtakatifu Petro mjini Vatican limejengwa juu ya kaburi lake.

Heri na Baraka zikatawale kwetu  sote katika mwaka huu mpya.
01/01/2026

Heri na Baraka zikatawale kwetu sote katika mwaka huu mpya.

DOMINIKA YA SHEREHE YA FAMILIA TAKATIFU Familia Takatifu ni jina linalotumiwa na Kanisa Katoliki kuitaja familia ya Yesu...
28/12/2025

DOMINIKA YA SHEREHE YA FAMILIA TAKATIFU

Familia Takatifu ni jina linalotumiwa na Kanisa Katoliki kuitaja familia ya Yesu, Bikira Maria, na Mtakatifu Yosefu. Inachukuliwa kuwa ni mfano bora wa kuigwa na kila familia ya Kikristo kwa sababu ya unyenyekevu, upendo, na utii wao kwa Mungu.

​Ni siku ya sherehe katika Kanisa Katoliki inayoadhimishwa siku ya Jumapili (Dominika) inayofuata baada ya Sherehe ya Noeli (Kuzaliwa kwa Yesu).

• ​Kutakasa Familia: Ni siku ya kutambua kuwa familia ni kanisa dogo na inapaswa kuwa mahali pa utakatifu.
• ​Mfano wa Kuigwa: Waamini wanahimizwa kuiga fadhila za Yosefu (ulinzi na kazi), Maria (upendo na imani), na Yesu (utii kwa wazazi).
• ​Kuombea Familia: Ni siku maalum ya kuziombea familia zote ulimwenguni zipate amani, umoja, na ulinzi wa Mungu dhidi ya changamoto za sasa.

TUWASIFU MILELE.....👋

Vijana Wote siku ya kesho tunakutana Jimbo la Bagamoyo, jitahidi usikose.
26/12/2025

Vijana Wote siku ya kesho tunakutana Jimbo la Bagamoyo, jitahidi usikose.


MTAKATIFU STEFANO, SHAHIDI WA KWANZA WA KANISA 26 DESEMBA Mtakatifu Stefano alikuwa Mwisraeli,  ambaye alikuwa na elimu ...
26/12/2025

MTAKATIFU STEFANO, SHAHIDI WA KWANZA WA KANISA

26 DESEMBA

Mtakatifu Stefano alikuwa Mwisraeli, ambaye alikuwa na elimu ya kigiriki. Alichaguliwa kuwa shemasi, yeye na wenzake 6.Walichaguliwa na mitume wote kwa pamoja, ili kusaidia kufanya kazi ya Mungu kwa pamoja.

Mtakatifu Stefano alijaa hekima, na uelewa mkubwa. Mara nyingi alikuwa akishiriki katika kufundisha, na kuelekeza mambo yote yaliyokuwa na utatanishi wa kuelewa na pia kujibu maswali mbalimbali.

Katika moja ya mikutano yake, alikutana na kundi la Wayahudi, ambao walianza kumuuliza maswali mbalimbali, kutoka katika maandiko matakatifu. Wayahudi hao, baada ya kuzidiwa busara na Mtakatifu Stefano, walimzulia tuhuma za uongo, kwamba alimkufuru Mungu.

Wakamuhukumu kufa, kwa kumpiga na mawe. (Mat.7:51-53)

Watakatifu wengine tunaowakumbka ni : -
Mt. Abadiu
Mt. Amaethlu
Mt. Archelaus
Mt. Papa Dionysius
Mt. Marinus
Mt. Neol Chabanel
Mt. Tathal
Mt. Theodore
Mt. Vincentia Maria Lopez Y Vicuna
Mt. Zeno
Mt. Zosimus

Mtakatifu Stefano, Wenye heri na Watakatifu wengine wote wa leo, Mtuombee 🙏

TUNAWATAKIA KHERI YA SIKUKUU YA NOEL ⛪🎄
25/12/2025

TUNAWATAKIA KHERI YA SIKUKUU YA NOEL ⛪🎄

Ee Baba yetu Mungu mkuu,Umenilinda usiku huu.Nakushukuru kwa moyo,Ee Baba, Mwana na Roho.Nilinde tena siku hii,Niache dh...
24/12/2025

Ee Baba yetu Mungu mkuu,
Umenilinda usiku huu.
Nakushukuru kwa moyo,
Ee Baba, Mwana na Roho.
Nilinde tena siku hii,
Niache dhambi, nikutii.

Naomba sana Baba wee,
Baraka zako nipokee.
Bikira safi, Ee Maria
Nisipotee nisimamie.

Mlinzi mkuu malaika wee,
Kwa Mungu wetu niombee
Nitake nitende mema tu,
Na mwisho nije kwako juu.

** Mungu akubariki katika siku yako mpya na wote tuseme AMINA.

Address

Dar Es Salam
41241

Telephone

+255713373731

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Viwawa Parokia Mt.stephano Shaidibuguruni DSM posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Viwawa Parokia Mt.stephano Shaidibuguruni DSM:

Share